Kwenye ukurasa wa mbele kuna habari iliyozua kasheshe Tanzania. Habari hii ilitoka kwenye gazeti la Mwanahalisi la Jumatano la kupokelewa kwake kumekuwa na hisia za aina yake kwani siku ya pili yake Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo iliandika barua kwa Mwanahalisi kutaka maelezo juu ya habari hiyo ambayo kwa maoni ya serikali inaonekana ni kiuchochezi na kiuchonganishi.
Watu wa serikali wanaona kuwa habari hiyo ilikuwa na lengo la kumchonganisha Rais na viongozi wenzake wa CCM hasa Mhe. Edward Lowassa na Bw. Mhe. Rostam Aziz.
Lakini zaidi ni mstari ambao unaonekana kumgusa Rais Kikwete na mwanawe Ridhiwani ambaye anaonekana kuhusika katika hicho ambacho gazeti la Mwanahalisi limekiandika na unaweza kusoma kwenye ukurasa wa mbele wa http://www.klhnews.com
Lakini hapa Bw. Kubenea anaelezea upande wake na tutajitahidi kupata upande wa serikali mwishoni mwa juma hili. Soma habari yenyewe, kisha amua kama kweli inaweza kusababisha gazeti kufungiwa, kama ni ya kichochezi kiasi cha kutishia Urais wa Kikwete na kama inasema jambo lolote ambalo halijawahi kusemwa na watu wengine (sisi Cheche liligusia suala la Lowassa kuwa Zuma wa Tanzania karibu mwezi sasa umepita).
Je gazeti hili limeendelea kuwakwaruza watawala na sasa wakati umefika kuliondolea uvivu? Je mipaka ya uhuru wa habari ni nani anaichora, watawala? Je mtawala ambaye ana uwezo wa kuamuru nini kisemwe na nini kisisemwe pale yanapokuja maswala yake anafanya hivyo kwa maslahi ya Taifa na Katiba au kwa sababu sasa ni zamu yake na kashikwa pabaya?
Je Taifa lisiloliinda Uhuru wa maoni ya kijinga, na ya kipuuzi, litaweza kulinda uhuru wa maoni ya heshima na yasiyoudhi na yanayoonekana ya kiakili? Je mtu mwenye maoni ambayo siyo ya kufurahisha anayo haki ya kuyatoa hata kama yanaudhi? Au haki hii ya maoni iko kwa wale waimbao sifa za watawala na wachezao ngoma ya watawaliwa!?
Title: KLH News Episode:
Serikali yaipiga mkwara Mwanahalisi, Kubenea ajibu hoja!
/entry/2008-10-09T22_54_00-07_00
mymedia/thumb/13384/300x300_1272427.jpg

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Mie sasa nishachoka na hayo mambo ya waandishi na kudai uhuru kila siku, mie naona nyie ni wanafiki tu hamna jipya lolote zaidi ya kuongelea mambo yasiyo mgusa mwananchi wa chini ambaye hajui hiyo siku ataioitishaje leo. Nyie mnakunywa chai ya maziwa na mikate yenye siagi (buttered bread) akati mtanzania wa kawaida tena aliye ndani ya jiji la Dar es Salaam wala si mkoani hajui yeye na watoto wake kwa siku hii ya leo atakula nini na atapata wapi kodi ya nyumba ya kulipia hicho chumba chake kimoja anacholala yeye na watoto wake wote. Hivi mnafikiri kuwa majority ya watanzania hawa masikini hawana pesa ya kununua mkate wao wa kila siku wanapesa ya kununua hayo magazeti yenu? Uzuma wa Lowassa sijui na nani utamsaidiaje huyu mlalahoi ambaye hata hilo gazeti hawezi nunua? Hebu sasa wewe Mwanakijiji kama kweli unanuchungu na umaskini uliokithiri utupe mikakati ya maana ya kuondokana na umasikini (sio kujiunga na Chadema au CUF au CCM, leave politics out of this), mikakati ambayo itanifanya nikuone wa maana na kweli una malengo ya kusaidia masikini wa nchi hii otherwise nitakuona ni wale wale wanaotumiwa na wanasiasa kwa maslahi ya wanasiasa na maslahi yao binafsi! Na hao majority ninaowazungumzia hapa hawasomi kijarida chako wala kusikiliza hizo podocasts sijui nini, ni minority ambao wanajua kula yao ya mwezi mzima itakuwaje (sio ya siku ya leo) ndio wana access na hizi information zako.

    Mwisho nafikiri Kubenea hana cha kuandika kwa sababu ni miezi mingapi sijui sasa anaandika habari moja tu ya Lowassa, sijui ni kwa ajili ya publicity ya Lowasa au sijui vipi kwa sababu hata bad publicity inalipa hufutiki kichwani au mawazoni mwa watu midamu unaandikwa japo vibaya! Nahisi kama Lowasa ama anamiliki hilo gazeti la Kubenea au ana hisa kubwa kwenye hilo gazeti. Haiwezekani hakuna toleo hata moja la Mwanahalisi likakosa habari za Lowasa kama ilivyokuwa wakati alipokuwa Waziri Mkuu, hakuna siku hata moja ambayo picha yake haikutokea kwenye gazeti, kama sio picha basi habari inayomhusu. Kama mtu anabisha aende Maktaba na kuchambua magazeti kama hatakuta kila siku Lowasa ametoka kwenye gazeti. Hivi hakuna habari nyingine kweli ambayo Kubenea anaweza kuandika au uwezo wake unaishia hapo anapoishia?

    ReplyDelete
  2. Hiyo habari hearding yake ni ipi. Wengine kweli kuingia kwenye magazeti na kuanza kusoma kila habari wala huo mda haupo. Please naomba uandike tukiingia kwenye hiyo link tusome habari yenye kichwa cha habari gani.

    Uhuru wa habari muhimu kwa kila mtu as long ni habari za ukweli na sio za uongo. Hao wanaoponga ndio hao wanaoruka kila siku na wanajinunulia Ny times na kuona ya wenzao yanayosemwa humo kila siku. Sasa iweje wao wasitake yao yasemwe kama ni ya kweli....Watumishi waserikali wa tanzania wamesahau kuwa sisi wananchi ndio tumewapa hiyo kazi na tuna haki ya kujua yanayoendelea. Kama mtu anahitaji private life baada ya kuwa public employee aachie ngazi. I know sometimes the kids are off limit lakini kama character zao ni mbaya sio mbaya kuwaweka hadharani. Ukiingia kwenye kazi ni sacrifices nyingi sana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...