hapa ni feri ya magogoni leo usiku saa nne na dakika 19. camera ni canon EOS 400D yenye lensi ya canon zoom ya spidi 1:2.8 na nimeipigia bila flashi huku nikiwa nimeegemeza kamera kwenye jiwe ili isipate mtikisiko. nimetumia sekunde 8 katika upenyo wa f8 huku kamera ikiwa 'manual'.mambo kama hayo na mengi mengine utayapata libenekelataswira.blogspot.com
ambako unakaribishwa kuangalia, kuchangia taswira na maoni pia na kupata ama kutoa darasa
-michuzi


Mdau ebu andika jina la blog yako vizuri,maana nimetafuta mpaka basi, kumbe kuna S imekosekana ,ni taswira na sio tawira, wacha wehu
ReplyDeleteJAMANI WADAU HATA KAMA KUNA MDAU ALIKOSEA NA KUANDIKA TAWIRA BADALA YA TASWIRA ISINGETOA PICHA IKATUMIWA HIVO.NAKUSHAURI MDAU ULIYEGHAFILIKA UPUNGUZE JAZBA KWANI ITABAKI KUWA TASWIRA HATA KAMA NENO LOLOTE LITATUMIKA LAKINI VIONEKANAVYO VITAASHIRIA NI TASWIRA.
ReplyDeleteTUPUNGUZE JAZBA WAUNGWANA NI MDAU WA BANANA DAR.
kwani ukitumia 40d lens yenye image stabliza kuna haja ya kuweka kwa jiwe? au trpod?? nijibu
ReplyDeletePicha nzuri sana! yenye hisia hata kama hayo mahesabu sielewi
ReplyDeleteHe he he..ngoja nigeuke MICHUZI nianze kuichambua hii picha...!
ReplyDelete1.Umechagua eneo zuri la kupiga picha, lakini unaonekana unakitetemeshi cha mikono au unabwia "ze bingwa" au GONGO sana, picha haiko clear!
2. Hapo tunashindwa kuelewa unataka kutuonesha nini, vurugu tupu!
3 Ungesubiri walau samaki atokeze hapo baharini ili uonehse uhai au kwenye hilo anga ungesubiri bundi wa usiku wapite, sio kuacha picha bila uhai (acha pupa, vitu vizuri vinataka subira)
4.Huo mtumbwi wakwendea Mtwara umeukata, we vipi, jicho la mtazamaji linakwenda moja kwa moja kwenye huo mtumbwi, ungeukwepa kabisa au ungeutoa wote!
5.Hayo majengo pacha ya BOT ungejaribu kukwepesha kamera yako, sababu jicho la mtazamaji litakumbuka ufisadi unaoendelea nchini, na kupunguza ladha ya picha..!
7.Ili usiwe na kitetemeshi kama unatumia camera aina ya canon EOS 400D, jaribu kuigandisha na "super glue" kwenye jabali kwa masaa 3 mpaka 5, naukipiga bana pumzi kama umeona "kinyesi kibichi njiani" kwa dk 20 hivi, au tumia camera aina ya KODAK VPIX 6000HD!
NB:Beauty lies in the eye of the beholder, kwa hiyo inategemea umewalenga watazamaji wa aina gani, kama ni mafisadi au wafisadiwa!
mbona hakuna uhai?
ReplyDeletePicha nzuri..sijui kwa nini hukutumia flash halafu umetumia aperture ndogo f8??? kwa picha kama hii inahitaji aperture kubwa ili kupata kuingiza mwanga ingawa shutter speed yako ni ndogo. Nimependa reflection katika maji buts its kinda dark and your white balance is a little way off.
ReplyDeleteMtaalamu wa Digital...