taswira 1
taswira 2
taswira 3
Salaam Kaka ze Michu ze Fulanaz. Tafadhali toa darasa la kuendeleza libeneke la picha ndani ya ndege. Hizo snepu ni jitihada za amacha kutumia kamera ya kiamacha ndani ya dege la wasasko.
Asante kwa kutupiga shule.
Ndimi Mdadisi,
-------------------------------------------------------------------
Mdadisi!
asante sana kwa taswirazzz mwanana. hapo mie sina neno zaidi ya kutoa nasaha mbili tatu kama ifuatavyo, pamoja na kukupa mfano wa taswirazzz inayovutia zaidi uwapo ndani ya ndege hapo chini. kumbuka kila mara kufikiria taswirazzz kama insha. yaani unataka kusema nini na kumwambia nani. kama unataka kusema kuhusu mbingu, basi zipewe kipaumbele kwa ukubwa (centre of attention), kama ni mbawa kadhalika, ama nenmbo ya shirika, kama si ukubwa/udogo wa bawa. hapo taswira 1. ndiyo bomba kwani SAA wanaweza kukuomba waitumie kutangaza nembo yao
1. tatizo la wengi wetu tunaotaka kupig picha kwenye ndege ni kuegemeza kamera juu ya kioo cha dirisha katika juhudi za kuepa mng'aro wa kioo (reflection). ukifanya hivyo una hatari ya kupata picha isiyo sharp kwani mtikisiko wa injini ya ndege utatibua mambo. sasa hapo kama una kamera yenye kofia (hood) ya lenzi, iweke kwani itasaidia kuzuia mng'aro. kama huna tumia kiganja cha mkono mmoja kukingia.
2. kamera yako usiiache kwenye automatik kwani hapo utailewesha isijue isome mwanga upi. angalia taswira 2 na taswira 3 kama mfano.
3. piga picha katika muda wa awali wa kupaa kwani mara nyingi kioo cha dirisha cha ndege iliyosafiri kwa muda mrefu hupata ukungu kwa nje na kukukosesha snepu nzuri.
4. kuwa tayari mnapokaribia kutua, hasa pale ndege inapolaza upande. huo ndio muda nzuri wa kupiga picha ardhini, vinginevyo huwa vigumu.
5. zima flashi yako kwani kwa picha za angani utakuwa unampigia mbuzi gita.
6. acha uvivu wa kupiga na kuweka picha kwenye globu yako.... (hahahaa... sitanii) maana maneno matupu kibao yana mushkeli saa ingine. au vipi?


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Asante sana kwa lekcha ya taswirazz Mheshimiwa kaka Michu!

    Kama bado hujaandika kitabu, nashauri kabisa ufanye hivyo. Wewe ni mtaalamu hasa na picha zako ni murua sana!!! Yaani hiyo taswirazz uliyoweka hapo chini ni bomba hasa...

    Nakutakia kila la heri katika kuendeleza libeneke kwa jamii...

    ReplyDelete
  2. Balozi wa Zain,hivi wale wapiga picha wa zamani(Samahani kama hawako hai)wa magazeti ya serikali kama Mwalimu Omari,Ernest Millinga,Madanga S.Madanga wako wapi?kama itakuwa mbaya kuipost unaweza kunijibu kwenye fridokazadi@gmail.com

    ReplyDelete
  3. Hivi tuition ikiisha hamna maswali....lol....naomba ufafanuzi wa hiyo point ya kwanza kidogo kama sina hiyo, umesema tumia kiganya kufunika....how and where...

    again thanks so much manake huweszi amini nakopy na kupaste kwenye my notebook comments zako zote unazoelezea.


    na kama alivyosema huyo hapo juu kama hujaandika kitabu try to do that ...

    halafu swali lingine limenijia kichwani unavyosema lazimaukipiga picha umakesure kuna uhai wowote? hii ni applied for reporters only au picha yeyote? I wonder kama mfano nikipiga picha za maua nitapata wapi huo uhai? Au maua yanahesabika kama kiumbe hai?

    Thanks

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...