Mkuu wa Wilaya ya nanii na balozi wa Zain,

nimepiga hizo picha jana kama unavyojua siku kuu ya Halloween inakaribia na huu ni wakati wa kipupwe. Naomba uzikosoe.
Mdau M. M. M.

--------------------------------------
Mdau M.M.M!
taswira 1. hii iko out of focus na mwanga ni hafifu. pia nembo umeikata kwa juu nahisi ulifanya haraka kama si uvivu kuangalia unataka kuwaambia nini wasomaji, ama ulipiga kwa kuibia na camera yako ambayo nadhani ni olympus FE210 ambayo pia ni maarufu kama x775 ambayo ni point and shoot yenye megapixels 7.1 na pia haina uhai. angekuwepo muuzaji ama mnunuzi ama wote kama lengo lilikuwa ni kuonesha biashara. kama lengo lilikuwa kuonesha bidhaa si vibaya kama ungelenga pia lebo za bei
taswira 2. hii nimeipenda kwani iko clear na bidhaa pamoja na kuonesha ukubwa wa duka vinaonekana vyema. ungenogesha kwa kuweka uhai japo kwa mbali kulee mtu angekuwa anachagua bidhaa ama anapanga. pia hapa uliposimama ungerudi nyuma kidoooogo ili zile shelf kule nyuma zionekane kwa ukamilifu wake. vnginevyo ni majaribio mazuri ukiondoa vijikasoro hivyo, kwa mtazamo wangu. maana nasisitiza taswira sio hesabu, hivyo kwangu inaweza kuonekana hivyo kwa mwingine vingine. kubwa la kuangalia ni nini unataka kusema, je uwezo wa kamera yako ukoje na unaufahamu? si vibaya siku ingine ukapiga ukiwa umeondoa flashi, ila inabidi ubane pumzi kuzuia mtikisiko ambao hata hivyo kwa kamera ndogo za point and shoot si mkubwa sana.
-michuzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...