vijana wamachinga kiasi cha 10,000 wanatarajiwa kufaidika na majengo haya ambayo yamejengwa mahususi kwa ajili ya kufanyia biashara zao badala ya kuzunguka nazo mitaani. hii ni utekelezaji wa moja za ahadi za JK katika kutafutia vijana ajira. majengo haya matatu yapo ilala nyuma ya uwanja wa kumbukumbu ya karume


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI KWA KUWAJARI MACHINGA

    ReplyDelete
  2. Hii imetulia. Hongera kwa Kikwete

    ReplyDelete
  3. hongera sana baba inaonekana unawajari sana shemeji zako wamachinga

    ReplyDelete
  4. Hofu yangu tunzaji tu wa jengo maana Watanzania wengi hatuja jadi ya kutunza vitu visivyo mali yetu. Naomba kuwakilisha

    ReplyDelete
  5. Ubunifu mzuri sana huu:Hongera serikali lakini angalieni angalau uwezekano wa kuwapunguzia kodi manake najua hapo TRA wanakodoa mimacho

    ReplyDelete
  6. Wenyewe wanawafikia wateja wao kwa urahisi kwa kutembea nyie mnawajengea majengo ya kifahari, itakuwa kama ile hadithi ya binti maskini aliyeolewa kwa mfalme akomba arudi kwao kwa kuwa kazoea kula ukoko na utandu na si wali. Bora wange watafutia usafiri waweze kuwafikia wateja kwa urahisi

    ReplyDelete
  7. Kazi nzuri.Lakini sio kujenga tu,jifunzeni kutunza pia.Nina uhakika baada ya wiki hili jengo litakuwa na mwonekano wa ajabu,takataka za kila aina zitazunguka maeneo ya hili soko.Watu watajisaidia kutani kama wafanyavyo Kariakoo,Temeke,kinondoni,manzese nk.Kukabana,kubakana kama kawaida

    ReplyDelete
  8. Hii inadhihirisha wazi kabisa kuwa serikali yatu haina macho wala mtazamoo wa mbali katika maeneo yote ya wazi ya hapa dar wameshinda kuwawepa wamachinga badala yake wanakuja kuwaweka katika ya barabara tena barabara kuu ya kwenda air port na imagine hiyo foleni yake sijui itakuwaje. kingine hili eneo linasifika sana kwa majini tangu walipochimbua yale makaburi yaliyokuwepo na kujenga barabara je usalama utakuwepo kwa wamachinga na biashara zao au ndio mambo ya Chuma ulete?

    ReplyDelete
  9. Issue ni kwamba watapewa machinga kweli au fix? na wakipewa machinga wanaweza kumaintain upande wa usafi na kuwa na security??????

    ReplyDelete
  10. This is a disaster in construction.....it's just waiting to happen,tusubiri tuone

    ReplyDelete
  11. Swali je hiyo sehemu ina parcking kubwa au public transportation ya kufanya watu waweze kwenda huko na kushop?

    isije machinga wawatu wakapewa kijisehemu na kuchajiwa kodi na wasipate biashara yeyote siku nzima. Na najua baada ya hapo watakuwa hawahitajiki kuonekana tena mitaani. Mbona NY city wapo wengi tu kila corner lakini wanavyofanya ni kulipa kodi na kumaintaine usafi kwenye biashara zao.

    ReplyDelete
  12. Kuhusu sehemu ya kupaki magari , mwanawane hiyo ni machinga complex iko karibu na soko la mchikichini, kuna parking ya kumwaga hapo mchikikini, lakini swali, nyie wenye ,magari mnaofanya shopping, ulaya na samora mtaenda huko kununua mitumba? au bidhaa machinga wanazonunua kwa jumla kariakoo na kuuza reja2? bora wahamie huko maana hapo mtaa wa Kongo tushachoka kuibiwa kwa msongamano.

    ReplyDelete
  13. Na uwanja huo ungetafutiwa watu kama NSSF n.k ili kutoa mkopo kujenga majukwaa ya kisasa kuzunguka uwanja huo wa kuingiza hata watu 15,000 ili iwe kitega uchumi cha wamiliki wa uwanja huo.

    maana hapo ni sehemu rahisi kufikika na watu mbalimbali wa vitongoji vya DSM

    Rocky
    London.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...