samule kabla ya upasuaji
samuel muda mfupi baada ya upasuaji hospitali ya wockhardt iliyopo mumbai
samuel alivyokuwa baada ya kuvuliwa bandeji
samuel akiandaliwa kwa upasuaji
samuel akiendelea kupata nafuu
nesi akimhudumia samuel
nesi akipiga stori na samuel na nchini ni manesi wanaomhuduma huko mumbai upasuaji wa kurekebisha sura ya mtoto samuel nkya huko india umefanikiwa na kwa mujibu wa mzazi wake, emmanuel nkya, aliyeongozana naye huko ni kwamba hali yake inaendelea vyema na sura yake sasa inatazamika baada ya kuathirika vibaya sehemu za pua na mdomo.

wasamaria wema toka kile pembe walijitokeza kumsaidia samuel mara baada ya globu ya jamii kutangaza matatizo yake na kuomba msaada wa hali a mali. kamati maalumu ikaundwa chini ya mwenyekiti wake david sawe na pia mpiganaji athumani hamisi ambaye naye yuo matibabu sauzi kufuatia ajali ya gari mwezi uliopita. juhudi hizo pamoja na huruma ya wasamaria samuel alifanikiwa kupata pesa za kutosha kwenda india kwa matibabu katikati ya mwezi uliopita.
kwa niaba ya wadau wote, globu hii inampa hongera mtoto samuel kwa kufanikiwa katika matibabu yake huko mumbai, na pia inatoa ahsante kwa wasamaria wema na wadau waliofanikisha zoezi hili kwa michango yao ya hali na mali pamoja na sala.

fuatilia historia yote ya mtoto samuel kwa kubofya hapa






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Nashukuru kwa kutupatia taarifa za maendeleo ya mtoto Nkya. Namwombea matibabu mema.
    Mdau
    Faustine
    http://drfaustine.blogspot.com/

    ReplyDelete
  2. Ohh God, nimefurahi kuona huyu mtoto anaendelea vizuri,utapona mtoto mzuri usijali,Mungu akubariki na kukuponya!

    ReplyDelete
  3. tunamuombea na kumtakia kila la kheri na fanaka .mtoto huyu apate nafuu mapema,tunashukuru kwa kutupatia taarifa za mtoto vile anavyoendelea....amen

    ReplyDelete
  4. Mimi I really don't trust Indian doctors, they are fool of scams.

    ReplyDelete
  5. Get well soon Samuel and God bless you and your family.

    ReplyDelete
  6. I am so happy to see the young lad is getting... Michuzi tunashukuru kwa kila jambo na tukiona juhudi zinafanikiwa hivi ndio maana both Blog na(net)sio kutukanana na kuchambuana.
    Get well Samuel
    Londoner

    ReplyDelete
  7. Huyo nesi picha ya chini (kulia mwa anayeangalia picha),sijui atamsindikiza mgonjwa kuja Tanzania?Nitajaribu kumwekea mtego naweza kuruka naye,ana macho ya kulegea yanavutia.
    ANYWAY:Dogo Samuel nakuombea upone haraka urudi masomoni mapema,usijali porojo za humu kwenye blog.

    ReplyDelete
  8. mtowa maoni wa october 08, 2008 1:59

    nami nakuona wewe kuwa miongoni mwa wale wajifanyao wanajuwa ilhali hawana walijualo, ona sentensi yako na kujifanya unajuwa kuandika english kumbe ni mbumbumbu.

    ReplyDelete
  9. Kwanza nampa pole mtoto Samwel. Pili namshukuru mola kuwa ameweza hatimaye kufanyiwa upasuaji na umeenda salama. Namuombea kidonda cha upasuaji kipone haraka na azidi kupata nafuu

    Pia tunaishukuru blogu ya jamii kwa kuchangia ktika kumtafutia mtoto Samwel udhamini wa kwenda India kwa matibabu, na kwa kutupa maendeleo ya afya yake

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...