







wasamaria wema toka kile pembe walijitokeza kumsaidia samuel mara baada ya globu ya jamii kutangaza matatizo yake na kuomba msaada wa hali a mali. kamati maalumu ikaundwa chini ya mwenyekiti wake david sawe na pia mpiganaji athumani hamisi ambaye naye yuo matibabu sauzi kufuatia ajali ya gari mwezi uliopita. juhudi hizo pamoja na huruma ya wasamaria samuel alifanikiwa kupata pesa za kutosha kwenda india kwa matibabu katikati ya mwezi uliopita.
kwa niaba ya wadau wote, globu hii inampa hongera mtoto samuel kwa kufanikiwa katika matibabu yake huko mumbai, na pia inatoa ahsante kwa wasamaria wema na wadau waliofanikisha zoezi hili kwa michango yao ya hali na mali pamoja na sala.
Nashukuru kwa kutupatia taarifa za maendeleo ya mtoto Nkya. Namwombea matibabu mema.
ReplyDeleteMdau
Faustine
http://drfaustine.blogspot.com/
Ohh God, nimefurahi kuona huyu mtoto anaendelea vizuri,utapona mtoto mzuri usijali,Mungu akubariki na kukuponya!
ReplyDeletetunamuombea na kumtakia kila la kheri na fanaka .mtoto huyu apate nafuu mapema,tunashukuru kwa kutupatia taarifa za mtoto vile anavyoendelea....amen
ReplyDeleteMimi I really don't trust Indian doctors, they are fool of scams.
ReplyDeleteGet well soon Samuel and God bless you and your family.
ReplyDeleteI am so happy to see the young lad is getting... Michuzi tunashukuru kwa kila jambo na tukiona juhudi zinafanikiwa hivi ndio maana both Blog na(net)sio kutukanana na kuchambuana.
ReplyDeleteGet well Samuel
Londoner
Huyo nesi picha ya chini (kulia mwa anayeangalia picha),sijui atamsindikiza mgonjwa kuja Tanzania?Nitajaribu kumwekea mtego naweza kuruka naye,ana macho ya kulegea yanavutia.
ReplyDeleteANYWAY:Dogo Samuel nakuombea upone haraka urudi masomoni mapema,usijali porojo za humu kwenye blog.
mtowa maoni wa october 08, 2008 1:59
ReplyDeletenami nakuona wewe kuwa miongoni mwa wale wajifanyao wanajuwa ilhali hawana walijualo, ona sentensi yako na kujifanya unajuwa kuandika english kumbe ni mbumbumbu.
Kwanza nampa pole mtoto Samwel. Pili namshukuru mola kuwa ameweza hatimaye kufanyiwa upasuaji na umeenda salama. Namuombea kidonda cha upasuaji kipone haraka na azidi kupata nafuu
ReplyDeletePia tunaishukuru blogu ya jamii kwa kuchangia ktika kumtafutia mtoto Samwel udhamini wa kwenda India kwa matibabu, na kwa kutupa maendeleo ya afya yake