kaburi likifukuliwa
kaburini ilikozikwa maiti kimakosa
maiti ikiondolewa kaburini
maiti ikiingizwa mochuari


Picha na habari na
Mdau Hudson Kazonta
wa HabariLeo

WATU saba wanahojiwa na Polisi kuhusu mtafaruku ulioibuka baada ya tukio la wafanyakazi wa Manispaa ya Singida kupewa kimakosa na kwenda kuuzika mwili wa marehemu uliokuwa umehifadhiwa katika hospitali ya Singida kwa muda.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa Celina Kaluba alisema tayari Polisi inawahoji watu saba kuhusu tukio hilo na watakaobainika kuhusika kwa uzembe huo watafikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Katika tukio hilo lisilokuwa la kawaida, Manispaa ya Singida iliuzika mwili wa marehemu aliyejulikana kwa jina la Mwanahamisi Omari (39) mkazi wa kijiji cha Kinyagigi katika halmashauri ya wilaya ya Singida, ambaye alifariki Oktoba 16 katika hospitali ya Nkungi kwa matatizo ya uzazi.

Mwili wa Mwanahamisi ulipelekwa katika hospitali ya mkoa wa Singida kwa ajili ya kuhifadhiwa siku moja kabla ya kwenda kuzikwa siku inayofuata.

Akizungumzia suala hilo, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa, Dk. Aubrey Mushi, alisema hali hiyo imesababishwa na uzembe wa muuguzi wa zamu pamoja na wafanyakazi kutoka Manispaa wenye majukumu ya kuzika miili ya watu iliyokosa ndugu.

Alisema katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali hiyo kulikuwa na maiti moja ya mahabusu mwanaume aliyejulikana kwa jina la Mwamanela Makumbi (32) ambaye alifariki Oktoba 16 mwaka huu.
---------------------------------------------------
Manispaa ya Temeke nako....
Wakati huo huo, utata umezidi kugubika suala la kukataa maiti ya marehemu Bakari Omari (30), baada ya ndugu zake kuendelea kudai si ya ndugu yao, licha ya jana kutambua nguo za marehemu walizokuwa wamemvalisha walipompeleka kumhifadhi katika Hospitali ya Manispaa ya Temeke Dar es Salaam.
Omari alifariki dunia Ijumaa iliyopita na kuzikwa kimakosa katika makaburi ya Temeke Wailes na mwili wake ulifukuliwa kwa amri ya mahakama juzi.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya Manispaa hiyo zilidai kuwa jana kuliitishwa kikao cha Mkurugenzi wa Manispaa, Mkuu wa Wilaya, viongozi wa juu katika manispaa hiyo pamoja na ndugu wa marehemu hao wawili waliochanganya maiti hizo.
Maiti nyingine ni ya marehemu aliyetambuliwa kwa jina la Yusuf Anthony ambaye hata hivyo hakuwahi kuzikwa na maiti yake iko hospitalini Temeke.
Katika kikao cha jana, inadaiwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Abdallah Kihato alikitumia kujadiliana na ndugu wa Omari kuhusiana na alama ya ndugu yao pamoja na kuwaonyesha nguo.
Kihato inaelezwa kuwa aliwataka ndugu wa Omari kuchukua maiti iliyofukuliwa kuwa ni ya ndugu yao, jambo ambalo ndugu hao walikaidi na kumtaka kuwapa nafasi ili wafanye kikao cha familia.
kwa habari zaidi za mkasa huu nenda

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Hivi wizara ya afya wana matatizo gani, juzijuzi tumesikia ya Temeke hospital, haya na huyu tena halafu naona hao jamaa wengine wameshilia groves tu na kushika mwili bared hivi ni lini tutajua kanuni za afya. Inatia huruma sana. Hata kama ni mwili wa nduguyo kama yupo infected na wewe unaambukizya na mwishowe wote kufariki kama ilivyokuwa Ebola.

    ReplyDelete
  2. Why do we blame wizara ya afya? Kwani hao wenye ndugu hawawajui ndugu zao? au hawakuwaosha ndugu zao? mochuari hawalazimishi kwamba huyu ni ndugu yako nendeni nae tu. Haya ndio matatizo kwamba unampa mtu wa mochuari akuoshee mwili wa ndugu yenu amtengeneze kabisa nyie mkachukue tu then mnapa kidogodogo. JAMANI WE HAVE RIGHTS TO THROUGH BLAMES KWA WENGINE ONLY IF YOU HAVE PLAYED YOUR PART FULLY

    ReplyDelete
  3. Kugombea maiti kuna faida gani? Mtu akishakufa ameshakufa. Kazikwa na nani mimi sioni ni tatizo.

    ReplyDelete
  4. mchangiaji wa tatu ndugu nakuuliza wewe hivi hujawahi kufiliwa na jamaa wako wa karibu? kuzika ndugu yako au mzazi wako au jamaa wako wa karibu ni very personal issue. Ni kitendo cha mwisho katika uhai wako unachomfanyia jamaa yako na ni vigumu mno kumwachia mwengine afanye. pia kuna issue na dini na imani, muislamu azikwe kikristo au mkristo azikwe kiislamu, hivi wewe hutojali kabisa? yaani jamaa yako unamwendea kinyume na imani yake ya dini na unamzika kwa imani ambayo ameikaidi maisha yake yote? hivi utaweza kuishi maisha yako kwa raha ukijuwa kuwa mzazi wako amezikwa kwa taratibu za dini asiyoiamini

    ReplyDelete
  5. hii kesi ya temeke naona ni rahisi kutatua, kama kuna maiti wawili, urahisi ni kuchukuwa memba wa pande zote mbili kuwapeleka mochuari na kutambua maiti zao, labda huyo aliewahi kuzikwa itakuwa kidogo mwili umeshaharibika, lakini still wanaweza kutumia mwili wa yule alokuwa hakuzikwa bado kumtambua.

    ama ya singida kinachonishangaza ni kuwa kwani maiti haziwekwi alama? yaani kadi yenye jina la marehemu, jinsia, umri, tarehe ya kufariki nk? mbona mochuari zote duniani zinafunga vikadi namna hiyo kwenye vidole vya mguu wa marehemu? sasa kama hiyo ipo itakuwaje watu wa mochuari watoe mwili wa mwanamke ilhali wameambiwa kuwa alokuwa hana jamaa ni mwanamme?

    pia hili suali la jamaa, hivi mtu anapofariki manispaa huhifadhi maiti kwa muda gani kabla ya kuamua kuwa hana jamaa na kuuzika? mtu amefariki tarehe 16 oktoba na mara manispaa wanasema hana jamaa? siku chache jamani weee! jee kama wako nje ya singida na hawajapata habari bado? au kwa kuwa alikuwa mahabusu basi hana haki za kuzikwa na jamaa zake?

    ReplyDelete
  6. aisee!!!ni siku 14 if taarifa haijafika kbs mochuari,manispaa wanazika,,,afu ata mie nashangaa wht kind of hosp maiti haina alama??me nipo hospitalini cjawaelewa awa jamaa wa temeke

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...