mwanaharakati wa shughuli za jamii john mashaka siku alipotutembelea ofisi za daily news/habarileo septemba 15, 2008 alipokuwa likizo fupi nchini akitokea marekani anakoishi na kufanyia kazi.
hii ilikuwa ni baada ya kufanya naye intavyuu ya video kwenye tovuti ya magazeti hayo ambayo hadi sasa video hiyo imevunja rekodi kwa kutazamwa na watu wengi zaidi ya video zote tulizozitundika mtandao wa www.dailynews-tsn.com toka tuanze libeneke hilo julai mwaka huu.
jumla ya wasomaji 6,486 wameiangalia video hiyo ambapo wasomaji takriban 41 wameweka maoni yao juu ya john mashaka.
ukitaka kuhakikisha hilo bofya hapa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Mbona amevaa miwani ya jua?

    ReplyDelete
  2. wabono wanataka kujua ujinga wake..

    ReplyDelete
  3. MIMI SIZURU HIYO TOVUTI MAANA SASA HUYU TUNAONA ANATAFUTA MISIFA.

    USINIBANIE HII

    ReplyDelete
  4. Jamaa wa kuigwa wanakuonea wivu kweli. Pole sana mdogo wangu, uzuri ni kwamba kila kitu unachokifanya ni cha maana na jamii inakukubali

    Ila mdogo wangu, waosha vinywa kama walivyo watakupaka kweli

    ReplyDelete
  5. Huyu amaekuwa ndio OBAMA wa Tanzania. anawakilisha nchi yetu vizuri, ila watu kutaka kumjua siyo kitu cha ajabu, wewe unasema watu elefu sita au comments 41, nenda Bongo Celebrity utakoma. comments zaidi ya 141

    http://bongocelebrity.com/2008/04/02/kutoa-ni-moyosi-utajiri-john-mashaka/

    Sasa mashaka ukija Tanzania jaribu kuwa mwangalifu, wa kukupamba watakuwepo na wa kukutaka kukuangusha hasa mapaparazi

    ReplyDelete
  6. Jamani, Kaka yangu Michuzi, unanifahamu vizuri tu. mimi ni dada mzuri tu,tena mstaarabu, nafanya kazi zangu za modelling Afrika kusini na jamii inanifahamu vizuri tu, sina kashfa ya aina yoyote na bila kuficha au kuzunguka mbuyu, huyu kaka nimempenda.

    Shida ni kitu kimoja, umaarufu unakuja na matatizo yake. Umaarufu wangu umewafukuza vijana wote ambao wangeweza kunioa na hata wazazi wao wamenikataa. Kwa sasa hivi kila anayeni approach ni watu tu wa kunichezea.

    umaarufu unafunika kila kitu isipokuwa watu wa kukuchafulia jina

    Jamani mimi namtaka Joni Mashaka, najua hajaoa na hana mchumba, kwa hiyo naomba mnipe njia ya kuwasiliana naye. nimesikia habari zake kwa watu tofauti, ni kijana mstaarabu sana

    M O

    ReplyDelete
  7. Ndio kavaa miwani ya Jua, ulitaka avae miwani ya mvua? au boxi ndo imekuwangukia jicho la kushoto

    Naona ulichamba kizee vibaya leo umerudi na maasira

    Wabongo bwana !

    ReplyDelete
  8. Mbona dogo mnampandisha chati hata zaidi ya OBAMA? Haya bwana tumekuona

    Mashaka, njoo basi utuhutubie hapa Wichita Kansas. Tutafurahi sana ukija na ile hotuba yako ya mnazi mmoja. hizo hela zenu za Wall-Street zinakutosha kununua tiketi ya kuja hapa maramoja kuwanona wenzio,

    W-Kansas

    ReplyDelete
  9. Wewe Mashaka, ulifanyiwa kafara ya kondoo mweusi baada ya kuzaliwa na kabla ya kuja marekani nini? Mbona sisi mambo yetu siyo safi hivyo?

    Huyo kondoo anaye vitukuu vyake? hata ngozi yake itanifaa. Umri wako ni mdogo sana kufanya mambo makubwa kiasi hicho ndio maana wengi wanakuonea wivu

    Haya bwana. Kila la kheri na kazi nzuri. Kaa na moyo huo huo wa ukarimu na unyenyekevu

    Mamo yako safi

    ReplyDelete
  10. Zile articles ulizo copy na ku paste za kifedha ndo chanzo cha hawa wageni kuzuri hizi sites. Zile articles siyo za mtoto zile, uliona wenye machungu, yalikuwa ni articles babu kubwa ndo maana watu wanamtafuta jonie

    Michuzi, unachokifanya ni kumtumia huyu jamaa kuvutia watazamaji kwenye globu ya jamii.Sasa kama anaandika articles kama zile unadhani tutafurahi na kumwangalia hivi hivi. Kila mtu lazima atataka jujua yeye ni nani, kwa maana zile articles hata hawa waandishi wetu hawana ubavu wa kuzindika

    ReplyDelete
  11. Ndiyo ni kweli, Mithupu anatumia umaarufu wa huyu jamaa kuvutia wateja kwenye site yake. Mashaka amekuwa sumaku, toto yote ya mafisadi ughaibuni yanataka kujua kulikoni na bwana mashaka na ni hao ndio wanaoweka comments chafu. kwa maana mashaka kawazidi kete, ila inabidi hawe mwangalifu kwa maana watajidai marafiki na kuanza starehe zao za kukuporomosha

    ReplyDelete
  12. ww balozi wa zein ulitegemea nini, huyo si ni John Mashaka, lazima tu watu watatfatufa kwa maana amakuwa ni cheche na mkuna vichwa siyo tanzania tu, hata huko marekani jina lake limekuwa cheche. aliyekuzaa angezaa wengi jamani

    ReplyDelete
  13. Balozi wa Zeina

    Mimi nina ma sista watato (5) miaka 19-hadi 31 na wote bado wapo nyumbani, mara wanazuka na wachumba wa miezi mitatu kisha kazi kwisha.

    Balozi wetu, mimi naomba usaidizi kumuozesha hata mmoja kwa mtu wa maana, nadhani muda umefika waondoke nyumbani

    Ni dada warembo sana na tabia nzuri ila meni hakuna DAR ni wazushi tu. Yaani jamaa (mashaka)tutamuozesha hata bure, hakuna cha mahari wala cha nini. Bure jumla jumla chaguo ni lake ilmradi wadogo zangu hata mmoja apate mtu wa maana

    Peter Msemvu Dar

    ReplyDelete
  14. KAKA MICHUZI MIMI NAMSUPPORT HUYU JAMAA KWA KILA MALI NA NINATAKA KUJIUNGA NAE KUSAIDIA JAMII YETU NILIKUWA NATAFUTA WATU SERIOUS KAMA YEYE, NILIKUWA NAOMBA INFO ZAKE ILI NIWASILIANE NAE, ILI TUSAIDIANE. email yangu ni sexyeyez08@yahoo.com

    DC

    ReplyDelete
  15. We SEX YEYE hapo juu hujatulia kabisa unafikiri mashaka anatafuta habari za mambo ya sex hapa. Mwanaume anapiga mzigo wa ukweli na jamii iko desparate kupata watu kama hawa. Acha kutaka kumtoa jamaa out of track pls pls tena pls sana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...