Kaka Michuzi,
Niko likizo St Lucia, na huku nimekutana na huyu jama mwenye Rasta ambaye anaongea Kishwahili vizuri sana lakini ni raia wa St Lucia. Hivi saa anasema anamtafuta Rafiki yake aitwae Juma alie mfundisha kiswahili miaka ya 70 huko St. Lucia. Wadau Juma ni nani na uko wapi?
Mdau Ayoub mzee

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Muulize vizuri huyo rasta sije akawa wakwetu(homeboy)aliyezamia meli na kulowea huko visiwa vya St. lucia Caribbean.

    Maana hata hapa London tunakutana na dizaini hizo za rasta akisikia unaongea kiswahili ana kuja haraka na kukuuliza habari za bongo. Na ukimuliza anakwambia kwao ni Bombambili Songea ana alizamia Uingereza miaka ya 1970.

    Mwambie ajiunge na blogu hii atawapata washikaji wenzake wengi waliozamia sehemu mbalimbali ulimwenguni.

    ReplyDelete
  2. wewe mchangiaji wa mwanzo namna gani? hukusoma post vizuri? huyo jamaa kasema kuwa kafunzwa kiswahili na mtu aneitwa Juma, sasa wewe unasema kuwa huenda akawa ni mbongo kivyeje?

    ReplyDelete
  3. Huyo Rasta wa Songea anaitwa Ramadhani?

    ReplyDelete
  4. hahahaah kweli jamaa hajasoma vizuri rasta kafundishwa kiswahili huyo, angekuwa kazamia angesema ukweli yeye mswahili sio ila kama umeweka comment kama jokes basi ni funny ha-ha-ha mwengine hahaah anauliza kama huyo rasta anaitwa ramadhani watu wanatafutana na masela wao wa vijiwe zamaaaaani hahaha nendeni ugiriki na italy ndio mtakuta ma baharia wa miaka ya 70 kwakwakwa raha sana blog hii sio kila mtu ulaya kaja kwa ndege wengine meli jamani. ila kweli jamani hakuna usafiri wa MELi kutoka tanzania na je ni rahisi pesa meli mpaka ulaya au barani amerika tufahamishiane jamani wengine tunaogopa kupanda ndege plz mnipe jibu. from Kijiweni

    ReplyDelete
  5. Naona bora mukamuulize ndugu Mhando Jiwe au Peter Chain wa hapo Syria ,Damascus wanaweza kumtambua.

    ReplyDelete
  6. sasa wewe unasema amuulize muhando jiwe vipi wakati muhando jiwe yupo bongo na huyo mtu yupo st lucia?au una kisasi na hao watu wa damscus nini.fuatilia maelezo ya habari na picha sio kuropoka kaka....basi kama ni hivyo itabidi tuumulize afisa mku wa uhamiaji..na hao unaowafananisha na huyo jamaa sio marastaa ..naona mtoa maoni umechanganyikiwa....na kwa taarifa yako damascus hakuna watu kama hao uliowataja..umechemsha

    ReplyDelete
  7. wadau huyo mzee rasta katikati ni mwenyewe burning spear na kushoto mpiga gitaa wake junior mavin kwa hivi sasa hawana kitu tena wameamuwa kuwa wavuvi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...