Mheshimiwa Balozi,
Mbona unatunyanyapaa? tunaomba tuambie matokeo ya simba na Yanga huko nyumbani nani ametoka kidedea? Mnyama au Kandambili.
Tunashauku ya kujua uamuzi wa Simba kumtimua Kocha wao Mzungu na kumleta Mzirai yamezaa matunda au la.Tuambie mambo yakoje huko msimbazi/Jangwani leo.
Tafadhali usitubanie
Mdau Cardiff
---------------
mdau, asante kwa ujumbe. siwezi kuwabania na nitarusha matokeo mara baada ya gemu, ila sio laivu kwani niko vekesheni kidooooogo huku sauzi. ila usikonde wala nini. pia kumbuka kabla ya gemu la watani wa jadi kutakuwa na gemu la timu ya maalbino na wabunge. nitabandika matokeo pia.
-michuzi
jamaa unataka kujua matokeo kabla ya mpira kuanza?au game ya leo imepigwa asubuhi?anyways,hivi hakuna kituo chochote kinachurusha mtanange huo,na kipo je kinatoa huduma hata ktk mtandao?tulio nje ya nchi nasi tungejidai kwa kuona mpambano huo.i miss vituko kabla ya game ya watani wa jadi.hahaha
ReplyDeletehabri ndio Hiyo toka Magogoni..
ReplyDeleteOF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail : press@ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425
PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Tumeona ni vizuri kuwashirikisha katika tukio hili la kuwakabidhi viongozi wa chama cha Maalbino Tanzania jezi zilizotolewa na Mheshimiwa Rais.
Mtakumbuka tarehe 19 Oktoba, 2008 wakati Rais alipopokea maandamano ya kulaani mauaji ya maalbino, pamoja na mambo mengine aliahidi kutoa jezi na vifaa vingine vya michezo kwa timu ya maalbino itakayocheza mechi ya kirafiki na waheshimiwa wabunge leo tarehe 26 Oktoba, 2008 katika uwanja wa taifa.
Vyombo vya habari vimekuwa ni wadau na washiriki wakubwa katika kufichua vitendo vya ukatili na unyayapaa wanavyofanyiwa maalbino. Mheshimiwa Rais anazidi kuwapongeza kwa juhudi zenu katika kipigania haki za maalbino.
Rai yetu ni kwamba tunaomba kwa pamoja tuendeleze ujumbe kwamba maalbino ni binadamu kama walivyo binadamu wengine wanaopaswa kuheshimiwa na kupata haki zote na fursa ya kushiriki katika shughuli zote za kisiasa, kiuchumi na kijamii.
Hii ndiyo maana Mheshimiwa Rais ameamua kutoa jezi 33 na vifaa vinavyohusiana na michezo vyenye thamani ya Shilingi Milioni Mbili Laki Moja Arobaini na Tatu Elfu (Shs. 2,143,00/=) kwa maalibino ili kuwawezesha kushiriki kikamilifu mechi ya leo kati yao na waheshimiwa wabunge.
Ahsanteni sana.
Kisare Makori,
Kaimu Mkurugenzi,
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais – Ikulu,
DAR ES SALAAM.
26 Oktoba, 2008
na mkibamizwa leo darajani usitubanie, tunakujua zako mishuzi.
ReplyDeleteBwawa leo linaogelewa uchi.
Mh. Balozi na vacation zako hizo. usiseme vacation hizo ni mission za kikazi. Umeondoka na JK kwenye ziara zake nini. Najua unaweza kupata matokeo kila ukipata tupachikie maana wewe ni rahisi kuyapata. Vile vile wadau angalia blog hii. http://www.yangatz.blogspot.com/
ReplyDeletempka sasa tumepigwa 1-0 simba 0 yanga 1
ReplyDeleteYANGA 1 SIMBA 0 Kipindi cha kwanza
ReplyDeletesasa ni mapumziko na mnyama amenyofolewa mara moja katika dakika ya 15 ya kipindi cha kwanza
ReplyDeleteyanga 1 simba 0. Cheers Yanga
ReplyDeleteYanga moja Simba wanalia msimbazi. My God sijui itakuwaje na Mziray wao. Mbulgaria nadhani hana kazi tena. Nilikuwa na hofu na bilionea wa Yanga Manji sasa mambo poa
ReplyDeletematokeo ni YANGA 1 SIMBA 0.mfungaji ni yule yule boniface ambani dakika ya 16.
ReplyDeleteYAnga 1-0
ReplyDeleteoyaa michuziiii..mnyama kapigwa moja bila.
ReplyDeletegoli la yanga kafunga ben mwalala dak ya 16.
mdau ughaibuni..
Bao ni moja bila Yanga imeibuka na ushindi na mpira umekwisha.
ReplyDeleteMnyama kauwawa...ingawa mjengwa ..katoa matokeo kwa unyonge...
ReplyDeleteMechi kali kati ya watani wajadi, Simba na Yanga imekwisha na matokeo ni kwamba Simba imelimwa bao 1-0 lililofungwa na Ben Mwalala katika Dk. 16. Pambano hilo lililofanyika kwa mara ya kwanza kwenye uwanja mpya wa kisasa jijini Dar es salaa na lilitawaliwa na ubabe miongni mwa wachezaji, refa alilazimika kutoa jumla ya kadi nyekundu 3, mbili Simba, moja kwa Yanga
ReplyDeleteAs far as I know here in US
ReplyDeleteYanga 1 Simba 0
YANGA 1 - SIMBA 0. habari ndio iyo, mpo hapo....???
ReplyDeletemdau. cape town
MATOKEO YANGA1 SIMBA 0,NDIO HIVYO MWANANGU,NA PREMIER YA ENGLAND CHELSEA 0 LIVERPOOL 1,ALONSO 10 MIN,WEST HAM 0 ARSENAL 2 ADBAYOR,SASA YUONE MSEME LIVERPOOL MBELEKO?
ReplyDeleteOCD
Matokeo
ReplyDeleteYanga---1
Vs
Simba---0
Michuzi wewe ni Simba ndio maana kimya na maandishi yako ya Kisimba na Liverpool. Lakini tuemewafunga
ReplyDeletemdau wa cardiff, mnyama kalala leo kaka.....
ReplyDeletehabari nilizo nazo ni kuwa chama langu (Yanga) imemchapa mnyama goli 1-0. Goli lilifungwa na Mwalala dk 16. Haruna Moshi na Meshack Abel wa Simba, pamoja na Mwalala wa Yanga walionyeshwa kadi nyekundu
ReplyDeleteMNYAMA KANG'OKA KIBOLO HUKO. KAMA WALIVYOONDOKA CHELSEA STAMFORD BRIDGE KWA KIBOLO DHIDI YA LIVERPOOL, JAMAA NAO WAMENG'OKA LEO BAADA YA MIAKA MITANO YA UTEJA
ReplyDeleteMatokeo ni Bwawa la maini 1 buluuz mikono mithupu
ReplyDeleteYanga ilishinda goli 1 - 0 lilifungwa na Benard Mwalala dk. 15mwamuzi Victor Mwandike ambaye alilalamikiwa sana na Simba kabla ya mchezo aliwapa kadi mara kwa mara wachezaji wa simba na baadaye alitoa kadi nyekundu 3, mbili kwa simba na moja yanga. Hata hivyo pamoja na kufungwa simba walionyesha kiwango kikubwa zaidi ambapo yanga walianza kuchelewesha mpira kwa dakika zaidi ya 60 baada ya kupata goli.
ReplyDeleteDuuuh kweli Michu yupo vekesheni manake hata habari ya bwawa la maini hadi leo hii haja ibandika ila mimi binafsi sitaki habari ya bwawa la maini wala watani wa jadi mimi nataka kujua mechi ya ndugu zangu maalbino na wabunge imeishaje?
ReplyDeleteDuh! Hivi hakuna proofread ya barua za Ikulu? Maana inasikitisha kwa ofisi kubwa kama Ikulu iandike 2,143,00/= badala ya 2,143,000/= .
ReplyDeleteWabunge= 2
ReplyDeleteAlbino = nunge
Albino wameonyesha kiwango kikubwa sana cha mpira, hasa ukizingatia walifanya mazoezi kipindi kifupi katika kuunda timu yao.
Albino waliwazibiti wabunge vilivyo, WAO TU walishindwa kufunga magoli kwa tatizo la macho, kwani jamaa walikuwa hawaoni vizuri goli,jua lilikuwa kali, mchezo ulianza saa 9 mchana. Na hata magoli waliyofungwa kipa wao hakuweza kuuona mpira vizuri, vinginevyo wabunge ( wengi wao mawaziri) wangelia!!!
LIVE LONG ALBINO
BWAWA OYEEEEEEEEEEEEE LIBENEKE KAMA KAWA
Hahahahahahaaaaaaaaaaa! Wana wa bwawa la maini siwasikii au kwa vile mmeloa jasho. Shauri yenu.
ReplyDeleteDhuuuuuu!!!!!!!!! EHeheeeeeeeehe uko msimbazi kuna ndokoda inavuka maybe M/kiti hana kiti tena, Uuuuuuuu Mziray Jamboooooooo!
Leo ni moja bila. Mlie na hicho kimoja kitawatosha. Next time mje kwa adabu. Malizeni bifu lenu halafu ndio mje sawasawaaaaaa!
Mimtori naye anaomboleza sijui!
BWANA KISARE WA IKULU SASA UNATUCHANGANYA SISI TULISOMA KTK VYOMBO VYA HABARI IKIWAMO BLOG YETU TUKUFU KUWA MAALBINO WAMEPATIWA VIFAA VYA MICHEZO NA SAMSUNG SASA WEWE UNATUAMBIA KUWA AMETOA RAIS TUNAOMBA MSITUCHANGANYE. MDAU HOLLAND
ReplyDelete"Duh! Hivi hakuna proofread ya barua za Ikulu? Maana inasikitisha kwa ofisi kubwa kama Ikulu iandike 2,143,00/= badala ya 2,143,000/="
ReplyDeleteHii ni ndogo mbona? Unakumbuka ile JK alikabidhiwa mfano wa chewue lakini kile kilichokuwa kinasomeka ni tofauti na kile kilichotolea. Wamezoea kukurupuka hawaediti mambo yao wala kuangalia makosa ndio maana wanasaini mikataba baadaye inatuumiza. Wavivu wa kusoma hawa watu wanafikiria mambo yao. Mdau Holland .
Mdau Holland nimekubali maoni yako, hawa watu ni wavivu wa kusoma walichoandika.Ndio maana wanasaini mikataba fake ambayo inatuumiza walala hoi.
ReplyDeleteJamani tusaidieni kupata ukweli, hata mimi niliona kwenye TV kampuni ya SAMSUNG imetoa vifaa vya milioni kumi na sita (16M) kwa ajili ya mechi ya wabunge na ma-albino.Ikiwa ni gharama ya vifaa. sasa huu ni usanii wa Ikulu au nini? msaada wajameni
ReplyDeleteYEah walibamizwa 1-0 dk 16 baada ya one kazi safi ya Chuji, Ambani then Mwalala what a finish....But wachezaji bado hawana nidhamu (sijui hawaoni prof wenzao Duniani)washabiki hawana nidhamu(Tabia mbaya ndio jadi sijui)sasa wanarusha chupa za maji kwa pitch damn mtakuwa lini wastaarabu! Vibaka nao wamo basi tabu tupu but Yanga wazuri na move unaziona na wataendelea kutesa sana kama kweli wanataka kucheza mpira na kutoka wana uwezo huo.
ReplyDeleteLondoner (Cruisin' in Bongo)