Mheshimiwa Balozi,
Mbona unatunyanyapaa? tunaomba tuambie matokeo ya simba na Yanga huko nyumbani nani ametoka kidedea? Mnyama au Kandambili.
Tunashauku ya kujua uamuzi wa Simba kumtimua Kocha wao Mzungu na kumleta Mzirai yamezaa matunda au la.Tuambie mambo yakoje huko msimbazi/Jangwani leo.
Tafadhali usitubanie
Mdau Cardiff
---------------
mdau, asante kwa ujumbe. siwezi kuwabania na nitarusha matokeo mara baada ya gemu, ila sio laivu kwani niko vekesheni kidooooogo huku sauzi. ila usikonde wala nini. pia kumbuka kabla ya gemu la watani wa jadi kutakuwa na gemu la timu ya maalbino na wabunge. nitabandika matokeo pia.
-michuzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 34 mpaka sasa

  1. jamaa unataka kujua matokeo kabla ya mpira kuanza?au game ya leo imepigwa asubuhi?anyways,hivi hakuna kituo chochote kinachurusha mtanange huo,na kipo je kinatoa huduma hata ktk mtandao?tulio nje ya nchi nasi tungejidai kwa kuona mpambano huo.i miss vituko kabla ya game ya watani wa jadi.hahaha

    ReplyDelete
  2. habri ndio Hiyo toka Magogoni..
    OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
    UNITED REPUBLIC OF TANZANIA


    Telephone: 255-22-2114512, 2116898
    E-mail : press@ikulu.go.tz
    Fax: 255-22-2113425


    PRESIDENT’S OFFICE,
    THE STATE HOUSE,
    P.O. BOX 9120,
    DAR ES SALAAM.
    Tanzania.


    TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

    Tumeona ni vizuri kuwashirikisha katika tukio hili la kuwakabidhi viongozi wa chama cha Maalbino Tanzania jezi zilizotolewa na Mheshimiwa Rais.

    Mtakumbuka tarehe 19 Oktoba, 2008 wakati Rais alipopokea maandamano ya kulaani mauaji ya maalbino, pamoja na mambo mengine aliahidi kutoa jezi na vifaa vingine vya michezo kwa timu ya maalbino itakayocheza mechi ya kirafiki na waheshimiwa wabunge leo tarehe 26 Oktoba, 2008 katika uwanja wa taifa.

    Vyombo vya habari vimekuwa ni wadau na washiriki wakubwa katika kufichua vitendo vya ukatili na unyayapaa wanavyofanyiwa maalbino. Mheshimiwa Rais anazidi kuwapongeza kwa juhudi zenu katika kipigania haki za maalbino.

    Rai yetu ni kwamba tunaomba kwa pamoja tuendeleze ujumbe kwamba maalbino ni binadamu kama walivyo binadamu wengine wanaopaswa kuheshimiwa na kupata haki zote na fursa ya kushiriki katika shughuli zote za kisiasa, kiuchumi na kijamii.

    Hii ndiyo maana Mheshimiwa Rais ameamua kutoa jezi 33 na vifaa vinavyohusiana na michezo vyenye thamani ya Shilingi Milioni Mbili Laki Moja Arobaini na Tatu Elfu (Shs. 2,143,00/=) kwa maalibino ili kuwawezesha kushiriki kikamilifu mechi ya leo kati yao na waheshimiwa wabunge.

    Ahsanteni sana.

    Kisare Makori,
    Kaimu Mkurugenzi,
    Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais – Ikulu,
    DAR ES SALAAM.

    26 Oktoba, 2008

    ReplyDelete
  3. na mkibamizwa leo darajani usitubanie, tunakujua zako mishuzi.
    Bwawa leo linaogelewa uchi.

    ReplyDelete
  4. Mh. Balozi na vacation zako hizo. usiseme vacation hizo ni mission za kikazi. Umeondoka na JK kwenye ziara zake nini. Najua unaweza kupata matokeo kila ukipata tupachikie maana wewe ni rahisi kuyapata. Vile vile wadau angalia blog hii. http://www.yangatz.blogspot.com/

    ReplyDelete
  5. mpka sasa tumepigwa 1-0 simba 0 yanga 1

    ReplyDelete
  6. YANGA 1 SIMBA 0 Kipindi cha kwanza

    ReplyDelete
  7. sasa ni mapumziko na mnyama amenyofolewa mara moja katika dakika ya 15 ya kipindi cha kwanza

    ReplyDelete
  8. yanga 1 simba 0. Cheers Yanga

    ReplyDelete
  9. Yanga moja Simba wanalia msimbazi. My God sijui itakuwaje na Mziray wao. Mbulgaria nadhani hana kazi tena. Nilikuwa na hofu na bilionea wa Yanga Manji sasa mambo poa

    ReplyDelete
  10. matokeo ni YANGA 1 SIMBA 0.mfungaji ni yule yule boniface ambani dakika ya 16.

    ReplyDelete
  11. YAnga 1-0

    ReplyDelete
  12. oyaa michuziiii..mnyama kapigwa moja bila.

    goli la yanga kafunga ben mwalala dak ya 16.
    mdau ughaibuni..

    ReplyDelete
  13. Bao ni moja bila Yanga imeibuka na ushindi na mpira umekwisha.

    ReplyDelete
  14. Mnyama kauwawa...ingawa mjengwa ..katoa matokeo kwa unyonge...

    ReplyDelete
  15. Mechi kali kati ya watani wajadi, Simba na Yanga imekwisha na matokeo ni kwamba Simba imelimwa bao 1-0 lililofungwa na Ben Mwalala katika Dk. 16. Pambano hilo lililofanyika kwa mara ya kwanza kwenye uwanja mpya wa kisasa jijini Dar es salaa na lilitawaliwa na ubabe miongni mwa wachezaji, refa alilazimika kutoa jumla ya kadi nyekundu 3, mbili Simba, moja kwa Yanga

    ReplyDelete
  16. As far as I know here in US
    Yanga 1 Simba 0

    ReplyDelete
  17. YANGA 1 - SIMBA 0. habari ndio iyo, mpo hapo....???

    mdau. cape town

    ReplyDelete
  18. MATOKEO YANGA1 SIMBA 0,NDIO HIVYO MWANANGU,NA PREMIER YA ENGLAND CHELSEA 0 LIVERPOOL 1,ALONSO 10 MIN,WEST HAM 0 ARSENAL 2 ADBAYOR,SASA YUONE MSEME LIVERPOOL MBELEKO?

    OCD

    ReplyDelete
  19. Matokeo

    Yanga---1
    Vs
    Simba---0

    ReplyDelete
  20. Michuzi wewe ni Simba ndio maana kimya na maandishi yako ya Kisimba na Liverpool. Lakini tuemewafunga

    ReplyDelete
  21. mdau wa cardiff, mnyama kalala leo kaka.....

    ReplyDelete
  22. habari nilizo nazo ni kuwa chama langu (Yanga) imemchapa mnyama goli 1-0. Goli lilifungwa na Mwalala dk 16. Haruna Moshi na Meshack Abel wa Simba, pamoja na Mwalala wa Yanga walionyeshwa kadi nyekundu

    ReplyDelete
  23. MNYAMA KANG'OKA KIBOLO HUKO. KAMA WALIVYOONDOKA CHELSEA STAMFORD BRIDGE KWA KIBOLO DHIDI YA LIVERPOOL, JAMAA NAO WAMENG'OKA LEO BAADA YA MIAKA MITANO YA UTEJA

    ReplyDelete
  24. Matokeo ni Bwawa la maini 1 buluuz mikono mithupu

    ReplyDelete
  25. Yanga ilishinda goli 1 - 0 lilifungwa na Benard Mwalala dk. 15mwamuzi Victor Mwandike ambaye alilalamikiwa sana na Simba kabla ya mchezo aliwapa kadi mara kwa mara wachezaji wa simba na baadaye alitoa kadi nyekundu 3, mbili kwa simba na moja yanga. Hata hivyo pamoja na kufungwa simba walionyesha kiwango kikubwa zaidi ambapo yanga walianza kuchelewesha mpira kwa dakika zaidi ya 60 baada ya kupata goli.

    ReplyDelete
  26. Duuuh kweli Michu yupo vekesheni manake hata habari ya bwawa la maini hadi leo hii haja ibandika ila mimi binafsi sitaki habari ya bwawa la maini wala watani wa jadi mimi nataka kujua mechi ya ndugu zangu maalbino na wabunge imeishaje?

    ReplyDelete
  27. Duh! Hivi hakuna proofread ya barua za Ikulu? Maana inasikitisha kwa ofisi kubwa kama Ikulu iandike 2,143,00/= badala ya 2,143,000/= .

    ReplyDelete
  28. Wabunge= 2
    Albino = nunge

    Albino wameonyesha kiwango kikubwa sana cha mpira, hasa ukizingatia walifanya mazoezi kipindi kifupi katika kuunda timu yao.
    Albino waliwazibiti wabunge vilivyo, WAO TU walishindwa kufunga magoli kwa tatizo la macho, kwani jamaa walikuwa hawaoni vizuri goli,jua lilikuwa kali, mchezo ulianza saa 9 mchana. Na hata magoli waliyofungwa kipa wao hakuweza kuuona mpira vizuri, vinginevyo wabunge ( wengi wao mawaziri) wangelia!!!
    LIVE LONG ALBINO
    BWAWA OYEEEEEEEEEEEEE LIBENEKE KAMA KAWA

    ReplyDelete
  29. Hahahahahahaaaaaaaaaaa! Wana wa bwawa la maini siwasikii au kwa vile mmeloa jasho. Shauri yenu.

    Dhuuuuuu!!!!!!!!! EHeheeeeeeeehe uko msimbazi kuna ndokoda inavuka maybe M/kiti hana kiti tena, Uuuuuuuu Mziray Jamboooooooo!

    Leo ni moja bila. Mlie na hicho kimoja kitawatosha. Next time mje kwa adabu. Malizeni bifu lenu halafu ndio mje sawasawaaaaaa!

    Mimtori naye anaomboleza sijui!

    ReplyDelete
  30. BWANA KISARE WA IKULU SASA UNATUCHANGANYA SISI TULISOMA KTK VYOMBO VYA HABARI IKIWAMO BLOG YETU TUKUFU KUWA MAALBINO WAMEPATIWA VIFAA VYA MICHEZO NA SAMSUNG SASA WEWE UNATUAMBIA KUWA AMETOA RAIS TUNAOMBA MSITUCHANGANYE. MDAU HOLLAND

    ReplyDelete
  31. "Duh! Hivi hakuna proofread ya barua za Ikulu? Maana inasikitisha kwa ofisi kubwa kama Ikulu iandike 2,143,00/= badala ya 2,143,000/="

    Hii ni ndogo mbona? Unakumbuka ile JK alikabidhiwa mfano wa chewue lakini kile kilichokuwa kinasomeka ni tofauti na kile kilichotolea. Wamezoea kukurupuka hawaediti mambo yao wala kuangalia makosa ndio maana wanasaini mikataba baadaye inatuumiza. Wavivu wa kusoma hawa watu wanafikiria mambo yao. Mdau Holland .

    ReplyDelete
  32. Mdau Holland nimekubali maoni yako, hawa watu ni wavivu wa kusoma walichoandika.Ndio maana wanasaini mikataba fake ambayo inatuumiza walala hoi.

    ReplyDelete
  33. Jamani tusaidieni kupata ukweli, hata mimi niliona kwenye TV kampuni ya SAMSUNG imetoa vifaa vya milioni kumi na sita (16M) kwa ajili ya mechi ya wabunge na ma-albino.Ikiwa ni gharama ya vifaa. sasa huu ni usanii wa Ikulu au nini? msaada wajameni

    ReplyDelete
  34. YEah walibamizwa 1-0 dk 16 baada ya one kazi safi ya Chuji, Ambani then Mwalala what a finish....But wachezaji bado hawana nidhamu (sijui hawaoni prof wenzao Duniani)washabiki hawana nidhamu(Tabia mbaya ndio jadi sijui)sasa wanarusha chupa za maji kwa pitch damn mtakuwa lini wastaarabu! Vibaka nao wamo basi tabu tupu but Yanga wazuri na move unaziona na wataendelea kutesa sana kama kweli wanataka kucheza mpira na kutoka wana uwezo huo.

    Londoner (Cruisin' in Bongo)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...