migogoro katika vilabu vyetu vya yanga na simba haikuanza leo wala jana. hii ni katika miaka ya 80 ambapo baadhi ya viongozi wa yanga walimkorofisha mwenyekiti wao enzi hizo mzee mangar tabu mangara lakini wachezaji wakawa bado na imani nae. hapa wanaandamana toka kilabuni mtaa wa mafia kuelekea mtaa wa swahili nyumbani kwa mzee mangara kuonesha kumuunga kwao mkono

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Ingekuwa wiki mbili zilizopita ningelaumu Swaumu.Tangu lini Yanga ikawa mafia na swahili streets?Hao watakuwa watoto wapotevu Pan africa siyo Yanga,michuzi.Uwe unaangalia unachokiandika kabla ya kukipandisha bloguni.

    ReplyDelete
  2. Kaka Michu!!

    Lakini umiona tofauti yake? Hakuna Polisi wala mgambo mambo yote yalikuwa shwari hapo unawaona akina Sembuli (Marehemu) na wadau wa Yanga!!! Lete snepu lolote la hivi karibuni kwenye kilabu chochote cha mpira hivi sasa utaona VIRUNGU vimetanda mtindo mmoja (dRU)

    ReplyDelete
  3. Huko Kushoto kabisa wa pili aliyevaa suruali ya miraba miraba ni marehemu Gibson Sembuli kwa hiyo hii ina maana kuwa sio 'miaka ya 80' kama ulivyosema bali ni kabla ya mwaka 1978 ambao nadhani ndio alifariki Sembuli. Nadhani huo ni ule mgogoro maarufu wa mwaka 1975/76 uliozaa 'Kandambili' na 'Raizon' kwenye klabu ya Yanga, mgogoro ambao uliishia kwa kuzaliwa timu ya Pan Africa.

    ReplyDelete
  4. We mdau wa kwanza ndio unatakiwa usome vizuri kabla ujatoa comment.hajakwambia kwamba club ya yanga hiko mtaa wa mafia na swahili,amekwambia wanaandamana kutoka mtaa wa mafia kuelekea mtaa wa swahili kwa mzee mangara kuonesha wanamuunga mkono.

    ReplyDelete
  5. HAWA WATU TUNAO WAONA HAPO SASA NI WATU WAZIMA YAANI WAZEE NA HESHIMA ZAO, KWELI SIKU HAZIGANDI KATUSEMEA LADY JD BALOZI WA NANIHIII, THAT TIME I WAS AROUND 19 OR 20 YEARS OLD.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...