


Na washindi ni kama wafuatao:
1. Panama
2.Philippines
3. Columbia4
. Tanzania
5. Greece
Mashindano ya Vazi la Taifa ya Miss Earth 2008 yalifanyika jana usiku (tarehe 28 Oktoba 2008) katika ukumbi wa PAGCOR jijini Paranque, nchini Ufilipino.
Warembo 85 walishiriki katika mashindano haya na Miss Panama alishinda tuzo kuu la Vazi bora la Taifa.
Miss Philippines alishinda tuzo la Miss Photogenic na tuzo mbalimbali maalum zilitolewa na wadhamini katika mashindano haya.
Miss Greece alipata tuzo 2 maalum - Miss Micu Confidence and Joel Cruz Signature Award,.
Miss Aficionado ilinyakuliwa na mrembo wa Tanzania - Miriam Odemba, ambapo Miss Venezuela alishinda tuzo la Face of Placentana tuzo la Face of the Night lilikwenda kwa Miss Colombia.
Vazi la Miriam Odemba lilibuniwa na mbunifu mahiri na mzoefu wa Zanzibar Farouque Abdela na limetayarishwa kwa kutumia mifuko ya plastiki na kunakshiwa na mikufu ya kimasai.
Fainali ya Miss Earth yatafanyika tarehe 9 Novemba 2008.
Odemba atabanana nao hata kama age imeenda.
ReplyDeleteAge doesnt matter anyway coz if it did she wasnt gonna be there at first. Good Job Odemba nice to see ya doing what you like to do.
ReplyDeleteNi waTanzania gani waliulizwa na kulipitisha hilo kuwa ndio Vazi Rasmi la Taifa?
ReplyDeleteMsijifanyie fanyie mambo kienyeji enyeji tu hapa!
Kiona mbali,
ReplyDelete1) Vazi la taifa la tanzania halipo, sasa ulitaka miriam asivae vazi lolote kwa kutokuwepo hilo vazi, au angoje kamati kuu na bunge ipitishe vazi la taifa ndio aende kwenye hilo shindano?
2) Siasa ya kwamba vazi limepitishwa, je hao washindani wengine wote mavazi yao yamepitishwa nanchi zao?
Conclusion, acha kuwa na fikra za kutokuwa na maendeleo, miriam na designer wa vazi lako hongereni sana, msiwasikilize watu kama kiona karibu anayejiita kiiona mbali!
Kwani mmeambiwa ni vazi la Taifa gani? mimi ngoja niulize kwanza, hilo vazi ni vazi la Taifa gani?
ReplyDeleteivi odemba alishinda lini Tz yan mashindano yaliendeshwa wapi adi akawa Miss Utalii Tz kuwakilisha "Taifa"
ReplyDeletevazi la Taifa ofkoz ni chochote utachojisikia kuvaa asa nchi ikiwa haina "vazi la Taifa",,teh teh tehee raha sana Tz
adi tujewafikia India na vazi zao?ipo kazi
Kweli waswahili tunapenda kuchonga! Lakini yooote yanaonyesha tunashindwa kuona kitu cha maana. Hili vazi la taifa la ubunifu au siyo? Naona hapo kuna nakshi ya kimasai n.k.
ReplyDeletePia mashindano haya ya Miss Earth si yale alioenda Richa mwaka juzi? Basi si geni!
Nilisoma ktk tovuti kwamba Miriam aliteuliwa kuwakilisha Bongo hakukuwa na mashindano yoyote. Lakini hilo haliondoi ukweli kwamba odemba kafanya vizuri! Au we annyonymus hapo juu ulitaka pia kushiriki?
Hongera sana Odemba unaiwakilisha vyema Tanzania, sisi tunaoishi ughaibuni tutakuja kukupongeza huko ufilipino!
Hongera dada kwa mafanikio, lakini next time usikubali kuvaa nguo za plastic inaonyesha haujali mazingira dada. Next time coton 100% sawa dada.
ReplyDeletekwakweli TZ inapepea bendera kisawa sawa kwenye mashindano makubwa ,Tanzania inajulikana sikuizi
ReplyDeleteongera zao wote wanaopepea bendera ingawa viongozi wa nchi dont give a damn kabisa mtaona kama atapokelewa kwa shangwe na viongozi wa hiyo bendera,washabiki tuuuuuu ndo watajitokeza.
Odemba, siku hizi unajichomokea tu. Mi nafikiri ungeachana na biashara hii urudi nyumbani UOLEWE. Utazeekea kwenye hayo mashindano dada yangu.
ReplyDeleteanonymous wa 9:45 unachekesha eti odemba aachane na biashara hii aolewe we kuolewa umeona deal kwa kati ya hela na mume umeona bure mume huyo odemba ana uzee gani akimbilie ndoa tena za waswahili wanaofumaniwa guest cku moja baada ya harusi.fanya vitu vyako odemaba we luv u so kip ur head up koz uko juu
ReplyDelete