Bwana Issa,
Pole kwa kazi na mahangaiko ya kutupasha yanayotokea hapa na pale duniani. Nimesoma leo katika gazeti la jana la nipashe kuhusu tamko la SMZ juu ya utata wa Zanzibar kuwa ni nchi au si nchi.
Wadau wengi wanaguswa, hasa Watanzania, na hususan Wazanzibari wanaguswa na kukereketwa na mjadala huu. Wengi tumoezowea kusikia na kusoma yatokayo kwa viongozi wa serekali zetu mbili ila hatusikii yasemwayo au kusoma yaandikwayo na upande upinzani.
Leo nimesoma hii makala iliyoandikwa na kijana wa Kizanzibari ambae anaonekana kuwa na uchungu wa hiyo (nchi/si nchi) Zanzibar.
Sina uhakika wa msimamo wake kisiasa kuwa ni mpinzani au la, ila anachokisema kinapingana na kauli za SMZ na SMT na kusomesha wengi juu ya kadhia hii.
Najua kwa nafasi yako inaweza kuwa vigumu kulibandika somo hili, ila ningekuomba tafadhali sana ulibandike ili wadau wapate kuelewa kilichopo upande wa pili wa sarafu. Makala inpatikana katika blogspoti ya huyu mwandishi
---------------------------
mdau asante kwa kundeleza libeneke. ila ningependa nikukosoe kidoooogo pale ulipotia shaka kwamba huenda kwa nafasi yangu nisingeweza kubandika libeneke hili.
mie bwana ukiona nimebania maoni ujue kulikuwa na uchafuzi wa hali ya hewa kama si kujeruhi roho ya mtu. mambo hayo kama hakuna mie hubandika chochote kinachohusu jamii. ndo maana ya hii kuwa globu ya jamii na si ya michuzi tena.
hivyo nakutoa shaka mdau wewe na wengine kwamba leteni mambozzz mradi hali ya hewa haichafuki ama mdau mwingine hajeruhiwi roho.
-michuzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 26 mpaka sasa

  1. Mheshimiwa Balozi, mimi sasa naanza kupata picha kwanini Wazanzibar wanaishikilia hii ajenda ya Zanzibar nchi au si Nchi. Nimeanza kugundua kuwa tatizo sio utaifa wa Wazanzibar isipokuwa hawa jamaa wanajaribu kutukumbusha ile hadithi ya Sungura na Fisi kwamba kuna cha wageni na cha wote.Au kwa maneno mengine wanataka kusema "chako changu na changu changu".Niliposoma hii habari kwenye hii blog ya huyo mhishimiwa, hata kabla sijafika mbali nikagundua kuwa kumbe ugomvi hapa ni suala la Mafuta.Huyu bwana anasema "Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar waliiambia wazi Serikali ya Jamhuri ya Muungano kwamba Wazanzibari hawako tayari kuona kuwa mafuta yao yanachimbwa na kugawanywa na Tanganyika. Ulikuwa msimamo wa dhati na madhubuti."Nafikiri kwa mtazamo wangu hapa ndio kuna tatizo.Lakini hawa wazanzibari wanasahau fadhira ya Punda.Hivi ni kwa muda gani hawa watu wamekuwa wakitumia umeme wetu bure bila kulipa hata senti tano na sisi hatukuwa tukisema chochote.Badala yake tukawa tunabeba mzigo wa kulipa bili zao!!Nafikiri Njeru Kasaka nawenzake walikuwa sahii kabisa kutaka kuundwa Serikali Tatu.Waswahili walisema tenda wema nenda zako usingoje shukurani.Imefika wakati sasa kwa Serikali yetu kuweka mambo wazi, watu majadili faida na hasara za huu Muungano.Kama faida ni chache kuliko hasara,basi nafikiri ni bora uangaliwe upya.Vinginevyo huko tunakoenda naona siko kwenyewe.Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania

    ReplyDelete
  2. Nimesoma mjadala mzima wa bwana Mohamed lakini sijaona nini amependekeza kifanyike kuhusu Muafaka au nini anataka kuhusu Muungano wa Tanganyika na zanzibar.

    Labda angeelezea nini anaona mapungufu yake na nini kifanyike ili malumbano ambayo yaneendelea yafikie Muafaka bila matatizo yoyote

    Kenge

    ReplyDelete
  3. http://swahilitime.blogspot.com/2008/08/muungano-maoni-ya-adamu-lusekelo.html

    ReplyDelete
  4. Wadau mimi naomba mnisaidie kujua muimbaji na jina la wimbo huu wa zamani: "Zanzibar oh Zanzibar, beautiful island of Africa." Nitashukuru.

    ReplyDelete
  5. alieimba huo wimbo ni abdalla issa na kikundi cha dumbak taraab,

    ReplyDelete
  6. mchangiaji wa mwanzo naomba uniambie ni mwaka gani ambapo zanzibar walipewa umeme kutoka bara bila ya kulipa hata senti tano? au ndio ropoka ropoka ya mitaani tu?

    Pili sio kweli kama issue nzima ni mafuta, lakini kama unataka kuzungumza suali la mafuta basi kwanza uliza kama zanzibar inapata nini katika masoko ya tanzanite, katani na bidhaa nyengine ambazo tanzania bara huuza nje ya nchi? ukishapata jawabu labda utaona ni kwa nini zanzibar haitaki kugawana mafuta na tanzania bara.

    Suali la zanzibar ni nchi au sio nchi ni hilo hilo kama linavyosema. point kidogo tu na za haraka ni kama hivi
    1 kama zanzibar sio nchi hii serikali ya jamhuri wa muungano, ni muungano gani huo?
    2. kama zanzibar sio nchi kwa nini wana wimbo wa taifa? kuna jimbo gani jengine tanzania lenye wimbo wa taifa, raisi, serikali, bunge, timu ya taifa, mwanasheria mkuu wao wenyewe.
    3. kama zanzibar ni mkoa wa tanznaia kwa nini viwango vya mishahara vya wafanyakaizi wa serikali zanzibar na wale wa tanzania bara ni tafauti sana?
    4. kama zanzibar sio nchi kwa nini mambo mengi yanayopitishwa tanzania bara huwa hayaihusu zanzibar ila pale baraza la wawakili linapopitisha uamuzi wake? mfano mzuri ambao mara nyingi umeshatolewa ni pale raisi wa tanzania anapopandisha mishahara ya wafanyakazi wa serikalini, wazanzibari mishahara yao haipandi?

    Labda pia ujiulize kwa nini ulipofanyika muungano nyerere na karume walikubaliana kuwepo kwa serikali ya zanzibar lakini kutokuwepo kwa serikali ya tanganyika? ukipata jibu labda utaona ni kwa nini wazanzibari bado wanasisitiza kuwa zanzibar ni nchi.

    Point moja tu ya kukusaidia kwa suali langu la mwisho ni kuwa wazanzibari wanaipenda na wako so proud kujiita wazanzibari, bila kujali kama nchi yetu ni tajiri au masikini, tunaweza kujiendesha wenyewe au hatuwezi, hayo hatuyajali, la muhimu zanzibar ni kwetu, zanzibar ni visiwa vyetu, zanzibar ni nchi yetu na hatukuwa tayari wakati wa muungano na hatuko tayari baada ya muungano kupoteza identity yetu. sio kama watanganyika ambao wamekubali kupoteza identity yao, hamujiiti watanganyika kabisa, infact kuna ambao ukiwaita watanganyika wanahisi kama unawatukana.

    Nakukumbusha jambo la mwisho kwa upande wetu sisi kwanza ni wazanzibari halafu ndio watanzania. utanzania tunaweza kuuvua (ni kama koti tu) lakini uzanzibari ni daima.

    ukipenda usipende huu ndio ukweli

    ReplyDelete
  7. wee jamaa uliandika hapo mwanzo jaribu kufanya utafiti unapotaka kusema usiwe unaropokwa tu.Nani aliekwambia kama zanzibar imekuwa ikitumia umeme wenu bure!!!! kwa taarifa yako miundo mbinu ya kufikisha umeme znz yote imetengenezwa na inaendeshwa na znz wenyewe na vile vile shirika la umeme znz linananunua umeme kama mteja wa kawaida kwa TANESCO.We unaishi dunia gani hata unashindwa kufuatilia mambo na kuyaelewa vizuri then kujifanya msemaji mzuri??????

    ReplyDelete
  8. Ndugu Michuzi,

    Nategemea unakula vekesheni yako kwa raha na starehe zote.

    Mimi ni mmoja wa wadau hapa na napinga usemi wako kuwa unachapicha maoni ya watu wote isipokuwa ya wale wanaochafua hali ya hewa au kutukana.

    Mara nyingi nilikuwa napenda kuandika maoni hapa lakini mara kwa mara uliyabana. Mara nyingi ni maoni yanayohusu siasa, Nyerere, uchumi wa Tanzania na CCM.

    Mimi sina tabia ya kumtukana mtu, yule anayetukana basi hawezi au hajasomeshwa shuleni ku debate na mwenzake au hajalelewa vizuri na wazazi wake.

    Tumeshazoea kutoa maoni huku nchi za nje bila ya kupelekwa kortini kwa " kukashifu kiongozi au Raisi".

    Una haki yote ya kuchapisha au kutochapicha maoni ya jamii kama mwenye blog hii, lakini wadau wengi hapa watakubaliana nami kuwa pia una tabia ya kuchambua maoni na yale ambayo huyapendi binafsi huyachapishi kwa sababu unayoijua mwenyewe.

    Ningependa uchapishe maoni yangu juu ya hili swala ili wadau wengine waweze kuwa na nafasi ya kuniunga mkono au kunipinga kauli yangu kuwa maoni mengi ya wadau unabana hata hama "hawachafui hali ya hewa au kutukana jamii".

    Natanguliza shukurani.

    Aluta Kontinua.

    ReplyDelete
  9. Mheshimiwa balozi naomba uniruhusu kwa mara ya mwanzo kabisa kuleta comments zangu katika blog yako hii.

    kilichonifanya niandike ni kumjibu huyo mwandishi wa mwanzo na kebehi zake za kuwa eti wazanzibari tumeshau fadhila (sio fadhira, kiswahili gani hiki).

    Kwanza nataka kujua ni wapi alipoona au kuambiwa kuwa zanzibar tumetumia umeme bila kulipa hata senti tano? kama tuna deni hapo ni kweli, deni limekuwa kubwa hapo kweli lakini hatukulipa kitu huo ni uzushi.

    Ama kusahau fadhila, nadhani watanzania bara ndio walioshau fadhila, wamesahu kuwa ndugu zetu chungu mzima walipoteza maisha yao katika vita ambavyo havikutuhusu abadani; ndugu zetu wa damu walivuka bahari kuja kupigana bega kwa bega na ndugu zenu kumngowa idi amini.

    Labda hamjaambiwa au hamkosoma mahali lakini kabla ya vita hivyo uchumi wa zanzibar ulikuwa wa hali ya juu, lakini vita vilipooanza nguvu zote zilielekezwa katika kufanikisha ushindi, wakati hali ngumu ikitupiga tulichoambiwa na nyerere ni kuwa tukaze mikanda!

    Labda emesahau kuwa ndugu zetu walioweza kurudi hai hawakupata chochote kutoka serikali ya muungano zaidi ya "hatuna cha kuwapa, cha kuwapa ni ahsante"

    labda hujui hili ila kwa vile mfumo wa mishahara ya tanzania bara na visiwani ni tafauti, ndugu zetu waliporudi vitani walijikuta hawakulipwa mishahara yao wakati wakiwepo vitani, walipojaribu kudai na kuandamana wote walifukuzwa kazi.

    Labda hujui hili, ila ndugu zetu waliporudi vitani hawakupewa counselling yeyote ile. walibahatika kubaki jeshini hadi leo ukiwaona unajuwa kabisa kama hawako sawa sawa kiakili! hadi hii leo wale waliofukuzwa jeshini wako kama wendawazimu wanapita wakisema peke yao, familia zao zimevunjika kwa sababu ya behaviour zao, walibahatika kubaki jeshini hadi leo ukiwaona unajuwa kabisa kama hawako sawa sawa kiakili! hizo ndio fadhila za serikali ya muungano na nchi ya tanganyika kwa wazanzibari.

    ReplyDelete
  10. Hili suala la "uzanzibari" na "uzanzibara" ni gumu sana, na muafaka wake wenda ukachukua miongo kama mbinu zitakuwa hizi hizi. Kwa nini tulumbane?

    Nasikitika kuwa sijamsikia kiongozi wa SMZ, Mh. Karume,akinena waziwazi juu ya hili kama Rais Kikwete alivyofanya. Mh. Karume nae azungumze, sote tumsikie, tujue nini msimamo wa wakuu hawa na hivyo kutoa picha na dira kamili.

    Yote 9, 10 ni kwamba kama alivyowahi kusema Mh. Mudhihir (Mb) wakati akichangi hoja bungeni, dawa ya Muungano huu lazima iwe "chungu" ili ifanye kazi vema. Tuwe kitu kimoja kamili i.e Zanzibar iwe kama mikoa mingine ya bara (kwa visiwani). Bendera, Rais (Kiongozi wa SMZ), kikosi na vingine vinavyoitenga Zanzibar vifutwe! Nchi iwe moja, Tanzania, chini ya Rais mmoja, period!

    Jamani, wenda kuna ajenda ya Siri upande wa Visiwani. Iwekwe bayana, tujadili na kufikia muafaka. NAKUSIHI MH. AMAN ABEID KARUME, KIONGOZI WA SMZ, NENA NAWE USIKIKE JUU YA HILI JAMBO. BARA HATUELEWI WENZETU WANAELEKEA WAPI NA WANATAKA NINI. Tatizo ni nini? Naamini sio mafuta tu! Kuna jambo, na wenda linafahamika na upande mmoja zaidi kuliko mwingine.

    Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.

    ReplyDelete
  11. mi nahisi huyo anayesema kuwa zanzibar inatumia umeme bure naona kanfurutu ada, tena yuaja nguoni. uwazi wa hili halitaki hata mtu asome gazetini au kitabuni. kama ni mtu mwenye common sense basi angejiuliza kabla ya kuandika "yawaje wananchi masikini na wafanya biashara wa njugu na tungule walipie bili za umeme na zanzibar kama nchi isilipe"? au angejiuliza "hiyo tanganyika yao ina utajiri kiasi gani wa kuweza kuipa zanzibar umeme bure"? sijui hata alikuwa wapi mtu huyu miaka michache iliyopita ambapo zanzibar ilikatiwa umeme kwa kuwa na deni kubwa? Mimi kama Mzanzibari namshukuru sana bwana Pinda kwa tamko lake la kuwa Zanzibar si nchi, Namshukuru pia Nahoda na Kificho kwa kulitia nguvu hilo. nahisi hii imekuwa ni chachu kwa wazanzibari kutetea nchi yao pendwa. natamani na watanganyika na wao wangekuwa na uzalendo kama wetu kudai Tanganyika yao.
    by scandinavian.

    ReplyDelete
  12. Michuzi, kwanza kabisa nikupongeze kwa kukubali kuiweka hii mada kwenye blogu ya jamii kwa kuwa ni wazi kuwa u-muoga au mbanifu wa maoni-chokozi. Kwa sisi wa taaluma za kinanihi tunasema libeneke la nonviolence conflicts linakupa usumbufu na pengine kwako ni uchafuzi wa hali ya hewa! Sio kosa lako, natambua! Ni mtindo wa kazini 'kwetu.' Hahahaha

    Kaka, nianze kwa kusema tu kwamba nalichukia jina Tanganyika hadi kwenye rbc zangu! Kama ndugu zetu wazanzibara watajitenga, naomba sisi tubaki na jina letu TANZANIA. We don't need be called Tanganyikans.

    Wabara, sisemi kuwa tushabikie kujitenga, la hasha, bali nasisitiza kama wenzetu watajitenga, sisi tubaki na jina letu Tanzania. Itaondoka "Jamhuri ya Muungano wa..."

    Kwenu wazanzibara. Mkiisha kujitenga, mkawa wazanzibara kamili, kama mlivyoanza na issue ya vitambulisho, tafadhali, msiishie hapo, bali endeleeni zaidi hadi kwenye upemba na uunguja. Natambua mtafika, tena mapema tu!

    Sote tukumbuke thamani ya amani ni kubwa sana. Lakini tutambue kokote duniani hakuna Muungano usio na vijikasoro vya hapa na pale. Watu hutafuta namna ya kuziba ufa, na sio kuuendeleza! Dhambi hii itawatafuna, naapa!

    Ni kwa nini mambo haya yatokee muda huu? Kuna ajenda gani iliyofichika? Najua tuna uongozi wa mtu mwenye hekima visiwani, Mh.Karume. Tunaomba muongozo wake juu ya jambo hili kwani hatuelewi msimamo wake. Chini ya uongozi wake thabiti kwa sasa tuna issue ya vitambulisho vinavyowabagua wabara!

    Kwa nini mambo haya yanazua utata wakati huu? Issue sio mafuta ndugu zangu. Kuna ajenda iliyofichika. Ajenda chini ya uvuli wa mafuta, madini, umeme, BOT, n.k ambayo nionavyo mimi inatambulika zaidi na wazanzibari.

    Wakati Serikali ya Jamhuri ya Muungano inawaza namna ya kuwafikia wote kwa vitambulisho vya uraia, SMZ inawaza namna ya kuwatenga wabara kwa vitambulisho vya uzanzibari.

    Mh. RAIS KIKWETE, Mh. RAIS WA SMZ, WADAU, WAHESHIMIWA WOTE, WANANCHI WAPENDA AMANI, MABIBI NA MABWANA. Ombi langu kubwa ni kuwa tuwe na mjadala wa pamoja na mjadala huu ili unoge, na uwe na mantiki, WAHESHIMIWA MARAIS TOKA PANDE ZOTE MBILI ZA MUUNGANO WAJITOKEZE HADHARANI WANENE KWA PAMOJA ILI TUWASIKIE WOTE WANASEMA NINI. TUJUE KAMA KUNA MWENYE KIGUGUMIZI. TUJUE KAMA KUNA ANAOGOPA KUSEMA WAZIWAZI.

    Kisha mjadala huu uchangiwe na wananchi toka pande zote mbili na kisha majumuisho yatolewe kwa mujibu wa kanuni na busara zitawale. Itakuwa ni njia halali, inayokubalika kimataifa na kitaifa na hata mbinguni, na njia ambayo haina gharama kama hizi zinazotumika kwa sasa, huku zikiacha malumbano kedekede yakiendelea.

    Wanasiasa wa vyama vyote wapewe fursa, nao watoe mchango wao tuwasikie. Watanzania sio wajinga, ni watu wanaojua kusoma mambo ya nyakati. Kwa hili tunasema kama kuna ajenda ya siri, iwekwe mezani.

    Mungu ibariki Tanzania. Na zilaze roho za marehemu Nyerere na Karume pema peponi. Amina.

    ReplyDelete
  13. anonymous wa October 27, 2008 6:22 PM ningelipenda kukuuliza ni kwa nini hulipendi jina la tanganyika? ume prove point ya ndugu yetu hapo juu aliposema kuwa wazanzibari (sio wazanzibara) tunajivunia uzanzibari wetu wakati watanganyika hamna majivuno hayo na kuna ambao hata wanaona kam unawatukana unapowaita watanganyika. utakataaje kuitwa mtanganyika ilhali jina la nchi yenu nitanganyika?

    Pia niambie ni kwa mantiki gani unataka mubaki na jina tanzania kama muungano ukivunjika? wewe ulienda skuli (shule)? hukufunzwa vipi jina tanzania limepatikana? labda nikupe somo la haraka TANganyika ZANzibar
    kwa hiyo TAN ZAN na ia ni kutoka pande zote za majina mawili.

    Mwisho mimi nataka kujua kwa nini kinawauma na kinawasumbuwa sana watanganyika juu ya kuvunja muungano? kuna wanaosema kutatokea machafuko visiwani, kuna wanaosema hatotoweza kujiendesha wenyewe n.k. suali ni inawahusu nini nyinyi? hii ni nchi yetu tuwachilieni wenyewe, kama tukibaguwana sawa hayajawahusu nyinyi. kusema kweli hizo zote sio sababu za kweli.

    mkitaka ukweli someni historia ya siasa ya ulimwenguni ilivyokuwa miaka ya 1964 wakati wa east and west blocks hapo ndio mtajua ni kwa nini nyerere alihimiza kuunda muungano.

    ReplyDelete
  14. anonymous wa October 27, 2008 6:22 PM hivi wewe umdogo sana hivi? unadhani suali hili la muungano na zanzibar kuwa ni nchi au sio nchi limeanza hivi leo? hebu uliza uambiwe ni sababu gani zilizosababishwa aboud jumbe avuliwe urais zanzibar? uilza uelimishwe ni namna gani seif sharif na wenzake walimuendea kinyume aboud jumbe wakati wa majadiliano na nyerere na kundi lake ilahali walipondoka zanzibar walikubaliana kuwa na msimamo mmoja juu ya suali zima la muungano? uliza kuelimishwe ni namna gani seif sharif baada ya kuahidiwa madaraka akamgeukia aboud jumbe, lakini mola si athumani na yeye yakamfika yalomfika mbele ya nyerere? hivi hujawahi kusikia ule msemo ulioibuka baada ya jumbe kuachishwa urais "moja na moja ni tatu"?

    sisemi mengine isije nikazuiliwa maoni yangu haya kutokea ukumbini

    ReplyDelete
  15. zanzibar sio nchi hilo ujuwe na tuko tayari kuitetea nchi yetu TANZANIA kama baba zetu walivyofanya walivofanya juu ya nduli na wajinga wajinga wengine cha fua ALAFU UONE tutakuja kukomboa KAMA ULIVIVYO KOMBOLEWA ANJUAN NA DAMU ZETU ZITAONEKANA SIKU YA USHINDI JADILI JINSI YA KUWAKOMBOA WATU KATIKA UMASIKINI NA SIO UTAIFA USIKUWA NA VICHWA WALA MIGUU HATA MWANZA AU ARUSHA WATU WATATAKA KUWA................ USIWE NA KUJIVUNIA NA UMASIKINI KAMA MJINGA MMOJA ANAJIDAI MZANZIBARA KUMBE MPUMBAVU TUU HUKU ULAYA WATU WANAFANYA KAZI KAMA HAWANA AKILI MPAKA WA BIBI WE UNACHEZA BAO TU KUTWA MAENDELEO YATAKUJA? NA KUJADILI KUBOMOA TUUUUUUUUU KUNGEKUWA NA PASIPOTI YENU........MUHIMU SUKUMIZA GURUDUMU LA MAENDELEO LIENDE MBELE SIO UNALETA UBAGUZI USIO NA MPANGO

    ReplyDelete
  16. Lazima tukubali kuwa utatuzi wa suala hili ni au kuwa na serikali tatu au moja. Kila utatuzi una faida na hasara zake, serikali tatu inaweza kuwa muafaka zaidi kwa pande zote ila gharama zake ni kubwa sana na hatuwezi kuzimudu pia dunia na wahisani wanaotupa misaada hawawezi kutuelewa, serikali moja ndio inastahili hasa upande wa gharama ila itasababisha zanzibar kufutika na kuwa mkoa. Inabidi tukubali kukabiliana na machungu yote na kufanya uamuzi, serikali mbili ni usanii na kila mtu anajua hili.

    ReplyDelete
  17. anonymous wa october 28, 2008 1:39 am umeprove point zetu. Kinawaumeni nini kama tunacheza bao, tunakula kashata na kahawa, tu masikini, wavivu, sawa yote hayo lakini je yanawahusu nini? pilipili usiyoila......

    wewe unaesema kuwa unafanya kazi huko ulaya kama huna akili, umeijenga vipi tanganyika yako? hivi kwa hali ilivyo tanganyika ni kusema kweli kuna maendeleo kweli? Kwa namna unavyojisifia mnavyofanya kazi, basi ujue kufanya kazi kama punda bila maarifa hakuleti maendeleo yeyote, lakini endeleeni hivyo hivyo.

    Kama kweli unajivunia nchi yako kwa nini wote hamtaki kiutwa watanganyika?

    na pia umeonyesha ni namna gani hujui hata historia ya nchi yako. Kwanza tanganyika hamkukombowa mmepewa uhuru, zanzibar tumepinduwa, hatukupewa uhuru wa karatasi mkononi. baba zenu wametetea nini?

    Umeonyesha pia kuwepo kuwa ulaya sio kustaarabika wala kuelimika. kuita wenzio wajinga sio ustaarabu wa kwetu, kwa hivyo mimi nitakujibu kwa kukumbusha tu umnosheapo mtu kidole kimoja vinne wajinyoshea mwenyewe.

    Eti unasema "zanzibar sio nchi na tuko tayari kuitetea.." nasi tunakwambia zanzibar ilikuwa nchi kabla ya muungano, ni wakati wote wa muungano na itabaki kuwa nchi baada ya muungano, sisi hatuna haja ya kutetea kwani tunajua na haibadili lolote kwa lolote lile mtakalosema"

    ReplyDelete
  18. Jambo ambalo linanishangaza ni hawa wenzetu wa bara, kila wakati wanasema wazanzibari wana kelele na tunawasaidia. kama mnatuona tuna kelele natunamipa hasara kwanini hamuamui moja tu, mkatuacha na umasikini wetu tukala mashelisheli na dagaa, na nyie mkala ma-tanzanite yenu.

    Zanzibar masikini sio masikini lakini tunajivunia uzanzibari wetu, kama nyinyi hamjivunii utanganyika wenu hio haituhusu.

    Zanzibar daima.

    ReplyDelete
  19. mimi napenda sana msemo ule unaosema usibishane na mpumbavu!!

    kama kunamtu anaishi kwa kutumia utaifa mwacheni abwabwaje akichoka atalala

    nchi zenyewe zakubishania na kukausha makoo ziko wapi??

    au ndiyo marelia zimewapanda??

    au mnataka pawe kama somalia kazaneni nawatakia kila la kheri na unzanzibar wenu.

    ReplyDelete
  20. Watanzania wenzangu mabibi na mabwana mimi najivunia kuwa Mtanganyika na natokea Tanga.Na siafiki hata kkidogo Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwani unakasoro kubwa sana hasa kwenye mgao wa fedha.

    Haiwezekani mikoa mingine izalishe sana na kupata mapato makubwa na mapata hayo yagawanywe kwa mikoa mingine ambayo haizalishi au uzalishaji wake ni mdogo.

    Nafahamu watu wengi hawapendi kuitwa watanganyika lakini tukumbuke utanganyika ni nchi ambayo iliitwa hivyo na Wakoloni na sio wananchi wenyewe na jina hiko linaweza kubadilishwa kama Ivory Cost walivyobadilisha jina na kuitwa Burkina Faso au Burma kuitwa Mynmaa, kwahiyo hapo sioni kama kuna issue yoyote ambayo inatatiza tunaweza kujiita watanzania bila Zanzibar pia hiyo ni sawa ni jina tu na wala hakuna maana yoyote hata wazanzibar ukiwauliza nini maana ya zanzibar hawatakuambia lolote kwa sababu kuna Unguja na Pemba.

    Issue hapa kama wao wanataka kujitenga wajitenge hakuna lolote ambalo mimi naliona baya wao kujitenga ila na Serikali ya bara nayo ihakikishe hata wao wanapokuja Bara wawe na vitambulisho na wachekiwe kama wengine wote. Jamaan tuweni straight forward let them do what they want and let us do they way we want.

    There should be one rule for both party.

    How many Zanzibar builds house in Tanzania and no body say a words to them but Its difficult for Mainlands residence to builds house in Zanzibar, what kind of republic is this?

    Come one let them go, we will move forward without them mates.

    Peace forever.

    Kenge

    ReplyDelete
  21. anaonymous wa october 28 2008 8:26 pm hii li kwako

    wazanzibari tunajua maana ya neno zanzibar na tunajuwa lina asili ya wapi.

    Issue ya kujitenga nadhani hapo ungeliwauliza wanasiasa wa tanganyika, kwani wao ndio wanaoshikilia kuwepo kwamuungano huu.

    Kama ulivosema ni kuwa mta move forward bila ya zanzibar, kwa nini viongozi wenu hawaoni hili na kwa nini wanashikilia kuwepo muungano? huoni kama kuna jambo ambalo limewekwa siri na hawakuambieni?

    kuhusu mikoa kuzalisha na mapato kugawanywa kwa mikoa mengine ambayo haizalishi, i hope humaanishi zanzibar. zanzibar hainufaiki na mapato ya mikoa ya tanganyika na ndio maana hatutaki kugawana mapato ya mafuta. i hope unajua issue nzima ya kutoanza kwa mradi huu. so kama unawaambia watanganyika wenzio hapo sawa, la unatulenga sisi naamini vidole vinne vinakuelekea mwenyewe.

    Unajua unanifurahisha sana na kwa kiasi naona kama unakubaliana nasi, huko nyuma ilikuwa kusafiri baia ya zanzbar na tanganyika ni lazima uwe na passport. kwa upande wetu ilikuwa anaeingia au kutoka ni lazima aonyeshe passport, lakini ni upande wa tanganyika ambaaoko walikuwa hawaangalii. sio zamani sana mfumo huu ukaondoshwa, lakini kama hiyo odea mnaitaka watangayika, sisi wazanzibari hatuna tatizo nalo kabisa!

    Unajua masuali yako yote naona uwaulize viongozi wako wa tanganyika, maana wao ndio wanaoruhusu yatokee yanayotokea kama hayo ya wazanibari kujenga nyumba tanganyika kirahisi kabisa.

    ReplyDelete
  22. anonymous wa october 28 2008 8:01 pm yes umesema sawa hatutobishana nawe mpumbavu. ungelikuwa sio mpumbavu usingeliandika ulichoandika baada ya sentensi yako ya mwanzo.

    ReplyDelete
  23. siasa kweli ni mbaya sana....wanasiasa wanalumbana kwa kukubaliana kula kwa pamoja wakati wananchi wao wanalumbana kwa kutukanana..hatari sana......
    hao viongozi wote wa tanaganyika na zanzibar lengo lao ni mlo tu hakuna jengine...na ndo mana at the end of the day wako kitu kimoja...japo kua ni dhahir kua zanzibar inamezwa na tanganyika...hilo kwa mtu mwenye akili timam analiona...haihitaji uwe umesoma saaana.
    any way saababu za zanzibar kutaka kujitenga na muungano ni kua wanaona hauna faida kwao...hiyo ni kiufupi kabisa..
    ungekua na faida wangeulilia uwepo.
    sasa weye unaesema kua wazanzibar wavivu au masikini....hemu jaribu kutoa points zinazoonyesha kua wako wrong na badala yake waupende muungano...au ndo kama hivo waunganishwe kwa lazima tuu...
    lkn tu jueni kua kila kitu kina mwisho wake....huwezi kuwaambia kua watu waungane milele...kuna siku itabidi tuu waunganuke ikiwa muungano wenyewe ni wa kisanii...

    ReplyDelete
  24. WEWE ANONYMOUS WA OCTOBER 29 1;10pm

    Hujatueleza nini maana ya Zanzibar na kama unajua maana yake weka wazi na sio unasema sisi wazanzibar tunajua maana yake kuwa Mkweli.

    Kuna jamaa anabisha kwamba hakuna mapato ya Tanzania bara ambayo yanaendeleza Zanzibar ni mpumbavu sana na hajui Historia nzima ya Muungano.Zanizbar inatumia mapato mengine ambayo yanatoka Tanzania Bara hilo halina ubishi na anajaribu kulaumu viongozi wa Tanzania bara ndio wanashikilia kama Viongozi wa Zanzibar wanataka kujitenga sio lazima wawasikilize wa Tanzania bara wajitenge tu na kuna njia nyingi ambazo wanaweza kufanya ili waweze kujitenge kama ilivyojitenga Kosovo.

    Wanaweza kufikisha swala zima Umoja wa mataifa na kueleza sababu zao za kutaka kujitenga na hapo watasikilizwa lakini nadhani viongozi wao wanatamaa wanataka mali za tanzania bara ziwe zao na zao pia ziwe zao na huu ndio upuuzi wa viongozi wa Zanzibar.

    Kama kweli wanataka kujitenga ni kuzungumza wazi na sio kuwa kimya nakusema pembeni.Sijawahi kumsikia Karume au Kiongozi wowote wa Zanzibar ambaye anasema wao wanataka kujitenga na kujitegemea kwa kila kitu, wanachotaka ni kuwa na Muungano lakini wapewe uhuru zaidi na ndio maana swala zima linakuwa gumu kuamuliwa.

    Mimi nadhani wakisema hatutaki Muungano wa aina yoyote na tunataka kuwa huru sidhani kama Viongozi wa Bara watakata ila wao ni wajanjawajanja hawasemi wazi nini wanataka na ndio maana swala zima linakuwa gumu.Kwa sababu wanataka muungano na muda huohuo wanataka nchi yao iwe inajitegemea.Ndugu yangu kwenye maisha huwezi kupata vyote ni wajitoe kabisa kwenye Muungano na wawe Nchi huru au kama hawataki basi wabaki kama walivyo na sio kusema viongozi wa bara wanawalazimisha kwani wao sio watoto kuna njia nyingi za kujitoa kwenye Muungano bila ya kuwashirikisha viongozi wa bara.

    Kuna mashirika ya kimataifa mengi ambayo wanaweza kulalamika na kujitoa kwenyeMuungano bila hata viongozi wa bara kuingilia kati.

    Swala la kujiuliza je wamefaya hivyo au nini wanataka?
    Ni upuuzi kulaumu viongozi wa bara wakati walipoingia kwenye Muungano hakuna ambaye aliwashikia Bunduki na kuwalizimisha wajiunge kwenye muungano na hivyo hivyo wakitaka kujitoa hakuna atakae washikia bunduki wasijitoe.

    Nadhani swala zima lipo kwa viongozi wa Zanzibar ambao wanataka Muungano lakini wanataka vyao viwe vyao na vyetu viwe vyao.

    Kenge

    ReplyDelete
  25. we kenge hao viongozi wa zanzibar nao ni miyayusho tu...wao si ndo hao hao wanaoburuzwa na ccm..tatizo la wazanzibar ni kua hii ccm tayari imeshawabomoa hawajitambui kabisa...viongozi wa zbar hawana sauti kabisa mbele ya viongozi wa tanganyika na hili lilikuwepo tangu zamani ila ndo kama unavosema kenge wanaogopa either kufukuzwa vyeo au consequences nyengine kuwakuta ndo mana wanaona bora waseme chini chini tu..lakini amini usiamini zbar hakuna mtu hata mmoja anaependa sura ya muungano uliopo hivi sasa...isipokuwa tu hao viongozi wa zbar ndo wanazuga zuga wasionekane na ccm wenzao wanapinga sera za chama...na kwa taarifa yako kenge toa data hizo unazosema kua zbar inatumia mali za tanganyika sio unaropokwa tu...
    asili ya neno zanzibar ni...zenj-baar
    neno la kiarabu lenye maana ya ardhi ya watu weusi.
    umesikia kenge??????
    sasa na weye toa hizo data zinoonesha kua zanzibar inatumia mali za tanganyika!
    usiropokwe kenge!tatizo lipo ila usitake kulikuza kiasi hicho....hao wanaoshughulikia muungano hivi sasa ni ccm.....na ccm kwa ccm ni walafi tu...hemu subiri zbar kupatikane na viongozi waliohuru na bad influences za ccm uone kama siku moja tu kero za muungano hazijatatuliwa!
    then usikie kama kuna mtu atapiga kelele tena..
    mimi ninae kaa zbar nataka nikitaka kwenda kuomba visa ya usa niombee hapa hapa tu zbar isiwe na haja ya kuja huko tanganyika...japo kuwe na kijiofisi kidogo tu lkn uongozi ulokuwepo saivi unapuuzia hilo!
    nikitoka safari zangu za kimataifa kusiwe na lazima nitue dar...na hili linawezekana isipokuwa viongozi waliopo sasa hawalipi kipaumbele
    tatizo la kero za muungano kutotatuliwa ni kua viongozi walokuwepo wote ni ccm na kunakua na kuogopana ndani ya ccm na mkubwa (tanganyika)kumpa amri mdogo(zbar)
    kimsingi hamna haja ya kuvunja muungano....tatua kero halafu uone kama kutakua na kelele.....kama haiwezekani basi kuna siku tu muungano utakua na mwisho kwa sababu hakuna muungano wa upande mmoja kuburuzwa daima!

    ReplyDelete
  26. Nilitaka kumjibu huyu jamaa anaejiita kenge na aloniita mimi mpumbavu, lakini ustaarabu na hulka za kikwetu zanzibar zimenizuia nisijiweke same level naye, besides mtu mwenyewe ameshajiita kenge kuna la zaidi la mimi kusema juu yake?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...