Mradi wa umeme uliopo kijiji cha Salasala uliojengwa chini ya mradi wa uendelezaji wa gesi ya asili ya Songosongo. Miradi mingine waliyoijenga ni maji, barabara na simu
Waziri wa Nishati na Madini Mh. William Ngeleja akimsikiliza Abdallah Mbonela Mwenyekiti wa kijiji cha Salasala wakati wa sherehe fupi ya kukabidhi miundombinu ya maji, barabara, umeme na simu katika maeneo ya Salasala na Kinyerezi iliyojengwa chini ya mradi wa uendelezaji wa gesi ya asili ya Songosongo. Hafla hiyo ilifanyika leo maeneo ya Salasala nje kidogo ya jiji la Dar

Waziri wa Nishati na Madini Mh. William Ngeleja akijibu maswali ya waandishi wa habari wakati hafla fupi ya kukabidhi miundombinu ya maji, barabara, umeme na simu katika maeneo ya Salasala na Kinyerezi iliyojengwa chini ya mradi wa uendelezaji wa gesi ya asili ya Songosongo. Halfa hiyo ilifanyika leo maeneo ya Salasala nje kidogo ya jiji la Dar

Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja akimkabidhi Ismail Mafita Mhandisi wa barabara wilaya ya Kinondoni hati ya miundombinu ya barabara za Kisalasala ili waweze kuzitunza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi miundombinu ya maji, barabara, umeme na simu katika maeneo ya Salasala na Kinyerezi iliyojengwa chini ya mradi wa uendelezaji wa gesi ya asili ya Songosongo. Wilaya hiyo imejengewa barabara tano za lami zenye urefu wa kilomita sita na nusu Hafla hiyo ilifanyika leo maeneo ya Salasala nje kidogo ya jiji la Dar. Picha zote na mdau Anna nkinda wa Maelezo




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Mradi gani huo unaokabidhiwa ukiwa mbovu? Unakabidhi nini wakati ni siku ya 3 leo salasala hakuna umeme!!!! giza tupu!!!!

    ReplyDelete
  2. poleni.............

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...