BWANA MICHUZI NI MIMI MZEE WA BUNJU TENA
LEO NAPENDA TUJIPIME SISI WADAU WA BLOG HII YETU PENDWA.
TUTAJIPIMA HIVI, KAMA ULISHAWAHI POKEA RUSHWA NA KAMA ULISHA WAHI TOA RUSHWA ILI IWE RAHISI KUJIPIMA KWA KAULI ZETU SISI WENYEWE ILI KWAMBA TUNAPOLALAMIKA KUHUSU TATIZO LA RUSHWA TUNAMAANISHA BAI UZOEFU AU KWA SABABU HATUNA NAFASI YA KUPOKEA???
1. SASA KAMA ULISHA WAHI TOA SEMA MIMI……… NAJUTA NILISHA WAHI TOA AU KUPOKEA EE MOLA NISAMEHE
2. AU USEME HIVI EE MOLA WANGU NASHUKURU MIMI SI MLA RUSHWA AU MTOA RUSHWA
NI HAYO TU. NA WEWE KAKA MICHUZI UKINIBANIA UJUE NAWEWE ULISHA WAHI KUNANIHII ………….
MZEE WA BUNJU

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Haha!! haaaaa!!!
    Kaka mimi nilishawahi kutoa rushwa Polisi (Buguruni) ili mdogo wangu apewe dhamana. Nakumbuka siku hiyo , askari aliyenidai rushwa (Tshs10,000)alitaka isipungue kwa sababu wanagawana na mkuu wa kituo.Hayo yalitokea februari,2005. Kuanzia siku hiyo, niliwadharau sana polisi pamoja na kazi yao kwani naona hawawezi kuishi bila rushwa. Siwezi kutubu kwa mungu ila namshukuru kwamba baada ya kutoa shs 6,000/=, mdogo wangu alipata dhamana. Naomba nami niulize: HIVI KUDAI RUSWA NI KWA SABABU YA KIPATO DUNI AU NI TABIA YA WATU KUTAKA PESA KWA AJILI YA ANASA BILA KUTOKA JASHO? Najua watu wengi wanaodai rushwa matumizi yao ni mabaya na mara nyingi wanakuwa wahanga wa MAGONJWA SUGU.

    ReplyDelete
  2. MIMI NAKUBALI KUWA MTOA RUSHA NA MPOKEAJI WOTE WANA MAKOSA.LAKINI WAKATI MWENGINE MTOAJI ANAWEZA KUWA NI "VICTIM" WA MAZINGIRA.

    KUNA WAKATI INAKUWA HAKUNA NJIA NYENGINE KUTOKANA NA "SYSTEM" INAVYOFANYAKAZI KAMA BONGO. SI LAZIMA UAMBIWE TOA RUSHWA LAKINI FAILI LAKO LITAKUWA "HALIONEKANI" KWA MIEZI HADI MIAKA, MPAKA UTAKAPOKOMA KUWA MKAIDI NA KUTOA HIYO KITU.
    UNAWEZA KUOMBA PASPOTI AMBAYO UNAIHITAJI KWA HARAKA KWA SAFARI YA NJE NA KILA UKIENDA KUSIKILIZA UKAAMBIWA BOSI ANAYEHUSIKA HAJALIPITIA FAILI MPAKA IKAFIKA SIKU AMBAYO UNATAKIWA URIPOTI CHUONI,BADO UNADUNDISHWA.UNAWEZA KULETA GARI YAKO BANDARINI UKADAIWA USHURU MARA TATU ZAIDI YA THAMANI YA GARI LENYEWE NA ITAOZEA BANDARINI IKIWA HUKUKOMA UBISHI. HUNA PA KWENDA, NI SYSTEM, KUANZIA JUU MPAKA CHINI WANAJUANA.
    KWANI KATIKA HILI SAKATA LA RICHMOND SI WATU WA TUME YA KUZUIA RUSHWA WALISEMA KUWA HAKUNA LO LOTE BAYA LILILOFABYWA LICHA YA KUTUMIKA KAMPUNI FEKI KUIIBIA SERIKALI NA UMMA WA TZ MABILIONI YA PESA ? NA MWANASHERIA MKUU ALISHAURI KUWA NI MRADI SAFI TU?NA SAKATA LA RADA? SASA UTAKIMBILIA WAPI UKIWA UNA HAJA NA HUTAKI KUTOA HIYO KITU.

    ReplyDelete
  3. Mimi binafsi nikihudumiwa vizuri serikalini huwa napenda kutoa ASANTE au TIP....sasa sijui hii ndo rushwa yenyewe. Ila ningependa saana kufahamu tofauti iliyopo kati ya RUSHWA na TAKRIMA.

    ReplyDelete
  4. Mzee wa Bunju asante sana kwa kuleta mada nzuri katika ukumbi. Haya ndio mazungumzo ya kujenga. Hata hivyo, inabidi kwanza tukubaliane tunaposema "rushwa" tuna maana gani? Kwa mfano, Yusuf Makamba ana maana yake tofauti na Wilbrod Slaa. Tunachokiita 'ufisadi' Makamba anasema ni 'rushwa'. Je, nasi tunaposema 'rushwa' tunajumuisha na 'ufisadi'? Hapa ninamaanisha je tunatumia 'rushwa' kwa maana ya CCM au kwa maana ya wananchi. Kabla hatujaendelea na mjadala inabidi kwanza tukubaliane juu ya dhana tunayomaanisha tunaposema 'rushwa'.

    ReplyDelete
  5. Kwa maoni yangu (si imani – i stand corrected; si utafiti hivyo msinihukumu!) : ni muhimu kutofautisha rushwa na ufisadi. Ninaitazama rushwa kama vitendo anuwai vinavyohusisha wananchi kununua upendeleo na kwenda kinyume cha haki. Wakati ufisadi, hutokea wakati ujumla wa matendo ya rushwa kama ilivoelezwahapo juu yamekithiri kwa wingi, kiasi na athari zake. Inakuwa kama mfumo mzima umeambukizwa na ugonjwa kulinganisha na rushwa, ambayo ni vitendo vya hapa na pale. Ni hali ya ujumla ya mmonyoko wa maadili kimfumo ndani ya jamii. Ndio maana hamna nchi ama jamii ambayo inaweza kutamka kuwa imetokomeza rushwa kabisa.
    Kwa mtazamo huu basi, rushwa YAWEZA sababishwa na mambo makubwa matatu makubwa (mara nyingine haya hujizonga na hivyo kuleta mchanyato sugu ‘complicated’):
    1. Hulka ya binadamu (mtoaji anaweza kuwa mtu ambaye ni mbinafsi mno kwa tabia hivyo hutaka apendelewe na hawezi kuvumilia kungoja hata kidogo mfano: watu wanaopenda kukatiza (‘antilog’) foleni; mtozaji pia aweza kuwa mlafi kupita kiasi –kumbuka binadamu wote ni walafi na wabinafsi kwa kiasi chao- asiyoridhika na alichonacho/anachopata). Ashakum, hapa unaweza kuiweka tabia ya ‘Waasia’ wengi tuliyoizea ya ‘kuflash’ pesa
    2. Umangimeza/Urasimu: Ndiyo hiyo mdau hapo juu anazungumzia kama ‘system’. Hii mifumo ama kwa kukusudia ama kutokukusudia (mara nyingine ni kwa ajili ya kuboresha mambo ama huduma) inaweza kusababisha walaji wakose uvumilivu wa ziada na hivyo waamue kutoa rushwa kuharakisha mambo. Hii ni ile iliyopita ni dhana za rushwa ambazo nafikiri zinadhihiri kwa kiwango kidogo kwenye jamii karibu zote duniani.........................UZENGERE

    ReplyDelete
  6. 3. Umasikini – katika nafsi tatu- njaa; mifumo dhaifu na ya kijima; maendeleo duni. Kwenye ‘njaa’ ni hali ya wananchi kutokua na kipato kinachoeneza matumizi yao, kama ya mwezi, wiki ama siku. Hapa pia ndipo wengi pia watakaosema wamepokea ama kutoa rushwa watakapoangukia miongoni mwa jamii zetu. Ikiwa kwa kila njia matumizi ya chini kabisa ya wananchi wa Dar es salaam kwa siku ni tuseme shilingi 3,667/- ni wazi kwamba kwa kiasi kikubwa wengi wanaponea rushwa (wengine watasema TAKRIMA) kuendesha maisha. Rushwa namna hii ni kama ya kimfumo vile sababu, mtunza mafaili anaipokea ili atoe faili lakini naye anaitoa ili akamlipe mwalimu amfanyie twisheni mwanae japokuwa mwalimu analipwa mshahara na serikali kwa kazi hiyo hiyo. Mwalimu naye anamchangia trafiki ili gari lake ‘mandemba’ lisikamatwe kwa upungufu wa namna moja ama nyingine. Trafiki inabidi akahongea kwa mwalimu mkuu wa shule yenye sifa ili mwanae aanzishwe darasa la kwanza hapo… na mwalimu mkuu anaenda kuhonga daktari na nesi ili mama’ake aliyelazwa apate uangalizi stahili.. na kadhalika na kadhalika. Penginepo, kima cha chini cha mshahara kingeeneza matumizi, kiasi kikubwa cha rushwa hizi zingefagiliwa mbali. Hili la ‘mifumo dhaifu’ linachangiwa na yale ya #1 na #2 kuleta mchanganyiko maalum na hatari (kwa kiasi kikubwa, waweza kuelezea mambo kama EPA na Richmond ya hivi karibuni). Mafisadi hawa ni ‘majitu’ yenye tama iliyokithiri kutaka kujilimbikizia mali bila kutoa jasho halali. Wanatafuta na kugundua mianya na baadaye kuvumbua njia za kutumia mianya hii kufisadi nchi na wananchi wenzao. Hulka za mafisadi hawa pia zachangiwa na maendeleo duni ya ki-akili – sina maana uchizi, hasha nna maana ujinga kwa maana yake halisi (mtu anapokuwa au ana njaa ama amekulia kwenye njaa, akili yake aghalabu ni katika ‘kubukanya’ na kuhodhi kupita kiasi ili abukanye zaidi. Si rahisi kusahau kwenye matatizo na kulala na njaa ulikotokea..mtu gani mwenye akili timamu na aliefuta ujinga atatelekeza kwa mfano dolari milioni moja kwenye current account yake badala ya kuziwekeza?). Hii pia yasaidia kuelezea vita vya mafuta kama vile Angola na sehemu zingine na vurugu kama za Somalia na kwingineko. Ikumbukwe pi a kuwa mifumo dhaifu yaweza kuwa matokeo ya ‘maendeleo duni’, na maendeleo duni yaweza kuchangiwa na ufisadi hasa ulopata mchango kutoka mafisadi wa kimataifa. Kwa vipi? Kwamba rasilimali za taifa badala ya kupelekwa kunakostahiki kama afya, elimu na miundombinu, zinaibiwa na mafisadi wachache. Unazalisha wananchi wajinga na wenye njaa. Hili ukichangia na hulka za watu na mifumo dhaifu (disorder) basi vizazi na vizazi vinaendelea kudumisha na kusherehesha ufisadi. Ndipo inapofikia mzee wako kijijini anakuona ‘mpumbavu’ sababu vijana uliomaliza nao shule wana nyumba na magari bila ya kuuliza vimepatikanaje… kwa hiyo nnapozungumzia maendeleo duni ki kulinganisha jamii moja na nyingine. Unapata mafisadi wenye hulka za rushwa kutoka jamii zingine ambao ambao wanawinda na kuvizia fursa kwenye jamii zenye maendeleo duni na mifumo dhaifu (Radar) – Scotland Yard ambayo ni sehemu ya mfumo makini ingekuwa ina sauti hadi pande hizi, ufisadi wa Radar ungedhihirika kuwa mgumu kuufanza. Kumalizia, nimeamua nipanue uwigo wa hoja hii ili angalau haki ya kimtazamo ipatikane. Hata hivyo, ashukuriwe mdau aliyetekenya hoja hii. Kwanza kuturudisha kutanabahi kwamba jambo hili limo miongoni mwetu na pili kutufanya tujitalii nafsini mwetu kama tumeshiriki ama laa. Kwenye ile ya pili, hata mimi nimeshiriki pia :p..siwezi jutia, maana katika mazingira tuliyomo sijui lini tena ‘nitatoeza’…Hii ‘ahsante’ ya kuwapa watu baada ya hudma ni ngumu sana kuiondoa kutoka mazingira ya rushwa, mara nyingi inatengeneza mazingira yaw ewe kupendelewa ‘next time’. Pia tukirudia ukweli, kama ingelikuwa mtumishi analipwa kima cha mshahara anachostahiki, vyereje apewe ‘bakshish’ tena? Hata hivyo kuna mas’ala mawili ya kufikiria: kwanza materiality – kama bakshish si pesa ni kitu/kifaa/chombo na thamani yake si ya kutisha. Tuseme kwa huduma ya milioni kadhaa umempa mtoa huduma kalamu ama kisu cha mfukoni ama kijikumbukumbu chochote cha thamani ya labda shilingi elfu 25, haidhuru sana. Pili ni ‘Mtihani wa kichwa cha habari cha Ukurasa wa kwanza wa Gazeti’. Hebu jiulize jambo ulilolifanya bado litaswihi kwako na wasomaji kama lingeripotiwa kama ‘kichwa cha habari kinachoongoza kwenye ukurasa wa kwanza wa gazeti la kila siku la hapo ulipo?.. Kama majibu kwa yote mawili ni ‘Ndiyo’, basi umefaulu mtihani wa rushwa. Wakatabahu, UZENGERE

    ReplyDelete
  7. Nimewahi kutoa rushwa na nilisikitishwa sana jinsi nilivyolazimika kutoa rushwa! Mambo ya ushuru yaani. Naamini wengi wameshakutana na yule mama wa kwenye vifurushi Posta Mpya! Anakutwanga kodi kubwa halafu anakuoffer utoe 50%! Yule jamaa 'mlemavu' anakuita kando akijidai kukusaidia kumbe wote kitu kimoja. What a shame jinsi nchi inavyokosa mapato na wachache wanavyotengeneza kwao! Mahesabu yangu yanaonyesha yule mama hakosi laki tano kwa siku pale! Next time nikienda nyumbani nanikiwa na muda wa kusumbuana na takukuru nitajaribu kumfisha angalau mtu mmoja wa TRA mahakamani! Hapo sijaongelea DAHACO na uhamiaji! Inabidi tuache kutoa rushwa!

    ReplyDelete
  8. wewe mzee wa bunju mbona mwenyewe hujajibu swali?

    ReplyDelete
  9. Mazingira ya kutoa rushwa anayatengeneza mwenyewe mtoaji rushwa! Mwingine wala hajaombwa na mtu hiyo rushwa lakini kwa sababu ama hataki kufuata taratibu zilizowekwa anataka 'fast track' basi atajishebedua mpaka atatoa rushwa. Mara atatafuta mtu amsaidie, mara atatafuta kama kuna mtu anamjua, ili afanye mambo yake haraka, yaani kama vile mbwa anavyojipeleka kwa chatu! Na inawezakana kabisa ukapata huduma Tanzania bila kutoa rushwa ila lazima ukubali uwehu kidogo, uondoe woga kabisa na utahudumiwa tena haraka haraka. Utakuta mtu anajua kuwa atakuwa na safari lakini anasubiri mpaka dakika za majeruhi ndio anaenda kuomba passport! Planning!! hatuna tabia ya kupanga mambo yetu, kama ni safari basi angalau uliiplan mwaka mzima kabla ulingojea nini bado miezi mitatu usafiri ndio unaenda kuomba passport? Mwezi mmoja kabla ya safari unaenda kuomba visa? Poor planning!

    Kingine ni kutokuficha maradhi na kuogopana, hatuna principles sisi tunaona kuwa ni lazima umpe mtu kitu kidogo ili mambo yako yaende. Wakati mwingine utawakuta watumishi wa serikali wamekaa standby wanasubiri kama chatu wanavyosubiri mbwa wajilete! Adrenalin!!! Nakwambia ingia ofisi ya mtu unajiamini kama vile wewe ndiye bosi pale, wasalimie hata kama polisi bila woga, ukisema, habari za leo, habari za kazi! (Polisi hawajazoea kusalimiwa eti lazima watashtuka) na adrenalin yako iko chini au normal (si unajua binadamu ni mnyama kama wanyama wengine ana sense level ya adrenalin na kukujua mara moja), basi atajua tu huyu mtu si wa kumchezea kwa ujinga atafikri labda ni kiongozi fulani hivi kila akijaribu kuvuta kumbukumbu amekuona wapi, hapati jibu atakuhudumia na kukuondoa hapo mara moja.

    Nimeshakataa mara kibao kutoa rushwa polisi, nssf, ofisi za ardhi, benk ya crdb, TRA. na sehemu zote hizo nikiona sipati huduma ninazostahili nakuwa mkali na kwenda kumuona bosi moja kwa moja, adrenalin ikiwa chini confidence iko juu! Huko TRA ukiwa na mzigo lazima uwatumie hao watu wa kutoa mizigo ma clearing agents, hao bwana wanashirikiana na watu wa TRA. Nitatoa mfano mmoja tu, kigari changu mtu aliona kuwa ni lazima anitoe upepo kwa sababu alitaka tu, kwa kushirikiana na hao agents, wakaweka file langu wanakojua halafu akaniambia kuwa kuna makosa katika documents zangu file liko kwa bosi. Kila nikimuuliza, file liko kwa bosi. Basi siku moja nikatoka ofisini saa nane mchana, nikamuomba ruhusa bosi wangu kabisa maana niliamua leo ni leo, kazi moja tu. Basi nikafika long room nikakuta watu kibao, nikauliza wapi nitapata huduma, wakaanza kuniambia ooh hukutakiwa kuja huku clearing agent wako ndio anatakiwa aje. Nikawajibu service yake hainiridhishi nimekuja kufuata majibu ya maswali yangu. Hapo Long room kuna kaunta imeandikwa FAST TRACK hata sijui kazi yake, nikaenda hapo dirishani nikashout 'nahitaji huduma ya haraka, fast track, naomba nihudumie natakiwa kuilipia shs ngapi?' (Hapo nimekula bazee la nguvu na mamikufu ya rusha roho na hereni, utafikiri nina pesa kweli.) Basi mbio mbio akaja mtu kunihudumia, akaniambia mama huduma hapa bure hulipii hata sentano sema shida yako. Nikamweleza, file likatafutwa mbio mbio bosi akaja tukamalizana hapo hapo kwenye dirisha la 'FAST TRACK' ndani ya masaa mawili nikawa nimeshalipia kodi ya gari langu nikaondoka nikwamwachia huyo agent mwehu kazi ya kumalizia kulitoa! Siku nyingine nitawaambia story ya nssf nilivyoenda kufuata mafao yangu ya miaka kibao, ambao ni tumilioni kadhaa ambacho kiliwatoa watu udenda, senti tano hawakupata na kwa bosi wao nikawashtakia, hundi iliyoambiwa itatoka baada ya siku kadhaa, ilitoka kesho yake! Au hadithi ya polisi ambaye aling'ang'ania leseni ya dereva wangu na kutafuta ufunguo wa gari langu usiku baada ya kumwendea central! Nina story kibao ambazo ninazo zinazohusiana na kukataa kutoa rushwa! Kuna mchezo wa kijinga kabisa Kariakoo ambao vijana wa kihuni walikuwa wanashirikiana na polisi, ukipita na gari kijana anajiangusha eti tairi limemkanyaga, basi tukaenda polisi, polisi wakasema subirini aende hospitali wakazuia gari yangu, mie nikasema tutampeleka huko hospitali nione mwisho wake. Huko hospitali nako wana mtu wao (Muhimbili huko),basi sikubanduka mpaka mtu akafungwa 'pop' kwenye mguu ulio mzima, kurudi nikapiga simu central traffic kuulizia kama ukifanya ajali polisi wana haki kuzuia gari yako. baada ya dkk 20 nikapewa ufunguo wangu huku watu wamenuna. lakini ndio nilishapoteza muda.

    Hivi vitu inabidi ukubali kupoteza muda kama hutaki kutoa rushwa. Mimi mtu akianza kujenga mazingira ya kutaka kuniomba rushwa basi mwili mzima hutetemeka kama nataka kupungwa madogoli!! Kwa sababu naichukia rushwa kuliko kuliko kitu chochote kingine kwani ni adui wa haki! Huko kwenye mahakama ndiko kumeoza kabisa kama hutoi rushwa basi hupati file, huko kwenye pesa za EACommunity mwisho walinichoka nilieenda wee wakaona mtu gani huyu haelewi, tangu 2005 mpaka leo mafao ya marehemu mzee wangu hawajanilipa, nimewaambia siku mkiwa tayari mtanilipa nitasubiri, mbona subira ninayo ya kutosha! RUSHWA NI ADUI WA HAKI NA HAITAISHA MPAKA KWA UMOJA WETU TUTAKOAMUA KUKATAA KUTOA RUSHWA, KUWA NA PRINCIPLES, KUTOKUTAKA SHORT CUT, FAVOURS NA KUZUIA HAKI YA MTU MWINGINE!

    ReplyDelete
  10. Mimi nimeshatoa rushwa. Kosa nilikuwa nimeacha leseni nyumbani. Ni kweli kuna sheria ya masaa 48 kuonyesha leseni lakini kwa sababu nilikuwa na haraka sikutaka kuwaachia gari. Alafu ngoja niulize swali? Ukionyesha leseni kabla ya masaa 48 bado unalipa fine ya Tsh 20,000? Anyway mie nikampa buku mbili alafu akaniambia "Ukisimamishwa na mwingine, usisimame". I still remember this statement to this day. Very shocking and sad.

    ReplyDelete
  11. Mimi naamini hakuna mtu anayefanya biashara Tanzania bila ya kutoa rushwa. Hakuna dereva anaeendesha gari nchini ambaye hatoi rushwa. Hakuna mama ama baba mwenye watoto wanaosoma hapa nchini ambaye hajawahi kutoa rushwa. Kama umeshawahi ku uguliwa na ukampekeka mgonjwa hospitali ya serikali, basi umeshatoa rushwa. Nasema hivyo kwasababu hakuna system yeyote hapa nchini inayofanya kazi ipasavyo bila ya wafanya kazi hao kupokea rushwa. Habari ndio hiyo, tuache kudanganyana. Uongozi wa nchi umeshindwa kabisa kwenye hili swala maana utamkamata nani na kumuacha nani. Poleni sana watanzania wenzangu.

    ReplyDelete
  12. Swali ni kwamba ulishawahi kutoa rushwa? Hapa naona watu wengi badala ya kesema ndiyo au hapana na kwa nini wao wanaanda kutoa maana ya rushwa au ufisadi. Hii maada ni nzuri sana na ikiwezekana Balozi wa Zain hii maada ipewe nafasi tena ili watu watoe ushahidi wao. Mimi nina imani tukuijadili rushwa kwa mifano na hata kutaja wahusika tunaweza kupata maisha bora.
    Mimi binafsi nilishawahi kutoa rushwa Polisi

    ReplyDelete
  13. NI KWELI KUWA KUNA WATU TANZANIA HAWAHITAJI KUTOA RUSHWA. JINA LAKE TU LIKITWAJWA BASI ATAPEWA HUDUMA YEYE MWANZO NA MAMBO YAKE YATAKWENDA HARAKA SANA. LAKINI KWA WENGI(MAJORITY) YA WABONGO INABIDI TUTUMIE MFUMO ULIOWEKWA NA UNAOLINDWA NA VIONGOZI WETU WA SERIKALI NA CHAMA TAWALA WA KUNUNUA HAKI.
    VIONGOZI HUPANDA MAJUKWAANI NA KUPIGA KELELE KUWA RUSHWA NI ADUI WA HAKI, LAKINI AKISHUKA TU KWENYE JUKWAA ANATOA RUSHWA KUNUNUA KURA.RUSHWA NI RAFIKI MKUBWA WA HAKI TZ.

    WENGI HAWATOI RUSHWA KWA KUWA WANA HARAKA NI KWA SABABU KAMA HUKUTOA RUSHWA UNAWEZA KUPATA HASARA KUBWA.NAKUMBUKA SHEMEGI YANGU MMOJA ILIBIDI MAISHA YAKE YAOKOLEWE KWA KUTOA RUSHWA PALE MUHIMBILI.BILA YA RUSHWA ANGEKUWA MAREHEMU BAADA YA WAHUSIKA KUSEMA HAWAWEZI KUMSADIA ETI DAWA ZINAZOHITAJIKA HAPANA. ILIKUWA NI SUALA LA KUFA AU KUPONA.
    NAMJUA JIRANI YANGU MMOJA ALIFUNGWA MIEZI SITA JELA BAADA YA KUKATAA KUROA HONGO KWA TRAFIKI NA HATA HAKIMU KWA KESI NDOGO YA GARI. HAKUGONGA MTU WALA HAKUHATARISHA MAISHA YA MTU.
    HABARI NDIYO HIYO.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...