MIMI BWANA KWA MAMBO YA SIASA NI LEYIMANI KABISA. NDO MAANA LEO NIMEONA WADAU WA BLOG YETU YA JAMII WANIELEIMISHE. MAANA TOKA NIZALIWE MIAKA MAKUMI MANNE SIJAWAHI KUONA MAMBO HAYA.
SISI ZAMANI ILIKUA HATA UKITAJA JINA LA RAIS USIKU UNAZABWA KIBAO NA KARIPIO LA HALI YA JUU TENA TOKA KWA BABA AKO AU MAMA AKO WATASEMA “ WE MWANA WE USITULETEE MATATIZO SISI UNATAKA TUFUNGWE??”
LAKINI LEO IMEKUA TOFAUTI. WATU WANAFIKIA HATUA YA KUPOPOA MSAFARA WA RAIS, JE WA MBUNGE ITAKUAJE??
SASA NAULIZA HIVI KUMPOPOA MAWE MHESHIMIWA NI
a) MAFANIKIO YA SEREKARI YA C.C.M KATIKA KUKUZA DEMOKRASIA??b) KUKATA TAMAA KWA WANCHI KULIKOKITHIRI??
c) WANANCHI WANAHISI KUA KIPENZI CHAO JK AMEWATUPA MKONO, NA WAMEMUA KUMUADHIBU ILI AJIRUDI??
d) TABIA YA WANANCHI KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI IMEPEA?? NA HATA KUFUKIA KUPOPOA MAWE RAIS??
e) AU NINAMNA YA KUONYESHA MAPENZI KWA RAIS WAO??
HIVI HAWA WAH. WABUNGE KWELI WANA WAKILISHA WANANCHI?? MBONA WATU WANAKUA NA WAHKA YA KUMUONA RAIS ILI WATOE DUKUDUKU LAO NA WAKIMKOSA WANA PANDWA NA JAZBA??
JE NJIA YA KUWAKAMATA WAHUSIKA ITARUDISHA NIDHAMU NA KUMREJESHEA AMANI RAIS WETU ILI PINDI ATUONAPO TUMEJIPANGA BARABARNI AFUNGUE DIRISHA LA GARI NA KUTIUPUNGIA KAMA ILIVYO ADA YAKE?? MAANA ISIWE IKAWA AKITUONA ANAINAMA CHINI KWA KUJUA ATA POPOLEWA MAWE!!!!
MUNGU IBARIKI AFRIKA,
IBARIKI TANZANIA,
MUNGU MBARIKI JK WETU MPENDWA...
ASANTE KWA KUNIVUMILIA
MZEE WA BUNJU
inavyoonekana jamaa wana tulet down kinomanoma. kwanza kigamboni yote imeuzwaa nyie hamjui.
ReplyDeletemkuu wa wilaya, na wewe unaelekea uko, kweli tukupe madaraka.
nani leo anapendwa kama michuzi?!!
nani alipendwa kama jakaaaaaa..ya superstaaaa.
Mimi nilitoa comment moja kuhusu JK kushindwa kazi ila naona bro Michuzi akaamua kuniminyia, siwezi kulalamika sana kwani hii ni nyumba yako.
ReplyDeleteIla kama mchangiaji wa kwanza alivyosema Tanzania mambo yanasikitisha saaaaana; ukiwa na uwezo wa kuangalia system kwa undani "read btn the lines" theni utajua kule tunakoenda sio kuzuri. JK aliyekuwa kipenzi cha watu, naona sasa anaanza kuwa adui wa watu mpaka anapigwa mawe.
Habari MH.DC NA BAROZI WA ZAIN,Mzee wa Bunju haya mambo ya kuvunja heshima kwa mh.RAIS yalianza taratibu na kufumbiwa macho na matokeo yake sasa yamefika mabaya,itambulike kuwa MH.RAIS pamoja na mambo mengine au hata tofauti tulonazo lakini ni kiongozi anae stahili kupewa heshima na nidhamu ya juu,ikumbukwe wananchi walianzisha mtindo wa kuzuia misafara ya Rais mabalabalani kwa kweli si jambo jema kuingilia msafara wa kiongozi wa juu kama Rais tabia hii ilifumbiwa macho ikaanza kuonekana ni ya kawaida na wananchi wakaanza kuitumia,sasa wakavuka mipaka na kuanza kupiga mayowe mbele ya Rais,na sasa wananchi wameingia ktk hatua ingine ya kupopowa mawe,hata hili lisipo kemewa vya kutosha litaigwa,hapa tunapata picha kuwa ktk ngazi za chini za uongozi wetu kuna matatizo makubwa ya kutosikiliza wananchi au kutotoa ufafanuzi wa baadhi ya mambo kiasi inafika Mkuu wa nchi anahitajika kutatua mgogoro wa wafanyabiashara wa soko kama ilivyo tokea Mbeya jambo ambalo lingemalizwa na Diwani au DC,RC sasa ni vyema viongozi wetu wa ngazi za chini MJIPANGE,MUWAJIBIKE,MUWE KARIBU NA WANANCHI Kuepusha adha kama hizi zinazo jitokeaza kwa mkuu wa NCHI.
ReplyDeleteHeshima ya rais iko palepale tu!!
ReplyDeletena hao wanaopopoa mawe mimi nawaona kama wanamaralia na njaa kali juu yao.
au bangi wamevuta bila kula. mtu mwenye hakili zake timamu ataanzia wapi kuokota mawe na kumrushia mtu?
ushauri wangu kwa rais siku nyingine aende mbeya na awatangulize f.f.u walio vaa ki raia kisha wale wanaopenda kupopoa mawe wapopoe tenakisha wapewe disprin kidogo tuone kama maralia yao itaendelea au itapona.au kama ni bangi je itawatoka au ndiyo itawakolea.
Tatizo hapa ni JK mwenyewe kujivunjia heshima na kuwalinda mafisadi wakati walalahoi wao wanateseka na hawajui ni lini wataikamata hata laki moja kwenye maisha yao, wakati mafisadi wanakwiba mamilioni ya pesa.
ReplyDeleteJK kama rais anatakiwa kufahamu mwizi akiiba polisi wanatakiwa kufanya uchunguzi na kama wakiona kuna mashtaka ya kujibu basi kesi inapelekwa mahakamani LAKINI yeye Mweshimiwa anaunda tume na anapelekewa ripoti,kama kwenye ripoti hiyo kukiwa na rafiki yake au jamaa waliodhamini CCM kipindi cha uchaguzi basi ndipo anajaribu kuwababaisha watanzania na kuikalia ripoti hizo.
Inasikitisha sana Tanzania utafikiri kwamba sheria hakuna.Mweshimiwa rais yupo radhi kutoa mifano ya kuwatishia wapinzani kama vile "Mimi ni rais na nikitaka leo Mheshimiwa Slaa atiwe ndani naamrisha tu, Mkuu wa polisi kamata Slaa tia ndani na Mkuu wa polisi asimuulize lolote"
Ingekuwa vizuri angetoa mfano kwa kusema Mkuu wa polisi wakamate mafisadi na watie ndani,hapo Watanzania wote wangesheherekea na kumuona yeye ndio kiongozi wa maana.
Hivi ni kweli JK hafahamu wananchi wanatake nini? Kama hafahamu basi rais wetu ni kipofu na inabidi anunuliwe mawani yenye lenzi kubwa ili aone matatizo ambayo wananchi wa kawaida wa Tanzania wanakumbana nayo.
Serikali na Chama chake tawala wanabidi wabadilike kwa haraka sana lasivyo mambo yatakuwa mabaya sana.
Leo Rais kapigwa mawe je kesho ni nini kitatokea?
Kenge
Wadau, mimi nafikiri ili uheshimike lazima uheshimu kwanza. Wale wanachi waliotoka kwa wingi na kumpigia kula Jakaya walifanya hivyo kwa heshima na mapenzi. Na walifanya hivyo wakitegemea kwamba kiongozi waliyemchagua atawaheshimu kwa kupigania haki zao.
ReplyDeleteLakini nini kilichotokea baada ya Jakaya kufika Ikulu? Serikali yake imeweka rekodi ya "ufisadi" na kinachosikitisha na kuwafanya wananchi wawe na hasira mpaka kumrushia mawe Rais wao ni kwasababu JK hajali.
Hajali kwamba gharama ya maisha inazidi kupanda wakati watu wachache wenye konekisheni na serikali wanazidi kuneemeka.
I was adamantly against his choice because I felt people chose him based on their "good feelings" and not their instincts
Mimi naona inachanganyika na hasira watu waliyonayo ya kutoweza kujieleza kwa viongozi wao na wala wale viongozi waliowachagua hawawaoni.
ReplyDeleteWabunge wa siku hizi ni jina tu. Ukipitia bubge page utaona kuwa wabunge wengi anuani zao ni Dar es salaam sasa ujiulize huko kijijini anakwendaga lini. Wabunge wa vijijini wamehamia dar.
Watu hawana wakuwaeleza matatizo yao na wanafikiri JK anaelewa yote lakini hafuatilii hili au kuwaachisha kazi wote wale ambao ni wabunge lakini wanaishi nje ya sehemu zao za kazi.
Wakiona raisi na cruise na magari mazuri hivyo halafu wao hata injini kiuno hawana licha ya nini watakula usiku....Hao watu wameshakata tamaa ya maisha and they think they have nothing to loose anyway....
Serikali ikifungia macho raia na kuondeleza kufanya maufisai yao itakua shida zaidi. na ukizingatia sas hivi internet ni kila manali kwa hiyo kila ovu la kiongozi linaanikwa kwenye mtandao na JK hata hawaengui hao waovu ....Hasira zitasidi sana....watu wameshachoka ile tittle tunayopewa kuwa TZ tuna amani ....lalini amani wakati tumbo liko njaa it is so hard to take it