kama kawaida ufukwe wa coco beach ndio ulikuwa kivutio cha wakazi wengi wa dar wakati wa sikukuu za iddi leo
wengine walifika coco beach kupunga upepo na kuangalia bahari ya hindi
furaha ya iddi baharini
wengine walifika kubarizi tu baada ya funga kumalizika

inaonekana sikukuu ni muda pekee ambao wengi, hasa watoto, huruhusiwa kuja kuogelea baharini.
hii ni changamoto kwa wawekezaji kwani kukosekana na mahali pa kwenda siku za mapumziko kunapelekea wengi kusherehekea coco beach ambako zaidi ya maji, ashkirimu na soda hakuna. kuna haja mjasiriamali mmoja akajitikeza na mabembea na michezo mingine kibao. kwa lugha ingine 'disney land' inahitajika bongo na wazee wa jiji wanashauriwa kutumia ubunifu kuifanya jamii ya walipa kodi ijione ina viongozi wanaowajibika ipaswavyo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. wananchi wa tanzania tujitolee tusisubiri serikali tizama hao watu baharini na watoto kuna uwezekano wa kuzama au kupotea waweke box na wasaidizi wa uokoaji majini na kutangaza kuna mtoto kapotea na watu wawafahamishe watoto wapi pa kwenda wakipotea hilo ndio muhimu tufurahi Eid tusubiri na sikukuu nyengine inshallah ahsante michuzi.

    ReplyDelete
  2. Uzuri wa bongo ni kuweza kwenda kwenye ufukwe wa dezo. Mjasiriamali akijitokeza kutunyang'anya fukwe chache za dezo zilizobaki makapuku tutaogelea wapi?
    Be careful what you wish for!

    ReplyDelete
  3. bwanaweee kuna coast guard hapa au baywatch au twavamia tukizama hope not tusije spoil eid yetu...
    eid mubarakaa waungwana

    ReplyDelete
  4. Wengine wapo kwa kazi maalum tu,kuwaibia wenzao yaani vibaka.

    ReplyDelete
  5. Anony wa kwanza ana pointi muhimu.

    Enzi za Africana Beach, nimeshawahi kuokota maiti ya mtoto wa sio wa zaidi ya miaka 5 au 6 katika pool yao. Wazazi wake walikuwa palepale karibu na baa ya pool lakini hawakumwangalia vizuri kwa dakika tu. Kwa kuwa pool inajaa watu bila kiasi, ilikuwa vigumu kumwona mwanao nadhani. Nilipokuwa natoka katika pool hio nikakanyaga mwili wake ambao ulikuwa umeshazama na hakuwa anahema kabisa nilipozama chini na kumtoa nje. Kelele za mama yake mpaka leo sitazisahau japokuwa tukio hili lilitokea miaka 20 iliyopita.

    Wale wadau waliokuwa nchi zilizoendelea watajua kuwa bahari zao huwa na lifeguard kila kona na pool zao haziruhusu watu kuogelea zaidi ya namba kadhaa ya watu kwa wakati mmoja. Tujaribu kuiga wenzetu kuepuka na ajali za baharini za kuzama, sio mpaka Mchina atujengee banda la lifeguard baharini halafu tukae na kujisifia kuwa Bongo tambarare sasa kama "Baywatch".

    ReplyDelete
  6. Michuzi nakuelewa una maana gani lakini naona uwezo wa dosney land hatuna sasa hivi lakini kuna vijisehemu vinaitwa chuckcheese huku ni kama watu wanavyowekeza kwenye majumba ya clubs na music ...tumesahau watoto wetu sana

    Halafu kwa baharini hivyo japo Corney Island kwa wale wanaopafahamu ....hatuna uwezo wa maaquarium au yale mabembea lakini vile vibanda vilivyo pembeni pale kama serikali ikiamua watu wangeruhusiwa kuweka ....wala haviitaji mabilions...boardwalks hata basi wangeweka unaona watu nanapanda kwenye hiyo cliff ili waone bahari vizuri lakini kungekuwa na boardwalks ingekua poa sana.

    Kuajiriwe lifeguards hata kwenye siku za holidays tu. hapo akizama mtoto anayejifunza kuogelea basi tena ndio ile wanasema aliwa na msukule kumbe

    Na hali yetu ya heewa hizo sehemu zingekaa mwaka mzima huku ni summer tu lakini wafanya biashara wanafungua na kufunga off season...

    kwanza ingeengeza govt tax revenue kwa vile ukienda kule Corney island unajikuta unatumia hela nyingi tu lakini kwa vile ni mara moja moja sio kila siku one wouldn't mind to do that

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...