Meneja wa Kanda ya Kati wa Zain Tanzania, Samsom Majwala akifurahia baada ya kupiga mpira na kuingia shimoni wakati wa mashindano ya gofu yaliyodhaminiwa na Zain kwenye viwanja vya gofu mjini Kilombero wikiendi hii
Meneja wa Kanda ya Kati wa Zain Tanzania, Samsom Majwala akitazama mpira aliopiga wakati wa mashindano ya gofu yaliyodhaminiwa na Zain kwenye viwanja vya gofu mjini Kilombero
Mshindi wa kwanza wa mashindano ya gofu ya Kilombero yaliyodhaminiwa na Zain, Patti Bennie akikabidhiwa kombe na nahodha wa klabu ya gofu ya Kilombero, Greg Ascough mjini Kilombero jana. Kulia ni Meneja wa Kanda ya Kati wa Zain Tanzania, Samsom Majwala.
Mshindi wa pili wa mashindano ya gofu ya Kilombero yaliyodhaminiwa na Zain, Jonas Fute akikabidhiwa kombe na nahodha wa klabu ya gofu ya Kilombero, Greg Ascough mjini Kilombero jana. Kulia ni Meneja wa Kanda ya Kati wa Zain Tanzania, Samsom Majwala.
Ofisa Mauzo wa Zain Tanzania, Niki Kazuka akichagua majina ya wachezaji walioshindana kwa makundi katika mashindano ya gofu ya Kilombero yaliyodhaminiwa na Zain mjini Kilombero jana huku akishuhudiwa na nahodha wa klabu ya gofu ya Kilombero, Greg Ascough.

MCHEZAJI wa klabu ya gofu ya Kilombero, Patti Bennie jana aliibuka mshindi wa jumla katika mashindano maalumu ya gofu yaliyodhaminiwa na Kampuni ya simu za mkononi ya Zain Tanzania na kurindima kwenye viwanja vya gofu mjini Kilombero jana.

Katika mashindano hayo ambayo Zain iliandaa mahsusi kwa ajili ya wateja wake wakubwa, Patti ambaye ni raia wa Afrika Kusini, alipata zawadi ya kombe kwa kuibuka mshindi wa kwanza, akifunga pointi 38 akifuatiwa na Jonas Fute ambaye pia alipata pointi 38, lakini akashindwa kwa pointi tisa zilizohesabiwa baada ya mchezo.

Kwa kuibuka mshindi wa pili, Fute pia alipewa zawadi ya kombe, huku Meneja wa Kanda ya Kati wa Zain Tanzania, Samsom Majwala akizawadiwa simu iliyotolewa na Zain, kwa kuibuka mshindi miongoni mwa wachezaji waliopiga mpira umbali mrefu lakini ukakaribia shimo (longest drive).

Majwala alishinda pointi 27. Katika mchezo huo wa mashimo tisa, mchezaji mwingine wa klabu ya gofu ya Kilombero, Abbas Sapi pia alizawadiwa simu aina ya Nokia iliyotolewa na Zain kwa kuibuka mshindi miongoni mwa waliopiga mpira ukakaribia kuingia shimoni (closest to pin).

Mchezaji mwingine wa klabu ya gofu ya Kilombero, Joseph Masasi alizawadiwa pombe kwa kucheza katika kiwango cha chini na kuambulia pointi 13. Zawadi zote zikikabidhiwa na nahodha wa klabu ya gofu ya Kilombero, Greg Ascough ambaye pia alishiriki mashindano hayo yaliyoshirikisha wachezaji zaidi ya 20.


Akizungumza katika hafla ya kukabidhi zawadi, Greg aliishukuru Zain kwa kudhamini mashindano hayo kwa zaidi ya mwaka wa tatu mfululizo, kitu alichosema kinatoa changamoto zaidi miongoni mwa wachezaji na wadau wa mchezo huo kwa ujumla.

Naye Meneja wa Kanda ya Kati wa Zain Tanzania, Majwala aliwashukuru wachezaji wote waliojitokeza kushiriki mashindano hayo ya siku moja, na akaahidi kwamba Zain yenye mtandao katika nchi 22 barani Afrika na Mashariki ya Kati, itaendelea kudhamini mashindano hayo.

Mbali na mashindano hayo ya Kilombero, Zain pia ina mkataba wa miaka mitatu wa kudhamini mashindano ya gofu ya Mkuu wa Majeshi yanayondaliwa na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kambi ya Lugalo, Dar es Salaam, ambayo yamekuwa yakishirikisha pia wachezaji wa mataifa mbalimbali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Kila siku huwa nawaambia jamaa zangu kuwa Kilombero ni kijiji cha kimataifa! Big up Michuzi ikibidi weka picha zingine za mji huu maana una maendeleo zaidi ya hata mikoa na wilaya za Tanzania.

    ReplyDelete
  2. Nimefurahi sana kuona picha hizi, last time ilikuwa ni match iliyokuwa sponsored by BP it was a nice get together! I miss home baaaaaaaaaaaaaad. Happy to see you all. Thanks Michuzi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...