balozi wa ufaransa nchini, mh. jacques champagne de labriolle akiongelea kuanza kwa tamasha la filamu la ulaya kwa mwaka huu alipoongea na waandishi jijini dar leo. kulia kwake ni mkurugenzi wa alliance francaise ya dar didier martin na shoto ni mjumbe wa kamati ya tamasha hilo rita bowen toka ubalozi wa ireland. kwa ratiba ya maonesho hayo ambayo hayana kiingilio na yatafanyika kila siku kwa siku 20 katika jumba la new world cinema kule mwenge, nenda tovuti ya dailynews-tsn.com ama bofya hapa
msanii mrisho mpoto akipigia chapuo tamasha hilo, akiwa ni mmoja wa wasanii walionufaika na jumuiya ya ulaya baada ya filamu yake ya karibuni kulamba bingo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. ubwete? ama kweli kiswahili kinabadilika kila siku! sijui kama visiwani wanalitumia neno hili kama brother michuzi alivyofanya hapa :)

    ReplyDelete
  2. naomba unisaidie hivi mkoa wa morogoro una radio na tv station ngapi na majina? pia kama kuna gazeti lolote hapo mkoani

    ReplyDelete
  3. naomba mnisaidie jamani hivi mkoa wa morogoro una tv station na radio station ngapi? na majina pia kama kuna gazeti la mkoa huo tafadhali

    ReplyDelete
  4. Mdau uliyeulizia vyombo vya habari mkoa wa Morogoro.

    Kuna Abood TV, Radio SUA na Radio Ukweli.

    Hakuna gazeti.

    Siku njema.

    //Mdau

    PS: Taarifa hii imegharimu Tshs. 120/- ikiwa gharama ya SMS kuwasiliana na mdau mwingine aliyeko Morogoro ambaye labda hajasoma ombi lako, au hana muda wa kujibu. Ukisema "asante" inatosha.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...