Watanzania waishio Southampton wanapenda kuwakaribisha watanzania wote kutoka miji mbalimbali kwenye sherehe ya kujumuika pamoja.

Ndugu watanzania kufika kwenu katika sherehe hii ndio ufanikishaji wetu.

Sherehe itafanyika tarehe 8/11/2008 kuanzia saa 12 jioni hadi saa 9 usiku, katika ukumbi wa African-Caribbean Centre, St Mary’s Area, Trity Road, Southampton, SO14 0BE.

Kutakuwa na chakula na vinyaji vya kumwaga vyote toka Tanzania na kumbuka kiingilio ni bure!!!!!

Usingoje kusimuliwa fika ujionee mwenyewe mambo mbalimbali tuliyoandaa kwaajili ya siku hiyo pia wageni kutoka miji mbalimbali hapa Uingereza.
Mgeni rasmi pia atakuwepo kuzuzungumza na watanzania watakao fika siku hiyo.

WOTE MNAKARIBISHWA.

Kwa maelezo zaidi usisite kuwasiliana na wahusika wafuatao:
Kangoma Kapinga 07961094455,
Sekela Komba 07717435287,
Vicky Kamata 07796428625.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. nini mnasherehekea?

    ReplyDelete
  2. huyu ni vicky kamata yupi yulemwimbaj au

    ReplyDelete
  3. Mtanzania apata ajali Marekani, agongwa na mtoto aliyeiba gari!



    Kijana wa Kitanzania Bw. Ndalima Nzaro yuko mahututi kwenye hospitali ya Chuo Kikuu cha Michigan, Ann Arbor, nje kidogo ya Jiji la Detroit nchini Marekani baada ya ajali iliyosababishwa na kijana wa miaka 15 aliyeiba gari kugonga gari la Ndalima lililokuwa limesimama kwenye taa za kuongozea magari likisubiri rangi ya kijani.

    Kijana huyo aliyegonga gari alikuwa anafukuzwa na Polisi. Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa mji mdogo wa Westland kijana huyo aliyeiba gari na ambaye hakuwa na leseni ya kuendesha gari alikuwa anaendesha kwa kasi zaidi ya maili 100 kwa saa na aliyagonga magari ubavuni yaliyokuwa yamesimama hapo kwenye taa za kuongozea magari kwenye barabara ya Merriman.

    "Wale madereva waliokuwa wanasubiri rangi ya kijani kuwaruhusu hawakuwa na jinsi yoyote ya kukwepa ajali hiyo" alisema Chifu Jim Ridener. Bw. Ndalima aliyekuwa anaendesha gari ndogo aina ya Honda Accord, alitibiwa kwa dharura kwenye hospitali ya Garden City lakini kutokana na majeraha yake aliitiwa Helikopta ya Hospitali ambayo ilimchukua na kumkimbiza kwenye hospitali ya Chuo Kikuu cha Michigan mjini Ann Arbor.

    Hospitali hiyo ni mojawapo ya hospitali zenye uzoefu mkubwa katika kuhudumia dharura za ajali katika eneo hili la Michigan. Mtoto huyo wa miaka 15 alikuwa anaendesha gari aina ya Mercedes Benz S55MG ambalo ni la rafiki ya kiume wa mama yake. Kutokana na kijana huyo kuwa chini ya umri jina lake halitajwi kwenye vyombo vya habari.

    Hata hivyo kijana huyo yuko mikononi mwa Polisi wakati uchunguzi ukiendelea na mashtaka dhidi yake yatategemea hali ya Ndalima inaendeleaje.Habari ambazo tunazipata sasa hivi, hali ya mgonjwa siyo nzuri.Tutawaletea habari zaidi kwa kadiri tunavyozipata.

    ReplyDelete
  4. Eh, Vicky Kamata ni yule mwimbaji?? Makubwa!!

    mbona hujatueleza mgeni rasmi ni nani? Naona unatuhamasisha tu kuna vinywaji na chakula vyote vya kumwaga.Tueleze mgeni rasmi ni nani huyo,isijekuwa ni ile mikutano yetu ya nanii tawala mkatuchota kijanja.

    ReplyDelete
  5. kiingilio bure! kinywaji bure! chakula bure! hapana lazima hapo pana mtego! mbongo yuko uk akodi mahali, anunue chakula, vinywaji, alipe dj yote hayo halafu akuite kwa bure, siamini

    ReplyDelete
  6. Mimi nawakia kila la Kheri Sekela Komba enzi hizo Wilolesi.

    ReplyDelete
  7. Mme kaa nje mmeshaiga tabia za wazungu. Mnaalikwa kwenye sherehe na kila kitu ni bure mnauliza.... why? Ndio za wazungu hizo ukimpa kitu anauliza why you are giving me this for free. Halafu anamalizia ...I can't accept this?

    heheheheheh ukarimu wa watanzania leo hamuutaki ati pana mtego hapo...

    ReplyDelete
  8. watu bwana,majungu tu!mkipigishwa viingilio hapo mtalipa?ovyo!

    sie tutakuja mwaya sekela. ujue watu hawaelewi sio kila mtu anataabika na maisha

    ReplyDelete
  9. Unajua kuna watu wanatafuta pesa za kununua dawa na wanafanya juu chini kutafuta hela....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...