Ikicheza mechi yake ya kwanza katika ligi ya daraja la tatu ADASL timu ya Tanzanite Fc ya Atlanta iliweza kuifunga timu Atlanta Silverbacks DIII "Buckeye" katika uwanja wao wa nyumbani (RE/MAX Greater Atlanta) kwa goli 3-2. Mechi hiyo iliyochezwa jumapili iliyopita ilikuwa nzuri na yenye kuvutia.

Magoli ya washindi hao wenye asili ya Tanzania yalifungwa na Fredy Mburushi "Dunga" Mzindwellah Gandnize "Muzi" na lile la mwisho liliwekwa kimiani na Elvis Doto Mnyamuru.

Huku wakionyesha kwamba wao sio kama "Timu bia, pilau na vitambi" zilizoibuka kutoka kila kona ya dunia hii Tanzanite Fc walishenesha vipaji vyake vyote huku wakiwa na safu iliyoundwa na wachezaji wapya waliosajiliwa msimu huu.

Pia katika kuendeleza na kujenga undugu na urafiki Tanzanite Fc ikishirikiana na Helpers10 entertainment wanampango wa kuandaa Soccer tournerment tarehe 25 mwezi wa kumi siku ambayo yule mwanamziki nyota anayetamba na kibao chake "Mc Muga" sensational ALI KIBA anatumbuiza hapa Atlanta.

Timu zitakazopenda kushiri zinaombwa kuthibitisha mapema.
tafadhali piga simu
404-477-7766
(Hadji Helper)
kama mnapenda kuingiza timu.

Nafasi za timu ni nane tu na tayari kuna timu tatu zimeshathibitisha nazo ni Jamhuri Fc, Mashada (alabama), na Tanzanite Fc kwa maana hiyo nafasi zilizobaki ni tano tu.

Kutakuwa na ada lakini ni kidogo sana kuchangia gharama za uwanja, marefa, bima nk. Pia kama timu zinaweza kuthibitisha kuwa zinaweza kusafiri mapema basi wanaweza kutoa taarifa ili mipango ya usafiri na malazi iweze kuandaliwa mapema. Ikumbukwe tunaweza kupata discounts kutoka katika Airlines Co. na hotel kama mkiweza kuja kama groups zenye idadi nzuri ya watu.
Welcome to Atlanta where players play!!
Njoo ujionee mwenyewe kipaji cha Kiba "Anatisha".
Tanzanite Fc
"History makers"

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Kwa picha zaidi za mechi tafadhali usikose kupitia www.tanzanitefc.blogspot.com
    pia kwa taarifa zaidi za msimamo wa ligi pitia
    www.tanzanitefc.com na www.adasl.com.

    ReplyDelete
  2. Kwa picha zaidi za mechi tafadhali usikose kupitia www.tanzanitefc.blogspot.com
    pia kwa taarifa zaidi za msimamo wa ligi pitia
    www.tanzanitefc.com na www.adasl.com.

    ReplyDelete
  3. Tanzania DC imethibitisha kushiriki kwa hiyo nafasi zilizobakia ni nne mpaka sasa!
    Jamhuri Fc (kenyan Atlanta)
    Mashada FC (Kenyan Alabama)
    Tanzanite Fc (Tanzanian Atlanta)
    Tanzania DC.
    Ahsanteni

    ReplyDelete
  4. wee dogo Haji acha kuchafua jina la timu kwa kumtangaza huyo dogo.Ya Musa apewe Musa na Ya Israili apewe Israili.acha uchafuzi wa hali ya hewa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...