Nilikua mwajiriwa katika kampuni moja maarufu jijini dare s salaam , katika kuajiriwa kwangu huko nikawa msaidizi maalumu wa bosi wa kampuni ile , basi siku moja moja nilikuwa naenda kujirusha na bosi wangu. Ukizingatia kwamba sikuwa na mume wala mchumba na kwa kweli huyu bosi ndio alikuwa mtu wa kwanza kufanya nae tendo la ndoa, hivyo nilifurahia mhemko wake na jinsi alivyokuwa ananipenda na kunijali kila kitu nilipata na zaidi.
Alifanya yote haya bila kunificha kwamba ana mke na watoto nyumbani kwake kwahiyo wakati mwingine chochote kinaweza kutokea nijiandae kwa shuguli hiyo pevu kama mke wake akishitukia dili hilo.
Tulikuwa na uhusiano na huyu bosi kwa miezi 4 hivi mpaka siku moja katika tembea tembea mitaani nikakutana na kijana mmoja mtanashati akanieleza kwamba ananipenda na kunizimia sana yaani ameshanifia.
Huyu kijana alihangaika kwa mwezi mzima mpaka siku nikaja kumkubalia akawa ndio mpenzii wangu halali sasa, nilimwamini sana na yeye aliniamini sana, miezi 3 tokea kujuana na huyu kijana aliniambia kuhusu kufanya nae tendo la ndoa.
Nilifikiria sana wakati mwingine nilitaka kulia jinsi alivyokuwa ananishika na kuniomba tendo la ndoa akiwa chumbani kwangu, alijaribu kunishika sehemu kadhaa akanivua nguo nami nilimtolea nje nilimkatalia.
Basi siku moja nikamwomba tukaangalie afya zetu, kijana wa watu alikasirika sana wiki nzima hakufika nyumbani kwangu wala kunipigia simu, kumbe alitaka tufanye tendo la ndoa bila kinga? sasa ningejuaje kuhusu afya yake? au ananiamini nini mimi?
Maisha yaliendelea na mambo mengine yaliendelea tu wiki ya 3 alinipigia simu akaniomba msamaha turudiane na alikubali kwenda na mimi kupata vipimo vya afya zetu kujua kwanza kabla hatujaanza mambo mengine yoyote yale.
Basi ndio hivyo majibu yalitoka mazuri, ndio mapenzi yetu yalikuwa zaidi na penzi nilimpa bila hiyana wala aibu yoyote, yeye mwenyewe alifurahia mambo yangu na kwanza alikuwa anatoroka nyumbani kwao kuja kulala kwangu wakati mwingine mwezi mzima.
Tuliendelea kwa miezi kadha na huyu kijana huku na mimi nikiwa na bosi wangu kule kazini, basi bwana siku moja , sisi officini tulitakiwa kwenda kutoa damu hospitali ya muhimbili katika maadhimisho ya siku ya afya duniani.
Watu walipimwa afya zao na mimi nilipimwa, majibu yangu yalikuwa ya kutatanisha sikuamini macho yangu wala masikio yangu , nilienda hospitali ingine napo majibu yalikuwa yale yale kwamba nimeathirika na UKIMWI.
Haya majibu yalimfikia mpaka bosi wangu nae akatambua hilo akasikitika sana na yeye alivyoenda kupimwa akakutwa hajaadhirika, basi nikajua moja kwa moja ukimwi nimepata kutoka kwa yule kijana wa mitaani na sio mtu mwingine.
Nikamwomba huyu kijana tukaangalie afya zetu kwa mara ingine tena hospitali, tukaenda kule kupima afya zetu, yeye ndio alikuwa wa kwanza kupokea majibu yake, alikutwa ameadhirika akupata mshituko wa ghafla yaani haamini.
Mshituko huo ulimpelekea aanguke chini na kuzimia watu walienda kumbeba na kumpeleka hospitali kupatiwa huduma ya kwanza basi hapo ndio magonjwa mengine yalianza kujitokeza na kujulikana sana.
Kumbe huyu kijana alikuwa na urafiki wa kimapenzi na shugamami mmoja mtaa wa pili huyu shuga mami mume wake alifariki dunia miaka 5 iliyopita kwa UKIMWI watu wanasema TB sijui , ndio huyu kijana kuona zile pesa za shuga mamy akaenda kwake.
Kijana aliumwa kwa miezi 3 hivi kisha akafariki dunia akaniacha duniani mwenyewe , kule kazini nilifukuzwa kazi na bosi wangu kisa nilitaka kumwambukiza ugonjwa wa ukimwi , lakini siku moja alinipigia simu kunieleza kwamba mke wake ameadhirika na UKIMWI pia lakini yeye anasema hajaadhirika.
Hapo ndio nilishangaa sana , kwanini mke wa aadhirike yeye asiadhirike au mke wake nae alikuwa anatoka nje ya ndoa bila mume wake kujua? basi hiyo ni siri yao nyumbani kwao mimi hayanihusu.
Lakini ndio hivyo nilikuwa nimeshaadhirika na UKIMWI kazi nimeshafukuzwa sina cha kufanya wala kutafakari nilifikiria zaidi kuhusu ugonjwa wangu wa UKIMWI na jinsi nitakavyoweza kuishi maisha marefu kwa matumaini.
KAHABA
Baada ya kuona maisha magumu na sina lolote la kufanya mimi kama mwanamke mrembo na mwenye mvuto niliamua kutafuta njia rahisi zaidi ya kujipatia kipitano nilifikiria njia nyingi sana ambazo zingeweza kunipatia angalau mlo na mavazi katika siku zangu za maisha zilizobakia baada ya kugundulika nina virusi vya ukimwi .
Nikaanza kutafuta sehemu ambazo naweza kuuza mwili wangu kwa pesa za chapchap niweze kuendeleza maisha yangu ya kila siku , nilikuwa na ramani yangu kwanza pale OHIO , JOLLY , MACHENI , BILLS NA LATAVERNA hizo ni sehemu 5 kuu za starehe jijini dare s salaam kwahiyo huko naweza kufanya kazi za kujiuza kwa wiki nzima kila siku bila kuchoka.
Ohio ilikuwa nzuri ila tatizo lake ni kwamba kila anayepita pale anakujua halafu unatakiwa uonyeshe maungo yako hazarani mimi sikuzoea tabia hizo na sikuwa na mhemko huo kwahiyo nilivaa miwani yangu na kuacha mapaja nje tu waangalie wenyewe kama wanapenda watakuja.
Kule kwa macheni tatizo lake ni mashoga wengi sana, yaani mwanaume anaweza akaja kutafuta Malaya akakuchanganya wewe ni shoga, wale mashoga wanaojiuza hawana tofauti na sisi wanawake tunaojiuza wakati Fulani ulitokea ugomvi mkubwa watu waliamulia tulimgombea mwanaume.
Billa nako kuzuri ila vijana wengi sana halafu hawana pesa , na vitoto vidogo vingi , nilikuwa naogopa matatizo na vijana wa kule sikupenda kufanya mchezo na watoto wadogo waliokuwa wananitaka hata kwa dau gani nilingoja wanaume wenye pesa zao tu sio zaidi.
Basi nilianza safari za kuelekea jolly club kwa ajili ya kujiuza mwili wangu nipate angalau chochote cha kula na kufanya katika maisha yangu , pale jolly club nilikutana na dada mmoja anaitwa Aisha, huyu dada nae ni kahaba mzoefu akaanza kunionyesha mambo kadhaa wa kadha kuhusu biashara ya ukahaba na kadhalika.
Hapa ndio nilijufunza kwamba sio makahaba wote ni masikini au hawajiwezi kuna wengine wanajiweza na wanazo fedha ila wanapenda kufanya ukahaba yaani wamechoka na dunia wengine walikuwa na wanaume wao wakaachika wakaamua kuja huku kwenda na mwanaume wowote yule anayekuja.
Wengine wana matatizo katika ndoa zao kupigwa na kadhalika wanaamua kuja huku kujiuza au kukaa huku ili kuepuka matatizo katika ndoa zao au mahusiano yao, wengine ndio kama hivyo waume zao hawana nguvu za kutosha kufanya nao tendo la ndoa wanaamua kuwa makahaba kila mtu na lake na mambo yake pia.
Wengine wanafanya huu ukabaha kwa ajili ya kupeleleza yaani ni wapelelezi wa polisi au watu Fulani katika serikali wako katika mitaa hii kuzuga tu , ili wafanikishe kazi zao za uchunguzi kama polisi wa usalama sehemu walizoko.
Mwisho wa yote siku hizi kuna vita kubwa katika biashara hii ya ukabaha mjini dare s salaam , mfano kule jolly kuna wazungu na wahindi wanakuja kufanya biashara ya ukahaba kwahiyo wewe mwamfrika unakazi ngumu kuwapita wale wazungu na wahindi au wachina.
Siku hizi wanaume wengi wanapenda kitu kinaitwa JICHO yaani kufanya mapenzi kinyume na maumbile , hii nayo ni soko kuu, mfano mwingine anaweza kuja kwako anataka jicho na wewe hutoi jicho maana yake unakosa soko suluhicho ni kujitoa mhanga na kufanya mapenzi kwa kuwa mteja ni mfalme.
Mbaya zaidi kuna wanaume wengine wanakuja wanaweza kukuchukua uende nao kufanya ngono kumbe wanakupiga filamu za ngono wakati unafanya kitendo hicho haswa wazungu wengine wanakupa ufanye mapenzi na mbwa wao au wanyama wao wengine mambo yanaenda hivyo.
Biashata hii ya ukahaba ilinichanganyia sana kwa miaka 2 niliyoifanya na kwa kweli hakuna aliyenijua kama nimeadhirika na ugonjwa wa ukimwi nilikuwa najitunza na kutuza siri zangu hizi kuu na sikupenda kuzoeana na watu sana hadi waniulize hivyo.
Siwezi kuhesabu ni watu wangapi nimefanya nao ngono lakini ni zaidi ya 300 siku zingine nafanya kazi na watu zaidi ya 3 kwa siku moja kwahiyo mambo yanaendelea halafu wengi hawakupenda kutumia mipira ya kiume yaani kondom walipenda kuja hivi hivi tu bila kinga chochote kile.
Na mimi nilikuwa nimeshaadhirika nilichokuwa natafuta ni fedha za kuendeleza maisha yangu kwahiyo hata kama nikifanya ngono zembe bila kinga mimi hainiumi sana kwa kuwwa nilishajua hali yangu sikuweza kuitengua siku wa chochote cha kufanya zaidi ya hichi.
Hii ilikuwa ni kulipiza kisasi kwa maasi ambayo yule kijana alinifanyia kuniambukiza UKIMWI kwa makusudi huku akijua kabisa ameadhirika siku nyingi ,kwakuwa yeye ameamua kuniuwa mimi basi na mimi nauwa wengi zaidi na sijali kuhusu dhambi hizi nilizozifanya na sijutii kabisa.
MAISHA YA MTAANI
Huku mitaani waliniita majina kama JLo wakati mwingine salma hayek yaani wale waigizaji maarufu duniani kwa urembo nilio nao na mvuto wake, hakuna hata mmoja aliyekuwa na mawazo kama nimeadhirika au la kwa maana yule kijana niliyekuwa nae kama mpenzi alikufa kifo cha ghafla watu walisema amekufa kwa pressure.
Mitaani napo nilikamua kinoma, waume za watu walikuja mpaka mlangoni kwangu na magari yao, wananipakia na kunipeleka katika kumbi za starehe na sehemu nyingine nyingi sana wengine walinihonga mali na mambo kibao kisa wamenipenda wanataka ngono.
Na kwa uhakika hawa wanaume niliwapanga sawia kabisa na hakuna aliyeweza kutambua mimi nina wanaume wangapi na wanaishi wapi wengi walijua ni washirika wangu katika kazi zangu na mambo yangu mengine kwanza sikupenda kuongea na mwanaume wowote chumbani kwangu wote nilikuwa nawaambia tukutane mbali kidogo na nyumbani haswa kati katika ya jiji.
Katika hawa wateja wangu kulikuwa na kijana mmoja anayeitwa juma huyu juma alikuwa na rafiki yake mmoja anayeitwa Shy, kijana mwembamba mwenye umbo la wastani, hana ndevu halafu ni mcheshi sana, alifanikiwa kuiteka moyo wangu, sasa nilitaka kumwambia mara kibao kwamba nimemzimia.
Tatizo ni kwamba anayekuja kunichukuwa pale ni juma , juma huja pale kwa kusindikizwa na Shy, basi juma akanitambulisha katika website moja inayoitwa darhotwire www.darhotwire.com, nyumbani nikienda kupumzika nilipenda kushinda katika tovuti hii kuchat na marafiki na watu wengine.
Huyu shy nae nilimkuta katika site hii usiku wa manane anachat na jamaa zake , ila siku moja nilikutana na kijana mwingine anayeitwa politeman , huyu ndio alinichanganya kabisa , kwanza jina lake na jinsi aliyokuwa anaongea kweli nilizimia mwenyewe bado nikawa na siri kubwa moyoni je hivi tukifanya ngono inakuwaje?
Maisha yaliendelea tu, basi nikimpenda politeman, huyu kijana akawa anakuja mpaka nyumbani kwangu wakati mwingine na huwa nampa computer yangu aitumie tukaenda zaidi nilimshitukia kumbe huyu polite ana urafiki wa kimapenzi na dada mwingine anayeitwa salma siku moja walipanga kwenda kufanya mapenzi lakini polite akakataa?
Sikuamini macho yangu wala masikio siku nyingi kama naota kumbe polite alikuwa na urafiki na dada mmoja anaitwa Maria Chipz?? Sikuamini , nilimuheshimu sana maria na sikutegemea kama anaweza kufanya hivyo hata siku moja , muda ukaenda kumbe kuna dada mwingine anaitwa REHEMA naye alikuwa anampenda Politeman Miss upanga Naye anampenda Politeman we acha tu.
Nikamwaga chini sikupenda tabia zake za kitoto kitoto anazowafanyia hao kina dada wengine ingawa nilifanya nae mapenzi kama mara 4 hivi na mara zote hatukutumia kinga na nilikuwa nimeadhirika ila ni siri yangu , polite hajui na wengine wote hawajui lakini ndio maisha hayo.
Haya ndio hivyo , nami sasa hivi nakaribia kufariki dunia niko zangu kitandani hapa hospitali ya Amana mkoani dar es salaam, kweli maisha ni safari ishi upendavyo na sio watakavyo , mwisho wa yote dunia sio hadaa wala dunia haikuchukii au haitaki kukufanyia chochote kibaya.
Bali watu ndio hadaa , hata kama ni ndugu yako rafiki yako , hakikisha humpi nafasi akutawale aweze kukumiliki wewe na kukuamrisha chochote kile anachotaka yeye, kama ukifanya hivyo ndio utaishia kubaya kama mimi Bosi wangu alinimiliki sana nikampa penzi, kijana wa mitaani nae alinimiliki mpaka sasa nimeaona faida zake na hasara zake.
Wacha ningoje siku zangu nife nizikwe niende zangu ahera
Kwaheri
USHAURI
SIKU ZOTE KATIKA HIZI CHATROOMS ZA INTERNET USIWE NA URAFIKI WA KIMAPENZI NA MTU AMBAYE HUMJUI KIUNDANI WENGI WANAKUWA NA WANAUME AU WANAWAKE ZAIDI YA 1 NA WENGI WANAAMBUKIZANA MAGONJWA NA KUPEANA MATATIZO SANA INA UMA SANA.
SIKU ZOTE KATIKA HIZI CHATROOMS ZA INTERNET USIWE NA URAFIKI WA KIMAPENZI NA MTU AMBAYE HUMJUI KIUNDANI WENGI WANAKUWA NA WANAUME AU WANAWAKE ZAIDI YA 1 NA WENGI WANAAMBUKIZANA MAGONJWA NA KUPEANA MATATIZO SANA INA UMA SANA.
By MaryAnn
a.k.a
Gurl4Real
Hivi wewe Marry Ann,
ReplyDeleteHapa umekuja kutusomea hadithi au ndo zile gia zenu za kumuingia kaka yetu Joni Mashaka?
Haya subiria waosha vinywa wakuchambulie hayo makala yako.Joni Mashaka hupo?
Hujaua watu 300 kama uliyoyaeleza hapo juu ndo uliyoyafanya, zidisha mara 300 ndo utapata idadi yake! Sasa unatuambia tukupongeze kwa kuua kwa makusudi au ndo nini? Heee! Dunia imeisha, moto unawaka!Tukanyage wapi?
ReplyDeleteDah.. Weye Dada hayo uliyoyafanya ni MAKOSA MAKUBWA SANA husingefanya hayo kuwaambukiza watu wengine.Sasa weye wasema khasira sasa ulimkasirikia nani ?? wakati hayo yalikuwa ni maamuzi yako mwenyewe ??
ReplyDeleteKwa kweli hapo UMEKOSEA SANA TENA SANA. M/MUNGU AKUSAMEKHE.
WASALAAAAAM.
hiyo ni dawa ya viwembe au wanasema mimi nakula mademu 10 ooh mimi sita mpaka kieleweke wabakie waaminifu kwenye ndoa zao tu.
ReplyDeleteSo what
ReplyDeleteMichuzi kama hii hadithi ni ya kweli nampa pole huyu dada na asali sama ili Mungu wake amsamehe. Zaidi ni fundisho kwetu wote ikiwa tumeathirika na huu ugonjwa au la...sasa hivi kulala na wanaume au wanawake tofauti sio sifa tena bali ni kukaribisha mauti. Asante dada kwa kutupa "Elimu dunia"
ReplyDeleteKwa kusoma tu hiyo nakala yako ni rahisi kusema kuwa wewe ni ignorant person. Kwa hayo uliyoyatenda ulikuwa unamkomoa nani? Kila mtu mwenye ukimwi angekuwa na akili inayofanya maamuzi kama yako basi hii dunia kusingebaki mtu. Kwa yote uliyoyatenda ni kwamba ulikuwa unafanya maambukizo kwa watu ambao ni innocent, na katika hiyo circle itazunguka na kurudi kwa watu wa kwenu huenda na dada au kaka yako, hivi kwa mfano ukijua kuwa wewe katika hao uliowaambukiza nao walifanya mchezo wako wa kishenzi wengine kwa makusudi na wengine bila kukusudia lakini katika hiyo cheni ikaenda mpaka kwa mtu wa ukoo au familia yako utajiskiaje kujua kuwa wewe ndio ulikuwa chanzo cha kusambaza hiyo cheni?
ReplyDeleteKwa mimi navyoona, lazima utakuwa na matatizo ya akili si vinginevyo, muhimu ukatibiwe pia kichaa maana kinachangia kukufanya uwe mgonjwa zaidi.
You are an idiot. Hell is waiting you!
hata kama not true story hii imetulia,kwa kifupi ujumbe umefika hasiye sikia na hasisikie.
ReplyDeleteHII IMENIFANYA NIWE MPOLE NA NITAFAKARI SANA JUU YA HAYA MAMBO YA NGONO ZEMBE.
Eeh mola nilinde na machafu ya dunia hii.
wadau tufuate yaliyoamurishwa na mola wetu kuepukana na hayo.
Tukusaidiaje?
ReplyDeleteUmeuwawa na kuua...the cirle of life goes on!
We cant judge you, just like the way U cant just us!
Ushauri:...Make Peace with your Maker!
P.S: no offence, but it sounds like a scripted story - alafu ndefu sana...kha!
mtoto
Hii stori ndefu kama ya kweli au feki, inaoana na maisha ya watu wengi humu duniani Jamani Tuwe na Makini na maamuzi katika yetu.Kama wewe dada upo kweli pole ila umefanya kosa kujua una ugonjwa na bado ukaenda kuua MAELFU ya watu, Mungu Baba atusamehe wote kwa maana wote ni wakosaji.Amin.
ReplyDeleteTHIS STORY IS A BARE FICTION, BUT WILL HELP TO INSTALL AIDS AWERENESS AMONG THE READERS
ReplyDeleteHADITHI ZA SHY KAJITAHIDI KUTUNGA
ReplyDeleteUlichofanya ni kibaya tena mno. Matatizo yako binafsi umewaharibia maisha mamia ya watu. Kweli kwa Hali hii Tanzania bila ukimwi itawezekana? Kama ulikuwa unaenjoy kufanya mapenzi, basi angalau ungedemand condom. Pia shukran kwa hadithi yako cz nifundisho kwa wengi wanaojifanya wajanja katika ngono. Yani katika mzunguko wako wa biashara yako, umeshamaliza watu zaidi ya 1000 cz kila uliyemtumia nae anampenzi mwengine.
ReplyDeleteakha hii hadithi nimeisomaa jamii forum lonooong time agoo,leo imekuwa mpya kwa kaka michu.where is utamu by the wayyyyy.tumekumisooooooo.Utamu alikuwa juuuuu mwananawe
ReplyDeleteukome siku nyingine kufakamia wanaume za watu
ReplyDeleteJamani hiyo sio True story bali ni hadidhi amhayo ilitungwa na na kijana mmoja anaitwa Shy na ilitungwa toka mwaka 2006 kama sikosei, lakini hii hadithi inamafunzo mengi sana.
ReplyDeleteHUYU NI MOJA TU WAKO ZAIDI YA "LAKIMOJA" HAPA DAR
ReplyDeleteHii story ilikuwa kule jamboforums na mwandishi wake ni Yona Maro a.k.a shy. Ni story ya kutungwa haina ukweli wowote
ReplyDeleteKwa hiyo wewe unaona ufahari kutueleza jinsi ulivyoamua kuteketeza watu,kama hiyo haitoshi unaeleza kwa ufahari tabia zako chafu bila hata woga, sijui unataka tukupe zawadi au? But zawadi kubwa tayari unalo. Nashindwa kupata picha wewe ni dada wa namna gani. Anyway shindwa na ulegee katika jina la YESU.
ReplyDeleteMOVIE YA KI-NIGERIA HIYOOOOOOOOOOOOO...............
ReplyDeleteDADA MCHANGA, wewe ni wa wapi kishimundu au wapi?
ReplyDeleteNimekutambua uchanga wako kwa style yako ya lugha
1. eti "ameadhirika"
2. walipenda kuja hivi hivi tu bila kinga chochote kile.
wewe umeona hapa ni mahali pa kujufunzia kuandika hadithi? nenda kwa eric shigongo labda atapenda hadithi zako aweke kwenye magazeti yake. lakini nakupa ushauri ujifunze kwanza kiswahili.
toba yarabi, naona tumeshakufa sote,tena unatembea nawaume za watu,sasa fikiria watu 300kati yao waume zawatu na wana wake zao jee wanawake wangapi hao wameambukizwa? na kati ya hao nawao wanakisasi kama wewe wanazidi kueneza.tumeshakwisha watanzania,unaweza ukawa namume kumbe anamtu mwengine pembeni muathirika,unaweza ukawa na rafiki kumuamini nae anamtu nmwengine.dunia ya mwisho hii,nyie mlioathirika kuweni na moyo wa huruma musiwe makatili sio uzuri kwa kuwambukiza na kulipiza kisasi jee huko kwa mungu mtaenda kusema nini?hivyo kujitoa humu unataka usamehewe kwa makosa yako,hakika hata ukiwa umesamehewa lkn ujuwe mungu hajakusameh.ilobaki hao watu uliambukiza wataje wote tuwajue ili labda itasaidia,lkn umefanya makosa makubwa sana .
ReplyDeleteINASIKITISHA WATOTO MAYATIMA WATAKUWA WENGI SANA NA WALIOATHIRIKA KUENGEZEKA.SIJUI SERIKALI WATAFANYA NJIA GANIHATA HUU UGONJWA USIZIDI KUTAPAKA?WAKATI HAO HAO WALIOATHIRIKA HUWAFATA WENYE MAPESA ZAO ILI WAWEZE KUNUNUA MAHITAJI YAO NA MADAWA.
wadau nilikuwa namaanisha mwandishi lazima atakuwa MCHAGA. Ndio maana nikaandika
ReplyDeleteDADA MCHAGA, wewe ni wa wapi kishimundu au wapi?
Nimekutambua uchaga wako kwa style yako ya lugha
1. eti "ameadhirika"
2. walipenda kuja hivi hivi tu bila kinga chochote kile.
wewe umeona hapa ni mahali pa kujufunzia kuandika hadithi? nenda kwa eric shigongo labda atapenda hadithi zako aweke kwenye magazeti yake. lakini nakupa ushauri ujifunze kwanza kiswahili.
Dawa ya UKIMWI ni moja tuu, NO ZINNAH. Kama watu hawata zinni then HIV itakosa mshabiki.
ReplyDeleteTanzania tunachance ya kueliminate UKIMWI lakini inaonekana hatutaki.
Inshallah mwenyezi mungu atuepushe na huu ugonjwa hatari
Kwa kweli hii ni zaidi ya hadithi kwani haya yote ni ya kweli, ukweli mtupu. Wengi tunakufa hivi hivi! Mungu wetu turehemu na hili janga, wanapata waliopo na wasio kuwepo.
ReplyDeletekuna ndugu yangu alikuja kuposwa na jeshi mmoja,sasa baba etu alikataa kuwaozesa hadi wakapime hiv,basi aliwachukua wote wawili hadi hosp kuchekiwa,majibu yalivyotoka kumbe yule jeshi alikuwa ameathirika.maskin baba angelichukua tu kuwaozesha bila kutoa dawa mdogo wangu angeliupata na yeye.kwa hivyo tusikubali kuoana bila ya kutoa hiv kwanza jinsi tunavyoeda na maradhi yanazidihii story hata kama imetungwa lkn ni kweli yanatokea sana story kama hii.
ReplyDeleteWHETHER IS TRUE STORY OR FICTION!
ReplyDeleteBUT THIS IS WHAT IS GOING ON IN OUR SOCIETY.
LET US USE THIS STORY AS A CHECK FOR OUR DAILY LIFE.
AIDS IS REAL TAKE CARE OF YOURSELF AND YOUR PARTINER.
whether ni story ya kutungwa au ni kweli, wapo wengi wanaoweza kuhusisha maisha yao na sehemu ama hata hadithi nzima hii, cha msingi katika vita hivi nadhani ni story ya kufundisha. suggestion kabla hujaridhika kuwa mwenza wako hajaathirika, ni vizuri kurudia kucheki mara mbili au tatu hivi.
ReplyDeleteHahaa! hii stori sio yake ameikopi na kupesti tu, isitoshe ni ya siku nyingi sana mtandaoni.. Pole
ReplyDeletePOLITE LEO HALALI
ReplyDeletetatizo watu hawapendi ukweli,ndio maana ukimwi hautaisha.
ReplyDeleteI dont care whether this is fiction or true story. What I believe is, this is exactly what is happening in our world today. I had to invite friends to read the story as this gospel is simple to understand. That is why I have decided to change my priorities, I will need a woman for company and not sex. After all, sex is a pleasure which last for hardly 10 minutes but if it is only for company from a wise woman, ten hours may not satisfy you.
ReplyDeleteMessage delivered!
God bless you so much MarryAnn.
am cryng. hii siyo mzaa ujumbe umefika, ni kweli kwenye enternet kuna hatari tupu. thanx dear japo ulifanya vibaya kuua viumbe wa Mungu bila hatia. yule kijana alikuua may b mmoja tu dear, sasa 300 wa watu jamani wamekukosea nini?? na nyie wanunuaji makahaba badirikeni kama mpo, na sie walioolewa tutulieni katika ndoa zetu jamani. ila siyo siri ninalia, story imenipaini hii. Tubu ndugu yangu ili uweze kuuona ufalme wa Mungu. husiseme haujutii juta dadangu.
ReplyDeletehapa msiseme nini wala nini eti ni hadithi hata kama sio true storry. ukiangalia watu wanavyoishi inaendana na storry yenyewe.huu ni wakati watu kubadili tabia aina haja ya kumchambua huyo dada au mwandishi aliye andika hii storry ndio maisha yenyewa tunayoishi ni wakati wa kubadili tabia zetu. thanks michuzi kwa kutuletea hii kitu maana umewamusha watu kidogo waliolala AIDS IS A KILLER
ReplyDeleteLo nimesikitika sana. Kama Mary anasoma haya maoni anahitaji toba kwa ajili ya maisha aliyoishi. Dada unahitaji kutubu ili Mungu akusamehe. Kwa Mungu hakuna dhambi kubwa wala ndogo zote ni dhambi kama ni motoni au jehanamu unakwenda tu. Tusimnyoshee kidole na kuhukumu hata siye ni wadhambi tu, kwa Mungu dhambi haina kipimo kinachotakiwa ni toba tu. Yatupasa tugeuke tumrudie Mungu wetu, tufate amri kumi za Mungu tumeambiwa tusizini. Natamani nimwone huyu dada niongoee naye.
ReplyDeleteDAH! NAWAASA MIDADA YA KIHEHE,KICHAGA,KIFIPA AH NISISAHAU MINYAKI MAANA HII KWA KUPENDA CHINI TENA KAVU-KAVU,MOLA AIEPUSHE NA MIBALAA HII.
ReplyDeleteKWAKWELI NI VERRY INTERESTING STORY WHETHER TRUE OR NOT BT IT TRIES TO GIVE US FULL PICTURE OF HOW THE WORLD IS MOVING SIMULTANEOUSLY WITH HIV-AIDS.MIJIMAMA TUEPUSHENI NA MIBALAA WATOTO WA WENZENU PIA MIJIBABA EPUKENI UTAMU WA VIBINTI,VIMESHACHAFUKA NA MINYENYELE PIA MITOTO YA SHULE NAYO DAH NDO IMEONJA ASALI YAANI NI FULL KUJAA NGOMA.
MIVIONGOZI YA VYAMA PIA SERIKALI MHHHHHH USISEME SIJUI SIKU SPIKA WA BUNGE AAMUE KUCHOMOA KIFAA CHA KUPIMIA NGOMA CHENYE KUWAKA TAA KWA POSITIVE RESULT HALAFU AAMUE WABUNGE WOTE WAPIMWE VINGINEVYO NO UBUNGE KAMA BUNGE HALITOBAKI TUPUUUUU,
MDAU DMAPENZI KIJANA WANGU
hawa watu wanaodharau hii stori ndio hao ambao wanaokwenda bila ya mipira na yote hayo yalio mpata mwenzetu humu ndani inaonekana kuna watu fulani haiwashitui kwani wao wamesha zoea ugahaba na jinsi maisha yalivyomagumu home ooh maskini wataenda wengi sana kwa kweli tanzania ukimwi uko juu sana na tumeshachelewa ni kumuomba mungu tu ni mtego wa panya alie kuwapo na asie kuwapo.
ReplyDeletewhether a fiction or true story, i don't care! what i do care is the effects of this story to the societies. Bro Michu story hii ina faida nyingi pamoja na hasara ndani yake.Faida zake ni kwamba inaleta picha halisi ya namna gani watu wajitahidi kuongeza jitihada zao katika suala la uaminifu na uvumilivu, lakini huwezi amini kaka story hii ina madhara pia tena kwa mtazamo wangu ina madhara makubwa kuliko faida zake kwa sababu zifuatazo. Kwanza imefanya promo kubwa sana ya "ulipiazaji kisasi". Uwezi amini inahamasisha wanawake ambao kwa bahati mbaya wameathirika kutokua na upendo kwa watu wengine wanaoendelea kuwafuata.Huyo muhusika kwa makusudi ameamua kuwauwa binadamu wenzake kwa kukusudia,si zani kama mbele ya mungu anamsamaha wowote kwa kitendo chake.Kwa kukiri kwakwe alistahili adhabu ya kifo(my view)
ReplyDeletePili,story yako imewahamasisha watu hasa vijana (na wanandoa wasio waaminifu) kutamani au kuingia ushawishi wa kutembelea sehemu alizozitaja huyo muhusika kwamba zinapatikana madada poa wa aina mbalimbali.
Tatu,story yako inawashawishi wanawake walio katika hali kama ya muhusika au kina dada aliowaelezea yeye,sababu za wao kujiingiza kwenye biashara hiyo haramu,uwezi jua stori yako inaweza shawishi takribani 3 au 5 kuingia kwenye mkumbo huo wa wale aliowaelezea au hata w muhusika mwenyewe,kumbuka kwamba wanawake wanaofanya biashara ile wanatoka kwenye jamii yetu,kadhalika wateja wake,na loop yake inavyokua inatisha.
Nne story yako inashawishi hasa vijana kutokata tamaa pindi mwanapokataliwa na mwisho wake kujikuta wameingi kwenye mkumbo huo,
Ushauri wangu ni kwamba story kama hizi kabla hujaitoa ni bora kuihariri ili kupunguza madhara ambayo yanaweza kuletwa na upande wa pili wa habari husika.
Binafsi nimeishia nusu,annony mwingine akipenda anaweza kuongezea alionalo yeye ni bora ambalo linaweza kisaidia kupambana na ugonjwa huu hatari, kwa sababu kwa mtizamo wangu matangazo mengi yanayotolewa ili kuhamasisisha vita dhidi ya maambukizi ya ukimwi ni ya kibiashara mno na huishia kusababisha maambuki ya ukimwi kwa vijana na wanandoa kwani huwaongezea ujasiri kupitia ujumbe uliondani ya matangazo hayo
I am real wondering! I thought this is the most educative and soul touching story ever written in this blog. Actually I am wondering why some people are becoming negative. While the nation is loosing her man power through AIDS, some people dare to shut down such a kindly warning voice. In contrary, I am healthfully thanking you so much as I know that today, somebodys life will be saved. Thank you very much for saving my life too. Today, I am not going to meet this beautiful looking girl we have planned to have sex today. Because, I don’t know her status yet. But knowing the status is not enough. Sometime you need to test several times. Like MarrAnn with her boyfriend tested once, they found nothing. When they went there after some times, the virus had already established themselves enough to be seen. So, it is good to take enough time with your partner before going for sex. You may need more than a year to be sure. Test at least three times with three months period between the first and second test.!
ReplyDeleteTanzania should be free from AIDS. Just play your part as safer Tanzania begins with you.
Jioni njema
NI MTUNZI MZURI SANA WA HADITHI.
ReplyDeleteHata kama ni mtunzi au ni kweli lakini hii ndio Tanzania.
ReplyDeleteUkipata kazi basi boss lazima ajipatie chakula naye hapo. Na kwa ajili ajira ni haba basi mtu upo radhi kutoa kwa boss ilimradi tu ukeep ur job...Sad.....
Halafu hizo triangles ndio basi tena
Then hata mtu ukipima mara ya kwanza kabla hamjaanza kitu baada ya hapo bila uaminifu it is worthless.
Wanaitajika watu waliosomea mambo ya counseling wakati wa kupima huu ugonjwa.
Huku tuliko kuna college zina pima anonymous ila hiyo ni wewe kwa wewe majibu unayapata kwenye simu sasa hapo uwe unajiamini.
Ukiwa huna familly dr au hujawa referral ukaenda ER, state ninyoishi mwaka huu imeanzishwa kuwa ni lazima utapimwa Ukimwi pia upende usipende.
Ila kama umeamua tu kwenda kwenye blood work kupima ukimwi....mhhhhh....utaulizwa maswali mengi na pia wana watu walio specialize kwenye kueleza watu kuwa wana magonjwa yasiotibika au kutokana na terminal illness zao mtu amebakiza mwezi tu kuishi etc etc
Bongo nasisi tungeweka hizi ajira za kuprepare watu in anything.
Yaani ile kasumba ya kufichanafichana bongo bado ipo na ndio inatumaliza.
Na awareness ni bado kabisa. Huyo boss kama ni kweli anasema yeye hana lakini mkewe na huyu girlfriend wanao....Sio kweli...anao kabisa...ila vijidudu vyake vinahitaji screening nyingine. Kupima mara moja sio kuwa basi huna ukimwi....unatakiwa upime mara tatu....huyo boss ni career tu hapo
EHHHH MUNGU UTUREHEMU
Hiyo hadithi ilitumwa kwenye address yangu ya hotmail kama miezi minne iliyopita na kama sijakosea niliwafowardia washkaji zangu kina iceberg na scouser haw...
ReplyDeleteInshort hizo ni hadithi za jamaa flani anajiita Shy(Kameme) alikuwa anachat pale dhw, ndo maana kataja majina mengi ya chatters wa pale dhw lengo lake ni kama kuwachafulia majina.
Anachofanya ni ujinga na michuzi kabla ya kupost story kama hizi ungekuwa unafanya uchunguzi kwa sababu hapo umewachafulia watu sifa zao, usikubali watu waigeuze chat yako kijiwe kama ilivyokuwa utamu.
Na wewe Shy (Kameme) get life, kama Snickly alikuban dhw kuwa mpole tafuta chat zingine uendelee na maisha badala ya kuwapaka watu ambao zamani ulikuwa unachat nao kule.
Ni hayo tu.
Navy
Hii ndio hali halisi tuliyonayo. Na hatukomi, hatujifunzi. Hongera SHY
ReplyDeleteJipe moyo kwa kusema hii ni story ya uongo na ndelea kufanya ngono bila kinga uone, kuna sister wangu naye kaong'oka kwa umeme sembuse wewe.
ReplyDeletejamani waTz hatukomi kweli hii haya ndio mazingira ya ukweli tunayoishi lkn wengine wanona wameguswa sana cjui mpaka waseme ni uongo,ukweli huko plaepale jirekebishe,jieshimu utaeshimuka na kuepuka mengi,hasa haya machafu na kutesa jamaa zako pia kwa ugonjwa usio kuwa na kinga.
ReplyDeleteakhsanteni
huyu mgonjwa mahututi anawea kutype duuh..anywy hii story imetungwa na shy na hez hatin on iceberg and qudus...wote hawa wa dhw chat!!!tushakushtukia shy get a life niga!!!
ReplyDeletedahaaa sister kwanza pole sana kwa kupoteza maisha yako kwsbb ya maisha yako pili najipa pole mwenyewe kwanza kabla sijawapa pole uliotembea nao enzi za uzuri wako ila dada kusema kweli umetuuua wote kwasababu kama umetembea na watu 300 unafikiri katika 300 hao wanawapenzi wangapi?wangapi? dada angu mbona unaniliza bila kutegemea.samahani sana nahitaji kuonana na wewe kabla mungu hajakuchukua ili nikuone jinsi gani ulivyo email yangu ni ngatunga85@yahoo.com pole sana dada kwa hiyo hadithi ambayo na hisi wengi itakuwa imetuingia vilivyo kinachotakiwa ni kumuomba mungu hakurehamu pale utakapokuja kulala baada ya kufa.
ReplyDelete