ndugu, jamaa na marafiki wa watoto waliopoteza maisha siku ya iddi kwenye disko toto tabora nje ya hospitali ya kitete

HABARI tofauti zinaendelea kumiminika kuhusiana na mkasa mzito wa kupoteza watoto 19 kwa mpigo wakati wa disko mjini Tabora kwenye sikuku ya Idd.

Baadhi ya watoto walionusurika kifo katika ukumbi wa Bubbles Night Club siku ya Idd mosi ambako wenzao 19 walipoteza maisha, wamesema wanaamini ulevi wa baadhi yao ulisababisha janga hilo.

Watoto hao walisema pia kwamba tathmini yao inaonyesha kwamba waliokuwamo ndani ya ukumbi siku hiyo walikuwa kati ya 1,000 hadi hata 1,500.Uwezo wa ukumbi huo ambao ulijengwa kwa ajili ya mikutano ni kuhudumia watu wazima 150.

Mmoja wa watoto hao akizungumza kwenye maziko ya rafiki yake ambaye walikuwa naye disko siku hiyo, Said Sudy (12) alisema siku hiyo ya tukio, mabaunsa wa ukumbi huo walikuwa wakimlazimisha kila mtoto aliyekuwa anaingia ukumbini kununua pombe aina ya Simba Gin.

Polisi inaendelea kuwatafuta mabaunsa hao ambao walikimbia baada ya tukio hilo .
Kwa habari zaidi ingia

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. mmmmmmmmhhh wasije wakatwist hadithi ili walio na bishara wanusurike...hata kama haoa watoto walilazimishw akunywa pombe lakini hall la watu 150 kuingiza watu 1500 hata kama hunywi pombe I am sure utashindwa kupumua. Hapo wataanza kutafuta hao ma bouncer na kusahau hao wafanya biashara na tena kama ni wahindi ndio kabisa.....watalaumiwa wasio na hela

    ReplyDelete
  2. Tatizo tumeshalijua sasa.
    Idadi ya watu ilikuwa zaidi ya uwezo unaotakiwa maradufu.
    Sehemu ya kuchukua watu 150 ilishinikizwa hadi kubeba watoto 1500. Yaani watoto 1350 zaidi ya uwezo. Hii ndio sababu kubwa.
    Lets be clear hapo ni nani wa kufungwa au kuchunguzwa zaidi.
    Tumeyaona haya MV Bukoba - idadi kubwa ya watu na mizigo.
    Tunayoana katika rumande na selo zetu za polisi nchi nzima, kuweka watu wengi zaidi katika vyumba vidogo.
    Tunayaona haya katika mabasi ya daladala na malori. Kubeba watu na mizigo zaidi ya uwezo wake.
    Na yote kila siku ni ukimya tu mpaka yakutokea yatokee.
    Haya ya kunywa pombe pia tumeyaachia kisogo huku tukiona yakiendelea kwa muda mrefu sana.
    TZ hakuna umri maalum wa watu kutokunywa pombe maana utakuta watoto wako Bar na wazazi wao kila siku bila watu wa kusema hii sio haki/sheria.
    Utakuta watu wanakunywa pombe na watoto wa high school au shule za msingi Bar na hakuna wa kuhoji.
    Utakuta mhudumu anapeleka pombe katika chumba cha gesti huku akijua mle kuna watoto wa shule na hakuna wa kuhoji.
    sasa imefikia hatua hadi ya kulazimishana kununua Simba Gin katika disco la watoto tabora. Maana hakuna anayejali sheria au haki ya watoto.
    Serikali yenyewe imeshawanyang'anya viwanja vyao zamani na ikaviuza kwa mafisadi.
    Leo wanakuja kusema tutaliangalia hili sasa nani alisababisha.
    Aliyesababisha ni serikali kuu na ya tabora. Walishauza sehemu za watoto muda mrefu sana hadi kuwafanya wakose sehemu ya kwenda wakati wa siku kuuu.

    ReplyDelete
  3. kwa wanasheria...kujaza ukumbi zaidi ya kiwango ni kosa la jinai (criminal offence)?

    Mtawashitaki hao mabouncers for manslaughter, murder au nini?
    Mimi naona labda wazazi wafanye civil litigation tu...wabebe hela zao.
    Mimi sioni cha zaidi ya negligence(samahanini kwa kiingereza...nadhani kwa kiswahili ni ujinga...wadau kosoeni) hapa.
    Hapa mtu atakwambia mimi sijaua...watoto wenyewe wameingia club kwa hiari yao.
    Hao watoto hawakufanyiwa autopsy?

    ReplyDelete
  4. Nilikwambia wataanza kutupindisha pindisha.
    Nimesoma IPP , wamesema eti watu wa Biashara Tabora hawakutoa kibali cha disco katika huo ukumbi mwezi huu bali miezi mitatu nyuma.
    sasa wao hawahusiki ila hao mabaunsa na sio serikali ya manisipaa. Uongo mkubwa.
    Iweje ulikuwa ukitoa siku za nyuma na hukumwandikia memo ya kusema nimekunyima mwezi huu kwa kuwa unazidisha watu.
    Hao waliotoa kibali mwezi uliopita pia washitakiwe maana walihusika sio siku hiyo bali kuanzia mwanzo wa hilo tatizo,walihusika kulijenga na kulikuza.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...