Mheshimiwa Zitto Kabwe akichangia hoja katika mkutano wa Wabunge wa Afrika Mashariki unaofanyika mjini Kigali Rwanda, Kulia kwa Zitto ni Mheshimiwa Zuberi Maulid, Kiongozi wa Msafara
Wabunge wa Afrika Mashariki wapigiwe kura na Wananchi wote– Wabunge
Na Saidi Yakubu, Kigali, Rwanda
Wabunge wa Tanzania wametaka ubunge wa Afrika Mashariki uwe ni wa kupigiwa kura na wananchi wote ili kuongeza kasi ya uwajibikaji ya wabunge hao badala ya utaratibu wa sasa kuwa wabunge ndio wanaowapigia kura.

Maoni hayo ya Wabunge wa Tanzania yametolewa na Mwenyekiti wa Bunge la Tanzania Mhe. Zuberi Ali Maulid alipokuwa akitoa salamu za Tanzania katika mkutano wa mahusiano ya Mabunge ya Afrika Mashariki unaofanyika mjini hapa.

‘’Katika kipindi hiki ambacho Bunge la Afrika Mashariki limekuwa likitunga sheria zenye kuathiri Wananchi kwa ujumla na kwa kuwa Wabunge wa Jamhuri hawana fursa ya kujadili maamuzi ya Bunge hilo, ni vyema wabunge hawa wa Afrika Mashariki wakawa wanachaguliwa moja kwa moja na wananchi’’ alisema Mhe. Maulid.

Mheshimiwa Maulid aliongeza kuwa ni muhimu pia kwa Mkataba wa Afrika Mashariki na Sheria za Tanzania kurekebishwa ili kuruhusu Wabunge wa Bunge la Tanzania kujadili na kupitisha maamuzi ya Bunge la Afrika Mashariki, ‘’ Maamuzi wanayoyatoa yana athari kubwa kwa watanzania wote, hivyo ni vyema maamuzi yao kabla ya kutekelezwa yapate baraka za Bunge la Tanzania kwa kujadiliwa’’ aliongeza Mheshimiwa Maulid.

Rais wa Rwanda, Paul Kagame ambae pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa sasa akifungua mkutano huo alisema kuwa bado kuna vikwazo vidogo vidogo katika kufikia ushirikiano wa pamoja kutokana na hofu zisizokuwa na msingi.

‘’Katika kipindi ambacho mazungumzo ya kuwa pamoja zaidi yanasuasua ni vyama wananchi wakaelewa kuwa kwenye ushirikiano huwa siku zote kuna hasara za muda mfupi lakini faida zake ni za kudumu", alisema.

Katika mkutano huo, Tanzania inawakilishwa na Mheshimiwa Zuberi Maulid ambae ndio kiongozi wa msafara na wapo pia Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mheshimiwa Zitto Kabwe pamoja na Waheshimiwa Godfrey Zambi, Masolwa Cosmas, Beatrice Shelukindo, Ruth Msafiri na Hassan Kigwalilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. wazo suri. Ligistics zutawezekana?

    ReplyDelete
  2. Hizo hofu 'zisizokuwa na msingi' anazozingumzia Rais Kagame lazima zitafutiwe ufumbuzi haraka,zinafahamika.Wabunge kuchaguliwa na wanachi,kama alivyosema bwana Nalitolela hapo juu litakuwa gumu kidogo.Linahitaji uchambuzi na utafiti wa kina

    ReplyDelete
  3. Hey kaka ichuzi hebu tuambie nini kimetokea huko home. naamkaga na CNN news asubuhi. Sasa naona sijui watu/madancer wamekufa kwenye stampede Tanzania- ni nini hiyo mpaka CNN watangaze huku? Imenibidi nifungue block yako kabla sijaondoka lakini sioni lolote kuhusu hiyo habari ndio maana nimeona niulize

    Asante

    ReplyDelete
  4. KAKA MICHUZI INASIKITISHA SANA KUSIKIA KUMBI YA STAREHE IMESABABISHA VIFO VYA WATOTO KIUZEMBE TU.
    kUCHANGANYA WATOTO WA MIAKA MITANO NA 19 IS UNTHINKABLE.
    sOMEONE HAVE PAY FOR THIS .
    POLENI SANA WAFIWA.

    ReplyDelete
  5. Huyo aliyekusanya mikono shavuni ni MKAPA ama ni kitu gani?!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...