WATU wengine wawili wamekamatwa wakituhumiwa kuhusika na tukio lililosababisha vifo vya watoto 19 waliokufa wakati wanacheza muziki siku ya Idd Mosi.
Polisi imesema kuwa waliokamatwa ni Meneja wa disko la One Ten Teck Jaffar Rashid na Meneja wa Bubbles Night Club, Vituko Salala.
Kabla ya kukamatwa kwa mameneja hao, Polisi waliwakamata wamiliki wa madisko hayo ambao ni Projestus Fidelis na Shashikant Manji Patel.
Kwa mujibu wa vyombo vya dola watu hao ndio waliandaa disko la watoto katika siku hiyo ya Idd.Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Abeid Mwinyimsa, alisema leo kuwa wakurugenzi hao na mameneja wanashikiliwa na polisi kwa ajili ya kuhojiwa kuhusu chanzo cha tatizo lililosababisha watoto hao kupoteza maisha.
Alisema Polisi imempa taarifa rasmi ya kushikiliwa kwa watu hao, huku ikimuarifu kwamba walinzi wa milangoni katika madisko hayo mawili "Mabaunsa" nao wanasakwa ili waweze kuhojiwa kuhusu sakata hilo.Mkuu huyo wa Mkoa alisema wakurugenzi hao, watahojiwa pia na Tume huru iliyoundwa kwa ajili ya kuchunguza mkasa huo, ambayo alisema ilianza kazi jana na kuwataka wananchi waipe ushirikiano ili iweze kupata taarifa za ukweli zitakazofanyiwa kazi na serikali.
Majuzi watoto 19 walikufa na wengine kulazwa hospitali ya mkowa ya Kitete baada ya kukosa hewa katika kumbi za disko wakatik wa sherehe ya idd.
jamani au mie tu mbona hii habari haieleweki vizuri? wanatuma picha ya jengo mie sioni kubomoka kwa jengo kama walivyodai mwanzoni kuwa ndio kisa. Kingine nasoma hapa walikosa hewa inamaana walifunikwa na jengo au ilikuwaje? Ok ukumbi ulijaa yaani hao walinzi wanzembe kiasi gani hadi watoto 19 wafe bila kushtuka kwua sasa hakuna he wa ya kutosha hata kufngua madirisha ? jesus this is way to far uzembe 100%
ReplyDeleteKuna mambo mawili nadhani yalitokea.Watoto walikuwa wanavuta hewa kali ya kuwasha kooni(chocking,Irritating smell,watalaam wa kemia wanaweza kutusaidia gesi zenye tabia hiyo.Chanzo cha hiyo gesi hakijulikani.Kilichowaua wengi ni 'Stampede'baada ya kuhisi hewa hiyo na joto.Kiswahili kisicho rasmi STAMPEDE ni kama kukurupuka kwa kushtuliwa kama nyumbu vile na kukanyagana ili kuokoa maisha.Mungu azilaze mahala pema peponi roho za watoto hawa.Sikuwepo nimesoma kwenye internet na magazeti mbalimbali.
ReplyDeleteStampede, ambayo inatamkwa stam'peed, it is a noun for a wild headlong rush, or flight of frightened animals, like a sudden mass movement of people at a common impulse. wahispania wanaita estampida, wafaransa wanaita estapar, wajerumani wanaita stamfon A ikiwa na alama kama kofia na O pia ikiwa na alama kama kofia KIUJUMLA HILI NENO LINS ASILI YA NENO STAMP, ikiwa na maana watu au wanyama wakikimbia kwa nguvu na ghafla kwa vishindo, si lazima wakanyagane, lakini kutokana na hali halisi ni kuwa watu au wanyama kama wako wengi sehemu moja wakashitushwa na jambo na kwa pamoja zikawajia fahama za kukimbia kwa nguvu zao zote kueleke upande mmoja kuna uwezekano ya baadhi yao kuanguka chini na uwezekano mkubwa wa aliyeanguka kushindwa kuamka kwa wakati ni mkubwa basi watu watakaokuja nyuma yake watamstamp/watamkanyaka wote na watakapoishi atakuwa hoi bini tabaani na mara nyingi itakuwa ameshakufa. STAMPEDE YENYEWE HAINA MAANA YA KUKANYAGANA, NI KUKIMBIA KWA GHAFLA BAADA YA TUKIO LA KUTISHIA MAISHA, NA KATIKA HIYO PROCESS WATU WANAWEZA WAKATOKA SALAMA AMA WAKAFA, KWA MFANO MMO NDANI YA DISCO MLANGO NI MMOJA NA NYUMBA INAUNGUWA NI WAZI WATU WATAKWAMA MLANGONI, WENGI KUFA.
ReplyDeleteKwa kweli hii habari haieleweki na inatia donge fulani kwenye shingo.
ReplyDeleteWaandishi a habari hawajawa-interview watu waliokuwepo eneo la tukio? maelezo ya hao waliokuwepo itatupa mwanga kuelewa kilichotokea ni kipi, maana kukosa hewa mchana kweupee mtu atakosaje hewa? hewa ya bure mtu ataikosaje? yaani Tabora nzima hamna hewa? jamani mbona nikiangalia nje ya hilo jengo pale inaonekana kama vile hewa nyingi tu mpaka inamwagika?
Mimi nahisi tumelaaniwa jamani, kila kitu tunacho lakini tunakufa masikini, sasa mpaka watoto 19 wanakufa kwenye jengo eti wamekosa hewa? aise we acha tu.