Makamu Mwenyekiti wa chama cha FCM Alumni Ephraim Mafuru akichangia mada katika warsha ya siku moja iliyoandaliwa na waitimu wa chuo kikuu kitengo cha biashara kuhusu madhara ya kiuchumi yatakayoipata Tanzania kama yalivyotokea nchini marekani

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Nafurahi kwamba Tanzania pia tuko mbele katika kuchambua mambo yanayoikumba dunia ili kuongeza ufahamu na kujiandaa kukabiliana nayo. Pia niwapongeze wasomi wote waliofanikisha shughuli hiyo.
    Kwa mtazamo wangu ni kwamba uchumi wa nchi zilizoendelea unatawaliwa zaidi na masoko ya hisa na mitaji kitu ambacho kwa Tanzania bado tupo nyuma sana. Kwa nchi zilizoendelea asilimia kubwa ya shughuli za kiuchumi zinamilikiwa na Public companies kupitia masoko ya hisa tofauti na Tanzania ambapo shughuli nyingi za kiuchumi zinaendeshwa kifamilia au kirafiki.
    Nasema hivi kwa sababu msingi wa matatizo ya Marekani na wezake ni kupungua kwa makampuni yanayokubali kutoa mitaji katika soko la mitaji kama ilivyokuwa kipindi kifupi cha nyuma, kitu ambacho ndio msingi mkubwa wa uchumi wowote wa kibepari(capitalism) na hii ilichangiwa zaidi na taasisi za kibenki kuuziana "bonds / securities" ambazo hazikomboleki kutokana na wadaiwa kutokuwa na uwezo wa kulipa.
    Na kingine ni kwamba sehemu kubwa ya "bonds" hizi zilitokana na biashara ya nyumba "mortage" ambazo walipewa watu wasio na sifa stahili, hii ilitokana na tamaa za utajiri wa haraka na kukosa uhaminifu kwa waajiriwa wa taasisi husika.
    Kupungua kwa mitaji katika soko la mitaji kumesababisha biashara nyingi kufa, watu wengi kupoteza ajira zao na pia kuongeza idadi ya watu wanaoshindwa kulipia mikopo na madeni yao ya nyumba hivyo kasi ya ukuaji wa uchumi kupungua (recession)
    Nimalizie kwanza kwa kusema kuwa Tanzania kuathirika kwetu sana sana ni kupungua kwa misaada kutoka nchi zilizoendelea kutokana na matatizo yanayowakumba mabepari na ili tunaweza kulipunguza kwa kuongeza kasi ya kujitegemea katika bajeti yetu.
    Pili ni kupungua kwa watalii wanaokuja kutembelea vivutio vyetu kutokana na kupungua kwa mapato ya watalii hao katika nchi zao.
    Tatu ni kupungua kwa mauzo ya bidhaa zetu katika nchi hizi zenye matatizo ya kiuchumi kwa sasa na hii inaweza kupunguzwa kwa kufanya biashara na nchi nyingine za kiafrika au nchi kuongeza uhusiano na nchi ambazo hazijaathirika sana.
    na mwisho tatizo lingine kubwa ni kwa wale wachache wenye "vijisenti" vyao nje ya nchi na baadhi ya makampuni ya kitanzania ambao ama wamepoteza au wako njiani kupoteza kutokana na kufa kwa nyingi ya taasisi hizi za kifedha za nchi za magharibi.


    Mdau Sam - UK

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...