Kampuni ya simu za mkononi ya Zain Tanzania kesho alhamisi inatarajia kuchagua washindi wengine wa muda wa maongezi katika mfululizo wa draw zake za kila wiki za promosheni yake ya Endesha Ndoto 2.


Mkurugenzi wa Mauzo wa Zain Hebert Loius amesema wateja wapatao 1,101 wa Zain leo watajinyakulia muda wa maongezi wenye thamani ya Tshs 7.6m ambapo mtu mmoja atapata muda wa maongezi wa Tsh 100,000, wateja mia muda wa maongezi wa Tshs 25,000 na wateja wengine 1000 muda wa maongezi wa Tshs 5000.


Zain imeongeza draw za kila wiki katika promosheni yake ya Endesha Ndoto 2. Zawadi za awali katika programu hiyo ni simu za mkononi aina ya Blackberry na Nokia zinazotelewa kwa washindi wa Ndoto Points na magari aina ya RAV 4 pamoja na zawadi kubwa ya Land Cruizer itakayotolewa mwezi Desemba.
‘’ Tunaomba wateja wetu leo wasizime simu yao ili waweze kujishindia zawadi hizi za muda wa maongezi na kunufaika kwa kuwa sehemu ya familia ya Zain,’’ alisema Herbert.


Mkurugenzi huyo wa Zain amemsema zawadi hizo za muda wa maongezi ni utekelezaji wa matakwa ya wateja ambao waliomba zawadi ziongezwe katika promosheni ya Endesha Ndoto 2 ili watu wengi zaidi wanufaika.
‘’Siku zote Zain inawasikiliza wateja wetu ili kukidhi mahitaji yao na hilo ndilo limetufanya kuwa mtandao unaoongoza Tanzania.,’’ alisema na kuongeza kwamba Zain imezindua promosheni hiyo ya uaminifu ili kuwazawadia wateja wa Zain kwa kuwa katika mtandao wa Zain.


Hadi sasa Zain imetoa magari mapya aina ya RAV 4 sita. Gari la saba litakabidhiwa mwezi huu Mkoani Tabora. Zain itatoa jumla ya magari 11 mwaka huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...