Kampuni ya simu za mkononi ya Zain yenye mtandao katika nchi 22 Afrika na Mashariki ya Kati imewekeza dola za Marekani bilioni 10 sawa na trilioni 11.7 katika sekta ya mawasiliano Barani Afrika tangu 2005 na kuchangia kukua kwa kasi kwa sekta ya mawasiliano Barani Afrika, Mkurugenzi Mtendaji wa Zain, Khaled Muhtadi amesema.

Mkurugenzi Mtendaji wa Zain alikuwa akitoa Mada juu ya Umuhimu wa Mawasiliano kama sehemu ya Miundombinu ya Uchumi wa Tanzania
katika Mkutano wa Kwanza wa Wawekezaji na Serikali uliohudhuriwa pia na Rais Jakaya Kikwete.
Mkutano huo ulioandaliwa na The Economist na Kudhaminiwa na makampuni mbali mbali ikiwemi kampuni ya Zain Tanzania.

Mkurugenzi huyo wa Zain alisema ni jambo lisilopingika kwamba kukua kwa sekta ya mawasiliano Barani Afrika kumechangia kukua kwa uchumi wa Afrika. Alisema, kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Taasisi ya London ya Biashara ya Leonard Waverman of the London Business School, ongezeko la asilimia 10 ya usambazaji ma miundombinu ya mawasiliano katika nchi zilizoendelea kunachangia ongezeko la asilimia 1.2 katika ongezeko la pato la taifa.

Pia alisema tofauti na masoko yaliyofikia kikomu kifu ya Ulaya, Russia na Austaralia, masoko yanayoendelea kama China, India, na Afrika yako katika hatua ya awali ya maendeleo na yataendelea kukua kwa kasi katika miaka ijayo.

Mkurugenzi wa Zain aliipongeza serikali kwa sera nzuri ya uchumi ambayo imeifanya Tanzania kupiga hatua kubwa ya kiuchumi. Pia alisema kwa watani kasi ya kuongezeka kwa pato la taifa katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita imezidi asilimia saba, na mfumuko wa bei uko kwenye tarakimu moja.

‘’Juhudi zako hapa Tanzania na nchi za jirani zinaifanya Tanzania kuwa nchi ya Amani na utulivu barani Africa, hongera sana,’’ alsiema na kuongeza kuwa mambo hayo yamefanya sekta ya mawasiliano, benki, madini na utalii kukua kwa kasi.

Katika Mkutani huo Rais Kikwete aliipongeza sekta ya mawasiliano. Zain inawateja milioni 50 katika nchi 22, 16 zikiwa katika bara la Afrika. Lengo la Zain ni kuwa moja kati ya makapnuni 10 ya simu za mkononi yanayoongoza ifikapo 2011 ikiwa na wateja 150 milioni.

‘’ Zain Tanzania iliingia katika Soko la Tanzania 2001, na imekua kwa kasi na kuwa kampuni inayoongeza kwa kusambaa zaidi nchini na kwa mauzo ya vocha za muda wa maongezi. Kukua kwa Zain kumechochea kukua kwa sekta binafsi na ya umma Tanzania,’’ alisema Muhtadi na kuongeza kwamba tangu 2005, Zain Tanzania imewekeza zaidi ya dola za Marekani 442 million katika miundombinu ya mawasiliano ya simu za mkononi.

Mapato kutoka Zain kwenda katika sekta binafsi ikiwemo usambazaji, wauzaji wa reja reja na matangazo yameongezeka na kufika Dola za Marekani 114 million US dollars 2008.
Mapato ya serikali kutoka Zain yanayotokana na Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) pamoja na kodi mbali mbali yameongezeka kutoka dola za marekani milioni 22.33 million mwaka 2002 na kufikia dola za Marekani 40.82 million mwaka 2008, aliongeza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. hii hadithi sithani kama inaukweli ndani yake sasa hivi dunia nzima hakuna pesa

    ReplyDelete
  2. Ok, ni sawa lakini gharama za simu nchini Tanzania kwa haya makampuni bado ni kubwa mno. Mheshimiwa balozi, kwa kweli nitawaona hao Zain wamaana kama watapunguza gharama za simu, ila kwa mtindo huu wa kutupatia mahesabu bado sijawaelewa, sio siri.

    ReplyDelete
  3. Anon wa kwanza hapo juu inaelekea unasikiliza sana CNN, BBC, etc.

    Kitu kimoja unapaswa kujua kuhusu vyombo vya habari ni kwamba vinapenda kukuza mambo ili kuvutia watazamaji.

    Pesa ipo, dunia sio Marekani peke yake.

    - China pesa iko (mauzo ya bidhaa kwa dunia nzima)
    - Middle East pesa iko (mauzo ya mafuta)
    - Russia pesa iko (mauzo ya mafuta, gesi, madini, silaha, etc)
    - Na Afrika pesa iko (waulize wazee wa EPA na RADAR watakwambia, au Mugabe anayeagiza meli ya silaha wakati CNN inasema uchumi wake umedorora)

    Na hata Marekani pesa iko tena kibao tu. Kuna raia wala hawajui Fannie Mae na FreddieMac ndio wadudu gani.

    //Mdau

    ReplyDelete
  4. Uncle Michu una hakika ni dola bilioni 10,yaani $10,000,000,000? That's a fortune!

    ReplyDelete
  5. Mdau wa October 09, 2008 1:27 AM

    $10,000,000,000 katika NCHI 22, TANGU 2005.

    Hiyo ni wastani wa $151,515,151 kwa mwaka kwa kila nchi.

    Sio hela ya kutisha sana kwa Kampuni kubwa kama Celtel/Zain, au sio?

    //Mdau

    ReplyDelete
  6. Eti pesa ipo, CHINA wanauza bidhaa nje, Russia wanauza mafuta, madini na silaha, Waarabu wanauza mafuta, Africa EPA nakadhalika, kweli huko ni kutokuelewa dunia inaendaje, hivi unadhani soko la CHINA liko wapi kama si Western countries, ikiwemo USA na UK bidhaa zaidi ya asilimia 80 za CHINA zinategemea western market, Russia pia anategemea kuuza mafuta na gas yake to Western countries, na hivi unajuwa kuwa budget za nchi nyingi za Africa more than 50% ni misaada inayotoka western countries, hivi pia una habari kuwa ZAIN hukopa toka Banks kufanya biashara yao, na mabenki mengi ya hapa duniani ni ya western countries na karibu benki zote zina hali mbaya. There ar two ways of rising capital when you do business, one by selling your shares if the company is plc or getting loans from outsiders, you show them in your balance sheet as bonds, that are debts in te form of IOUs sasa kama hao wa kuwakopa wanashida na pesa unadhani utapata wapi pesa za biashara, it is a matter of time and days hii hali mbaya ya pesa tuta-ifeel Africa and it gonna be worse that ever.

    ReplyDelete
  7. Anon wa October 09, 2008 6:18 AM

    Kwa hiyo na wewe huamini kwamba Zain wanaweza kuwa na mapesa kiivyo?

    Anyway hayo ni mapesa ya toka 2005, kwa hiyo hakuna haja ya kubishana ni mambo yaliyopita.

    Tungoje taarifa yao ya Mwakani ambapo tutaona waliperform vipi during the credit crunch.

    //DM

    ReplyDelete
  8. Ndugu Anon unayedhani Middle East choka mbaya hebu sikia maneno hii:

    http://news.airwise.com/story/view/1223307298.html

    Poleni wadau wa US. Mumelikoroga lazima mulinywe. Na tunataka Iraq muijenge kama mlivyoikuta kabla ya utaahira wenu.

    Eti Obama anashangaa serikali yake kutumia bilioni kumi kwa mwezi wakati serikali ya Iraq in bilioni 70 kwenye akaunti.

    Kwani Iraq iliwaiteni kuja kufanya utaahira wenu? Hela zetu mnazitakia nini?

    ReplyDelete
  9. That's a lie... Jamani hata hao wahindi wanatudanganya>>>>>
    10 billion dolllars?? Even Tanzania entire budget is less than that..
    Alafu watatumia hizo hela kwa nini?? Kutibu malaria? Kununua vitabu???
    10 billion shillings.. let's get it right

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...