Hi Bro.Michu. Habari za majukumu, pia ninawasalimu sana wapenzi na mashabiki wote wa blog hii ya jamii, natumaini wote wazima wa afya njema na mkifurahia ushindi wa Obama.
Msaada tutani kwa jambo hili: Naomba misemo au methali 12 ya kiswahili ihusuyo watoto, anae jua naomba anisaidie tafadhali.
Asanteni sana kama mtaweza kunisaidia kwa hili.
Ninawasalimu sanaaaa...!!!
Kila lakheri kwa yote!
B.F.CHIBIRITI.
Sasa Chibiriti umepata Tenda ya kufundisha Methali huko una maanisha unataka kufanya ufisadi kwa kutumia vichwa vya watu, yaani kujipatia pesa kwa wazungu kwa kuutuuliza maswali mmh hujambo hapo~! nakupa njia moja wasiliana na baraza la kiswahili hao wana methali na vitendawili vingi sanaa watakutumia maana hao nia yao ni kusambaza kiswahili.
ReplyDeleteMdau south Korea
1. Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo
ReplyDelete2. Mtoto wa nyoka ni nyoka
3.
1.Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo
ReplyDelete2. Mchelea mwana kulia hulia yeye
4 Samaki mkunje angali mbichi
5 Asofunzwa na mamaye hufunzwa na walimwengu
6 Asie sikia la mkuu huvunjika guu
7 Mchuma janga hula na wakwao
8 Mtoto kwa wazazi hakui
9 Nyota njema huonekana alfajir
10 Uchungu wa mwana aujuae mzazi
11 Mtoto wa nyoka ni nyoka
12 Mtoto akililia wembe mpe, ukimkata shauri yake.
BONUS: Mtoto wa mwenzio ni mkubwa mwenzio, usione soo mpe somo...!
Asofunzwaa na mamaye hufunzwa na ulimwengu.
ReplyDeleteMwana umleavyo ndivyo akuavyo.
Mtoto wa nyoka ni nyoka.
1. Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo. Kama wewe Chibiriti!
ReplyDelete2. Mtoto akililia wembe mpe.
3. Mtoto asipochafuka atajuaje..!!?
4. Mtoto Mkaidi hafaidi mpaka siku ya Idd
5. Mtoto akijamba ujue kashiba
5.......wengine...
mtoto akililia wembe mpe umkate.
ReplyDeletemwanga mpe mtoto kulea.
mwana wa ndugu kirungu.
1. DUNIA NI WATOTO.
ReplyDelete2. ASIYE NA MTOTO NA ABEBE JIWE.
3. RAHA YA DUNIA NI WATOTO.
mtoto umleavyo, ndivyo akuavyo
ReplyDeletemtoto akililia wembe mpe
mtoto mkaidi hafaidi mpaka siku ya idd
mtoto si nguo ukaomba mtu
mtoto wa nyoka ni nyoka
usipoziba ufa, toto iko chungulia
by nana
czech republic
1. Ngoma ya kitoto haikeshi...
ReplyDelete2. Mtoto halali na fedha bali na kinyesi
1)MTOTO HALAZIMISHWI KULA ANALAZIMISHWA KUSOMA
ReplyDeleteSIMBA MWENDA POLE KAFUNGWA SPEED GAVANA
UKITAKA CHA MVUNGU FUNUA MATANDA CHUKUA
HABA NA HABA TAHAMAKI NAKWISHA
MWANA MTEMBEZI HULA MIGUU YAKE
Jamani muoneneeni chibiriti huruma. waonsha vinywa hamna dogo? Chbiriti anale watoto. anafanya kazi kwenye day care, kwa hiyo anapaswa kuwafundisha watoto lugha tofauti ili wawe bi-lingual
ReplyDeletehongera kaka chibiriti
Esther Mswalu ---- Rome.
1. Wimbo mbaya haimbiwi mtoto
ReplyDelete2. mchawi mpe mtoto amlee.
3. mtoto alilia wembe mpe umkate
4. mkono mmoja haulei mwana
5.mwana mkaidi hafaidi hadi siku ya idi
6.mwana mkuwanawe ni mwenzio
7.kulea mwana si lelemama
8.kulea mimba si kazi kazi kulea mtoto
9.mwana wa kuku hafunzi kuchakura
10. mwana wa mtu ni kizushi akizuka zukanae.
11.mwana maji wa kwale kufa maji mazoea.
12ucheshi wa mtoto ni anga la nyumba.
wako mdau
james
Holland
1.Gemu la Yanga na Simba mtoto hatumwi soda dukani kwani atabaki hukohuko
ReplyDelete2. Usicheke kundu la nyani kwani lako hulioni.
3. Shetani kampanda jini.
4.
Chibiriti hii methali Maalum inafundisha subira na kusamehe kama mzazi kwa mtoto na wengine wanaokuhusu kwa UKARIBU MNO--- MTOTO AKINYEA MKONO HUUKATI UKAUTUPA---Unajisafisha maisha yanaenda.
ReplyDeleteusa
Mtoto si Nguo kwamba utainunua.
ReplyDeleteIt takes the whole village to raise a child
ReplyDeleteThe first half of our lives is ruined by our parents, and the second half by our children.
A child educated only at school is an uneducated child
Children are umpredictable
It is a wise father that knows his own child.
Children are like fruits they are sweetest just before they turn bad
1. Mtoto wa mwenzako ni mkubwa mwenzio. Unaweza kumla tu.
ReplyDeleteWe mdau wa soth Korea hauna jipya. Mpe methali mwenzako. Siyo mpaka aende baraza la kiswahili. tema cheche kama unajua issue. vinginevyo ushauri wako ni potofu.
ReplyDelete"MTOTO WA MWENZIO KIZUKA AKIZUKA
ReplyDeleteZUKA NAE"
jamani wadau mmesahau...........
ReplyDeleteheri ya paka kukamata panya kuliko mtoto wa kambo vitendo anavyofanaya.
Mwana wa mwenzio mbebe kalala akiamka si wako.
ReplyDeleteTeke la kuku halimuumizi mwanawe.
Dubai.
Ukali wa simba lakini anazaa.
ReplyDeleteUnanunua mbeleko na mwana hajazaliwa.
Dubai.
chelewa chelewa utakuta mtoto si wako.
ReplyDeleteDUUH KUMBE HOLLAND KUNA WASWAHILI. INGEKUWA MASHINDANO MDAU WA HOLLAND KASHINDA NA FIKIRI ALIWAKUWA NA MBARUKU KTK KIPINDI CHA MINU ZA KISWAHILI AU KWAO NI MSA
ReplyDeleteMDAU WAKO
KISIJU PWANI
Asanteni sana wadau, kwa msaada wenu.Nimefurahi sana.
ReplyDelete