Mashindano hayo yaliyoandaliwa na klabu ya Scorpion Shotokan Karate Club kupitia mwavuli wa Japan Karate Association (Tanzania) yalishirikisha zaidi ya watoto 50, wakiwemo wasichana watano ambao walishindana katika mtindo wa Kata na Kihon Kumite.
Mkufunzi mkuu wa klabu ya Scorpion, Sensei Jerome George, alisema jijini jana kwamba, klabu hizo za Iringa na Genesis zilifanya vizuri katika mashindano hayo yaliyoshirikisha watoto wa kuanzia miaka 7 hadi 15.
Kwa upande wa Kata, katika kundi la watoto wa umri wa miaka 7-9, Ally Bahati Kassim kutoka klabu ya Nyuki Shotokan ya jijini ndiye aliyeibuka mshindi, wakati nafasi ya pili ilikwenda kwa Husaim Said (Fitness 1), Ayubu Tamba (Iringa) akishinda nafasi ya tatu, Sergio Kisaka (Genesis) nafasi ya nne, David Mgondo (Genesis) nafasi ya tano, na Elisha Mtega (Genesis) nafasi ya sita.
Katika kundi la miaka 10-12, Said Salum wa Iringa aliibuka mshindi na kuwaacha Ally Jumbe (Iringa), Anwar Hillal (Fitness 1), Babu Sudi (Iringa), Said Said (Fitness 1), na Brian Yegela (Genesis).
Aidha, kwa kundi la miaka 13-15, Elias Alfred wa Iringa alishinda na kuwaacha Ahmed Nassoro, Tonny Kambo, Mohammed Mdota na Hudhaifa Daudi wote wa Iringa, pamoja na Mohammed Said wa Fitness 1.
Helia Talebi kutoka klabu ya Fitness 1 alishinda katika Kata kwa upande wa wasichana, akiwaacha Kulthum Selemani (Iringa), Sana Ishak (Fitness 1), Marise Hopkins (Fitness 1), na Michelle Hopkins (Fitness 1).
Aidha, kwa upande wa wa Kihon Gohon Kumite, Ally Bahati Kassim kutoka Nyuki Shotokan alishinda tena kundi la watoto wa umri wa miaka 7-9, akifuatiwa na Nadir Abdallah (Genesis), Tawana Mbaya (Genesis), Elisha Mtega (Genesis), Suheil Ishak (Fitness 1), na Gerald Rwehumbiza (Fitness 1).
Kwa kundi la miaka 10-12, Ismail Juma kutoka Iringa alishinda akifuatiwa na Brian Yegela (Genesis), Michael Shayo (Genesis), Said Salum (Iringa), Ebrahim Haiderbhai (Scorpion) na Ally Jumbe (Iringa).
Kwa upande wa miaka 13-15 Iringa walitamba na kushika nafasi zote tano za juu, ambapo mshindi alikuwa Elias Alfred akifuatiwa na nduguye Raymond Alfred, Ahmed Nassoro, Tonny Kambo na Mohammed Mdota, wakati Mohammed Said wa Fitness 1 alishika nafasi ya sita.
Helia Talebi wa Fitness 1 alishinda pia upande wa Kumite kwa wasichana akifuatiwa na Marise Hopkins, Sana Ishak na Michelle Hopkins wote wa Fitness 1, wakati Kulthum Selemani wa Iringa alishika nafasi ya tano.
Washindi wa kwanza mpaka wa tatu walipata vikombe, wakati washindi wa nne hadi wa sita walipata medali, huku washiriki wote wakipatiwa pia vyeti.
Mgeni rasmi katika mashindano hayo, Nicholas Bulamile aliyemwakilisha Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo nchini Leonard Thadeo, aliwapongeza washindi hao na kuhimiza wazazi na jamii kuunga mkono juhudi za kuendeleza mchezo huo ambao unazingatia zaidi nidhamu.
"Karate inahimiza zaidi nidhamu, na zaidi huu ni mchezo kama ilivyo mingine, hivyo serikali na jamii vinapaswa kuungana pamoja kuunga mkono juhudi zinazofanywa na watu kama Scorpion ili kuinua mchezo huu. Naamini tunaweza kupata wawakilishi wazuri wa taifa hili wakatuletea sifa," alisema.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...