Mwasisi wa mziki wa reggae nchini Tanzania Jah Kimbute,atapanda jukwaani mjini Tempere,Finland,siku ya tarehe 7 February 2009 katika onyesho kubwa la aina yakeAfrica winter Jam festival.
Mwanamziki huyo nyota wa reggae Jah Kimbute pia atakuwa na ziara ya kikazi barani ulaya kuanzia February 2009.
Mwaandaaji wa onyesho hilo Bwana Mernard Mponda, amezitaja bendi zingine zitakazo shiriki onyesho hilo ni bendi maarufu barani ulaya The Ngoma Africa Band inayoongozwa na mwanamziki nyota Ebrahim Makunja aka ras Makunja yenye makao yake nchini ujerumani.
Pia Mwanamziki Lulu ya Tanzania Bi.Tabia Mwanjelwa ambaye kwa miaka mingi amekuwa kimya ataibuka katika katika onyesho hilo kwa kasi mpya!!!!!
Bendi ya Ngoma africa itawasili Tempere, Finland kwa kazi moja tu ya kuwatia kiwewe na kuwadatisha akili washabiki.
Jah Kimbute naye atatoa burudani ya aina yake kama walivyo mzoea washabiki wa scandinavia kwani sio mara ya kwanza kwa mwasisi huyo wa reggae kutumbuiza katika nchi hizo.
Tabia Mwanjelwa mwanadada wa Tanzania mwenye sauti ya kumtoa nyoka pangoni na kuleta mafuriko ya washabiki amehaidi kutoa burudani ya aina yake
Wadau Finland kaeni mkao wa kula.
Habari ndiyo hiyo...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

 1. INANIKUMBUSHA KIMBUTE ALIPOMPONDA LUCKY DUBE KUWA HAJUI MUZIKI WAKATI LUCKY ALIPOFANYA ZIARA TANZANIA MIAKA YA TISINI. KISA, ALINYIMWA TIKITI YA KUINGIA KWENYE ONESHO BURE!

  ReplyDelete
 2. aaaah..aaaa sina mbavu.

  Hawa waandaaji wa Finland mbona HAMCHOKI.

  RAY 2007 ikawa longo longo

  JHIKOMAN 2008 Feb akiwa longo longo.

  MATONYA Oktoba2008 LONGO LONGO...

  haya sasa mnaamua kuchafua tena majina ya wasanii wengine..eti Ngoma afrika....kama watoto wadogo wamewashinda kuwapeleka finland mtaweza kumpelekea tabia.  MI NILISHA APA SITAUZURIA HATA MARA MOJA MAONYESHO HEWA.

  ETI WATU WAKAE MKAO WA KULA?SEMENI WATU WAKAE MKAO WA KULIWA PESA ZAO....

  ACHENI USANII JAMANIIII HAMCHOKI NYIE TAMPERE..SALAAAM NYINGI KWA JOJI MATOVU AMBAYE NI MSAIDIZI WA MPONDA...

  SAFARI HII MTAWAONA WATU WATAMPERE TU KWENYE HIZO SHOW ZA KISANII..HATUJI NG'OOOOOOOOOOOOOOOO MPAKA MJFUNZEE KUWA WASTAARAAABU..NYIE WATU WAZIMA HIVYOOO AU HAMJUI ILO?

  UJUMBE UMEFIKA HATA KAMA UKIBANA MICHUZI

  ReplyDelete
 3. Waswahili nao! Anon wa December 01, 2008 2:51 PM hapa siyo mahali muafaka kutoa malalamiko yako hayo ambayo yanayoonyesha chuki binafsi. Kuandaa maonyesho au onyesho siyo rahisi kama unavyofikiria na hutokea sehemu nyingi tu watu kushindwa kufanikiwa. Kama mafanikio Mponda ameonyesha kwa kufanya na kuandaa matamasha yaliyofanikiwa, kushindwa kufika kwa hao walioshindwa inaweza kuwa nje ya uwezo wa waandaaji. Kwa nza inaonekana uko huko huko Finland maana uantaka au umesema hutohudhuria basi na wewe andaa tamasha lako! Big up Mponda, waosha vinywa hawakosekani humu.- Kippä, Malmö

  ReplyDelete
 4. "Hawa waandaaji wa Finland mbona HAMCHOKI.

  RAY 2007 ikawa longo longo

  JHIKOMAN 2008 Feb akiwa longo longo.

  MATONYA Oktoba2008 LONGO LONGO...

  haya sasa mnaamua kuchafua tena majina ya wasanii wengine..eti Ngoma afrika....kama watoto wadogo wamewashinda kuwapeleka finland mtaweza kumpelekea tabia.  MI NILISHA APA SITAUZURIA HATA MARA MOJA MAONYESHO HEWA.

  ETI WATU WAKAE MKAO WA KULA?SEMENI WATU WAKAE MKAO WA KULIWA PESA ZAO....

  ACHENI USANII JAMANIIII HAMCHOKI NYIE TAMPERE..SALAAAM NYINGI KWA JOJI MATOVU AMBAYE NI MSAIDIZI WA MPONDA...

  SAFARI HII MTAWAONA WATU WATAMPERE TU KWENYE HIZO SHOW ZA KISANII..HATUJI NG'OOOOOOOOOOOOOOOO MPAKA MJFUNZEE KUWA WASTAARAAABU..NYIE WATU WAZIMA HIVYOOO AU HAMJUI ILO?

  UJUMBE UMEFIKA HATA KAMA UKIBANA MICHUZI

  December 01, 2008 2:51 PM"

  Kwa kuwa uko Ufini basi uwe unasomaga na habari kutoka Ufini pia. Pata uhondo hapa utajua nini maana ya kuandaa shughuli http://www.hs.fi/kulttuuri/artikkeli/Elton+John+perui+Helsingin+konserttinsa/1135241566742
  Kwa ufupi Elton John ameahirisha onyesho lake la leo usiku pale Helsinki. Longolongo nayo??

  ReplyDelete
 5. Hii! Jah Kimbute naona unaanza na moto mpya wa kiaina yake!
  Lakini kazi unayo! hao unapapanishwa nao Ngoma Afrika! Kazi unayo jamaa hawana mchezo katika libeneke

  ReplyDelete
 6. We anon dec 01,2008 2.15 PM. Acha mambo ya kishamba unaonekana kabisa una chuki binafsi na hawa jamaa.Kwanza hata jina la huyo mwandaaji mwengine hujui kuandika eti JOJI chukua darasa jina linaandikwa GEORGE rudia kuandika mara mia mpaka uzoee.
  Hawa jamaa wameandaa matamasha mengi ambayo yamekuwa gumzo kila mara kwa njisi yalivyofana.
  Nawaunga mkono kwani kwenye maandalizi kam haya lolote laweza kutokea.Hiyo Ya Matonya mbona show zake nyingine zilibidi kufutwa!!!!
  Bwana Mponda Na Matovu endelezeni libeneke la kutuletea maraha kwani ni wachache wanaoweza kufanya hayo na yakafanikiwa achaneni na hao wapika majungu, sisi tuko nyuma yenu an hlk tutakuja wengi tu, huyu mwenye roho ya kwanini yuko pekee yake.

  ReplyDelete
 7. Anon 01,dec 2008 2.51 Sidhani hata shughuli yako ya kuzaliwa unaweza kuandaa. Acha fitna, watu wote wamekupiga dongo. mliokuwa Finland kwa kweli kaeni mkao wa kula kwani hao Ngoma Afrika sio mchezo plus nguvu nyingine kutuka kwa Jah Kimbute, nawaonea wivu. Poa tu wakati wenu huu

  ReplyDelete
 8. MNYONGE MYONGENI HAKI YAKE MPENI.

  Waandaaji wanajitahidi sana kuhakikisha mambo yanakwenda sawa achilia mbali wakati mwingine mambo yanakuwa nje ya uwezo wao.


  Ukichukulia karibu wasanii ambao mdau kawataji walikuwa ni wasanii wa "KUONGEZA SHAVU".Ila wakamuaji wenyewe wanafanya vema siku zote.

  Tuwe wepesi kukumbuka na MAZURI pia.Nina hofu kama mdau hapo juu kama kweli ni muhudhuriaji wa matamasha.

  Mbona ujaelezea kuhusu Spice Ndombolo,Momocat....

  Tuunganishe jitihada zetu kunyanya WASANII wa nyumbani na muziki wetu.

  Waandaaji msivunjike moyo..Tupo pamoja ..

  TUTAFIKA TU

  ReplyDelete
 9. NIMEONA NI HERI NICHANGIE LANGU:
  Ndugu yangu sijui nikuite jina Anon Dec1 2.15 naomba ujue kila jambo lina mapungufu yake.Kwenye kuandaa tamasha mambo mengi yanaweza kutokea tena dakika ya mwisho na usiwezi kufanya lolote hata kama una mamilioni. utamlipa msanii advance yake, utamnunulia ticket, utamlipia hotel n.k lakini litafika tatizo kama msanii kujieleza kwa uhamiaji, status yaken.k mambo kama haya huwa yanatokea na usiwezi kuyatatua hata kama una fedha kiasi gani Authority wakisema NO ni NO. Naona umeorothesha kila msanii mabye ameshidwa kufika Finland, lakini je unajua ni kwa sababu gani!!?? sababu ziko wazi.
  Jhikomani Katumbiza Finland mara mbili mara ya tatu ikashindikana, Ray C dau likapanda zaidi ya makubaliano. na ili kumbunguza makali ya gharama za kuleta wasanii ndio Waandaaji huwa wanashikiana na kufanya TOUR.Kwa kweli Matamasha mengi yamekuwa mazuri kasoro zipo na uwezi kumridhisha kila mtu, kwa hilo mtusamehe.
  Lakini hujui sio kazi rahisi na kuingia hsara ili kuwaridhisha Wateja ni asilimia 80%.
  Yote haya inatokana na baadhi yetu kutoona umuhimu wa kulipa Mlangoni lakini wakienda kwenye matamasha ya wazungu wana uwezo wa kilipa Euro 50-100 wakati huku ni Euro 8 na utakuta kuna show zaidi ya 4 na Dj 3.
  Sina mengi samahani kama nimemkweza Mtu.
  N:B Na jina langu ni George sio JOJI :)
  George Matovu.

  ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...