Super model Sasha(Cutie Malisa) ni mrembo aliekuwa kileleni mwa mafanikio,nafasi ambayo kila mschana wa leo angependa kuwa nayo.

Pressure ya kazi pamoja na kutojiamini kunampelekea Sasha ajiingize katika utumiaji wa madawa ya kulevya hatimae mrembo Sasha anapoteza kila alicho kijali na kukipenda vikiwemo mumewe mpenzi Brian(Tito Zimbwe) ajira yake ya uanamitindo ambayo ndiyo iliyo muweka mjini Dar es salaam katika maisha ya kifahari na kumpatia umaarufu mkubwa.

Baada ya kukataa ukweli kwa muda mrefu Sasha anabaini kwa rafiki yake mpenzi Gabriella (Chuchu Hans) kama ameathirika na madawa ya kulevya na kukata tama ya maisha baada ya kukiri kuwa alijaribu kwa muda mrefu na kushindwa kuachana na tabia hiyo.

Jee Gabriella atachukua uamuzi gani kunusuru maisha ya Sasha? Ujio wa Mudrik(Khalfan Ahmed”Kelvin”) utabadilisha vipi muelekeo wa maisha ya Sasha?

Nini kitamfanya Sasha atambue kama umaarufu na urembo ni vitu vya kupita? Nini jamii itajifunza toka kwa mlimbwende Sasha?

KWA MAJIBU HAYO NA MENGINE MENGI JIPATIE NAKALA YAKO HALISI
FILAMU INA SUBTITTLES KATIKA LUGHA ZA
ENGLISH
FRENCH
ARABIC
PORTUGUESE
KWA WATEJA WA TANZANIA FILAM ZINAPATIKANA KATIKA MADUKA
YOTE YA FILAMU.
kwa wadau watakaopenda kununua wasiliana na
+447971224493

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. does anyone know kama hizi movies za tanzania zinapatikana hapa marekani? if yes please let us know...it will nice to support our actors

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...