JK akiinamisha kichwa kwa masikitiko wakati alipopata habari ya kifo cha mbunge wa jimbo la Mbeya vijijini Mheshimiwa Richard Nyaulawa kilichotokea jijini Dar Es Salaam usiku wa kuamkia leo. Tangazo la kifo cha mbunge huyo lilitolewa na Naibu katibu mkuu wa CCM Bara George Mkuchika wakati wa kikao cha Halmashauri kuu ya CCM kilkicchofanyika mjini Dodoma leo.Mipango ya Mazishi ya Mbunge huyo inafanyika Nyumbani Kwake Kawe jijini Dar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Ni kipigo kikubwa:

    Moja, tumempoteza m-Tanzania mwenzetu!

    Mbili, alikuwa m-Bunge. Kaacha nafasi ya kugombaniwa...and of all the places, Mbeya Vijijini, kwenye waliko wavurumisha mawe! Sijui, itakuwa kama Tarime?

    Ni lazima JK ainamishe kichwa kwa hayo mawili!

    ReplyDelete
  2. Poleni familia, ila picha ya JK ina mambo mengi.... one anaweza kuwa anamlilia Nyaulawa.... mbili anawaza uchaguzi mdogo..... tatu .......Mungu aiweke roho ya marehemu pahala pema peponi

    ReplyDelete
  3. Kuna mengi yanamliza huyo JK, unazani raha atapata wapi wakati kati ya wezi wa pesa za EPA alikuwa nao bega kwa bega na pesa zao na mikono yao yenye dhambi ameipokea.
    Mungu amlaze marehemu mahali pema peponi na yeye pekee ndiye mwenye uwezo wa kujaji na kuhukumu . Basi tuzidi kumuombea heri roho yake ikapumzike kwa amani.

    ReplyDelete
  4. Eti magazeti yanaandika hakuwa na makundi. Mbona hayatuambii nani wenye makundi? Sifa za Marehemu bwana

    ReplyDelete
  5. Huyu jamaa ndio alikuwa mwanzilishi na mmiliki wa magazeti ya majira na modern newspaper printers, na rafiki yake Mohamed Mbughuni. Ni siku nyingi tu alikuwa na ngoma, hata kabla ya kuingia kwenye siasa, huku kwenye jimbo tulikuwa tunamhesabia siku tuu tufanye uchaguzi wetu mdogo!!!

    ReplyDelete
  6. Lazima kichwa kimuume sana, kwani CHADEMA ni lazima wachukue hicho kiti cha Ubunge kwani wao CCM bado wanahangaika kujisafisha na kashfa zao za Ufisadi.

    ReplyDelete
  7. Whats the problem with our CCM Vice Chairman,Msekwa?He looks Dehydrated from the look of his eyes?Working Too Hard for the elections?Or busy postulating some other new socialist ideals that could transform this battered peasant economy into An Economic PowerHouse of the 22nd Century?

    ReplyDelete
  8. Tarime somo kubwa sana kwa CCM 2010. JK lazima asikitike mno akizingatia mawe alirushiwa yeye kama mwenyekiti, itakuwaje wakienda vibabu viwili (Makamba na Msekwa).Patamu hapo.
    Wafiwa poleni.

    ReplyDelete
  9. JK anafikiri jinsi atakavyo mfikisha shemeji yake rostam mahakamani.....Balozi Mithupu umesikia MAMA AFRIKA MARIAM MAKEBA AMEFARIKI?? TUPE MINYUUUZ bwana hizi habari za mafisadi wetu tumeishazizowea.

    ReplyDelete
  10. kila binadamu yeyote hata mchawi ukipata habari za msiba za mtu wako wa karibu au mfanyakazi wako lazima upate mshangao tumeumbwa na kifo lakini hakuna mtu anayemuombea mwenzake aende huko kwahio kwa Rais wetu kupata uchungu ni kitu cha kawaida kwa binadamu yeyote yule anaye jali maisha ya wezake hapa kama angesikia mbunge wa upinzani kafariki angepata mshtuko sawa kabisa inaelekea Rais wetu anaupendo wa kibinadamu mungu aiweke mahali pema roho ya marehemu Amin

    ReplyDelete
  11. R.I.P

    Hapo raisi anaonyesha hata yeye ni binadamu na ana feelings kama mtu mwingine jamani.......

    Ila kinachonisikitisha ni jinsi kila mbunge siku hizi anayoishi Dar. Wageishi Dodoma ningeelewa lakini kuishi Dar wakati watu unaowawatumia wako hundreds of miles away it doesn't make sense.

    ReplyDelete
  12. Anonym. wa 9.03 kuwa makini, sote tuwaosha vinywa lakini kuna mahala pake. Hebu fikiria ni ndugu yako, au mzazi wako ndo huyo amefariki, afu kuna mpuuzi anaosha kinywa kwa kebehi zisizo na msingi sijui utajisikiaje hasa. Naomba waosha vinywa tuwe na busara kidogo.

    Kwa familia ya marehemu nawapeni pole sana, hasa katika kipindi hiki kigumu cha msiba wa ndugu yetu, hakuna la zaidi hata kama tutampa sifa za namna gani bado pengo lake dhahiri lipo palepale. Kwetu sisi tulobakia hakuna cha kumpa zaidi ya kumuombe dua kwa mwenyezi mungu.

    mola aiweke roho ya maremu mahala pema peponi.
    AMINA.

    Q

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...