
. Inathamini umuhimu wa kazi yao
. Asema kuwa mgomo sasa umekwisha
.Asema kuwa yaliyopita siyo ndwele, tugage yajayo
. Aonya kuwa Serikali imevumilia kiasi cha kutosha
. Asisitiza kuwa watakaojaribu kuvuruga amani na usalama wa nchi watashughulikiwa ipasavyo
Na Mwandishi Maalum,
Mahenge, Ulanga, Morogoro
Serikali haina chuki wala ugomvi na walimu, Rais Jakaya Mrisho Kikwete amesema katika kijiji cha Lupiro, wilayani Ulanga, Mkoa wa Morogoro.
Rais Kikwete pia amesema kuwa kwa kadri Serikali inavyohusika mgomo wa walimu umekwishakupita na kuwa yalipita siyo ndwele.
“Na ndugu zangu kama mnavyojua yaliyopita siyo ndwele. Sasa tugage yajayo,” amesisitiza Rais Kikwete.
“Serikali hii ni ya watu makini. Hatuna chuki na mtu na wala hatuna kinyongo na mtu. Kwa hakika hatuna chuki, ugomvi wala mgororo na walimu. Tunatambua na kuthamini sana kazi yao,” Rais Kikwete amesema.
Alikuwa anazindua mtambo na kiwanda cha kukobolea mpunga cha Saccos ya Walimu katika kijiji hicho kwenye siku ya tatu ya ziara ya Mkoa wa Morogoro.
Saccos hiyo ya walimu imepata mtambo huo kwa njia ya mkopo usiokuwa na riba wa kiasi cha sh milioni 35 kutoka Serikalini, kupitia Wizara ya Kilimo na Chakula. Ni Saccos ya kwanza ya aina yoyote kupata mkopo wa namna hiyo usiokuwa na riba kutoka Serikalini.
Amesema Rais Kikwete: “Ukiondoa maneno mengine ya kipuuzi, Serikali ninayoingoza mimi haiwachukii walimu. Hivi kama tungekuwa hatuwapendi tungewapa mkopo usiokuwa na riba? Si tungeliweza kusema wacha walimu wale jeuri yao na tukawanyima huo mkopo? Wangelifanya nini?”
Lakini Rais amesema kuwa Serikali imeamua kutoa mkopo huo kwa walimu kwa sababu inatambua umuhimu wa kazi yao na kujali maslahi ya walimu wote nchini.
Ameongeza Rais Kikwete, “na wala msije mkadhani kuwa tumetoa mkopo wa mashine hii kwa sababu ya tishio la mgomo. Bado tungewapa mkopo tu, kwa sababu wanafanya kazi nzuri kwa taifa letu. Tunaona wajibu wa kuwaunga mkono kwa sababu tunathamini sana kazi yao na kuheshimu mchango wa walimu katika taifa letu”
Hata hivyo, Rais Kikwete ameonya kuwa Serikali yake haitavumilia mtu yoyote ambaye anajaribu kuvuruga nchi na kusababisha kuvunjika kwa usalama na amani kwa sababu ama kisingizio chochote.
“Hatumavumilia mtu wa namna hiyo. Ndugu zangu tumevumiliana sana. Na sasa tumechoka. Kumbukeni kuwa hata Simba aliyenyeshewa mvua, bado anabakia samba tu.”
Rais pia amewashauri walimu na wananchi kwa jumla kutokuogopa kuchukua mikopo benki ili kuendeleza shughuli zao za kiuchumi. “Msiogope kukopa, hizi ndizo taratibu za dunia za kuendesha biashara.”
“Kazi ya mabenki ni kukopesha fedha. Hata wafanyabiashara wakubwa duniani kama vile Bill Gates na Warren Buffet hawatumii fedha yao katika kuendesha biashara zao, wanakopa. Hivyo, msiogope kopeni na vile vile rudisheni fedha za mabenki,” amesema Rais na kuongeza:
“Nilipata kushuhudia makala kwa makala zikiandikwa kuhusu mtu mmoja ambaye alikopa fedha benki ili kuendesha biashara. Makala zile ziliandikwa kama vile kukopa ni dhambi. Kukopa siyo dhambi, baya ni kuiba. Sasa walikata afanye nini aibe fedha za umma ili kuendesha biashara zake?” ameuliza Rais.
“Bila kufafanua zaidi, Rais amesema kuwa makala hizo za kila kukicha zilionyesha jinsi baadhi ya wananchi hawana kazi.
Baadaye, Rais Kikwete amezindua nyumba za kuishi watumishi wa Halmashauri ya Ulanga, mjini Mahenge na akaweka jiwe la msingi katika ujenzi wa ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo. Baadaye amehutubia mkutano mkubwa wa hadhara mjini Mahenge.
Baadaye usiku, Rais Kikwete amepokea taarifa ya utendaji wa Serikali katika wilaya hiyo ya Ulanga.
Wakati anapokea taarifa hiyo, Rais amewatadharisha madiwani wa halmashauri hiyo na wengine wote nchini na wenyeviti wa vijiji kuwa makini katika kugawa ardhi ya vijiji na maeneo ya miji.
“Msije kuingia katika mikataba ya akina Carl Peters (mkoloni wa Kijerumani) na Chifu Mangungu, mkahongwa shanga na bunduki, ili kugawa ardhi yote ya wananchi bila kufiria kiasi cha kutosha kuhusu vizazi vijavyo,” amesema na kuongeza:
“Nilipata kukuta mkoa mmoja ambako Mkuu wa Mkoa huo alikuwa anataka kugawa ardhi ya kiasi cha ekari 100,000 kila mmoja kwa wawekezaji watano. Nilimwambia kuwa alikuwa anauza mkoa wake kwa kisingizio cha kutoa ardhi kwa wawekezaji. Msije kudanganyika kwa sababu wengi wa hawa wanatumia hati za miliki ya ardhi ya Tanzania kukopa fedha kutoka mabenki mbali mbali duniani ili kuendeshea shughuli zao nyingine katika nchi nyingine.”
Kuhusu miradi ya maji, Rais amewataka viongozi wa halmashauri, wilaya na mikoa kuandaa programu za kubuni, kuibua na kujenga miradi ya maji kwa ajili ya wananchi bila kusubiri ufadhili wa wakubwa ikiwamo Benki ya Dunia.
“Iwepo ama isiwepo Benki ya Dunia lazima tutafute namna ya kuhakikisha kuwa wananchi wetu wanapata maji safi na salama. Huu ni wajibu wetu, siyo wa Benki ya Dunia,” amesema Rais Kikwete wakati anasikiliza taarifa hiyo iliyosomwa kwake na Mkuu wa Wilaya ya Ulaya, Dk. RM Rutengwe.
Mapema kabla ya kuwasili mjini Mahenge, wilaya ya Ulanga akitokea wilaya ya Kilombero, Rais ametembelea eneo la Malinyi ambako amezindua daraja jipya katika Mto Furua, moja ya madaraja matatu yatakayounganisha wilaya ya Ulanga katika Mkoa wa Morogoro na wilaya ya Namtumbo katika Mkoa wa Ruvuma.
Njiani amesimama katika vijiji kadhaa kikiwamo cha Itete Njiwa, Mtimbira na kwenye makao ya tarafa ya Malinyi ambako amewaambia wachungaji kutoka mikoa ya Arusha na Mwanza waliovamia mabonde ya wilaya hiyo kujiondoa wenyewe mapema katika mabonde hayo kabla ya Serikali kuchukua hatua.
“Kama mmevamia ardhi oevu, ni vyema mkajiondoa wenyewe katika eneo hilo mapema kwa sababu ni dhahiri kuwa Serikali itachukua hatua. Kama waliondoka Bonde la Ihefu hata huku wataondoka tu. Hatuwezi kuruhusu nchi nzima ikawa kama wilaya za Bariadi, Maswa na Meatu.
migomo inanedesshwa na wakristu na chadema,
ReplyDeleteMzee Michuzi,
ReplyDeleteHii imekaaje!? Inahusianaje na hii ya walimu.
Today someone played me this number (song) by PINK (a female singer based
in the US), and I thought you might also find it worth listening to.
Dear Mr President
come take a walk with me
Lets pretend we're just two people
and you're not better than me
I'd like to ask you some questions
if we can speak honestly
what do you feel when you see the homeless in the streets?
who do you pray for at night before you go to sleep?
what do you feel when you look into the mirror?
are you proud?
how do you sleep when the rest of us cry?
how do you dream when a mother has no chance to say goodbye?
how do you walk with your head held high?
can you even look me in the eye and tell me why?
Dear Mr. President
were you a lonely boy?
are you a lonely boy?
How can you say 'no child is left behind'?
we're not dumb, and we're not blind
they are all sitting in your cells
while you pave the way to hell
what kind of father will take his own daughter's rights away?
and what kind of father might hate his own daughter if she was gay?
i can only imagine
what the first lady has to say
you've come a long way
from whisky and cocaine
how do you sleep...
let me tell you about hardwork
minimum wage with a baby on the way
let me tell you about hardwork
rebuilding the houses after the bombs took them away
let me tell you about hardwork
building a bed out of a cardboard box
let me tell you about hard work
hardwork
hardwork!
you don't know nothing about hardwork
hardwork
hardwork!
how do you sleep at night?
how do you walk with your head held high?
Dear Mr. President
You'd never take a walk with me.
Haki huinua Taifa
Je, hii ina tofauti gani na mithali hii!!!?-nimerushiwa na rafiki yangu hii. Ni kimombo lakini nadhani wengi wanaovinjari mtandao huu kiinglishi kinapanda, maana anajuaje tungo ya michuzi-post a comment!? Kwa hiyo hii pia wadau nadhani mtaielewa na kutoa maoni au kufurahia
ReplyDelete>A man walks past a beggar every day and gives him shs100 and
>that Continues for a year. Then suddenly the daily donation
>changes to shs 50
>
>"Well," the beggar thinks, "it's still
>better than nothing."
>
>
>A year passes in this way until the man's daily
>donation suddenly becomes shs 20
>
>"What's going on now?" the beggar asks his
> donor.
>
>"First you give me shs 100 every day, then shs 50 and
>now only shs 20. What's the problem?"
>
>
>"Well," the man says, "last year my eldest
>son went to university. It's very expensive, so I had
>to cut costs. This year my eldest daughter also went to
>university, so I had to cut my expenses even further."
>
>"And how many children do you have?" the beggar
>asks.
>
>"Four," the man replies.
> "Well," says the beggar, "I hope you
>don't plan to educate them all at my expense."
>
Huyu mtu anayeandika kuwa wakristu na chadema ndio wanaendesha migomo anamaanisha nini?
ReplyDeleteWatu kama hawa ambao hawajasoma na kuelewa vitu gani vinajenga na kubomoa amani, watatuletea balaa. Lazima tutambue kuwa kugoma ni haki ya msingi kwa mfanyakazi yeyote, usione weusi marekani wamefika walipofika sasa, waligoma mengi na mengi yaliwadhuru lakini haukusabisha waache kugoma, soma
India pia itakusaidia kuelewa migomo. Walimu na wanafunzi vyuoni wana haki ya kugoma ili malalamiko yao yasikilizwe, mengi yamekuwa yakipuuziwa kwa muda mrefu, mbona wao (Wabunge na mawaziri) hela zao huwa hazicheleweshwi? Ina maana wao ndio wanahitaji sana hela kuliko wengine au? Mfanyakazi yeyote yule kama hatendewi haki ana haki ya kugoma, kuliko azuiliwe kugoma aanze kufanya kufanya mengine maovu(Wizi,ujambazi,rushwa.....)Hawa wabunge wanaokuja juu bila kuelewa undani wa suala migomo wananishangaza,lakini inaonesha pia elimu yao bado ni duni,wakati wa kuburuzana unaisha,udikteta hakuna tena! JK anajitahidi lakini asiahidi mengi aje ashindwe kutimiza, kuondoa migomo kunahitaji mengi ($$$$$ sana), lakini maendeleo katika maeneo mengi yanahitajika kwanza katika kuondoa matatizo kama haya. Asubuhi njema!
it makes me believe the saying that Tanzanians will ever remain poot just because they never appreciate anything on basis of selfishness.
ReplyDeleteI have gone thru Mr. President's speech but i find nothing to disagree with... cant you be at least at once!! appreciate only one thing out of a thousand from your clean President??
I hate being called among you JEalous Tanzanians....
JK will win this war against Mafisadi and Migomo whether you swallow it or no...
it makes me believe the saying that Tanzanians will ever remain poot just because they never appreciate anything on basis of selfishness.
ReplyDeleteI have gone thru Mr. President's speech but i find nothing to disagree with... cant you be at least at once!! appreciate only one thing out of a thousand from your clean President??
I hate being called among you JEalous Tanzanians....
JK will win this war against Mafisadi and Migomo whether you swallow it or no...
it makes me believe the saying that Tanzanians will ever remain poot just because they never appreciate anything on basis of selfishness.
ReplyDeleteI have gone thru Mr. President's speech but i find nothing to disagree with... cant you be at least at once!! appreciate only one thing out of a thousand from your clean President??
I hate being called among you JEalous Tanzanians....
JK will win this war against Mafisadi and Migomo whether you swallow it or no...
exactly,,,,
ReplyDeleteannon wa kwanza mmmh!!!una yako mambo rohoni,unajua why so many pple hawaendelei na so inferior???ni km ivo wewe ulivo
machache kwa leo
Bwana Michuzi,
ReplyDeleteKwanza hongera sana kwani Blog hii nimeipenda sana.
Katika swala hili mimi nadhani serekali imepunguza ukali wa moto lakini bado kuna kazi kubwa sana ya kuondoa chanzo cha moto huu.
Ukiona binadamu amefikia hatuwa ya kusema liwalo na liwe, inaonesha alishavumilia kwamuda mrefu sana.
Mimi ninachoiomba serikali ni ichukue muda zaidi kuchunguza haswa chanzo cha kuwafanya hawa waliokubali kufanya kazi hii ya wito kuona kwamba wanaonewa kuliko wengine kama wanajeshi, askari na wengine wengi...
Sidhani kuwa fedha ndio tatizo kuu
hii ni story ile ile ya kutafunwa na panya. kwa mheshimiwa rais anawapa bichwa walimu kwa kuwasifia umuhimu wa kazi yao halafu anawatisha wasipiganie haki zao kwa kutumia kisingizio cha kuvuruga amani na usalama. Panya akikutafuna huwa wakati huo huo anakupuliza. Mheshimiwa rais labda angelijaribu kuzuia mishahara ya mawaziri. manaibu waziri na wakuu wa mikoa wake na wa kwake mwenyewe kwa miezi kama mitatu halafu aone kama viongozi wote wataendelea kufanya kazi zao bila ya kulalamika.
ReplyDeleteMi nahisi elimu ni muhimu katika kila taifa. Tatizo lililoko nchini kwetu tunasema tunathamini elimu lakini walimu hatuwalipi ipasavyo. Tunasema tunathamini elimu lakini tunaandaa walimu ambao wameshindwa katika mitihani (divisheni foo).
ReplyDeleteAu hatuwalipi kwa sababu walipata foo (maana pia sijaona mwalimu mwenye wani).
Kwanini serikali isithamini elimu hivi: ilipe mishahara ya juu zaidi kwenye elimu ili kuweka ushindani wa vipanga kukimbilia kazi za elimu ili mwalimu awe ndiye kipanga/genius wa nchi? Na pia watoto wetu wajuwe mwalimu ni jinias.
Hakuna kitu kilichokuwa kinaniboa shuleni kama kujuwa walimu wangu walipata foo mimi itakuwaje?
Nchi zilizoendelea, walimu wake ni vipanga ndo maana tunaona wananendelea kielimu na kiteknolojia.
ACHA UDINI ETI MIGOMO INAEBDESHWA NA WAKRISTU NA CHADEMA! WATU WANAIBA PESA YA EPA TUCHEKE TU, HALI YA WALIMU MBAYA TUCHEKE TU, WANAFUNZI HAWAPATI MIKOPO TUCHEKE TU, WALIMU WOTE NI WAKRISTU NI CHADEMA, WANAFUNZI WOTE NI WAKRISTU NA CHADEMA? WACHA UDINI, KUENDESHA NCHI SI MCHEZO!!!
ReplyDeleteUkweli unauma lakini inafika mahali inabidi usemwe, nadhani hata mie naanza kuamini maneno ya huyo anon wa kwanza kuwa ni wakristo hasa wa pentecoste na Chadema pia. Maana humo makanisani kwao kumejaa mahubiri ya siasa ya kuleta migomo na fujo! Vile vile hata ukiangalia huyo Dr. Slaa mwenyewe wa Chadema alikotokea mhu sio baraza la maaskofu kweli? Na kama sio wao ndio vinara mbona wakati haya ya wizi wa EPA yakitokea enzi ya Mkapa walikaa kimya? Wizi huu haukuanza wakati wa utawala wa JK bali ulianza mwaka 2000 (Soma kijarida cha Cheche cha KLH/Mwanakijiji). Je hamkuwa mnaona kuwa huu ni ufisadi? Na ufisadi mwingine mkubwa mkubwa ulifanyika wakati huo huo wa Mkapa, mbona hata hao wanaotoa nyaraka hizo kuwapa hao Chadema na vyombo vya habari hawakuzitoa wakati huo? Lengo lilikuwa nini? Kumlinda mkristo mwenzao? Kwanini JK alaumiwe sasa kwa hali ambayo ameikuta? Wala mtu asitie mdomo wake kusema eti Richmond, Richmond ni cha mtoto ukilinganisha ni mikataba ya IPTL na mikataba mingine ya madini na NBC iliyosainiwa wakati wa utawala wake. Je maaskofu walikuwa hawayaoni hayo?
ReplyDeleteNa hii migomo ya walimu hata walimu wenyewe wengine wanashangaa! Kama ni madai yako miaka na miaka na miaka yote kumi ya Mkapa hakuwalipa madeni yao, na hawakufanya mgomo usio na mwisho, na hii sentensi ya kusema kuwa haya mwaswala yana udini nimeisikia kutoka kwa baadhi ya walimu wanashangazwa enzi ya Mkapa kuna kipindi walikuwa wanacheleweshwa mishahara yao kwa muda mrefu ilikuwa mbinde kupata hiyo mishahara? Mbona hawakugoma kusiko kikomo? Na hiyo ilikuwa ni mishahara sio madai ya kupandishwa cheo wala madai ya matibabu wala posho? Je hii nayo imekaaje? Hawakuona hilo tatizo wakati huo mpaka waje kugoma leo hii? Ndio maana kuna kundi kubwa la waalimu hawakugoma wameshajua kuwa hayo mambo yana udini na siasa zaidi.
Na nyie wote mnaojitia kusema eti amani sijui nini mkisikia tu neno dini limetajwa nawashangaa, tena nyie ndio pengine hao hao mnaochochea vurugu, migomo na kudai ni haki ya msingi, ni kweli ni haki ya msingi kama watu watafanya hayo kwa wakati wake, sio madeni yako yana zaidi ya miaka kumi leo unajitia kugoma bila kukoma, je ungegoma pale yalipokuwa yana miaka miwili si ingesaidia kuzuia kuwa na deni kubwa? Na hili la ufisadi nyie mngempigia hizi kelele Mkapa mbona mngeokoa mapesa kibao kuliwa na mafisadi, mlinyamaza kimya na wengine ambao mmehamia Chadema kwa kuwa tu mnatoka Kaskazini mlinufaika sana na uwepo wa Shemeji Ikulu leo mnaona manufaa au njia za kufisadi zimefungwa ndio mnapiga kelele? Mie naona huu ni unafiki na udini na Uchadema!
Vidonge hivyo mkimeza mkitema shauri yenu! Hata enzi ya Mzee Mwinyi mlipeleka puta Mzee wa watu na hakuiba hata senti tano, na aliyvoingia mkristo mwenzenu mlikaa kimya wakati anafanya mabiashara na kujikusanyia ma mamali, hakuna hata mmoja laiyesema kuhusu majumba aliyojichukulia mama Mkapa, wengine ilibidi wafanyakazi watolewe apewe hayo majumba. Na mpaka leo hatusikii mkipigia kelele hilo kama si udini ni nini jamani. Nyie waislam amkeni huo usingizi wenu wa pono mnaliwa huku mnajiona! Sisemi muandamane ila mtayatazame mambo jinsi yanavyoenda na mtafakari wenzenu mikakati inapangwa huko inakuja kutekelezwa hapa!
Na uibanie hii shauri yako lakini message sent!
duh jamaa number kumi na tatu umeongea maneno ya maana sana,afadhali watu wameshawajua chadema nia yao,ndo maana chama cha upinzani chenye nguvu kitabakia kuwa CUF,ni wapinzani wa kweli,si chadema!!
ReplyDeleteHaya naona tunaendelea kuongelea suala la dini, tunasaidia watu wenye nia mbaya kuviunga maswala ya siasa na dini, kuna umuhimu wa kutenga haya mawili siku zote, Ili swala kwamba watu wanapiga kelele kwa JK kwa sababu yeye ni mwislamu limetoka wapi? Watu wamepata nafasi ya kuongea sasa hivi, JK anasaidia kwa sababu anasikiliza, malalamiko mengi yatakuja kwa sababu ya utendeji wake mzuri, sio kwa sababu ya dini yake. Timu yake ina kila aina ya watu, wakristu,waislamu na hata wasiokuwa na dini!
ReplyDeleteInasikitisha kuona hata baadhi ya wasomi wanataka kutumia suala la udini kwenye siasa, hakuna nafasi ya dini wala siasa katika utendaji wa kazi, JK anazingatia zaidi misingi ya kazi kuliko dini, msitake kumvuta upande mmoja wa dini, huyu ni raisi anatetea wananchi na sio dini. Walimu wanagoma, wanafunzi wanagoma, wote hawa wanatafuata suluhisho, na walijaribu kwa WM wakaona hawasikilizi, lakini bado waligoma, JK anawasikiliza,anataka kusikia kilio cha kila mtanzania ili aweze kutafuta suluhisho la kudumu, huu ni mwanzo tu, anavyozidi kulala Ikulu ndio hekima inamjaa, mpeni muda, anachoandaa sasa ni umuhimu kwa miaka inayokuja, utendaji mzuri wa kazi, hasa kwa watu wa serikalini. Acheni kuongelea udini, halina uhusiano na chochote. Jioni njema.
unataka debate ya dini/imani ianze hapa bloguni?????
ReplyDeletena wale waislamu wnaoandamana wameshawishiwa au wamesilimu na kuokoka yan wamekua wakristo???
safi sana
MICHU BANA HII SASA,SII UMETAKA
hear, hear, hear!!! udini unanyemelea!! and people are stooping so low ili kutisha watu..Jamani mama mwalimu na sio chadema.
ReplyDelete