
Bwana michuzi pole kwa kazi ndugu yangu nashukuru sana kwa yote unayotuletea katika huu mtandao wa jamii.
Ningependa kukufahamisha ile album ya mzee wetu Maestro Kikumbi Mwanza Mpango a.k.a King Kiki iliyochukuwa jina la Raisi wetu Jakaya Mrisho Mikwete imetoka na inapatikana hapa Uingereza katika duka la sterns music lilipo pale Warren st.
Sasa hivi albamu hiyo iko kwenye chart ya juu pale dukani na ni namba mbili kwa mauzo na inategemea kuingia kwenye maduka ya hmv na zavvi next week, na hapa chini nyimbo namba tatu coco imepigwa kwenye radio froots ya Uk,bbc.na pia album imepata review kutoka katika magazeti kama froots uk.sound of city na charlie gillet wa bbc.
watanzania wote mnaoishi nje ya nchi tununue album ya huyu mzee wetu kutoka pale www.sternsmusic.com
ili na wazee wetu wanufaike na jasho lao.Album imetengenezwa katika kiwango cha kimataifa.Na kule Dar es salaam itaziduliwa mwezi wa kumi na mbili iko na nyimbo tisa.
Bofya hapa kwa habari zaidi:
na hapa:
Mdau Yusuf, London
/2008-10-13T14_52_39-07_00
KING KIKI YUPO LONDON SIKU IZI?
ReplyDeleteDUH HUYO REMMY NDIO KANENEPA HIVO SIKUIZI. SASA MBONA KASIMAMA NA WANADUNIA?
heeee we anonymous 3:59 vipi wewe??yani kama Remmy kaokoka ndio asisimame na watu ambao hawajaokoka?????kwani kuna ubaya gani hapo??wako wanatenda dhambi kwani??we vipi?????
ReplyDeletetupe option ya kununua online. si unajua maisha yetu huku ...
ReplyDeletemichuzi tunaomba sisi tulio huku utusaidie tupate cd za miziki ya remmy .
ReplyDelete