Ndugu waheshimiwa,
Kwa niaba ya wa watanzania waishio Massachussets (Mtandao wa watazania Massachussetts, MTAMA), Worcester County, Napenda kuchukua fursa hii kuwakaribisha nyote, kwenye hafla ndogo ya kuimba kwaya na chakula cha jioni.
Madhumuni makubwa ya hafla hii ni kuwakaribisha watanzania wenzetu toka Iringa Pommermini Lutheran Choir. Watanzania hao wamealikwa na Pastor Peter Cook, kuja kuimba hapa ili kuchangiwa kwa ajili ya ujenzi wa visima vya maji safi huko Iringa vijijini.
Mahali (Location Address),
Dinning Hall located at Atlantic College, Lancaster.
338 Main StLancaster MA 01523
Directions:
The Dinning Hall is a red brick building,
located at Prescott Street which is off Main Street/MA Rt 70.
Tarehe (Date): November 08th, 2008
Muda (Time): From 4:30 PM to 10:30 PM Incase of emergency Call
Peter Kiure 978-413-1052
Casmir Marwa 978-537-7911
Sangiwa eliamani 978-846-9898
Bube Rupia 978-227-6345

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

 1. basi wabongo vitu kamahivi vya kusaidia kwao ahaaa kimya hata comment moja hakuna waambie wakasherekee labour day au hallowen na shopping wataenda even kushop lift kujifanya wamarekani ebu nendeni katoeni michango sio kusubiri wazungu wawachangie angali nyie mnashindwa kujitolea

  ReplyDelete
 2. ni jambo jema sana kujichangia wenyewe km wabongo na sio adi misaada,wobongo mlioko uko mwende mkawachangie watumishi wa Mungu awa

  ReplyDelete
 3. Haya maswala ya dini ni ya binafsi zaidi kuliko yalivyo ya jamii.

  ReplyDelete
 4. Sasa wewe hapo juu unataka watu wa comment nini? Wabongo bwana mnawashwa na midomo sana.

  Ujumbe umefika na kwenda huko tutakwenda. sasa sijui unataka tuanze kuchukua number humu kwenye blog ya kaka michuzi?

  Watu wakicooment ujue kuna tatizo lakini hapo everything is well said sasa sijui nini tucomment...kwanza mengi humu ya party za watu yakitangazwa wanaocomment ni watu walioTZ. Kutaka kukandia tu.

  ReplyDelete
 5. Sisi tunaohisi mambo ya dini ni binafsi zaidi kuliko ya jamii ya kitanzania hatuendi.

  Ila ikiitishwa harambee ya kitanzania itayohusisha watanzania bila kujali imani tutaenda.

  Sanasana kama kuna nyimbo za kiinchi na kizalendo au basi za kitanzania.

  ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...