Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu ch Dar es Salaam sehemu ya mlimani wakiandamana jana kuishinikiza serikali kupatiwa mkopo wa asilimia 100 ya fedha za masomo na mahitaji mengine chuoni hapo


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 28 mpaka sasa

  1. dah aya maisha UDSM bado yapo??ni mateso sanaaaaaa maskini watoto wa watu na "boom" lao+ 60% support si mchezo na life la kibongo
    ndo ivo tena madenti,EPA wanatesa nyie mnasota,mkiingia sirikalini wengine watakua MA-EPA tu kwa ufinyu huu wa ada

    ReplyDelete
  2. Hi serikali haina mkakati wa muda mrefu kukomesha hii migomo?
    Hapo kitakachofuata chuo kitafungwa kwa muda usiojulikana halafu watawarudisha (devide and rule),serikali yeti inaacha kutatua kiini cha tatizo wanaleta siasa!!!Siasa kwenye ELIMU ni kuipeleka nchi kuzimu.

    ReplyDelete
  3. HIVI HAWA WANASOMA LINI, WANAMALIZA MODULES ZOTE KWELI? HALAFU MANATAKA KUCOMPARE NONDOZ ZA ULAYA NA ZA BONGO, WATU KILA SIKU MIGOMO, VIRUNGU VYA FFU, MAZINGIRA MABOVU, HAKUNA VITABU LIBRARY, COMPUTER MOJA WATU NANE....

    AAH, WACHA NIKAJINYAKULIE NONDOZ ZANGU MAJUU.

    ReplyDelete
  4. Kugoma ni haki ya msingi ya kila mtu lakini lazima tujue hasara na faida zake. Mimi binafsi naunga mkono uchangiaji wa elimu ya juu. Sababu inayonifanya niunge mkono ni kutoa nafasi kwa watu wengi kupata elimu ya juu. Pamoja na hayo, nadhani unatakiwa kuwekwa utaratibu mzuri ili wanafunzi ambao uwezo wao ni mdogo waweze kulipa kidogo kidogo hiyo asilimia iliyobaki ili waendelee na shule bila kukatiza masomo yake. Kwa mfano mwanafunzi anaweza kuzuiliwa cheti chake cha kuhitimu ila apewe statement of result kama hakumaliza ada yake mpaka wakati wa kuhitimu. Kitu kingine kinachonitia wasiwasi kuhusu maandamano ya wanafunzi ni namna wanavyojichanganya wenyewe. kwa mfano utakuta wanaolalamika wengi wamesomeshwa sekondari na wazazi wao kwa ada kubwa (200,000, 500,000, 1,000,000 n.k) lakini wawpo chuo wanataka serikali ifanye kila kitu wakati uwezo wake ni mdogo, na wakati huo huo wanatumia vibaya fedha wanazokopeshwa (ulevi, umalaya, n.k). Jamani wasomi tujifunze kwani hata huko ulaya na marekani ambapo wanatusaidia wananchi wao wanachangia elimu hivyo basi tusitegee misaada yao finyu itupatie elimu bure. kumbukeni uchangiaji utasaidia pia kuboresha elimu kwa kupata vifaa na technolojia mpya.
    Namaliza kwa kusema kuwa, nahisi kuna wanafunzi wanataka kufaidika kisiasa kwa kuandaa maandamano haya au nyuma yao wapo wanasiasa.

    ReplyDelete
  5. Sasa hao waliopozi kwenye picha, Hivi hawajui akina Mukandara na trup lake wata tumia hio picha kuwahukumu! Sisi enzi zile za "mzee" hatuku ruhusu mwandishi wala mpigapicha akatize tukiwa kamkunji. Ewe "mzee" huko uliko inabidi ufufuke ukawaokoe vitukuu vyako pale mlima manake vimepoteza mwelekeo kabisa!

    ReplyDelete
  6. Wanafunzi elimu ya juu, Migomo imeshaprove failure. Tangu mlianzaga kugoma mpaka leo watu hata hawawachukulii serious tena, sijui hamjashitukia hilo?? tafuteni njia mbadala, ya dialogue, muwaweke wanaojua kufafanua HOJA. Muwasemee mpaka waone aibu. Mwl.Nyerere angedai uhuru kwa jinsi hii, tungeumia au kufa wengi tu. Fanyeni tathmini ya migomo kama imewasaidia, nyie si wasomi bwana? Majazba hayafai

    ReplyDelete
  7. KAKA YANGU NALITOLELA P.S HIVI NA WEWE ULIYAPITIA HAYA MATATIZO ULIPO KUWA MUZUMBE? MIMI NILIPO MALIZA PALE MUZUMBE HAYA MATATIZO HAYA KUWA MAKUBWA SANA ILA KUNA KAKA MMOJA ZERUZERU ALIKUWA LECTURER ALITUMALIZIA MABINTI WENGI SANA,SIJUI ANA HALI GANI SASA HIVI SIJAENDA MUROGORO SIKU NYINGI SANA. ANYWAY PETER KAMA UNAUSHAURI WAKO WA BUSARA SIUNGETUPA HAWA WATOTO WAENDE DARASANI SASA ULISIKIA WAPI MTU ANA ANDAMANA ILI APEWE MKOPO? MIMI NINAFIKIRI MKOPO NI MAAMUZI YA MTOAJI HUWEZI KUMLAZIMISHA MTU AKUKOPESHE? SASA HII INAKUWAJE? MICHUZI DARAJA LETU LA MTO MTONGANI BADO HALIJATENGEMAA TUNAVUSHWA NA MIKOKOTENI SASA HUKU MBAGALA HAKUFIKIKI.BASI NI VEMA KAKA YANGU PETER WA ULAYA NAOMBA NASAHA ZAKO! NDIMI MDOGO WAKO PETER NALITOLELA WA EX MUZUMBE NA ST. ANTONY MBAGALA THE SMART KID!

    ReplyDelete
  8. Hamuwezi kuwafikia talibani, wanafunzi pekee waliopiga na serikali. Nyinyi ugomaji siyo njia nzuri ya kutafuta elimu. Mataishia kuwa vilaza. Bora mshinikize serikali kushusha gharama ili muweze kumudu sio kudai pesa.

    ReplyDelete
  9. peter hivi ni murogoro au morogoro na hii muzumbe au mzumbe au ndo mshabadilisha majina huko bongo ingekuwa ni makosa ya english ningekuelewa hata lugha yako pia makosa kibao mhhh powa kazi ipo na kuandamana sio africa tu hata nchi zilizoendelea wanaandamana lakini kwa bongo viongozi viziwi maandamano hayasaidii kitu hawaoni wala hawasikii

    ReplyDelete
  10. Jambo la hakika: Wanangu kamwe hawatasoma nchini Tanzania, ingawa mimi ni Mtanzania damu. Halafu Wakenya wakichukua kazi Dar es Salaam tunalalamika nini? Miaka si mingi tutatawaliwa kwenye nchi yetu na majirani zetu. Shule za msingi hakuna walimu, sekondari hakuna walimu, vyuoni kugoma kila kukicha, serikali yenyewe inahesabu majengo ya mashule na kusema Ilani ya CCM imefanikiwa. Eeeeh! Ama kweli!

    ReplyDelete
  11. Nipo India kwa sasa,najionea mwenyewe,hii india ni nchi ya kwanza duniani inayoongoz kwa migomo,si wanafunzi si raia,na wakifanya migomo kinaeleweka,sasa hapo bongo...mh ULE KALAGABAO........NAWAKILISHA.

    ReplyDelete
  12. jamani kwa haili hii bongo haitaendelea mana kila siku migomo kila siku maandamano na serikali yetu haitaki kusikiliza tunawaomba wajifunze kwa wenzetu sistem zao ziko sistematik lililoko kwenye ratiba ndilo linalotekelezwa sheria ikiwekwa ni lazima kuifuata hao ndugu zangu ilibidi waseme mapema soon mkopo ulipoamuliwa kutolewa pengine marekebisho uyangekuepo.

    ReplyDelete
  13. dah....tanzania we acha tu!!

    ReplyDelete
  14. WEE MDAU WA 3:01 UNATUPA JAMVI LAKO KWA AJILI YA GODORO LA MWENZIO. HUKO MAJUU UNAKOKWENDA UNAKOKUSIFIA UNAFIKIRI KULIDONDOKA TOKA MBINGUNI CHOKA MBAYA WEEEEEEEEEEEE. MSOMI GANI UNAE TUNIA FUVU BADALA YA UBONGO

    ReplyDelete
  15. MIMI NAULIZA MAANA NIMEMALIZA MUZUMBE MUROGORO CHUO KIKUU, NILIKOPESHWAGA MIKOPO YA HELA LAKINI SIJARUDISHA WALA NINI NA HAKUNA ANAYE NIDAI NADHANI WADAU WENGI AMA NI WA MUROGORO AMA DARESALAMU NANI AMERUDISHA MUKOPO? SASA KAMA HATUDAIWI HIYI MIKOPO HAO WATOTO WANAOANDAMANA WATAPEWA NINI NA PILI KWANI MUKOPO NI LAZIMA UPEWA SIMPAKA UTIMIZE MASHARITI! AMA MPAKA HIZO FEZA SIWEPO? SASA KUMBE NI NINI HAWA WATOTO WANAKIMBIZANA MITAANI KAMA PIMBI?KAMA MUTU HATAKI KUKUKOPESHA SIUNATAFUTA MBINU NYINGIZE ZA KUJIHAKIKISHIA TU VISENTI MUFUKONI? AU MUNASEMAJE MAJEMEDALI? HAYA BWANA ACHENI KUSOMA NA MUENDELEE KUKIMBIZANA KAMA PIMBI MUKILAZIMISHA HIYO MIKOPO AMBAYO HAMULIPI MWISHOE MUWE VIHIYO

    ReplyDelete
  16. Huyu Pita Nalitolela, pamoja na upuuzi wake lakini maneno yake yana mantiki. Watanzania wengi hatujui maana ya mkopo, kwa sababu haturudishi mikopo ili iendelee kukopesha wengine. Wengi wetu hapa tumesoma kwa hiyo mikopo je tumerudisha? Au na sie tunafanya ufisadi?

    ReplyDelete
  17. Kwanini kusiwe na sector fulani..kwanza iwe private sector inayodeal na mikopo hii?

    Kwani mkopo ni lazima umlazimishe anayekukopesha akupe 100% aghhhhh

    kwanza hao wanaosoma hapo hawalipi ndio wakisha maliza ndio maana fund ya mikopo inakua inapungua au inakwisha...Wengi tunawaona wamemaliza na kuondoka hapo nchini bila hata kulipa kidogo....Sasa kweli hii mikopo itakuapo tena

    Ingetakiwa kuwe na chombo kinachokopesha na unakwenda kwa mashartu yao....hutaki basi

    Na chuo kikuu hivyo vingetakiwa viwe vya serikali tu (yaani cheap fees) lakini sio wao wawe resposnsible na malipo yao tena...Ulimwengu ushabadilika basi na siye tubadilike.......

    Watu tunachacharika kulipa tution fee nyie mnalazimisha mikopo ilipwe 100% acheni ghadhabu and don't take anything for granted......

    ReplyDelete
  18. HIYO NI BOYS VARSITY? MBONA SURA ZOTE ZINAFANANA TU

    ReplyDelete
  19. Nyie wanafunzi wa chuo kikuu sasa mnatia aibu na hayo maandamano yenu ya kila siku, kama shule imewashinda muende vijijini mkalime,kwa ninavyoelewa haki ya mwanafunzi ni kusoma, kumaliza shule na kwenda kujenga taifa upishe nafasi na wadogo zako nao waje kutumia chuo nao wapate nondo, sasa ukienda na mwendo wa kugoma shule utasoma lini? Halafu mnashangaa wenzenu wenye umri mdogo kuliko nyie wamesomea ulaya wanakuja na nondo zao wanajichukulia kazi bila shida hapa nchini, nyinyi mnapoteza muda kudai 100% kwa serikali.Ningewashauri mkaandame kwa wazazi wenu waliowaleta hapa duniani maana ndio jukumu lao la kuwasomesha serikali inawapa favor tuu.

    ReplyDelete
  20. Mdau Saidi hapo juu nakuunga mkono, hawa wasomi wetu wataipeleka hii nchi kuzimu. Asilimia kubwa ya hao wagomaji majumbani kwao hata ugali unawashinda leo vifua mbele wanaandamana, fikiria ulikotoka, elimu ndio njia pekee itakayoiokoa familia yako kwenye shida soma umalize usaidie familia yako.Wanafunzi kama shule hamuwezi achieni ngazi waachieni wasomi halisi wasome msiwawekee wasomi wa kweli usiku.

    ReplyDelete
  21. Nafikiri serikali inahitaji kutafuta mbinu itakayoweza kuwasaidia wale watoto ambao kweli hawana jinsi yoyote ya kupata hata hiyo asilimia ya mkopo inayobaki kwa ajili ya kuchangia elimu yao ya chuo. Jamani twende mbele turudi nyuma, wapo watoto ambao hawana uwezo kabisa wa kutoa hiyo pesa.

    Nitawapa mfano, mdogo wangu ndio ameanza mwaka wa kwanza hapo chuo kikuu. Yeye alikuwa na rafiki yake, ambaye walikuwa wakijisomea pamoja (study group), ambaye alimuomba mdogo wangu kuwa kama nitakubali, aje afanye kazi za ndani kwangu, ili nimpatie pesa ya kurudishia fomu za mkopo kwenye bodi ya mkopo. (mkumbuke kurudisha fomu ni shsh 10,000 tu!). Kama mtanzania ambaye angalau elfu kumi nina uwezo nayo, niliumia sana.

    Huyo ni mmoja tu, nina hakika wapo wengi sana wa jinsi hiyo, Tanzania si tunaifahamu na watu wake tunawafahamu? Tusiangalie tu maeneo ya miji mikuu ambayo watu kidogo wana nafasi ya kuzungusha pesa, maeneo ya miji midogo na vijijini ni issue jamani!

    ReplyDelete
  22. Wanahaki maana wengine huwa wanasikia tuu Migomo kwenye TV, ila sasa ukiona wanafunzi wanagoma ujue Mitihani imekaribia halafu shule haijapanda kwahiyo wanajua wakigoma watafukuzwa na kwenda kupata Muda wa kusoma kwa wale wajanja.

    Tunayajua haya.

    ReplyDelete
  23. Kwahiyo mchangiaji 12, 2008 9:58 AM alishindwa kumsaidia huyo kijana elfu 10 ukaamua kumtumikisha, wakati biere umekunywa zaidi ya elfu10 na kuonga nyumba ndogo ndo usiseme.
    Jama ehe! huyo Nalitolela si ndo alitimulia kipindi kile, alijiunga college na vyeti fake, check anavyochangia, huwezi kusema mjamaa ni graduate..eti yule lecture zeruzeru, tumia tasfida...albino, nasikia alikumegema dem wako na dada yako, mchizi sasa ivi yupo hazina, anakula kuku na mafisadi.
    Hawa wasomi wetu wa baadae wanatakiwa watathmini migomo imewasaidia vp badala ya kupambana na serikali ambayo haipo tayari kusikiliza kilio chao. Tulisha sema tuipige chini CCM, lkn wazee wao huko vijijini ndo wanaipa ushindi ccm kila uchaguzi kwa ufupi muungano wa serikali za vyuo, waombe kikao na waziri maghembe na pinda wajadili na waone watamaliza vp matatizo haya...kwa stahili hii tutapata watalaam kweli?? cku hizi lijamaa fresh from college, lets say Bcom, yani unajiuliza mchizi amefaulu vp huyu coz hajui kitu kuhusu kazi aliyoomba...kumbe issue ni migomo daily kwahiyo ikifika kipindi cha paper, hasa madada zetu lecture anapewa uroda maisha yanaendelea.

    ReplyDelete
  24. Katika mambo yanayonikera ni ya hawa wanafunzi wa elimu ya juu kung’ang’ania wapewe mkopo wa asilimia 100 kwa ajili ya kuweza kusoma katika vyuo kadhaa vya elimu ya juu.

    Binafsi wanaoniudhi zaidi ni hawa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) ambao wamekuwa kama mtoto wa miaka mitano anapoelezwa na mama yake kuwa hana fedha, lakini yeye anang’ang’ania kuwa anataka koni na lazima anunuliwe.

    Naweza nisieleweke hasa kwa wale wanaotaka kupatiwa asilimia 100 ya ufadhili wa masomo, lakini ukweli utaendelea kubaki hivi hivi kuwa ndugu zangu hawa wakiwa kama wasomi tunaowategemea kuliongoza taifa hili, wanatakiwa kupima madai yao pamoja na kauli ya serikali na si kulazimisha wapatiwe wanachotaka wao.

    Kwenye hili naomba nitofautiane sana na hawa ambao jamii inayowaona ni wasomi, ambao mimi sasa ninawashusha thamani na samani lakini siwaoni kama ni wasomi kweli kwani hoja zao hazionyeshi chembe ya usomi.

    Nimetangulia kuweka wazi wanaonikera zaidi ni wanafunzi wa UDSM kutokana na kwamba wao ndiyo hadi sasa wanaolazimisha kupatiwa ufadhili wa asilimia 100 hadi wamefikia hatua ya kuandamana na kupoteza muda badala ya kwenda kusoma.

    Serikali imeshaweka wazi kuwa haina uwezo wa kuwalipia wanafunzi wote na badala yake wameamua kulipia kulingana na uwezo wa mzazi wa mtu kwa nia nzuri ili watoto wengi zaidi waweze kupata elimu ya juu na taifa hili liweze kuwa na wasomi wengi zaidi.

    Miaka ya nyuma tulishaona serikali ilipokuwa ikiwalipia asilimia 100 walikuwa wanafunzi wachache wakipata nafasi hiyo na wengi wao walishindwa kusoma licha ya kufaulu au kuwa na uwezo mkubwa wa kusoma.

    Leo serikali inawapa mkopo wanafunzi 60,000 wakati kwa fedha hizo hizo ilizo nazo ingewalipia kwa asilimia 100 wangeweza kupata wanafunzi 40,000 pekee na waliobaki wangekosa nafasi hiyo ya elimu.

    Hebu wanafunzi wa Kitanzania tujilinganishe na wenzetu wa Kenya na Uganda kama tulivyozoea, tuone wanafunzi wa nchi gani wana nafuu kwenye hili la mikopo. Kenya wanaopewa ufadhili ni wanafunzi 10,000 kati ya 120,000 wanaodahiliwa wakati Uganda wanapata 4,000 kati ya 30,000 wanaodahiliwa. Hivi na serikali yetu ingeiga Kenya au Uganda wanafunzi mngesemaje?

    Sisemi serikali ipongezwe kwenye hili, lakini lazima tukubali kuwa imejitahidi sana tukiangalia na nchi nyingine zaidi ya Afrika Mashariki ambapo serikali zao haziwalipii lakini wazazi na watoto wao wanajitahidi kuitafuta elimu.

    Ikiwa serikali imeshasema inawalipia asilimia 100 wale wasiokuwa na uwezo na kwa wale yenye mashaka nao basi bodi ya mikopo itakwenda kuhakiki makwao kujua kama kweli hawana uwezo, kwa nini wanafunzi wa UDSM walazimishe wakopeshwe asilimia 100? Binafsi naona kuna ajenda nyingine, nani asiyejua wanafunzi wa elimu ya juu wanazitaka fedha hizo kwa ajili ya ‘matanuzi’, ikiwemo kununua majokofu, home theatre, TV na wengine wanafikia hata hatua ya kununua viwanja?

    Wanafunzi wa UDSM sasa mnapaswa kuwa makini na kutambua kuwa wanaochochea maandamano na migomo wana ajenda zao na wanatumia mwavuli wa wanafunzi wote ili watekeleze yao, tumeshaona viongozi fulani wa chuoni hapo waliendelea kulumbana na serikali wakati walikuwa wameshamaliza chuoni hapo. Hivi watu wa aina hii tutawaonaje? Si wametumwa hao?.

    Kwa ushauri wa bure tu, wanafunzi msikubali kutumiwa na wachache wenu huku mkapoteza muda wa kuweza kusoma lakini kwa upande wa serikali nionavyo mimi mmewabeba sana wanafunzi hawa, sasa msiwaendekeze tena hata kama ni haki yao kugoma au kuandamana sasa wanakwenda sipo, wametuchosha.

    ReplyDelete
  25. jamani kumbukeni hawa viongozi waliopo madarakani walisoma free tu enzi za mwalim nyerere na mzee rukhsa

    ReplyDelete
  26. Mi nadhani tusiwalaumu wasomi hao kwa hatua waliyoichukua,kama wangekuwa wanapewa 6o% na hawazuiwi kuendelea na masomo endapo watashindwa kumalizia fees halafu wanaandamana ningewalaumu.Tatizo linakuja pale ambapo wasio na uwezo wanakatishwa masomo kwa kushindwa kumalizia ada,na hapo ndipo mgomo unapoanza kwa kudai 100% ili kuwanusuru jamaa zetu wasioweza kumudu gharama hizo.Wapo wanaoweza kumalizia 40% ila wanawapa tafu wenzao ili kuongeza nguvu,serikali ingelitilia maanani hili jambo na haitakuwa na maana mtu unarudi nyumbani kwa kukosa 40% na hatimaye kujikuta serikali inapoteza wataalamu watarajiwa kwa uzembe wa viongozi wachache wanaojali matumbo yao wakati na wao walisomeshwa bure na Nyerere,pu***@#*& zao.Enway yote maisha ila inaniuma sana ninapoona watu wanatesekea haki zao na wengine wanazifaidi bila hata ya kutoka jasho!
    Yani ukiangalia nchi hii Tz inavyotawaliwa unaweza ukamnanilii mtu bila hata huruma,aah inakera kwa kweli...

    Potz.

    ReplyDelete
  27. anony wa 1.43 am,aaagh! eti mnachacharika kutafuta school fees,at least si mna hizo nyenzo....unaingia tuu 'BOX' unazichanga...hao wenzenu hizo AJIRA wazitoe wapi???
    me kwanza nikiona watu 'wachache' wanavyofuja pesa za umma..wkt watu wanagoma ili tu wapate MKOPO..100%..inanichefua....ilitakiwa wasome FREEEEEEEEEEEEEEEE!

    NEY-BHAM

    ReplyDelete
  28. Kwa waliosoma uhasibu na uongozi mnajua wazi. Fedha asilimia mia haipo, na kama chuo na serikali hamuwezi kuipata , mnawaambia wanafunzi ni kiasi gani watapata. Wanafunzi wakikakataa kwa kufikiria kwamba hiyo fedha ipo ila mnawanyima na wakachagua kugoma basi mnavuta muda. Na kama tena kibaya wakafikiri fedha za EPA zikirudishwa basi hazina kazi ila ni zao basi wamejidanganya.
    Kinachofuata ni kwamba , kama hakuna cha kukubalika kati ya uongozi na wanafunzi, njia rahisi ni kufunga chuo.
    Ukifunga chuo unapunguza gharama za kuwalipa wanafunzi katika muda waliokuwa wanataka, na kukufanya wewe kama uongozi kusubiri hadi utakapowaita kwa fedha iliyobakia.
    Aliyeshinda Uongozi/serikali moja na wanafunzi zero.
    Kuhusu kurudisha fedha sahau, wote tuliosoma pale hatujalipa hata senti moja, namna tunayoilipa ni katika mishahara wanayotoa kwa wahitimu wa vyuo Dar. Huwezi kumsomesha mtu kwa Tsh millioni mbili hadi tatu kila mwaka kwa mwanafunzi kwa chuo kikuu TZ, na kwa miaka minne ni Tsh millioni 10, halafu ukamdai arudishe kwa malipo unayompa mshahara wa Tsh 300,000 kwa mwezi au chini zaidi.
    Hivyo sahau, unakatwa kwa kulipwa mshahara mdogo, that how it works.
    Wanaotakiwa kulipa ni wale wanaopata kuanzia Tsh laki nane na kuendelea, na hasa waliosoma chuo kikuu Dar kwa kulipiwa kwa mikopo au bure na wanafanya kazi mashirika ya nje yaliyopo TZ.
    Migomo ni sawa, ila iwe na mafaniko na sio kila mara mnashindwa nyinyi kwa kufukuzwa na kurudi nyumbani kila mara. Mnapoteza muda wa kumaliza chuo na kuanza kujiajiri au kuajiriwa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...