Hapa nilipokuja Bongo,nikaenda kujionea Uwanja wetu wa Taifa,nilifurahia kila kitu,japo hiyo mechi golikipa wa Ghana alisawazishagoli kiaina.Sasa ukiangalia hiyo attachment utashangaa jinsi wabongotunavyofanya mambo kinyume na matarajio ya wengi.Hapo ni kwambele,badala ya ku-park magari kwenye zege watu wame-park kwenyenyasi.

Tutafika kweli?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 63 mpaka sasa

  1. mmh Sijui labda ni mambo ya Tanzania, lakini mbona hayo magari yame park kwenye majani instead of on the concrete?? Huku Newala majani ni ya watu ..na concrete hio ndio magari yange park. Hii pic inaleta utata...hii ni "my opinion" labda nyinyi mnaona je???

    ReplyDelete
  2. Sasa wakipark kwenye zege halafu wakanyage majani? mmeshaambiwwa waliojenga waliplan hivyo na it seems to work okay so far. Just imagine kukiwa na mvua watu wataweza kukanyaga hayo majani?

    Knicks and Knacks too much tushukuru hata hiyo uwanja unaonyesha unapendeza

    ReplyDelete
  3. Hii ni ajabu na kweli. Magari ya Polisi ndio ya kwanza kupaki kwenye nyasi. Hii ni bongo kweli. Nani amuelimishe mwenzie?

    Nina wazo, kuna haja ya kutangaza jinsi ya kutumia huu uwanja. Kuanzia kwenye parking mpaka namna ya kutumia vyoo na vifaa vingine ndani.

    Toa aoni yako.

    ReplyDelete
  4. wewe ndo hujui. hiyo ni parking ya kissa, unapark kwenye majani. sasa wakipaki kwenye concrete watapishana vipi

    ReplyDelete
  5. We Michuzi acha mabo yako! Hizo ziko kila sehemu duniani. nilienda hapo Wimbley nikakuta jamaa wanafukuzwa ku-park pale nje kwenye eneo la supermarket! hao je?

    Nadhani muhimu tusiwaone wabongo kama ndiyo wako nyuma sana na mazuzu. Huko Uliko Ethiopia tuletee habari zao. washamba sana hao

    ReplyDelete
  6. hayo manyasi wazee wenzangu sio ya kupark magari, magari duniani kote yanapark ktk zege,nadhani hao wachina hawajakuelezeni kwavile hilo linaeleweka,na ni aibu kubwa kwa mtu yoyote mgeni kuiona hio hali ya ajabu ya kupark magari ktk nyasi,hizo nyasi zitaanza kuungua kwa tairi za gari muda sio mrefu na tutashindwa kuzipanda tena,au itagharimu milions kwaajili ya kupanda nyasi,tff na kila anaehusika hili suala huyu mdau hapo juu amengea suala la maana sana.ni aibu sana,thankx

    ReplyDelete
  7. ndio wachina walivotwambia sasa shekhe!

    Hamad

    ReplyDelete
  8. Yaani Ni Noma..Labda Mbunifu Wa Neshno Ana Malengo Yake,Atufafanulie Tafadhali.
    Byabusha Mwengine

    ReplyDelete
  9. O.M.G yani wanapark magari kwenye garden jamani watu wamazingira nao wana hakiri fupi hivi? brother michuzi wambie wasipark magari kwenye majani,au majani ya plastic? hata kama jamani naona haya kuangalia hii picture najifuni kichwa kwa haya

    ReplyDelete
  10. We need a mental emancipation, not just on a car parking, but on a much varieties of issues.

    It says a lot about us as developing nation,
    This is just a tip of an iceberg, who to blame ?

    I envision 2050, we will get there! Change is coming!

    By Mchangiaji.

    ReplyDelete
  11. Mdau wa hii picha mambo ya uwanja mwachie mkandarasi ana maana yake kubwa kufanya hivyo na kuweka hiyo parking si lazima kila kitu mtoe kasoro kama huko uliko wa utaratibu tofauti ni wao,na si kila sehemu lazima kuwe na utaratibu sawa kwani gari kupaki kwenye nyasi kuna kasoro gani?? watanzania tukifanyiwa jambo jema tunatoa kasoro kwanini?? tuwe na shukrani maendeleo hayaji kama mvua inayoshuka pole pole tutafika kwa maana hatukitegemea kama kuna siku tutakuwa na uwanja mzuri kama huu sasa tumepata baada ya kushukuru unaanza kusema ooh wapepaki pabaya,sijui nyasi ,wewe kama una wwe ni mtaalam wa parking system, uko nje ya nchi ila jifunze utaratibu wa huko mzuri na mbaya acha huko,
    By
    KAMATI YA UWANJA WA TAIFA/ULINZI

    ReplyDelete
  12. naona kama hamna kosa penye majani ndo pa kupark gari,ukiangalia parking nyingi za kichina huku utakuta wamepanda majani na magari ndio yanapaki kwenye majani, pembeni ni side walks,ndo wanavyofananya, na huo uwanja wamejenga wao, tutapost parking zao za huku tulinganishe

    ReplyDelete
  13. Cha kushangaza zaidi ni kuwa kuna gari la polisi pia limepark hapo....Duh!
    PaulSifa

    ReplyDelete
  14. hapo wabongo hawakwenda kinyume na matarajio ya wengi, ni sahihi walivyopark, sio kosa kaka,

    ReplyDelete
  15. siyo kila kitu mnalaumu wabongo, huo utaratibu umewekwa na wachina waliojenga uwanja.

    ReplyDelete
  16. Hapo kweli Neshno ni tambarare, kinachoudhi ni hiyO type ya parking tu. Nyasi zinatakiwa ziwe green na clean,siyo na michoro ya matairi. Sijui kwanini hakuna hata mtu mmoja anayeshtuka na hiyo aina ya parking hapo Bongo.Wasimamizi wa National JAMA JAMA!

    chagga girl, boston

    ReplyDelete
  17. Mh... sasa mbona kila mtu amepaki kwenye nyasi? Ina maana kila mtu kakosea au ndo utaratibu wenyewe? Whatever the case, nadhani wanaohusika na management ya uwanja ni bora wakitoa maelekezo tosha hata ya vibao vyenye alama kuonesha watu wapaki vipi magari yao

    ReplyDelete
  18. Hata mimi nawashangaa!! sana wabongo kwa hili!!. yale majani japo ni artificial (yapo kama kapeti), lakini unapopaki magari kila siku majani hayo yanachafuka, magari mengine ni vimeo yanadondosha oil chafu nk, baada ya muda mfupi yatakuwa hayatamaniki kwa uchafu. Ni bora wapaki kwenye zege ambalo laweza pigwa deki au vipi wadau.
    Mdau
    Mkereketwa wa ustaarabu

    ReplyDelete
  19. Wewe huelewi nini? Kule kwetu Nyasi kibao, Cement ndiyo mali adimu. Kwahiyo wanaheshimu cement ni afadhali wapaki kwenye majani. Wengine tumekulia kwenye nyumba hakuna kupiga deki, unamwagia maji kwenye sakafu ambayo ni udongo, kisha unafagia, cement kwetu ni kitu cha kuheshimu sana.
    K.L.S (USA)

    ReplyDelete
  20. Yaani wewe ndo Maharage kabisa tulishakuambia Mwanzoni hiyo ndio sehemu maalum ya kupaki magari,sasa wewe unataka yapaki kwenye sakafu halafu yanapotoka yakanyage nyasi? hiyo ni sehemu special kwa parking usidhani waliopaki hawana akili kama unavyodhani, Uliwahi kutoa picha hii nikakuelewesha lakini huelewi.wewe ni Maharage kabisa.

    ReplyDelete
  21. zikipaki ktk zege zikitaka kutoka zitapita ktk nyasi kwa upande wangu naona bora zipaki ktk nyasi zikitoka zipite ktk zege
    mdau
    kisiju pwani

    ReplyDelete
  22. Hata designer nae ni mshamba vilevile. Sijui ndio staili ya hina au wapi.Sijaona parking lot kama hiyo Marekani. Hata wakipaki kwenye zege watatembea kwenye zege. majani ya nini karibu na parking lot. Aisee hii ni kichekesho sio tu kwa wanaopaki.Poor planning and designing.Blame should go to them LOL!aha aha kama maohoka vile eee jamani mabavu zangu hii hahaha!

    ReplyDelete
  23. Hilo ni tatizo la Manager wa uwanja ambaye nafikiri ni mswahili mswahili.Katika hilo inabidi pengine aje Mchina toka Beijing amfundishe namna ya ku-run mradi kama huo. Kimsingi traffic control inataka tu kuweka matangazo ya kuzuia ku-park kwenye nyasi na kuweka mtu mmoja au wawili kuongoza magari.Tatizo la kufanyakazi kwenye idara/hirika la umma ni kuwa mtu anapoingia kazini/ofisini akili mukichwa intokea dirishani!!

    ReplyDelete
  24. Hivi hayo majani ni special for parking? yani wa tz siwaelewi kabisaaaaa

    ReplyDelete
  25. Mnapenda kukandia tu vitu vya kwenu bila kuchunguza kilichofanyika. Kwenye hizo nyasi kuna pavement blocks na hizo nyasi zimepandwa in between kwa makusudi kabsa.Nadhani inasaidia sana kwa mwonekano mzuri, imagine kama pale pote pangekuwa kokoto kama unavyopendekeza.

    ReplyDelete
  26. MSWAHILI HAACHI ASILI, UNAPAKI GARI KWENYE NYASI, UNAVUA VIATU KUPITA KWENYE HIYO SAKAFU, HAJA NDOGO UNAMALIZIA KWENYE HAYO MAUA.

    ReplyDelete
  27. wachina wenyewe ndo walivyoelekeza na wao ndo washafika

    ReplyDelete
  28. wabongo kaka bado hatujajielewa kabisaaaa

    ReplyDelete
  29. Hapo wa kulaumiwa ni designer wa hiyo parking na sio watumiaji alie plan hiyo PARKING ni kihiyo wewe ukiangalia hiyo ni parking?? au hata kama mtu akipark kwenye hiyo zege unadhani wakati wa kutoa hiyo gari hata zikanyaga hizo nyasi??? kama alitaka kuweka mapambo ya nyasi angeweka kwenye hiyo round hapo na kote huko kukamwaga zege kuna mambo mengi ya kufanya eneo lipendeze na si lazima nyasi angalieni parking za wenzetu.

    ReplyDelete
  30. MIE KWA MAWAZO YANGU NADHANI WALIOEGESHA MAGARI KWENYE MAJANI WALIFIKIRIA KWA MAKINI SANA. WANGEPAKI KWENYE ZEGE, BASI MAJANI YANGEKANYAGWA VIBAYA MNO, HASA UKIZINGATIA ILIKUWA SIKU YA MCHEZO. MAANA SEHEMU YA ZEGE ISINGEPITIKA SABABU YA MAGARI. HIVO NI SALAMA KIASI FULANI GARI KUKAA HAPO KULIKO UMATI WA WATU KUKANYAGA SIKU NZIMA YA MCHEZO. NA PIA SEHEMU YA ZEGE WALA HAIJAWA DESIGNATED KWA KUEGESHA MAGARI INAVYOONYESHA. HAKUNA MISTARI ILIYOCHORWA. NADHANI TUSILAUMU SANA KAMA HATUJUI KWANINI WALIEGESHA KWENYE MAJANI. KUMBUKA HAPO NI HOME - BONGO. USILINGANISHE KILA KITU NA SEHEMU ZENYE MITA "LUKU" ZA KUEGESHA MAGARI.

    Marko - United States of A.

    ReplyDelete
  31. NA BAHATI MBAYA KUNA FREELANDER MBILI ZA POLISI KWENYE NYASI, LABDA WANAOGOPA KUCHAFUA SAKAFU SI UNAJUA MAMBO MAPYA!!!!!!!!

    ReplyDelete
  32. kaka hapo naona ndio panavyotakiwa, ndio parking yenyewe hiyo, waliopark hawakufanya makosa wala kinyume kama ulivyosema.

    ReplyDelete
  33. Taarifa Muhimu kwa Watumiaji wa Blogu hii:Bei ya Petroli leo hii 20/11/2008 nchini Marekani(USA)ni Dola US$2.33 per Galon.Hiyo ni sawa na Shs.773/= kwa Lita Moja ya Petroli hapa nchini Tanzania.(source:CBS News/tny).Galoni moja ya Marekani ni sawa na Lita 3.71,na Dola moja leo 1US$ ni sawa na Shs.1,231/= BOT.Kokotoa mwenyewe uone jinsi tunavyo nyolewa bila maji katika nchi hii ya Tanzania.Bei ya Petroli iliyopo hivi sasa hapa nchini imedumu toka wakati ule Pipa Moja likiuzwa kwa US$140 na hivi leo limeshuka bei hadi chini ya US$60 kwa Pipa lilelile!Its easy to see what the role of the Government is under these Two Scenarios!When the dire Ignorance of the innocent Populace is exploited as an important resource to further individual whims!Whats the use when even the word TAX itself is also Taxed?

    ReplyDelete
  34. Wandugu, natafuta blog ya THE UTAMU. Mbona haifikiki? Au imebadilisha jina? Tafadhali nistueni mwenzetu

    ReplyDelete
  35. Ama kweli kutokujua si ujinga, ila siwalaumu wadau kuegesha magari kwenye nyasi, badala ya zege.
    tatizo hapa ni kuwa hakuna alama zinazowaongoza watu wapi pa kuegesha magari yao.
    Au basi wangeweka waongozaji wa kuwaonyesha watu wapi pa kuegesha magari.

    Shukrani mdau aliyetukumbusha vijimambo vya nyumbani.
    Ila tutafika tu.

    mdau ughaibuni.

    ReplyDelete
  36. Hiyo ndio bongo, baadhi ya watu hawataki kuumiza vichwa kufikiria. Tena hao wenye magari ndio wengi wasomi na wanasafiri nje ya nchi, ilibidi wajifundishe mengi kuhusu kutunza mazingira, lakini wapi!

    Wabongo hawapendi au sijui hawajui vitu au mazingira mazuri? Ndio maana hata kila kizuri kikijengwa baada ya muda mfupi huanza kuharibika.

    Kingine cha kushangaza. Wahusika walikua wapi na kuwaruhusu watu waegeshe magari yao sehemu kama hiyo? Tunaonekana jinsi gani tusivyokua na majukumu katika sehemu zetu za kazi.

    Kweli bongo tambarare kwa michongo hii.

    ReplyDelete
  37. Labla ndivyo walivyoelekezwa.Maana kama wote hao wamepark katika majani tusemeje sasa?Tuseme katika wote hao hakuna mwenye upeo wa kufikiria jamani?Kazi ipo!

    ReplyDelete
  38. JAMANI WABONGO VIPI TENA, MBONA TULISHASTAARABIKA. GAFLA TU MNAENDA KUPACK KWENYE NYASI ZILIZO NUNULIWA NA MWAGILIWA KWA MIEZI KAZAA. HIVI ZEGE HILO LINAKAZI GANI HAPO? MECHI IJAYO KWA HESHIMA NAA TAADHIMA TUNAWAOMBA MPAKI KWENYE ZEGE, MSITUAIBISHE.

    ReplyDelete
  39. NYOOOOOOOOOOTe nyie hamjui bora hao wameamuwa kwendak inyume na wengine kua park kwenye nyasi Je Hiyo Round ya mzunguko wa magari hamjaiona kama Jamaa kakosea kuzunguka Kisheria? hahaahah Na hiyo basi pigine comment watu kwa kukosoa humu hahaah jamaa kapita moja kwa moja bila kuzungusha gari hapo kwenye mnaita Raundi abauti. Masudi Wa Shamba.

    ReplyDelete
  40. Inaelekea wengi wenu mliotoa comments hamjawahi kufika Taifa siku za matches, au mpo ughaibuni na huwa hamrudi likizo, na hata mkirudi, hamna hata pesa ya kwenda kuwatch matches.
    Ukifika hapo unaonyeshwa pa kupark, na ni ktk majani, ndivyo uwanja ulivyojengwa hivyo. Na kana alivyosema mdau mmoja hapo juu, majani yapo katikati ya blocks, so tairi halikanyagi udongo palipopandwa hayo majani, so hayaharibiki, na pia yanakuwa tramed kila mata so yapo usawa wa hizo blocks. Nadhani mmenielewa.
    Na nionavyo mimi, pamependeza zaidi kuliko pangekuwa hapana majani, pangeonekana plain zaidi

    ReplyDelete
  41. Mnaochangia bila kufikiria hamuelewi mnachokiongea. Katikati ya kila sakafu ni kokoto na juu ya kokoto ndio nyasi, magari yanapaki juu ya kokoto na sio juu ya sakafu. Hii ni current design ya parking ambayo inatokea China. Kwa asiyeamini na kuona kama vile Watanzania wako nyuma (kumbe wako mbele) waangalie design ya parking za uwanja maarufu wa Olympic wa china (the bird nest). Parking zao zinafanana kabisa na za national. Sasa US ndio wamebaki nyuma na ujima wao wakati China na Bongo wanaendelea.

    ReplyDelete
  42. Samahani!Hivi nyie watu mnaotuma hizo comment mnamjua hata aliye design huo uwanja? Ok, kwa taarifa tu designer ni Mtanzania, Mzee wa kichaga anaitwa Bw. Mushi kwahiyo alikuwa ana maana yake kudesign parking ya namna hiyo, na labda lengo pia ni kuweka tofauti ya kiwanja chetu na viwanja vingine duniani.

    ReplyDelete
  43. Kwa ambaye hajafika National, mistari ya parking imecchorwa humo humo kwenye majani. Actually ni line za zege zinazotenganisha sehemu za kokoto za kupaki na ambazo juu yake zimeoteshwa majani kuzuia movement za kokoto kwenda kwenye sakafu. In addition, sakafu ni ya urembo yenye michoro mingi mizuri ambayo sio sensible kuifunika na magari.

    ReplyDelete
  44. Minaona watu bado mnaendeleza ubishi, kaka michuzi mimi kesho nitakuletea picha ya huku uholanzi sasa watu waone parking ya majani. Hiyo ndo ilivyo ndugu zangu tuache kuwalalamikia wabongo eenh.
    Mzee wa kukomenti

    ReplyDelete
  45. SASA SIKIA THE WAY I SEE HAPO DESIGNER HAKUMAANISHA PARKING LOT, HIYO NI FRONT AREA AMBAYO AMEDESIGN KUPENDEZESHA MACHO, WABONGO MNA PARK MAGARI YENU.........

    Haya bwana ni mimi mshamba mshamba wa hapa hapa bongo

    ReplyDelete
  46. KITU TUNACHOSHINDWA KUFAHAMU NI KWAMBA "NEW NATIONAL STADIUM HAVE NO PARKING SPACE AT ALL". HAYO MAGARI MNAYOYAONA, NI MAGARI YA WAKUBWA "WENYENCHI" YALIYO RUHUSIWA KUPITA GETINI, NA KWAMBA YAKO NDANI YA SEHEMU YA UWANJA. HIYO SEHEMU HAIKUJENGWA KAMA PARKING SPACE, BALI NI BUSTANI/SEHEMU INAYOPENDEZESHA UWANJA WETU. WALALAHOI(WANANCHI WENYE MAGARI) HAWARUHUSIWI KABISA KUINGIZA MAGARI YAO HUKO, LABDA UTOE RUSHWA. HUWA WANAPARKI KAMA WANYAMA POLINI NJE YA SEHEMU YA UWANJA. AND NO BODY CARES. DISIGNERS/ENGENEERS WAZAWA/NA WANA SIASA WETU(PAMOJA NA MARAISI NA VIONGOZI WETU WENGINE), KAMA ASILI YETU ILIVYO, BADO KABISA HAWAJUI UMUHIMU WA PARKING SPACE, NA NDIYO MAANA MPAKA LEO, HAKUNA HATA SEHEMU MOJA KATIKATI YA MJI AMBAYO IMEJENGWA KAMA PUBLIC PARKING SPACE. GOD BLESS TZ.

    ReplyDelete
  47. haahaaaa! sasa na hawa viongozi wote na kujifanya kutembea kwao nje, is this what they actually see when they travel? Cars on grass in lie of concrete? mmh! Even if the Chinese said so, this is stupidity to the fullest, and they better change or else ni kujidhalilisha tuu. Besides, the pavement doesn't need to be that neat anyway, it is just for cars and walkway. gosh!
    Do they really think while spending tax payers money??

    ReplyDelete
  48. Mnashangaa parking? Ni vile tu jana niliogopa kudundwalakini ningeweza kuwapa picha za yanayojili chooni wakati wa mapumziko pindi wananchi wanapoenda kudrain mambo flani, yaani ni jambo la kawaida kumuona mtu mzima shingoni kabeba kichwa kilicho na akili timamu then anakojoa kwenye sinki la kunawia mikono!
    Au fulaha ya goli wao hurusha chupa za maji kuelekea uwanjani...,
    Pia nafahamu kwamba mkandarasi bado hajakabidhi uwanja ila jana angeweza kusababisha mauaji pale uwanjani kwa kitendo chake cha kuzungushia uwanja mabati kisha kuacha njia nyembamba ya kutosha gari moja kupita kitu kilicholeta tafrani wakati wa kutoka kutokana na msongamano mkubwa huku kila mmoja akiwa na haraka,shukrani ni kwa vibaka wasamalia walioamua kung'oa mabati na kusepa nayo!

    ReplyDelete
  49. Site planner hakuacha Manual, then wabongo should have use FUCKIN GOOGLE lol
    majani was meant to be garden then zege la kupark magari then FOOT PATH kutembelea maana wakipaki kwenye cement watatembea kwenye majani kituko bongo yetu

    ReplyDelete
  50. wabongo tunaumwa mavi

    ReplyDelete
  51. BONGOZ! Nilini tutaacha kutetea upumbafu. We always have answers even for damn stuff. Achana na hawa akili mkichwa waliopanda juu ya toilet seat, ni vigumu kuamini still waosha vinywa wanapojaribu kujustify their wrong doing.

    ReplyDelete
  52. NATIONAL STADUM HATERS ONLY!

    HAKUNA MAKOSA WALA NINI ILA NYIE PIMBI SIJUI MME KULA AMA MMESINDIA MIWA NA MIHOGO MNAKUJA NA KUJIFANYA WHANDISI WA KWENYE VIBANDA VYA BATA SASA KWA TAARIFA YENU WACHINA WAMEKUJA NA DESIGN YAO KAMA MMEZOEA YA HUKO MNAKO KAA POA HII NDIYO STYLE YA BONGO INAPENDEZA SASA KAMA HMTAKI MJINYONE BASI.KWANZA WNGI WENU MSHUKURU HII BLOG MAANASIJUI HIZI HABARI ZA BONGO MNGEZIPATA WAPI WAKATI HATA BONGO HAMWEZI KUJA KWA SABABU VIZA ZIMEKWISHA ZA SHULE AMBAYO HATA KWENDA HAMWENDI KAZI KUOSHA VIBIBI, KWANZA NYIE MNA ALANA NYIE KUCHAMBA VIBIBI LOH!KAMA MNAIPENDA BONGO BASI RUDINI TUENDELEZE RUMBA MNAOGOPA KWENU!

    ReplyDelete
  53. Hivi Mnabishana nini Nyie Wadanganyika...!!!!!!! mnaacha kujadili mambo ya maendeleo kama ujenzi wa daraja la kigamboni,Udhibiti na uimarishaji wa Mfumuko wa bei,Ujenzi wa Dhahanati na Hospitali vijijini, Uimarishaji wa miundombinu kama barabara,mawasiliano na technology mpya na za kisasa Mikoani,Planning za Miji na upanuzi wake,Kilimo cha kisasa, Ufufuaji wa viwanda na ujenzi wa viwanda vipya kwa ajili ya kubadili ghafi kuwa dhamani,vivuko vya majilini mikoana mikoani, mfukowa majanga kama mafuriko na njaa pale yanapotokea na jinsi ya kupambana nayo kabla na si kusubiri pale yanapotokea mfano usindikaji wa chakula e.g national milling na ufufuaji wake,miundombinu ya mawasiliano mfano planning za barabara za mijini na utatuzi wa magari yaendayo kasi, Kujali muda kwa kila jambo,Uanzishawaji na Uboreshwaji wa Taasisi za Utafiti na Ubunifu na mengine mengi kwa ajili ya maendeleo yetu sisi watanzania...... Nyie mnabishana kuhusu parking..!!!! Parking...!!! parking...!!!! kweli!!!!! hivi ukitafakari kwa makini na kuangalia kwa makini sana hiyo snap na muundo halisi wa hiyo parking hupati jibu.. au nyie mnaangalia waliotangulia wamesema nini na wewe uonekane mchangia mada.... Tanzania tunasafari ndefu na mambo mengi ya kufanya.... anyeni kubwabwaja fanyeni kazi kama wajapani na wachina ili hapo mbele mpate angalau kuwa wabunifu au wakandarasi wa nchi za wenzetu na hata nyumbani.....
    Mdau wa Moshi. Kilimanjaro. Tanzania...
    Papaa Stan

    ReplyDelete
  54. Ila siwashanga sana Wadanganyika...... kwani hata Mwalimu kwenye 80's alipoalikwa kwenye chuo Kikuu cha wahandishi wa habari jijini dar es salaamu alisema haya Nanukuu "ndugu zangu mnanishangaza sana leo hii zikaja habari mbili moja mwalimu katembelea mkoa wa kilimanjaro kuangalia mashamba ya ushirika ya kilimo cha kahawa na mwalimu amefuraishwa sana na utunzaji na faida wapatazo wakulima wa zao hilo na amependekeza mikoa mingine iige mfano huo..... heee heee hii kweni ninyi si ya muhimu sana ila ikija habari hii ya pili " mwalimu amepigana na mkewe du....!!! heee heee hiii hata ndugu yako alie nchi za magharibi utamtumia hata barua kumjulisha..." haya si yangu mimi ni mwalimu wenyewe tena miaka hiyo naona bado yapo hadi leo zaidi ya miaka ishirini iliyopita...!!! kweli kazi tunayo na safari ndo kwanza inaanza na sifahamu si jui ni lini tena mtabomoa kazi mlioifanya kwa muda wote na kuanza mwanzo tena...!!!
    Mdau wa Moshi Kilimanjaro Tanzania.
    Papaaa Stan

    ReplyDelete
  55. nyie wote mliotoa maoni hapo juu nadhani hamjaangalia hiyo "layout" ya hapo mbele ya uwanja, nionanavyo mimi ni kwamba hiyo sehemu ya mbele haijawa design kuwa parking ya magari bali ninaweza kusema ni bustani, sema viongozi wetu wameishazoea kuvunja sheria. hata kama kulikuwa kuna ulazima wa kuegesha basi yalitakiwa magari machache sana kama magari yasiyozidi kumi tu. tena yanatakiwa kuegesha kwenye concrete badala ya kwenye nyasi.

    ReplyDelete
  56. WATANZANIA TUKUBALI KUKOSOLEWA NDIO TUTAJIFUNZA, TUACHANE NA VIJITABIA VYA KURIDHIKA RIDHIKA TU BORA LIENDE, INTERNATIONALY WATU WANAPARK MAGARI KWENYE CONCRETES NA SIO KWENYE MAJANI PERIOD. HALAFU PEMBENI KUNAKUWA NA SIDE WALKS ZA WATU KUTUMIA. ETI OH SIJUI WACHINA WANAPAKI HIVYO SO WHAT, KWA HIYO KAMA WACHINA WAMETUJENGEA BASI NDIO HATA KUWA NA BASIC IDEA TU YA MAMBO YANAFANYIKAJE ULIMWENGUNI ILI WALAU NA SISI TUSOGEE SOGEE JAPO KIDOGO TUSIWE NAYO JAMANI? KAMA KUNA WANAOPARK HIVYO NI VERY WRONG, HAKUNA JUSTIFICATION YOYOTE.
    ULIMWENGU MZIMA SASA HIVI UNAPROMOTE THEME YA "GO GREEN" WAKIMAANISHA MAZINGIRA YETU ASILI KWANZA!! TABIA YA KUWA SATISFIED NA VITU SIMPLE SIMPLE KAMA HIVI NDIO VINATURUDISHA NYUMA, HALAFU WATU WAKITOA COMMENTS ILI TUJIFUNZE MNAJUSTIFY UJINGA, OO ETI KWA SABABU MKO NJE NDIO MAANA, UJINGA MTUPU, TUNAPENDA NCHI YETU NDIO MAANA INATUUMA.
    KWELI TUNA SAFARI NDEFU, LABDA TUTAFIKA SIKUMOJA!
    Mkereketwa,
    Canada.

    ReplyDelete
  57. 1)HUYO ANONY ALIYESEMA UWANJA HUU UMDIZAINIWE ETI NA MZEE MUSHI NA ALIKUWA NA PLAN YAKE, BASI HUYO MZEE MUSHI ANA MATATIZO TENA MAKUBWA SANA, KABLA HAJADIZAIN ANGEFANYA RESEARCH YA KUTOSHA KWANZA KABLA HAJACHEMSHA, HUO NI MCHEMSHO WA MWAKA MTAKE MSITAKE.

    2)KUNA MTU HAPO JUU KASEMA ETI PARKING NDANI YA UWANJA NI KWA AJILI YA WAKUBWA TU, BASI THERE'S NO POINT YA KUJENGA UWANJA KAMA KWENYE PLAN YAKO HUJAKEEP INTO CONSIDERATION PARKING ZA RAIA ZITAKUWA WAPI, UWANJA UNAREMBWA HALAFU RAIA WANAPAKI NJE, KWA MAONI YANGU HII ILIKUWA NI UPOTEZAJI TU WA NAFASI.

    ReplyDelete
  58. this area wasn't intended to be parking area at all. if u know chinese architecture and their open space designs then yu will agree that this area wasn't intended to be a parking. ni ushamba wa hali ya juu kupaki magari kwenye majani.

    ReplyDelete
  59. INAWEZEKANA WACHINA WALITOA INSTRAKSHENI YA KUPAKI MAGARI SIKU YA TEREHE MOSI MWEZI WA NNE, AL MAARUFU KAMA SIKU YA MAPIMBI!!

    mdau wa Azania kigogo

    ReplyDelete
  60. Hey Bro Michuzi asante saana kuonyesha uzembe unaofanywa na wa Bongo wa kuendekeza mambo mabaya tu katika jamii, na tukiona nchi nyingine kama Rwanda wanajali usafi tunakaria wivu tu nakusema mambo ya vita we mtu mwenye akiri kabisa ana park gari kwenye nyasi na zege ipo???? yaani mi nashanga TZ imekua nchi ya kuendekeza mabaya mara viongozi mafisadi mara uchawi wa kila aina watoto wanaokunywa damu za wenzao, mara watu wanao uawa ma zeruzeru kwa imani za kishirikina mara wachuna ngozi mara wetekaji sasa hiyo ni amani gani kweli?? yaani mimi natamani niishi irac kuliko Bongo kutokana na ushetani uliyo kithiri katika nchi hii let us pray for our country

    ReplyDelete
  61. Ama kweli wabongo si ni noma wenzetu wote wanaenda mbele si pekeetu ndo tunarudi nyuma vere interesting

    ReplyDelete
  62. KWA KAWAIDA KWENYE CAR PARKING HUWA KUNA PAVEMENTS ! NA UNAWEZA PAVE THE AREA KWA SOLID MATERIALS MBALIMBALI SASA HAO WALIAMUA KUTUMIA KITU KINAITWA GRASS PAVER ! NA HUWA INA MATUNDU/SPACE AMBAZO HUWA ZINAWEKWA UDOGO NA KUPANDWA NYASI ! NA HUWA SEHEMU YA UDOGO WA NYASI HUWA ZIKO CHINI KIDOGO NA SEHEMU YA CONCRETE AMBAYO HASWA NDIO TAIRI YA GARI HUKANYAGA ! NA SEHEMU AMBAYO IMEBAKI CONCRETE TUPU NDIO SEHEMU YA DRIVE WAYS AMBAYO MAGARI HUPISHANA NA KADHALKA ! KWA HIYO HAPO HAKUNA CHA AJABU SANA ZAIDI YA KUFAHAMISHANA NI KITU GANI !NA KWA KWELI HUPENDEZA SANA KWA MBALI INADANGANYA KUONEKANA KAMA NI MAJANI LAKINI YAMECHANGANYIKA NA CONCRETE.
    Mzushi !

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...