Familia ya Rashidi Kisigo, Japan, inasikitika kutangaza kifo cha dada Amina kisigo kilichotokea ktk hospital ya Tokyo Ika Daigaku hospital leo saa saba mchana.
Hivyo basi Jumuiya ya watanzania Japan inaomba michango ya hali na mali ili kuweza kusafirisha mwili wa marehemu kwenda nyumbani kwa mazishi tunaomba michango ya hali na mali kila mtu anaombwa kutoa yen 10000 aliye nje ya japan usd 1000 kupitia bank ya
mizuho,tawi la kokubunji,
tawi namba 275,
account namba 4092974
jina Simba Ally Yahaya
tunaomba ushirikiano wenu wa hali na mali ktk kufanikisha safari ya mwisho ya dada yetu kipenzi , mshauri wetu ,umetuachia majonzi makubwa yasiyopimika, ila ni kazi ya Mungu wote safari yetu ni moja.
Maendeleo zaidi tutawajulisha mawasiliano zaidi piga simu 080-3235-4043 Mweri,090-8451-3632 Kapinga, 080-3414-4460kippaya.asante Ktb Mwenezi D. Mweri .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 25 mpaka sasa

  1. Mna maana kwamba usipokuwa na USD 100o huruhusiwi kuchanga?! nadhani alieandika hili tangazo inabidi kulirudia kwa makini

    ReplyDelete
  2. R.I.P Amina!
    Byabusha Mwingine

    ReplyDelete
  3. POLENI SANA KWA MSIBA. KAMA MLIVYOSEMA HII NI NJIA YA KILA MMOJA WETU. ILA NAONA KAMA MAJONZI YAMEWAZIDIA MPAKA MKAAMUA KUWEKA KIWANGO CHA KUHANI MSIBA. NAFIKIRI MNGESEMA TUU NI KIASI GANI KINAHITAJIKA THEN WATU WATAJITOLEA KWA KADIRI YA UWEZO WAO.

    ReplyDelete
  4. Dola 100 au dola 1000?

    ReplyDelete
  5. Jamani wenzetu huko Japan, mchango wa dola 1000 kwa kila mmoja ni mkubwa sana, kwani wenzetu kusafirisha maiti huko kwenda nyumbani ni kiasi gani mpaka kila mmoja achangie pesa zote hizo??

    ReplyDelete
  6. NAPENDA KUTUMA SALAMU ZANGU ZA POLE KWA WAFIWA.
    LAKINI HUO MCHANGO? YEN 10,000 NI SAWA NA DOLA 100 TU.
    AU KUNA SABABU GANI HASA YA KUWATAKA WALIO NJE NA JAPAN KULIPA DOLA 1000? AMBAYO NI YENI 100,000?

    ReplyDelete
  7. Poleni sana kwa msiba ndugu zanguni hasa kipindi hiki kigumu.

    ila sijaelewa hiyo USD 1000 Mnamaanishi nini?? yaani millioni na upuuzi ooh wenzetu kweli mnapesa!!! yeye ameshakufa sidhani kama kuna kitabu chochote cha mungu kilichosema kwamba yoyote atakaekufa akazikwe kwao, au atakaezikwa kwao atapata ufalme wa mbinguni au kuingia peponi!!!

    USHAURI KWA WANAOISHI NJE YA NCHI: Kama mtu ana imani ya kweli hasa sidhani kama angehangaika kusafirisha hizo maiti toka nje, mie naona kikubwa kitakachosaidia kumuombea marehemu na hiyo michango ambayo mnakusanya kwanini msije kusaidia kwa ambao wako hai wanataseka na dunia hii kama watoto yatima, wagonjwa mahospitalini wanahitaji matibab nje ya nchi hawana uwezo wale ndo wanahitaji msaada na si mtu alokufa, tembeeni vijijini muone, kwanini michango ya kusafirishia watu walikufa msisaidie kwa walio hai ambao wanateseka mtapa malipo kwa mola mie sidhani kama ukitoa msaada kusafirisha maiti kuna malipo zaidi ya kumpa mtu ambae anateseka kama yatima na wagonjwa????!!!

    Tena kwa huyu dada muislam kama sikosei atakuwa muislam yaani katika uislam kumuweka maiti siku zote hizo ni kumdhalilisha na kumtesa ni bora mumzike akapumzike.

    Mungu amlaze mahala pema peponi, Amin.

    KUMBUKENI ARDHI YOTE NI YA MUNGU TU. POPOTE UNAHIFADHIKA.

    ReplyDelete
  8. NAWAPA POLE SANA WAFIWA. NINA SWALI JAMANI. WATU WALIOKO NJE WACHANGIE $ 1000? IMEKAAJE HII? HUO MSIBA SI UTASAFIRISHWA NA WATU WACHACHE TU KAMA NDIO HIVO. DOLA ZOTE HIZO WAKICHANGA WATU 50 KWA MFANO MTAPELEKA WAPI? MNATAKA MRADI? TUWE WAKWELI JAMANI. USA KWA MFANO HATUWEKI VIWANGO. UNATOA ULICHONACHO. NI WAZO LANGU JAMANI. SAMAHANI.

    MDAU - USA

    ReplyDelete
  9. USD 1000?!?!

    ReplyDelete
  10. duh!kwanza poleni na msiba mzito wa dada ila hio ya kuwaomba mchango wa usd1000 walio nje ya japan limekaaje kaaje hilo?si mtakusanya hela nyingi sana kwa mtindo huo jamani wafiwa?

    ReplyDelete
  11. poleni wahusika pia pamoja na pole zetu nawaomba mtupunguzie kima us dlollar 1000 ni nyingi

    ReplyDelete
  12. Nulikuwa nataka kuchanga ila kwa bahati mbaya hazijafika USD 1000 kwa hiyo nasubiri next month nikipata mshahara nitachanga. Poleni sana, mkae na Amani.

    ReplyDelete
  13. Poleni na msiba ndugu wa marehemu. Wote tupo njia hiyo moja may her soul rest in peace.
    Kumradhi Jamani naomba kueleweshwa je mtu aliye nje akitaka kuchanga less na hiyo $1000 mchango hautapokelewa? maana naona tunapangiwa kiwango.

    May Amina's soul rest in peace and the family wawe na uvumilivu katika hiki kipindi cha majonzi.

    ReplyDelete
  14. hairuhusiwi chini ya hizo??maana kama ni rambirambi,wengine wana moyo wa kutoa lakini sio kiasi hicho.

    ReplyDelete
  15. Poleni sana Watanzania Japan.. ila mchango wa dollar $1000 {Tsh.Milioni moja na ushehe} ni nyingi sana jamani.
    Atleast hiyo Yen ¥10,000{Tsh.Laki moja na ushehe} tunaweza kujipiga piga kidogo.
    Bwana amrehemu marehemu.
    AMEN.

    ReplyDelete
  16. poleni sana wafiwa mungu ailaze roho ya marehem peponi amin. sasa kuhusu mchango sasa hii simtu atoe alichonacho au lazima idadi hiyo iliopangwa kwani nnavyojua mimi mchango ni hiari ya mtu na kutoa pia ni imani ya mtu sasa kama mtu hana hicho kiasi kilichopangwa afanyeje na kila mtu na uwezo wake sio wote ambao wanacho au mnasemaje wadau

    ReplyDelete
  17. Poleni sana na msiba uliowapata. Hii ni typo au ni vipi $1000.00 kutoa mchango. Mimi ninafikiri mngeomba tu mchango kuliko kuweka kiwango cha $1000.00 hiyo ni pesa nyingi, mtawavunja watu moyo. RIP

    ReplyDelete
  18. poleni sana wafiwa, wote tuko safarini , mungu aiweke roho ya marehemu mahala pema peponi.Muandishi wa hii habari unakimbiza watu kusaidia kusafirisha mwili wa ndugu yetu unaweka na kiwango kabisa?? kama hana huo uwezo huo ?? ila anacho kidogo anataka kuchangia??

    ReplyDelete
  19. Poleni sana na msiba.
    I am 100% sure that aliyeandika dola elf moja alimaanisha dola mia (100), hiyo itakuwa ni typo tu maybe kwa sababu ana majonzi ya msiba. Ndugu tonakuomba uje uwahakikishie wadau.

    ReplyDelete
  20. POLENI SANA WAFIWA ,MUNGU AIWEKE ROHO YA MAREHEMU PEPONI.
    NAHISI MUANDISHI WA TANGAZO HILI AMEKOSEA KUHUSU HIYO $ 1000 ,ILIKUWA AANDIKE $100 AMBAYO NI SAWA NA Yen 10000.

    ReplyDelete
  21. NDUGU YANGU KWANZA ULITAKIWA USEME NI KIASI GANI KINA TAKIWA ILI KUWEZA KUSAFIRISHA MWILI WA DADA YETU,HALAFU NDIO UOMBE MSAADA, ILI WATU WAKIONA WANAJUA NIKIASI GANI WACHANGE SIO KUWAPANGIA

    ReplyDelete
  22. R.I.P Amina

    Some of you guyz mlioacha comment bila kutumia common sense hio was obvious typing Error sounds like 100 and not 1000 if u kno numbers hapa tunatakiwa kuwa na wafiwa kuwapa pole na sio kubishana kuhusu typing mistake... huyo anon aliyesema usaidie yatima tanzania naye anajua ni kiasi gani ina cost kuzika mtu nje ya nchi? je ndugu za marehemu watawezaje kupata fursa ya mwisho ya kumuaga mpenzi wao? lets just use common sense

    this was not something to write wenzio wakiwa na majonzi

    May her Soul Rest in Eternal Peace AMEN

    ReplyDelete
  23. Asalaam aleykum, Inna lillah wainna ilaihi rajuun
    Poleni sana na msiba ndugu zetu wa japan'
    Mimi binafsi yangu sijaelewa kwann muwapangie watu michango, Hivi hamjui mwanzo wa wingi ni moja? sasa ina maaana mtu kama hana dola 100 asitoe??? Mimi sijawahi ona michango ya kupangiwa labda ni kwa wana familia na sio watu baki.Kama mlitaka zote hizi mngeweka insurance ya kifo mngepata hata us dollar 100,000 au zaidi.
    Ila nahisi ni kuchanganyikiwa ndo maana mmeweka kiwango hivi mnajua dollar mia mtu anaipataje???


    Mdau Amsterdam

    ReplyDelete
  24. Poleni wafiwa lakini hata kama ni typo error kweli kuwapa watu kiwango cha kutoa sio jambo jema. Kama hao watu ni wa umoja wa jumuiya yao ni sawa kuwaambia hivyo lakini tulio nje ya japan kuambiwa ni lazima kutoa $100 mhhhhh

    Sisi huku wenye kuambiana kiwango cha kutoa ni wale tlio katika community moja wa nje ya state wala huwaambii ni lazima kiasi fulani kitolewe. Na watu wanatoa kwa moyo wote kutokana na uwezo wao.

    Na huyo anayeuliza kwanini tusizikage huku huku...kwanza kumbuka ndugu yako akizikwa nje ya mahali hata siku moja hamtaweza kwenda kutazama kaburi sio vizuri na nadhani unafahamu hilo. Pili kuzika huku miji mingine gharama ni hizo hizo kama kusafirisha kama imepungua ni hela chache sana.

    Mungu awape faraja katika kipindi hiki kigumu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...