roho iliniuma sana kukuta mgambo hawa wa jiji wakisanya biashara ndogondogo za machinga sehemu ya magomeni usalama, dar. nikawa najiuliza hivi hawana kazi ingine zaidi ya hii?
wadau mnasemaji juu ya hili, ukizingatia jiji lina mambo mengi ya kusimamia ikiwa ni pamoja na kugomboa viwanja vya wazi zilivyotekwa na wenye nazo, kupigwa kufuli kwa bustani ya mnazi mmoja garden na mambo mengine ikiwa na kupiga uzio fukwe za bahari ama kukatazwa kufanyia shughuli kama za harusi na kadhalika. hapo sijaongelea usafi kulinganisha na jiji la kigali. hii imekaaje wadau?
-michuzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. its about time we stand up for those who cannot defend themselves. what the police do to these petty traders is ilegal and wrong. at the end of the day they will become theaves.
    So next time you see them do these terrible acts DO SOMETHING!
    A VERY ANGRY
    TANZANIAN

    ReplyDelete
  2. Hiyo haijatulia Michuzi Mgambo wa jiji wanashughulia kazi zenye ulaji wa moja kwa moja kwanza!! kufunga magari...kuzuia watu kukaa beach...na mambo kama hayo!!Naona ulipiga hii picha ukiwa kwenye gari...ulikuwa unaogopa kichapo wangekustukia unawachukua ze taswira? hadi wajue Wewe ni michuzi...aaahh ngeu mbili tatu tayari mwanawane!! na siajabu ulikuwa tayari kwenye gear ya kuondokea!!! aminia

    ReplyDelete
  3. ahh infact kaka yangu ukikaa na kutafakari baadhi ya mambo yanayoendelea katika nchi yetu kweli unaweza kububujikwa na machozi. Nimefurahi saana kwa topic yako hii ya mgambo na machinga hii hua inaniumiza saana roho ila tu hakuna la kufanya. Unakuta maskini kijana anajitafutia riziki yake hana mtaji mkubwa wa kusema afanye biashara kubwa mtaji wake ndio unamruhusu yeye kuuza chewing gum, kama ulivyoshangaa kuwa hawa mgambo hawana kazi zingine ukiwakuta wanawatuhumu wamachinga huwezi kuamini kama kijana anayefanyiwa hivyo ni kijana anayejitahidi kutafuta riziki yake ya halali utasema ni muhalifu mkubwa, vijana wanakua treated vibaya mno wanabebwa vibaya na sometimes hata kupigwa virungu yaani anavyochukuliwa mbakaji na mnyanganyi ni tofauti kabisa na hawa vijana. Ama kweli mnyonge siku zote ndio anayeonewa. kaka michu ukistaajabu ya musa utayaona na ya firauni.

    ReplyDelete
  4. UKIONA HIVYO UJUE NI MUENDEKEZO WA NJAA KWANI HATA HAO MIGAMBO SIDHANI KAMA MPAKA WANAENDA KAZINI KAMA HATA CHAI WALIPATA !!!! TUMEZIDI KUENDEKEZA NJAA ZETU BADALA YA KUFANYA KAZI ZA MAANA BASI WAO NI KUWAONEA HATA WANAOTAFUTA RIDHIKI KWA TABU !!!! MH. KIMBISA WAPE SHULE/SEMINA HAO VIJANA WAKO KABLA YA KUWAPANGIA KAZI

    ReplyDelete
  5. Asante sana mdau uliyeleta hiyo picha ya mgambo wa jiji. Ukweli ni kwamba hao mgambo wameajiriwa bila job description sasa inabidi wakamate kamate watu hovyo ili kuhalalisha uwepo wao. Naomba tushirikiane kuwatengenezea JD kama ifuatavyo halafu Michuzi aifikishe kwa rafiki yake Meya Kimbisa:
    1. Kusimamia usafi mkubwa kwenye kila Kata kila Jmosi ya mwisho wa mwezi.
    2.Kukamata viongozi wa mitaa michafu na wale wasiotenga maeneo ya kutupa taka.
    3.Kukama na kuwafikisha mahakamani watu wote waliojenga kwenye viwanja vya michezo kwenye makazi yetu.
    4.Kukama wanaokusanya kodi za magulio bila kufanya usafi wa masoko.
    5. Wafanyakazi wa jiji wanaojidai kusafisha mitaro ya maji taka, wanazoa uchafu na kuuacha kando ya barabara za jiji nao KAMATA!

    List iendelee...

    ReplyDelete
  6. Hii ni kutokana na kuwa nchi zetu hizi hazina kitu kinaitwa NGUVU YA UMMA. Vitendo kama hivi vya uonevu vinafanywa mbele yetu na hatuna hata uwezo wa kalalamika na kuvipinga, mgambo wa jiji wameisha geuka kundi la wanyang'anyi. Ni jamii tu yenye uwezo wa kushinikiza ukomeshwaji wa tabia hizi chafu

    ReplyDelete
  7. Michuzi nunua gari nyingine, kama hii ninayoiona hapa ni katika kio cha mlango wa gari yako basi ni nze na imechoka sana.
    Chukua gari mpya achana na mambo kuhusu hao mgambo wa jiji Wanafanya kazi yao waliotumwa na sheria ya jiji , inayowapa mishahara yao.Wakale wapi, ni sawa na wewe unavyowapiga picha , bila kupiga picha huenda ungekuwa Polisi.

    ReplyDelete
  8. Naombeni mnisamehe nitakuwa tofauti na watoa maoni walionitanguliia kidogo. Hivi kila mtu leo akiamka na kujisikia kufanya biashara zake popote anapojisikia itakuwaje? Miundo mbinu ya jiji hili ni mibovu tokea mwanzo ndio sababu jiji linajiwekea limit ya sehemu za biashara ndogo ndogo na pia kupunguza magonjwa ya mlipuko kama Pindupindu na nk. Hapo Magomeni ndio usiseme utakuta machinga kibao na vitoroli vyao wanamenya machungwa na mananasi wameziba service road!! Hiyo ni sawa? Hayo matunda wanayomenya na kuuza wanayaosha? Ni kweli pale kuna biashara sana sababu ni kituo kikubwa cha madalala, Na wale wa Ubungo je? kila siku wanafukuzwa lakini wapo tuu!! wanaziba njia ya waenda kwa miguu ukijaribu kukatisha huku wamepanga nyanya, kushoto wamepanga samaki za kukaanga, ivi nyama yakuku iliyokaangwa, vile mashuka, mapazia viatu vya mtumba, t-shirt za mtumba, karanga sigara ubuyu, vyombo vya jikoni n.k. yani vyote ivyo wamepanga njia ya waenda kwa miguu na inakuwa ni kero ile mbaya. Nyie mnaowatetea naona mna magari kama mpiga picha wa picha hapo juu. CHA MUHIMU SERIKALI INASAHAU KUWATENGEA HAWA NDUGU ZETU SEHEMU YA BIASHARA ZAO. SERIKALI YETU IMEKUWA YA KIBABAISHAJI. Ingewafikiria tokea mwanzao kuwajengea sehemu ya biasahara kama wanavyofanya pale KARUME sasa. Kuwafukuza bila kuwapa mitaji na maeneo sahihi ya biashara zao ni kazi buree. Kero hii itaendelea tu ispotafutiwa ufumbuzi yakinifu. Ni mimi M-TZ mwenye uchungu; Nanyori.

    ReplyDelete
  9. Wewe anon unayemwambia mwenzio ange "do something",ungekuwa ni wewe ungefanya nini wakati hicho ni so called "chombo cha dola" na wewe ni raia na unahitaji kulindwa na hicho hicho chombo cha dola kinachomnyanyasa mwenzio?, kama hakikumlinda mmaching awewe utafanya nini? Naomba utujibu ili na sisi next time tukiona unyama huu "to do something".

    ReplyDelete
  10. Hawa mgambo wakikamata mama lishe, wanachukua msosi na kwenda kuukandamiza wenyewe!!!!loo njaa hizi!!!balaaaaaa

    ReplyDelete
  11. WALE WANAOSHANGAA KUMUONA JEETU PATEL AKIPITA MAONEO YA ST.PETER KWANZA WATUELEZE HAWA WAHINDI WALIOPO TANZANIA WOTE HAWATENDI MAKOSA, NA LINI WALIKUTANA NA MFUNGWA MHINDI! TUNAWAONA MAHAKAMANI TU KISHA WANAYEYUKA KAMA MVUKE. KESI ZA JEETU HAZIJAANZA LEO, YEYE NI MZOEFU MAHAKAMANI SIKU NYINGI TU.

    ReplyDelete
  12. Jamani waacheni mgambo kwa kweli wa manispaa ya Ilala wala sio wa jiji. Hawamhusu Kimbisa bali meya abuu jumaa. Tangu lini machinga akawa na mtaji. Hivi hamjui kuwa hawa ni mawakala wa wahindi wenye biashara kariakoo na kwa kuuza hizo bidhaa hao wahindi wanakwepa kulipa kodi. Hongera sana mgambo kwa kuwashughulikia machinga. Kwanza jengo lao karibu litakuwa tayari. Subirini na muone kama wataenda kwenye hilo jengo.

    ReplyDelete
  13. Jamani acheni haya comments about wahindi's... wahindi, waafrika, warabu na sasa
    wachina wote wapo kariakoo...jamani tu ache
    kuwaonyea hawa wahindi...wahindi wote wale wapo kariakoo wanalipa kodi zao...na wasipolipa wantishwa na hawa watu wa trc au mgambo...kwamba tutakupelekeni kituoni msipotoa chai...wengi sasa wanaacha mabiashara zao na kuondoka huko ulaya amabapo wengi wanaendelea na mabiashara zao...wahindi wengi wamesha hamia kutoka singida, itigi, moshi, mbulu, karatu, etc etc...na sasa hizo towns are empty...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...