Mh. Balozi wa Zain na Mkuu wa wilaya ya nanihiii,

nakupa zawadi hii wewe na wadau huku nikiwa na dukuduku moyoni, kufuatia ubishi mkali uliozuka kijiweni kwetu leo. Natumai wewe na wadau mtachangia ili kieleweke.

ubishi wenyewe ni kuhusu hizi simu za mkononi. unajua, kuna wengine wakiwa na mai waifu ama mai hazbendi wao huwa inakuwa nongwa sana kwa mmoja kugusa simu ya mwenzie, iwe kimya ama inalia. utakuta mmoja ama ni wote ni wakali kweli mwenzie akigusa simu yake kupokea ama kupekua meseji.
Tena wengine utakuta hata akienda bafuni kuoga anaenda nayo, hata kama kavaa taulo ama bukta isiyo na mfuko, na huko bafuni nako ukute hata sehemu ya kuiweka. ataoga kwa kutumia mkono mmoja kashika kata mwingine kashika simu. alimradi hachezi mbali na simu yake mamsapu akiwepo.

sasa bwana, tunaomba moani. kipi sahihi hapo. kila mtu ashike lake na asimbughudhi mwenzie na simu yake ama wote wawe huru na kuachiana.

Naomba Kuwasilisha

Mdau

Ilala Shariff Shamba, Dar

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 23 mpaka sasa

 1. huyo ambae mpaka bafuni anaenda nayo basi ujue ana lake jambo..normally it shouldnt be a big deal. simu ikilia unapokea,meseji unapokea simu si yako bwana?kuwa huru..and when you are faithful,mwenzi wako wala hata kuwa na haja ya kupekua pekua,ila hata kama atapenda kupekua pekua,hamna lolote la kuhofia,si upo faithful bwana? mi naona wanaozificha ficha ni ma fisadi tu!

  ReplyDelete
 2. kwa upande wangu nadhani trust na respect ni muhimu.

  Mimi mvivu na sipendi simu basi tu. kwa hiyo hata yangu ni uvivu kupokea au kama ni tx msg kusirudisha ni kazi....Kwa hiyo wala siwazi kupokea au kuanza snooping or easy dropping kwenye simu yake.

  Kama mtu sio mwaminifu hata ukimuandama vipi kama mtu anacheat atacheat tu na anayecheat you will never find any suspecious number on his/her phone....kwavile atakutime.

  Na sijui huko bongo lakini hata kama anakeep his phone all the time with hime lakini ukitaka kama hamna paper bills zinazokuja pia you request na unaletewa na utaona simu zote zinazotoka na kuingia kwa mwezi mzima kwenye simu yake just by calling the CS na kuomba...Kama wewe ni mume na mke means account mnashare so you have the right to get all the information.

  lakin it doesn't worth kama trust hamna means hiyo ndo imeshaisha imebakia picha tu

  ReplyDelete
 3. we anony wa 1.12AM ni mnafiki. simu ya mkononi ni personal. mtu mwingine kuipekua au kupokea ni ishara mbaya ya kuingilia uhuru wa mtu. Ili mtu mwingine aweze kuipekua au kupokea inabidi anayefanya hivyo awe amepata ridhaa ya mwenye nayo. full stop.

  ReplyDelete
 4. topic imenigusa
  Sioni haja ya kuogopa simu yako inaposhikwa na mamsapu kama upo perfect.Kama una "vimeo" nje ni bora usivipe number yako anayoijua mamsam,bongo handset mpaka ya elfu 20,000 unapata wakati line ni tsh 100 so ni bora ununue handset na line special kwa ajili ya vimeo tu na muhimu ni kuhakikisha simu hiyo haikanyagi anga za nyumbani.Namaanisha kama ni mfanyakazi basi ni kuhakikisha simu hiyo inalala, kuamka na kushinda ofisini but ole wako uende nayo nyumbani!!!!!!!!!umevunja ndoa. Yote kwa yote UKIMWI upo na VIMEO vinaongoza kwa kugawa
  ni hayo tu

  ReplyDelete
 5. Mimi ni mvulana naelekea utu uzima nina mke. Kusema ukweli sijatulia. napenda sana medemu bomba. Mara zote simu yangu ndio chanzo cha ugomvi na maiwaifu(My wife. Hii inatokana na sms za mapenzi, appointments nk. Maiwaiu kila ninapoacha sim yangu lazima aipekue iwe nimelala au nimeiicha tu.Nimejaribu ku-save majina ya wanawake kama ya kiume. Lakini sms ndio zinaniumbuaga. Sasa hivi nimenunulia line (namba) nyingine amabyo ni siri yangu mimi na madem zangu. Ninaiacha ofisini au nikifika home ninaiweka ndani ya kiatu yaani uvungu wa ulimi wa kiatu. Shida hii inaninyima raha na amani kwani kwani wife akijua ni msala.Naungana na mtoa mada ni kweli simu ni keroooo, bora zisingekuwepo.
  Sasa hivi naona bora tu nimtafute Mungu niachane na upuuuuziii huu, hata lini nitakuwa najificha ficha???

  ReplyDelete
 6. Simu ya mkononi inakaribiana sana na vitu ambavyo mtu anaviweka moyoni mwake bila ya mtu mwingine kuvijua... huwezi kufungua moyo wa mtu na kuujua awazalo na afanyalo halikadhalika simu hizi zinaficha sana mambo au vitu 'partener' wako asivipende na hatakiwi kuvijua... ukiviona sana sana utaumia mwenyewe ni vitu 'personal'basi viwe siri.... Mdau from Upanga

  ReplyDelete
 7. Kupokea simu ya mwenzio wkt haupigiwe ww sio uungwana na sio tabia nzuri. Anayepiga anamtaka mkeo wewe mume unapokea ya nini?! We acha kama mwenyewe hayupo akirudi atakuta missed call yake.

  Ila suala la kutumia simu ya mwenzio kama kusoma message, kubrowse phonebook, call register, nk hakuna ubaya wowote. Ila hii ni ngumu kwa wasio waaminifu. Na ukiona mtu anakatazia simu yake basi jua tu sio muaminifu, hilo halina ubishi.

  Na ukiona wanandoa wamekualiana kila mtu asiguse simu ya mwenzie basi wote SIO WAAMINIFU, Wana maovu ya machafu wanayo yaficha.

  WASIRI WA SIMU SIO WAAMINIFU, full stop.

  ReplyDelete
 8. Hasiyetaka simu yake iguswe ujue amejaza vimeo huyo,kama unajiamini huwezi kufanya hivyo ni ukicheche tu ndo unaoasumbua yaani fikuria mtu simu yake mwenyewe lakini anafikia hatua yakuficha line kwenye kiatu si ujinga huo na kujikosesha raha,haya mambo yapo tu wazuri wanazaliwa kila siku sasa ukutaka kubadilisha kila siku utaishia pabaya ni vema ukatulia na mmoja uliyenaye na mkaaminiana

  ReplyDelete
 9. Kama alivyosema mdau ni kutokuleta mademu yako kwenye simu yako personal kama una mke. Mradi umeamua kuoa hakuna kitu personal tena kila kitu pamoja una taka personal be single. Mi mwanamke si pekui simu LAKINI ukianza kujishuku heti ukienda jikoni waichukua, au bafuni unaogopa kuiacha nikiwepo yaani unachunga simu yako my friend hapo umenipa sababu ni pekue vizuri.Hutaki kupekuliwa simu basi give me respect.

  ReplyDelete
 10. simu yako yako tu hatakiwi mtu yoyote kugusa labda uwe umempa ruhusa wewe mwenyewe.mke wako hatakiwi kugusa simu yako iwe tu umemruhusu wewe. cha msingi uaminifu tu.

  ReplyDelete
 11. Yaani hao wanaosema eti hakuna kuingiliana kwenye simu wananishangaza sana, tena hasa katika dunia hii ya leo ambao ukimwi uko kila kona. kwanini watu tusibadilike na kuwa faithful kwa mpenzi mmoja? na ukihisi umemchoka ambianeni ukweli hata kama ikiwa baada ya miezi mitatu muachane na utafute mwingine it doesnt matter nae utakaa nae muda gani lakini at that time uwe nae peke yake. kuna wakati mtu huitaji kuangalia simu ya mwinzio ila kuna mazingira ambayo yeye anayatengeneza yanakufanya utake kujua zaidi kulikoni. kwa mfano utakuta mume/partner wako mko nae na before simu zenu mlikuwa huru kila mmoja kuzushika lakini ghafla mwanaume anaanza kutwa simu iko mfukoni na akilala kama iko ON italazwa chini ya mto. mwisho anaona yote hayo haitoshi anaamua ikifika saa 3 anazima kwa madai hataki usumbufu wa kupigiwa simu usiku. cha kushangaza nategemea ukishazima simu si uiache tu lakini tena inafikia mtu ameizima simu na bado anaificha mara juu ya kabati, mara kwenye suruali, mara kwenye gari na asubuhi akishaingia tu kwenye gari lake anaiwasha. hebu niambieni huyu mtu anachokificha ni kitu gani? na kwanini ahangaike na kupata mateso yote haya?? na ikumbukwe mtu kama huyu mara kadhaa hapo nyuma ishatokea umeshika simu yake baada ya kuona mambo hayeleweki na kukuta sms za mapenzi kwa wanawake tofauti ambapo atatoa sababu lukuki na kuwakana!! hivi ni kweli jamani anaificha simu baada ya kuzima kwa sababu pia hataki usumbufu wa simu za usiku au ana yake???

  ReplyDelete
 12. Anon wa kwanza "easy dropping" ndio nini?, jamani kiingereza hikiiiii

  ReplyDelete
 13. unapekua simu ya mwenzio ya nini? kama wewe ni mke/mume basi kuwa na amani. Mwamini mwenzio na mwache awe huru. huo upekuzi utaleta ugonjwa wa moyo bure. kuna wengine hata ukipekua you will never get a clue kwasababu anakuwa very smart. simu zozote za nyumba ndogo mwisho ni saa moja usiku na akifika nyumbani anahakikisha msg zote za ajabu ajabu zimefutwa pamoja na calls zote...sasa utafanya nini? muhimu ni kuheshimiana...ukiona unahangaika kuficha ficha mambo au kupekua pekua basi huna heshima wala amani kwa mwenzio actually hukuwa tayari kuingia kwenye ndoa.

  ReplyDelete
 14. Huu mtundiko uko poa sana, mi nina swali moja, kama mnapendana kwanini kuwepo na siri kati yenu kama ni mke na mume hakuna siri tena kati yenu hata katika biashara za kawaida na maisha ya kawaida hivyo kwa mwenzi wako kupokea simu yako ni kitu cha kawaida sana hao wanaosema ni personal ni wale wanaofanyia mapenzi gizani wako kwenye ndoa lakini wanajificha. It's not a big deal lakini kama hampendani ndo hapo kunaanza kuwa na siri kati yenu.

  ReplyDelete
 15. Hii mijadala mingine ya uswahilini inabidi izungumziwe hukohuko.. kavaa bukta au Taula au kabeba kata??????? Siyo watu wote humu wenye vyoo vya kiswahili ndugu yangu..Majority vyoo ni vyumba vya kupumzikia...kwa hiyo kuchukua simu is not an issue..

  ReplyDelete
 16. Wewe uneyesema unapenda vimwana sasa kwa nini msiachane uendeleze ujana wako tu? Huoni unahatarisha maisha ya mwenzako?

  Nachukia haya maisha na culture zetu za watu kufikiri kuoa au kuolewa ni kupata heshima. Kumbe kuna watu wengine ndoa zao ni za watu kuwaona tu nje lakini ndani kila mtu analala kitanda chake. Ni heri niwe single forever kuliko kuolewa ili kuwafurahisha watu wengine.

  Na hizi ndoa zetu za bongo "till death do us apart" wala hazina mpango. Umasikini wa wanawake kuolewa wakiwa wadogo bila kuwa na elimu au career itakayoweza kumsaidia kuishi bila kutegemea mwanaume, dini zetu za kikristo zisizo na talaka, na hakuna sheria za kuprotect mwanamke na watoto once ndoa ikiisha ni shida sana. Ni heri ingekua easy kupata divorce kama it doesn't work kila mtu achukue zake. Kuliko kuishi na mtu ambaye feelings zako ziko kwa wengine.

  Kwanza wewe unayefichaficha utapata heart attack watch out. Wasiwasi sio mzuri kama umri umeenda.

  ReplyDelete
 17. topic imenitachiiiiii!!mie jamani wadau nina boyfriend yeye kutwa kutizama simu yangu na akipiga mtu lazma aulize nani huyo wakati yeye akipokea anenda kuongelea chooni! mie naona solution ya hii kitu ni kuweka security code kwenye cmu ...basi! kila mtu awe na uhuru wake bwana ahhh!

  ReplyDelete
 18. Hivi tunazungumzia mahusiano gani? Ndoa au boyfriend/girlfriend?? Kama watu wameoana, then inabidi wakasome vitabu vya mungu vinasema nini (two shall become one). Unless simu hiyo ya mkononi ni ya ofisi, kwa maana unapata simu za kikazi then si sahihi mtu yeyote kuijibu. Kuna wengine wanaweka password kwenye simu zao maana huwezi kujibu kama huna hiyo password (sijui kama bongo ipo hii). Mume na mke hawana sababu ya kufichiana simu kama ndoa yao ni safi. Wazazi wangu wanashare simu ya mkono (nazungumzia watu waliokaa kwenye ndoa miaka 40). Hii yote inaonyesha jinsi jamii inavyopotea, na hii yote inaletwa na kutokuwa waaminifu katika mahusiano yetu. Kwa nini ubebe simu chooni? KUNA NINI? KUNA NINI KAMA MKEO AKIPOKEA SIMU YA RAFIKI ZAKO NA KUKUPA KAMA UPO BAFU AU UNAFANYA SHUGHULI NYINGINE? WOTE WANAOFANYA HIVI KUNA JAMBO WANAFICHA, NA WENGI WALIOPATA NAFASI YA KUZISOMA MESSAGE ZA WATU HAWA WAMEGUNDUA MENGI KUWA WAPENZI WAO SI WAAMININIFU. THIS IS ONE OF THE SIGN SHOWS YOU THAT YOUR SPOUSE IS CHEATING ON YOU. GOOGLE "HOW DO YOU KNOW YOUR SPOUSE IS CHEATING?" MAJIBU UTAKAYOYAPATA UTACHOKA MWENYEWE. KAZI IPO????????

  ReplyDelete
 19. Wanawake walio wengi ni wambea na hawawezi kutunza siri za wandan wao,akiona lolote lazima aliongee kwa watu wa nje,hii inafikia hatua wanaume kuwa wasiri kwa wake zao.Heshima na kutoropokaropoka ovyo ni kitu kikubwa sana ndani ya nyumba,kasoro hii yaweza kukufanya usiruhusiwe hata kugusa simu ya mumeo na hata kuiona ndoa chungu.Roho mbaya pia,wanawake wengi roho mbaya zimewajaa,msg yoyote itokayo kwa ndugu wa mume inaweza kupewa maana tofauti na kuleta mifarakano na kutoelewana ndani ya nyumba.

  ReplyDelete
 20. hii kero ya simu ni kila nyumba topic nzuri sana mie ugomvi hauishi kwaajili ya sms zengine niwrong number lakini mupenzi haelewi kwahio sasahivi simu yangu full pasword na ipoipo tu huwezi kufungua kitu chochote bila password na tatizo lengine sie wake zetu wasiongea kiswahili ukipigiwa na mwanamke anaongea kiswahili basi mke wako balaa tupu mwanzo wa matatizo makubwa nyumbani ni cellphone na ndo inaleta deal kwahio kuiacha haiwezekani bora kuwa mwaminifu tu hunahaja ya kuzimisha simu nyumbani wala kuificha unawaambia ukweli una mke wako wasikupigie simu usikua au una stick kwa mkeo full stop lakini sie mijana mume wa kibongo hatutosheki na na demu mmoja ndo tatizo hahahah mke wangu cell phone anaitaa trouble maker hahah kazi kweli usanii umetuzidi

  ReplyDelete
 21. Simu ya mkononi ni kama chupi, wengi hawavaliani lakini wengine wanavaliana.
  Kama mwenza wako ameamua kujipinda nje utang'ang'ania simu utachoka atajipinda tu. Kama humwamini au hauko tayari ku-shea na usiowajua bora uchukue njia yako umwache na yake kuliko kutafuta ugonjwa wa moyo.

  ReplyDelete
 22. Mada nyeti hii!!!
  Ukisikia mtu ameoa au ameolewa kwa bahati mbaya au premature ndio haya yanayozungumzwa hapa. Mimi nilifikiri watu wakishaoana wanakuwa mwili mmoja, na chochote alichonacho mke au mume yeyote kati yao ana haki ya kutumia iwe simu, gari, sahani au shuka. Haya inakuwaje mnakuwa wakali katika simu tu wakati account za bank mnashare??? ipi kati ya pesa na simu ni hatari kushare?? Ni privacy gani au uhuru gani unaodaiwa hapa? kwenye simu kunamdudu gani anayetufanya tutengane kwenye kuitumia?. Kwa nini mke au mume akigusa simu yako unakuwa bogo na akichukua pesa kwenye kabati au mezani unamuuliza taratibu? Hapo ndipo penye hekima. Mimi sioni kama mke anafanya kosa kukagua/ kutumia simu ya mume na vilevile mume kucheck ya maiwafu. Watu wengine wakiachiwa huru wanakuwa huru kweli kweli mwishowe wanaleta kifo Ukimwi, ni heri mume amlinde mke na mke amlinde mume kwa kila hali, kama ni kwa kukaguana simu, pesa, masaa ya kurudi, marafiki nyendo zetu, mikoba briefcase nk ili mwenzi asijaribiwe au asijisahau akaishia huko mzimamzima. Hata kama jamaa au mamaa ni mroho wa virukanjia itafika mahali speed itapungua kidogo si sawa na kumuacha huru tu.

  Kinachoniudhi saaaaana ni pale mgeni au rafiki anapovamia simu ya mwenyeji wake au mgeni mwingine na kuanza kuipekua akijidai anaangalia model. Hilo kwa kweli ni balaa ila mke au mume RUKSAAAAAA!!!! ni hoja tu!!

  ReplyDelete
 23. Kiingereza hiki, 'easy dropping' nadhani ni 'eavesdropping' yaani kusikilza habari/taarifa ambayo haikuhusu bila ya mhusika kujua. Wataalamu watanirekebisha. Hii mada ya cm ya mkononi, we acha tu. Mi niliamua kutoipokea hata ilie namna gani au msg ziingie ngapi. Najua nilikuwa najidanganya kuwa everything is cool lakini niliamua kuwa nisilolijua halinisumbui, hawa waume zetu, we acha tu

  ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...