*Matangazo kurushwa nchini kote
*Yanalenga kuuelewesha umma zaidi kuhusu Safari Lager
*Safari Lager yaendeleza historia yake
*Yanalenga kuuelewesha umma zaidi kuhusu Safari Lager
*Safari Lager yaendeleza historia yake
Safari Lager, kilaji kinachoongoza kwa mauzo hapa nchini inazindua matangazo mapya yanayokusudia kuendeleza mvuto iliyo nao kwa wanywaji wake wa kila siku na wakati huo huo kuvutia wanywaji wapya.
Matangazo hayo yanakuja baada ya bia hiyo kuzindua sura yake mpya jijini Dar es Salaam mwezi uliopita ambayo bado inaendeleza utamaduni, ladha pamoja na ubora lakini sasa katika muonekano mpya na wa kisasa. Matangazo hayo yatarushwa kwenye televisheni na radio nchini kote.
Akizungumza sambamba na uzinduzi wa matangazo hayo, Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) David Minja alisema, “Tunafuraha juu ya matangazo haya ambayo yanafuatia uzinduzi wa chapa mpya ya Safari Lager.
Ni muhimu kwa wanywaji wa bia hii kuendelea kujua kuwa bia yao ina sura mpya lakini imebaki na ladha ile ile pamoja na sifa nyingine zote zinazohusishwa nayo. Matangazo haya yanakusudia kusisitiza ujumbe kuwa bia hii inaendana na Mtanzania mchapakazi wa kawaida.”
Matangazo hayo yanaonyesha uzuri wa Tanzania yakiwemo maisha ya kila siku yanayojumuisha watu wanaofanya kazi na kuifurahia kwa moyo wa umoja na kujivunia uchapaji wao kazi. Kuanzia wavuvi hadi wakulima, wajenzi hadi wachimba migodi, wafanyakazi wa maofisini hadi wacheza ngoma za asili wote wakifanya kazi kwa pamoja na baadaye wanajumuika kusherehekea urafiki na umoja wao. Kwa kawaida Safari Lager inahusishwa na wachapakazi ambao kila siku inapomalizika hujipongeza na kufurahia matunda ya kazi zao.
Fimbo Butallah, Meneja wa Bia ya Safari Lager alizungumzia matangazo hayo kwa kusema, “Huu ni wakati muafaka kwa matangazo haya kuzinduliwa kwa sababu watu tayari wameshaiona sura mpya ya Safari Lager, lakini ni muhimu pia kwao kuendelea kuifahamu bia yao. Kwa kulifikia soko letu kwa ndani zaidi kupitia matangazo yanayoendelea kuwepo kila wakati tuna uhakika kila mnywaji ataweza kuielewa na kuikumbatia zaidi bia yetu na kwa kufanya hivyo kuwa sehemu ya sifa zake.”
Mara ya mwisho Safari Lager kuzindua matangazo kama haya ilikuwa mwaka 2003 na haya ya sasa yanakuja wakati ambapo bia hiyo imeongeza mauzo na umaarufu wake hasa kutokana na kujihusisha kwake na michezo kama mpira wa miguu ambapo mapema mwaka huu ilidhamini mashindano ya Taifa Cup.
Vilevile bia hiyo ilidhamini mashindano ya taifa ya pool yaliyofanikiwa kupata timu ya taifa iliyoshiriki mashindano ya kimataifa nchini Swaziland pamoja na mbio za baiskeli za Dar es Salaam zilizofanyika hivi karibuni.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...