JK akiamkiana na dogo katika mojawapo ya ziara zake mikoani hivi karibuni

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Shikamoo,naomba dala.

    ReplyDelete
  2. DOGo anamuuliza JK, ivi kuna siku na mimi ntaja kuwa kama wewe....JK anajibu YES YOU CAN

    ReplyDelete
  3. Inaonesha ni jinsi gani viongozi wetu walivyo na maisha mazuri na wananchi wakiwa na maisha mabaya na ya kutisha, Ni Khali halisi ya kila Mtanzania wa chini dhidi ya mafisadi wetu.

    Ni noma ile mbaya, we cheki tu tofauti iliyopo!! Wafadhili wakiona hii picha sijui kama tutapewa misaada, cheki nguo ya dogo, cheki khali yake, cheki JK ndani ya ndinga la mamilioni, cheki hali ya JK... Ni aibu kubwa.

    ReplyDelete
  4. Michuzi Hii picha ina eleza mengi sana kuliko maneno. Picha hii imenitachi sana. Hawa viongozi wetu hawaoni aibu? Angalieni wenyewe hiyo gepu ya kati ya wanaoongozwa na wanaoongoza. Bila kubadirika Tanzania itakuwa nchi masikini kuliko zote duniani. Naona wageni tu ndiyo waokula raha bongo. Kila gari zuri au jumba zuri ujuwe ni mali ya mhindi au mwarabu au mchina au mzungu au kaburu kama ni mzalendo ujuwe huyo ni jambazi au la ni fisadi. Jamani tuiokoe nchi hii tunaenda kubaya tutakuja kuuwana huko mbele.
    Mdau Stockholm

    ReplyDelete
  5. Kwa nini Marais na viongozi wetu wanakaa siti za mbele kwenye gari? hii sio sahihi, kiongozi alitakiwa akae siti ya nyuma.

    ReplyDelete
  6. ...Two very DIFFERENT Worlds...!

    ReplyDelete
  7. Nakubaliana na mdau wa 5:33 PM kwa asilimia mia moja. UMENENA YOTE

    ReplyDelete
  8. sasa wewe wa hapo juu yangu unataka sasa jk atembee kwa mguu au?,au agawie hela kila mwananchi,hiyo siyo kazi ya serikali.huwa nashangaa mnaotumiaga muda mwingi kulaumu bila kutumia akili ulizopewa kufikiri.umaskini upo na utaendelea kuwepo pasipo kujibidiisha ukidhani rais atagawa hela mtaa kwa mtaa.

    ReplyDelete
  9. Anony wa Tarehe November 11, 2008 9:22PM, Unataka kusema kazi ya serikali ni kuwa mafisadi ktk nyanja za madini, nishati aka Richmond, EPA, na wizi mwingine mkubwa wa nchi sio? Kwa nini huo wizi ulio fanyika na unao endelea kufanyika pesa zake zisitumike ktk kuweza kuondoa umasikini wa Mtanzania na kuzidi kumuendeleza kimaendeleo, elimu, afya, n.k

    Hacha kutufanya sie hatujaenda shule, Kama kweli viongozi wetu wangekuwa wa kweli basi Tanzania isingekuwa nchi masikini duniani wala tusingeomba misaada ukizingatia utajiri tulio nao, hacha utajiri tu, kama hiyo misaada inayo tengeneza bajeti ya nchi yetu ingetumika ipasavyo bila ya wao kuiba na kuchukua ten percents ktk hiyo misaada na contracts wanazo ingia basi Tanzania ingekuwa nchi Tajiri Afrika nzima na ingekuwa moja ya nchi tajiri duniani.

    CCM na Viongozi wetu wote ni wezi, Hakuna Kiongozi aliye madarakani na aliye kuwa madarakani ambaye hajawai kuibia nchi na kupokea rushwa. wote ni wezi.

    Cha kushangaza, Tanzania wanafanya Uongozi kama kazi na njia mojawapo ya kuongeza utajiri wao na familia zao na biashara zao, badala ya kufanya Uongozi kama ni njia ya kuendeleza Taifa na wananchi wao. Hili Tatizo ni kutokana Hakuna Kiongozi mwenye kuonea uchungu Taifa letu.

    Angalieni maliasiri ya Gas na mafuta yanayo endelea kugunduliwa, Ni kiasi gani cha mapato yatakayo wekwa wazi, waambieni viongozi wetu waweke wazi mikataba iliyo wekwa kati ya Serikali na kampuni ya nje yaliyo kuja kugundua Gas na mafuta na utaona rushwa rushwa tupu.

    Angalieni mikataba ya madini, na uliza ni kiasi gani Tanzania inapata mapato na kiasi gani Makampuni binafsi inapata basi utaona rushwa rushwa...

    Sasa ukisoma toka juu mpaka mwisho wa hii comment na ndio utaona ni jinsi gani moja ya Kazi ya serikali ilitakiwa iwe inafanya, Kazi hiyo ni kutetea maslahi ya Taifa la Tanzania na wanachi wake, na sio nafsi ya wachache wanao iba na kuachwa wazi wafaidi mali ya Mtanzania.... cha kushangaza wanafuatilia EPA tu, je Richmond inakuwaje???????????????? Migodi ya madini???????? Gas na mafuta?????????

    Ni hayo tu... Ujumbe umefika... wasipo angalia nchi itakuja kuwa kama CONGO au zaidi ya CONGO...

    ReplyDelete
  10. Wabongo wenzangu nakubaliana na Jamaa wa Tarehe November 11, 2008 7:35 PM,
    Maneno yake na mawazo yake ni sahihi kabisa ,mie kila summer naenda bongo lakini sijaona mtanzania anaye angaika ki-vyake bila kuiba wala ku-gushi dokumenti ,asiye na ushirikiano na EPA ana maisha mazuri ,ukisikia ahaa yule jamaa katokamo jua basi mwizi...mshikaji wangu wa karibu ambaye alikuwa anahesabika successful nafungua michuzi yuko kwenye list ya watu wa EPA jamani tunapata elimu ili kusaidia nchi au kuiporomosha nchi huyu mtu kamaliza shule juzi tu kaisha jihingiza kwa wizi...hii nchi bwana mie sijuhi .... lakini ina niuma sana kuona watanzania(black Tanzania) ndiyo waendesha taxi ,wasukuma mikokoteni ,utingo,walinzi ,houseboy kwa wahindi na wa wahudumu mahotelini.. ukienda hoteli ya standard bongo huwezi kukuta ngozi amekaa anatumia no wao wako milangoni watu wengine ndiyo wana kula raha sasa jamani kama nyumbani kwetu tunakuwa treated hivyo sijuhi nchi za watu itakuwaje....
    huyu JK kwanza aibu hana nalisikia nilivyo kuwa bongo last summer kwamba ana mpango wa kununua BMW X5 (10) kwa ajili ya msafara wake kwenda mikoani ...wanafunzi chuo kikuu wanakosa hata hela ya kununua vitabu ambao hao ndiyo wanategemewa kuendeleza nchi katika karne ya science /technology ohooo bongo (wachina wana methali isemayo ukitaka long term plan for society give them education ...yaliyo baki watajua wenyewe) sie tunapanga kununua X5 wanafunzi chuo kikuu tunawapelekea FFU baada ya hela ya vitabu..haya bwana sie yetu macho...BONGO TAMBARARE..
    MKELEKETWA WA UGHAIBUNI..

    ReplyDelete
  11. Wee wacheni uwongo wenu hapa hakuna hata nchi moja duniani kusipokuwa na tabaka la masikini na matajiri. Hebu huko Ulaya na Marekani mlipo kakae tu usifanye kazi yoyote kama utasurvive. Acheni nyie, kwanza hao watoto wa kijijini nguo nzuri ni siku ya sikukuu au kanisani, leo mnajifanya kama hamjui mlikotoka wengine mmecheza Dar mjini kabisa lakini mlikuwa vumbi tupu kwa michezo ya kitoto hasa mpira. Picha ya mtoto alivyovyaa haiwezi kukwambia umasikini au utajiri wa wazazi wake. Tena inawezekana kwao wamejaza chakula ghalani kwao anaishi kwenye nyumba yao wenyewe japo imeezekwa makuti, wana mashamba yao wenyewe wanamiliki. Nyie huko kwenye vibanda vya kuazima mlipie kodi mwisho wa mwezi, hamna hata mnachomiliki zaidi ya magari mnayoendelea kukatwa kila mwezi, pressure za maisha, watoto wenu hata pa kucheza hawana, ndio mnajiona nafuu?

    Mwingine naye anakuja na hadithi ya kununua BMW 5 za kuendea safari za mikoani, huu si uongo ulitukuka hizo BMW zitapita barabara ya kijiji gani? Au ndio kujifanya hali halisi ya kwenu mmesahau, wengine makwenu hakuendeki mpaka kwa mtumbwi (barabara zilivyo na mashimo) au helikopta kama sio 4WD za nguvu kama Nissan au Landcruiser sasa huto tu BMW tutpita wapi? Acheni uvivu. Watu hawataki kufikiri, kufanya kazi, mamvua yamenyesha mpaka madaraja yanabomoka lakini utashangaa watu watatalalamika mwaka huu hatuna chakula, njaa, hatukulima serikali ituletee misaada! Misaada, ukieguka huko msaada kwenye tuta, mtaacha kufa kwa umasikini!

    ReplyDelete
  12. HUYU NI KIONGOZI WA KWELI KABISA MIA KWA MIA.HONGERA MUHESHIMIWA RAIS MUNGU AKUJAALIE KILA LA KHERI,,AMIN

    msemakweli

    ReplyDelete
  13. Uongozi wa nchi ambayo ina idadi ya watu zaidi ya milioni 20 siyo kitu rahisi wajameni!!! Si kweli na haitakuwa kweli kwa yeyote atakaye shika madaraka ya nchi kama Tanzania kuwapatia maisha ya kulingana watanzania wote na hasa mlingano wa kiongozi na mwananchi wa kawaida kabisa, na ndiyo maana kwenye jamii yeyote duniani kuna "classes" hii ipo hata nchi za ulaya kwani hamkuona aibu ya marekani wakati wa kile kimbunga!!!? Hivyo ninasisitiza kusema JK amejitahidi na anajitahidi hasa kuwa karibu na mtu wa kawaida wa kitanzania, anayoyafanya sasa ni muhimili wa kujenga Tanzania ijayo na kam apatapatikana tena uongozi kama wake kwa awamu nne zijazo basi nina imani Tanzania tutakuwa katika historia ya kundi la watu wenye unafuu mkubwa kimaisha... YES WE CAN .. (dRU)

    ReplyDelete
  14. Hatukatai kuwepo kwa maskini na tajiri; lakini muheshimiwa rais "ange-downgrade" gari la kwenda nalo kijijini. Hiyo ndinga hata huku majuu inatisha... yeye ndo kaenda nayo kijijini! Kuna sehemu ambazo ametua na helikopta kabisa... wanakijiji wakafikiri Yesu karudi - kumbe raisi! Sehemu kama hizi awe anaigia na Land Rover 109 angalao ataonekana walao hajajikweza sana.

    ReplyDelete
  15. Hivi wdau mnaobishia hizo BMW mpo Dar au ughaibuni? Ina maana hamjaziona kama motorcade ya JK imebadilika?

    Nakubaliana na wadau kuwa levels za umasikini na 'kujiweza nafuu' lazima zipo katika taifa lolote lile, mimi kinachoniuma zaidi ni hata ule mgawanyo wa huduma/mahitaji muhimu kama maji na zahanati. Sawa inawezekana mwanakijiji amejaza ghala lake kwa vyakula alivyojilimia, lakini maji ndiyo ayafuate zaidi ya kilometa tano?! Na zahanati kadhalika?! Yaani ningetamani sana kama zile pesa za EPA zilizorudishwa zingepelekwa kwenye mpango wa kuhakikisha maji vijijini yanapatikana, kwa heri au kwa shari!

    ReplyDelete
  16. Kid :"My President, what is a Tanzanian's Dream?!"
    Mr. President:"UFISADI(Corruption), You can make it if you try!"

    ReplyDelete
  17. ANON WA wed Nov 12 01:26 AM.

    Unaenesha hujui BMW X5 ni gari ya aina gani.

    Search the net. maana unaitenga BMW na 4WD's.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...