Mmoja wa mamodo akipita jukwaani wakati wa onyesho la
mitindo ya mavazi la Swahili Fashion Week lililodhaminiwa na kampuni ya simu za
mkononi ya Zain Tanzania kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee hall Dar usiku kuamkia leo. Supa modo anayefanya shughuli zake Afrika Kusini,
Happiness Magesse, akipita jukwaani wakati wa onyesho la mitindo ya mavazi la
Swahili Fashion Week lililodhaminiwa na kampuni ya simu za mkononi ya Zain
Tanzania kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee hall usiku kuamkia leo

Modo akipita jukwaani wakati wa onyesho la
mitindo ya mavazi la Swahili Fashion Week ukumbi wa Diamond Jubilee
Mwimbaji mkongwe wa muziki wa taarab, Bi. Kidude akitumbuiza kwa
kuimba huku akipiga ngoma wakati wa onyesho la mitindo ya mavazi la Swahili
Fashion Week lililoshirikisha wanamitindo kutoka nchi mbalimbali Afrika na
kudhaminiwa na kampuni ya simu za mkononi ya Zain Tanzania kwenye wa kuamkia leo
Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

 1. hivi michuzi unaelewa maana ya SUPER MODEL au unalitumia tu? Hapiness hajawa level ya super model yet

  ReplyDelete
 2. Misoup
  Nimempenda sana huyo dada picha ya tatu...she has a beutiful body; she can play the game (fashion)for many years

  ReplyDelete
 3. zile mbili za kwanza zimetulia, zina haiba. Kasoro kimtandio kfufunika mabega mbele ya wastahiki. Hii ya mwisho haikidhi viwango vya utamduni wa mswahili. Si uswahili kuonyesha sehemu hizo nyeti kadamnasi.

  ReplyDelete
 4. michuzi nimependa sana hizi dizain,na nahitaji kujua who designed it and how i can get hold of 1,unaweza nijibu plz?

  ReplyDelete
 5. JAMANI HAKO KAZEE SI MUTAKIMALIZA? SI KITAKUJA KUPINDUKA NA HILO GOMA NA KUJIFIA KWENYE STEJI?

  ReplyDelete
 6. JAMANI MBONA TUDANGANYANA, SWAHILI FASHION NI LEBO ZA ZAIN KWENYE KILA NGUO...MBONA HATUONA MAMBO YANAYOENDANA NA "SWAHILI" KWENYE HIZO NGUO KAMA NGALAWA, MILIMA, WANYAMA, MISHALE, MINAZI N.K??!!!

  KWA NINI WASINGEITA HAYA MAONYESHO "ZAIN FASHION WEEK"???

  ReplyDelete
 7. WAJUKUU WA BI KIDUDE ACHENI UVIVU, FANYENI KAZI ILI MMUUDUMIE BIBI, AMECHOKA SASA, LAKINI ANADAI WAJUKUU ZANGU WATAKULA NINI,NAMPENDA SANA BI KIDUDE LAKINI MWEEE ANASTAHILI KUSTAAFU, UMRI UMESOGEA SANA, BUSH QUEEN.

  ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...