Kushoto) Ofisa Uhusiano wa Tigo Bw, Jackson Mmbando akikabidhi hundi ya shilingi milioni 10 kwa Mwenyekiti wa Tanzania Mitindo House, Bi Khadija Mwanamboka kudhamini Onesho la Mavazi la Red Ribbon Gala lililoandaliwa na Tanzania Mitindo House kwa lengo la kukusanya pesa zaidi ya shilingi milioni 200 kwaajili ya kujenga kituo cha watoto wanaoishi katika mazingira magumu wa kituo cha Magomeni.Onesho hilo litafanyika tareh 28 katika hoteli ya Move n Pick Dar. Katikati kulia ni wanamitindo washiriki Asia Idarous na anefuata ni Rose Valentine.



Leo hii kampuni ya Simu ya mkononi ya Tigo tunajisikia faraja kuungana na Tanzania Mitindo House (TMH) kwa kudhamini onesho kubwa linalofanyika kila mwaka la Red Ribbon 2008 lenye dhamira ya kukusanya pesa kwaajili ya kusaidia kituo cha watoto yatima ambao wazazi wao wamepoteza maisha baada ya kuathirika na virusi vya ukimwi.

Dhamira ya Tigo kudhamini onesho hili ni kuwaunga mkono Tanzania Mitindo House na kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu kwenye kituo chao cha Magomeni kupitia Onesho la Red Ribbon"

Tigo tumechangia shilingi milioni Tano kwa kutambua umuhimu mkubwa wa kusaidia jamii hii kwa kuwa ni njia mojawapo ya kurudisha kwa jamii kiasi cha faida tunayopata kutokana na ushirikiano mzuri kwenye biashara yetu hii ya mawasiliano kwa wateja wetu wa Tanzania.

Hivyo basi Tigo tunawapongeza waandaaji wa onesho hili na kuwashukuru wanamitindo waliojitokeza kuunga mkono wazo hili lenye dhamira nzuri ya kuimarisha ushikiano na undugu wa Watanzania kusaidiana ambao ni ROSE VALENTINE, ALLY REHMTULLAH, ROBBY MORO, ZAMDA GEORGE, FRANKO DESIGNS, KHADIJA MWANAMBOKA, ASIA IDAROUS, JAMILA SWAI, PAKA WEAR, AIDA SYKES, KIM DEAN, pamoja na JOHN KAVEKE kutoka Kenya na FAROUK ABDELA kutoka Zanzibar.

Bado Tigo tutaendelea na utaratibu wa kupokea na kusaidia michanganuo mingi nchini Tanzania inayoonyesha kuifaidisha jamii katika sekta mbalimbali ikiwemo Afya, Michezo, Elimu na mazingira ya jamii,

Hivyo tunawaomba watanzania kuiga mfano mzuri wa Tanzania Mitindo House kuhakikisha wanatumia vizuri nafasi zao kuandaa matukio yenye lengo la kuileta burudani pamoja na kusaidia jamii nzima ili iweze kuwa na maisha bora zaidi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. i am suspecting the acrobates behind this big money handouts...lets wait and see...

    ReplyDelete
  2. Jamani leo NBC nightly news wameonysha Anne Curry akipanda mlima kilimanjaro. Nadhani mnamfahamu yule mwanadada wa to catch a predator show. Basi ndio yeye. I was so happy ingawaje hakumaliza...Anyway wataonyesha tena kesho asubui katika today's show channel 4 NBC NY

    ReplyDelete
  3. Duh! Wengine mafisadi dada! Usicheke namna hiyo hadharani

    ReplyDelete
  4. Jamani nakumbuka Joni Mashaka alilimwagilia miela milioni 12 hili taasisi la TMH. Zile hela ziliishia wapi kwa maana hawakutaka hata kumtaja huyo kaka kama ndiye aliyekuwa mdhamini wao tangu walipoanzisha NGO yao.

    Niliwaona wakina khadija EATV wakisema kwamba walitoa misaada mingi kwenye jamii kutokana na udhamini kutoka nje ya nchi.

    Waandishi hatukupewa hata senti tano wakati tunafukuziwa na huyu dada kuandika habari zake

    Haya yasiwe ni ufisadi , kwa maana naona hesabu zenu ni kubwa ki dizaini. Mimi nanusa harufu ya ufisadi kusema kweli

    Mwandishi, Mdhibit Ufisadi

    ReplyDelete
  5. Khadija aunty Mola akuzidishie kwa juhudi zako.Nilikuwa karibu sana na marehemu mama yako,Mola amueweke peponi wakati huo ulikuwa mdogo.Mie rafiki wa aunty Ashura bonto.Mola akupe nguvu uzima ueendelee na moyo wa kujitolea Amin.

    ReplyDelete
  6. We annon Nov21: 3:29 acha ushamba wako hapa! Kama ulijuana na mama yake ku na sababu gani ya kusema hapa! Acha UFISADI wako wa kinamna ha

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...