PROMOSHENI NYINGINE KUGAWA MTAJI KWA WATEJA WAKE WA ZANZIBAR
.
Zanzibar November 25, 2008

Kampuni ya Simu za mkononi ya Tigo imeendeleza dhamira yake ya kutoa mawasiliano kwa gharama nafuu kwa wateja wake kwa kuzindua promosheni mbili kabambe kwaajili ya wateja wake walioko Tanzania Visiwani.


Akiongea na waandishi wa Habari Zanzibar Afisa uhusiano Tigo Jackson Mmbando alisema “ Leo tunazindua promosheni mbili kabambe hapa Tanzania visiwani, Sasa mteja ataweza Kulonga akiwa Zanziba kwa shilingi 1 tu kwa Sekunde wakati promosheni nyingine itaasaidia wateja wetu kujishindia MTAJI na kuendelea kuzalisha mali kwaajili ya maisha yao ya kila siku.


Promosheni ya Longa Zanzibar itakuwa maalum kwaajili ya kumfanya mteja yeyote wa Tigo kuwa na uhuru wa mawasiliano kushiriki kikamilifu katika ulimwengu wa sasa kutokana na gharama za mawasiliano kuwa nafuu kupitia Longa Zanzibar kwa shilingi moja tu kwa Sekunde
Kwa mteja yeyote wa Tigo anaetoka sehemu yoyote kuja Zanzibar hivi sasa akiwa na Tigo atalipa shilingi 1 kwa sekunde kwa kila Simu atakayopiga kutoka Tigo kwenda Tigo.


Hauhitaji kujiandikisha ili kujiunga na promosheni, unachotakiwa kufanya ni kujiunga Sasa na familia ya Tigo ukiwa Zanziba na moja kwa moja utakuwa umeunganishwa kwa kuwa promosheni hii dhamira yake ni kuwashukuru wateja wote wanaofanya Tigo iendelee kuwa mtandao unaokuwa kwa kasi kuliko yote Tanzania.


Hii ni zawadi nyingine kutoka Tigo kama ilivyo huduma ya Xtreme itakayoendelea kutoa nafasi kwa wateja kuendana na ulimwengu wa kisasa wa mawasiliano na uzalishaji kupitia mawasilino ya gharama nafuu.


Promosheni yetu ya Mtaji itaendelea kutoa Zawadi kwa kila mteja wa Zanzibar atakaeshiriki kikamilifu.


Hii ni kati ya dhamira zinazoijenga Tigo kutaka kuwa karibu na wateja wake, Ili mteja kushiriki anachotakiwa kufanya ni kutuma neno MTAJI kwenda 15302 mara nyingi ili kujiongezea nafasi ya kujishindia zaidi kwenye kila droo ya wiki.


Zawadi zitakazotolewa kwenye Promosheni ya Tigo MTAJI ni Baiskeli 20, Charahani 20, Trela za Baiskeli 10, Simu za Mkononi 20 pamoja na Muda wa maongezi kutoka Tigo.


Zawadi za Prpmosheni hii ya Mtaji zitatolewa katika mfululizo wa wiki 8 kuanzia leo.


Promosheni ya Mtaji ni maalum kwa wateja wote wa Tigo walioko Zanziba wa malipo kabla na wale wa malipo baada, prosheni itadumu kwa muda wa siku 60 tu ambapo tutakuwa tukifanya droo moja kila siku jumanne ya wiki alhamisi tutakabidhi zawadi kwa washindi wetu hapa hapa Zanzibar.


Ni imani yetu Tigo kuwa kwa kuanzisha promosheni hizi mbili kabambe Mtaji Promosheni na Longa Zanzibar kwa shilingi 1 kwa kila sekunde kila wakati, moja kwa moja Tigo tutakuwa tumechangia kwenye maendeleo ya wateja wetu wa kudumu wanaotumia Tigo kila siku katika mawasiliano ya jamii na kibiashara kwa kubadilishana ujuzi kutokana na mawasiliano haya ya gharama nafuu zaidi.


Tigo iko kwenye makakati madhubuti wa kuimarisha na kupanua mawasiliano ili yafike kila mahali; hali ya kuendelea kusambaa kwa huduma hii ya mawasiliano kila mahali imetoa msuko kwa Tigo kuhakikisha kila mteja anapata huduma kwa gharama nafuu akiwa popote kwa kuanzisha huduma nyingi ndani ya mtandao zinazoendana na mazingira ya Mtanzania ili aweze kumudu mawasiano na kufanya mawasiliano na mtu aliyeko sehemu yeyote kwa kutumia mtandao wa Tigo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...