JK katika mazungumzo na kiongozi wa Chama cha upinzania nchini Zimbwabwe MDC Bwana Morgan Tsvangirai ikulu jijini Dar asubuhi, na chini akimsindikiza baada ya mazungumzo yao. Mambo yakienda mswano Tsvangirai atashika nafasi ya Waziri mkuu wa Zimbabwe wakati serikali ya shirikisho itakapoundwa.

Na Mwandishi Maalum
Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumatano, Novemba 5, 2008, amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu Mteule wa Zimbabwe, Morgan Tsvangirai.

Katika mazungumzo hayo Ikulu, Dar Es Salaam, Tsvangirai ambaye pia ni Kiongozi wa Chama cha Movement for Democratic Change (MDC-T), amemwelezea Rais Kikwete kuhusu jitihada za kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa nchini Zimbabwe.

Waziri Mkuu huyu mteule wa Zimbabwe amewasili Dar Es Salaam asubuhi, na alitarajiwa kuondoka kurejea kwao baada ya mazungumzo yake na Rais Kikwete.

Tsvangirai pia amemweleza Rais Kikwete kuhusu maandalizi ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi za SADC uliopangwa kufanyika Jumapili ijayo, Afrika Kusini, ili kujadili hali ilivyo katika Zimbabwe.

Vyama vya siasa vya MDC-T, ZANU-PF na MDC-M vilitiliana saini makubaliano ya kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa katika Zimbabwe Septemba, mwaka huu, lakini tokea wakati jitihada za kutekeleza makubaliano hayo zimekwama.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Kikwete peleka majeshi yakamngoe Mugabe madarakani.

    ReplyDelete
  2. we anon wa 1 unaongea pumba gani,ye mwenyewe anaitaji kung'olewa apo alipo!

    ReplyDelete
  3. Ndo maana WAAFRIKA wameamua kushangilia demokrasia ya marekani. Maana hapa kwetu hatuna cha kushangilia..ni wizi tuu wa kura na utawala wa mabavu!

    Ama kweli tofauti ni kubwa!

    ReplyDelete
  4. prezidaa wetu kwa kung'aa tu... hana mpinzani afrika...rais utadhani rock star....

    ReplyDelete
  5. Mzee Tsvangiraiacha kupoteza muda na hayo makauboi ya Afrika...kama una matatizo nenda kule 'jumba jeupe' yaani kwa mjaluo Obama!!!

    ReplyDelete
  6. KWANINI MPAMBE WA RAISI NI KIJANA WA CCM? NAONA AMEVAA KIJANI NA NYEUSI. AU NINA MAKENGEZA?

    ReplyDelete
  7. WEE TSVANGIRAI.. HUYO HANA UBAVU KWA BOB!!! NA ZIMBABWE HAINA WAISLAM WENGI KAMA COMORO, UNATEGEMEA NINI SASA.
    KUMBUKA HIVI MMESHINDWA KUKUTANA KWA KING MSWATI, HAYA HARARE HAKUNA KITU, JE HUKO KWA MBEKI SHOGA YAKE NA BOB NDIO MTAFANIKIWA KWELI, HUENDA MWOMBENI MZEE ZHUMA AINGILIE KATI LA SIVYO HATA UKUMBI WA MAZUNGUMZO HAMTA PATA. JITAHIDI UTUMIE NAFASI YA SHEREHE HIZI ZA USHINDI WA OBAMA, WAWEZA KUFANIKIWA JAPO SIJUI HISIA ZA BOB ZIKOJE. KUBWA ZAIDI, UKIMTAZAMA BOB NAONA KAMA HANA TATIZO, TATIZO LIPO KWA WAPAMBE WAKE AKIWEMO GOVANA DR. GONO, BI. MDOGO WA BOB, NA MAGENERALI WA JESHI (WAR VETERANS) AMBAO WAMESHAFISADI NA KUJILIMBIKIZIA MALI ZA WAZIMBABWE.
    UTAMKUMBUKA SANA MAREHEMU MWANAWASA.
    NITAENDELEA........

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...