Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumatano, Novemba 5, 2008, amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu Mteule wa Zimbabwe, Morgan Tsvangirai.
Katika mazungumzo hayo Ikulu, Dar Es Salaam, Tsvangirai ambaye pia ni Kiongozi wa Chama cha Movement for Democratic Change (MDC-T), amemwelezea Rais Kikwete kuhusu jitihada za kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa nchini Zimbabwe.
Waziri Mkuu huyu mteule wa Zimbabwe amewasili Dar Es Salaam asubuhi, na alitarajiwa kuondoka kurejea kwao baada ya mazungumzo yake na Rais Kikwete.
Tsvangirai pia amemweleza Rais Kikwete kuhusu maandalizi ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi za SADC uliopangwa kufanyika Jumapili ijayo, Afrika Kusini, ili kujadili hali ilivyo katika Zimbabwe.
Vyama vya siasa vya MDC-T, ZANU-PF na MDC-M vilitiliana saini makubaliano ya kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa katika Zimbabwe Septemba, mwaka huu, lakini tokea wakati jitihada za kutekeleza makubaliano hayo zimekwama.
Kikwete peleka majeshi yakamngoe Mugabe madarakani.
ReplyDeletewe anon wa 1 unaongea pumba gani,ye mwenyewe anaitaji kung'olewa apo alipo!
ReplyDeleteNdo maana WAAFRIKA wameamua kushangilia demokrasia ya marekani. Maana hapa kwetu hatuna cha kushangilia..ni wizi tuu wa kura na utawala wa mabavu!
ReplyDeleteAma kweli tofauti ni kubwa!
prezidaa wetu kwa kung'aa tu... hana mpinzani afrika...rais utadhani rock star....
ReplyDeleteMzee Tsvangiraiacha kupoteza muda na hayo makauboi ya Afrika...kama una matatizo nenda kule 'jumba jeupe' yaani kwa mjaluo Obama!!!
ReplyDeleteKWANINI MPAMBE WA RAISI NI KIJANA WA CCM? NAONA AMEVAA KIJANI NA NYEUSI. AU NINA MAKENGEZA?
ReplyDeleteWEE TSVANGIRAI.. HUYO HANA UBAVU KWA BOB!!! NA ZIMBABWE HAINA WAISLAM WENGI KAMA COMORO, UNATEGEMEA NINI SASA.
ReplyDeleteKUMBUKA HIVI MMESHINDWA KUKUTANA KWA KING MSWATI, HAYA HARARE HAKUNA KITU, JE HUKO KWA MBEKI SHOGA YAKE NA BOB NDIO MTAFANIKIWA KWELI, HUENDA MWOMBENI MZEE ZHUMA AINGILIE KATI LA SIVYO HATA UKUMBI WA MAZUNGUMZO HAMTA PATA. JITAHIDI UTUMIE NAFASI YA SHEREHE HIZI ZA USHINDI WA OBAMA, WAWEZA KUFANIKIWA JAPO SIJUI HISIA ZA BOB ZIKOJE. KUBWA ZAIDI, UKIMTAZAMA BOB NAONA KAMA HANA TATIZO, TATIZO LIPO KWA WAPAMBE WAKE AKIWEMO GOVANA DR. GONO, BI. MDOGO WA BOB, NA MAGENERALI WA JESHI (WAR VETERANS) AMBAO WAMESHAFISADI NA KUJILIMBIKIZIA MALI ZA WAZIMBABWE.
UTAMKUMBUKA SANA MAREHEMU MWANAWASA.
NITAENDELEA........